uhura / sw_gen_val.json
ebayes's picture
Upload 30 files
597042a verified
raw
history blame
13.8 kB
[
{
"q": "Matokeo ya utafiti ambayo wanafunzi hawakuyategemea:",
"a": "[\"Wanapenda kusoma uso kwa uso\", \"Wanajifunza mapishi\"]",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Kitu gani kilimfanya Wambui asikate tamaa baada ya safari ya kwanza?",
"a": "Mshahara",
"context": "Wiki iliyopita nilisoma habari kuhusu Wambui Chege, Mkenya mwenye urefu wa wastani na nywele zilizosokotwa. Yeye ni miongoni mwa wapagazi wachache ambao ni wanawake wanaofanya kazi katika Mlima wa Kilimanjaro uliopo Tanzania. Anapokuwa kazini, yeye huvaa suruali na mabuti mazito.\n\t\t\t\t\t\nShughuli wanazofanya wapagazi ni mojawapo kati ya zile zinazoingiza mamilioni ya fedha ili kukuza uchumi. Pia huduma wanayoitoa huonyesha sura bora ya nchi. Huduma hizi ni kama kuwapa maelfu ya wapandaji milima fursa ya kujishughulisha na zoezi la kupanda mlima bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu mizigo yao kwani wapagazi huibeba. Wao ni wenyeji kwa watu wanaopanda milima.\n\t\t\t\t\t\nWapandaji wengi huwa na ufahamu wa kimo kirefu, lakini hushangazwa na kasi ya upepo wa theluji na umati wa watalii wanaokabiliana nao. Wambui anakubaliana nao kwani katika mahojiano yake alisema kwamba mara ya kwanza alipoupanda Mlima wa Kilimanjaro alikata shauri kwamba kamwe asingetaka kurudi tena mlimani huko kutokana na sababu hizo.\n\t\t\t\t\t\nLakini alipopokea mshahara uliokuwa mkubwa kuliko alivyotegemea akaamua kuendelea na kazi hii. Na hadi hivi sasa ameshaupanda mlima huo zaidi ya mara hamsini. Mwanzoni Wambui alichoka sana na hata alishindwa kutembea vizuri kwa maumivu, lakini sasa shida kubwa anayoiona ni ile ya watu wengi kumwambia kwamba upagazi ni shughuli ya wanaume, si ya wanawake. Wao wanahisi kwamba wanawake hawatakiwi kufanya kazi ngumu.\n\t\t\t\t\t\nWambui hakubaliani na mawazo hayo. Alisema kwamba watu wote ni sawa. Yeye kama mpagazi anahitajika zaidi katika maeneo ambayo hayana barabara na anafanya kazi pamoja na wenzake kama waongozaji na wapishi ambao ni wanawake kwa wanaume. Waongozaji ndio viongozi wenyewe na wao hufanya maamuzi yote kuhusu safari. Kwa mfano, huamua muda wa kuanza safari. Wapishi hutayarisha milo pale wasafiri wanapofika katika kambi tofauti. Wambui alifafanua kwamba Mlima wa Kilimanjaro una kambi au vituo vikuu vitatu, navyo ni Mandara, Horombo na Kibo. Wambui alisema kutoka kituo kimoja hadi kingine wapandaji wanaweza kuchukua muda wa saa sita, au hata zaidi wakati wa jua la mchana. Kwa hivyo, mara nyingi waongozaji hufanya uamuzi wa kuukwea mlima gizani, hasa kutokea kituo cha Kibo kuelekea kileleni.\n\t\t\t\t\t\nBaada ya kusikiliza mahojiano ya Wambui nilibaini kwamba kazi wanayofanya wapagazi ndiyo hasa uti wa mgongo wa safari za milimani. Wao hubeba takribani kilo ishirini za vitu muhimu kama mahema, mablanketi, chakula, dawa na maji. Pia hubeba vifaa kama meza, viti na hata magodoro. Hivi sasa Wambui anafanya mafunzo yatakayomwezesha kuwa mwongoza watalii. Hiyo ndiyo ndoto yake. ",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Kwa nini kazi ya upagazi ni muhimu kwa nchi? Taja sababu mbili.",
"a": "1. Huendeleza uchumi\n2. Huonyesha sura bora/taswira",

"q": "mita 8.45 − mita 1.81 =",
"a": "mita 6.64",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
},
{
"q": "Mlima wa Kilimanjaro una changamoto gani zisizotegemewa? Taja changamoto mbili.",
"a": "1. Kasi ya upepo\n2. Umati wa watalii",

"q": "Fikra za vijana kuhusu matumizi ya simu za mikononi darasani.",
"a": "[\"Kujikengeusha darasani\", \"kusaidia ufahamu wako wa (muktada wa) mada\", \"kupata majibu kwa rahisi zaidi.\", \"Kama hupendi mwalimu wako\"]",
"context": "Kweli wanafunzi wa leo ni wenyeji wa enzi za kiteknolojia. Kulingana na utafiti uliochapishwa mwaka uliopita, vijana watatu kati ya wanne siku hizi wana simu za kisasa na wengi wanazileta shuleni kila siku. Lakini je, ni wazo zuri kuwaruhusu wanafunzi walete au watumie simu zao darasani? Tulizungumza na walimu, wanafunzi na wazazi kufahamu zaidi.\n \nFarouk ni mwalimu wa hesabu katika shule ya kimataifa Kampala. Alianza kufundisha miaka kumi iliyopita, wakati ambapo hakukuwa na wanafunzi wo wote wenye simu. Anaona kwamba simu zinaweza kuwasaidia walimu, kwa mfano kusambaza taarifa na kuwatumia wanafunzi mazoezi ya kazi za nyumbani. Lakini anataka wanafunzi wasiruhusiwe kabisa kuzileta darasani. ‘Kwangu, simu darasani ni hatari tu. Kwanza, zinawawezesha wanafunzi kuibia katika mitihani, na kweli tatizo hili limeenea sana hivi sasa. Pia wanafunzi wenye simu hawasikilizi darasani na hukengeushwa nazo mara nyingi. Darasani ni kazi ya wanafunzi kusikiliza na kusoma, na ni kazi ya mwalimu kuhakikisha kwamba hakuna fujo. Kwa maoni yangu simu ni kipingamizi tu.’\n \nKhadija na Jonathan wanaishi Moshi na ni rafiki wa miaka mingi. Wote wawili wanasoma kwenye shule moja ya sekondari Moshi. Jonathan ana miaka kumi na mitano, na anapenda sana masomo ya sanaa. Hakubali kwamba matumizi ya simu za mikononi huleta shida darasani, bali anafikiri shida ni walimu wasiojaribu kufanya madarasa yawapendeze wanafunzi. ‘Ninampenda sana mwalimu wangu wa sanaa – madarasa yake ni ya kuvutia na sina haja ya kuangalia simu yangu. Lakini walimu wengine wanaongea tu na ni vigumu kukaa na kusikiliza kwa masaa mengi mfululizo.’\n \nKhadija anacheka na kuzungusha macho kwa mzaha. Yeye ni msichana mwenye umri wa miaka kumi na minne, na ni mwanafunzi hodari aliyetunukiwa Tuzo la Darasa mwaka uliopita. Mama yake alimnunulia simu kama zawadi kwa kupata Tuzo hilo. Khadija anakubali si shida kubwa kutumia simu darasani, lakini bora uzitumie kusaidia ufahamu wako – sio kujikengeusha tu. ‘Simu yangu ya kisasa inanisaidia kupata majibu kwa urahisi zaidi. Sasa sihitaji kumwuliza mwalimu maswali na ninaweza kufahamu zaidi muktadha wa mada zinazofundishwa. Kwa mfano, juzi tulikuwa tukisoma kuhusu Azimio la Arusha na niliweza kupitia makala na magazeti pale pale nilipokaa darasani!’\n \nMama Khadija alikuwa na hofu kidogo alipomnunulia mtoto wake simu, kwa sababu wazazi wengi walikuwa wamemlalamikia kuhusu athari za simu za kisasa kwa watoto wao. ‘Wengi waliniambia kwamba alama zao zilishuka mno. Wanalalamika kwamba watoto wao hawataki kufanya kazi zao za nyumbani, bali wanapendelea kutumia masaa kwenye mitandao ya kijamii au kucheza michezo ya simuni tu.’ Lakini anasema bado hajaona athari mbaya kwa Khadija. ‘Alama zake bado ni za juu, na hutumia simu yake kusambaza taarifa kati yake na rafiki zake kwenye vikundi vyao vya masomo ya shule. Pia sasa simu ni sehemu ya maisha tu na usipoweza kuzitumia utapitwa na wakati. Sijamwekea masharti yo yote, na nimeona ameitumia kwa makini.’ Khadija anatabasamu na kuongeza: ‘Kwa kweli, nilishukuru jinsi mamangu alivyoniamini na nilitaka kumthibitishia kwamba alikuwa sahihi. Kwa hivyo, nimekuwa nikitumia simu kwa uangalifu.’\n \nMwalimu Ida Hamdani alianza kufundisha miezi sita iliyopita. Yeye hakutaka kupiga marufuku simu darasani. Bali, amegundua kwamba simu zinaweza kuwa chombo cha kuboresha mazingira ya masomo darasani kwa wanafunzi na walimu pia, mradi tu unasimamia jinsi zinavyotumiwa. Kwake, hali halisi ni kwamba vijana hutumia simu kila siku, tena watapaswa kuzitumia katika maisha yao yajayo, na ni wajibu wa walimu kuwasaidia kuzitumia kwa njia sahihi. ‘Kitu cha muhimu ni kuweka sheria kwa matumizi ya simu darasani, pamoja na kueleza wazi wanafunzi watakavyoathirika zikitumiwa vibaya. Ukijaribu kuwazuia wanafunzi wasitumie simu kabisa, wataasi tu, lakini ukishirikiana nao kuhakikisha kwamba wanazitumia kwa njia nzuri, watakubali.’",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Wajibu wa walimu:",
"a": "[\"Kusahihisha kazi.\", \"Kuwasiliana na wanafunzi wao (kwa kutumia simu au barua pepe) / kujibu hoja\"]",
"context": "",
"grade": "GCSE",
"category": "Reading comprehension"
},
{
"q": "Badilisha mita 67,000 kuwa kilomita.",
"a": "kilomita 67",
"context": "",
"grade": "4",
"category": "Mathematics"
}
]