text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
Kutokana na ongezeko la matumizi ya simu tamba na za kisasa pamoja na kuimarishwa kwa mitandao, imekuwa rahisi kwa idadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na RICHARD MUNGUTI |
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Ijumaa alizimwa na mahakama kupeperusha katika mitandao ya kijamii video... Na RICHARD MUNGUTI |
KUNDI jipya la mawakili sita waliokuwa wanamwakilisha aliyekuwa gavana wa Nairobi Bw Mike Sonko Jumanne walijiondoa... Na RICHARD MUNGUTI |
RIPOTI ya daktari wa tiba za akili imesema Alhamisi kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko anaugua maradhi ya... Na RICHARD MUNGUTI |
MAHAKAMA ilielezwa jana kuwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko angali amelazwa katika Nairobi Hospital... Na RICHARD MUNGUTI |
UFICHUZI wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko kwamba mtu aliingia kwenye seli anamozuiliwa katika kituo cha... Na BENSON MATHEKA |
Aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko anajuta kwa vitendo alivyofanya akiwa mamlakani; akiepuka kuadhibiwa kwa... Na RICHARD MUNGUTI |
KAMA kuna wakati wenye changamoto tele kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ni sasa. |
Maji yalizidi unga hata... Na RICHARD MUNGUTI |
MASAIBU ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, yaliongezeka Jumatano ilipofichuka kuwa serikali inapanga... Na RICHARD MUNGUTI |
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliangua kilio kortini Jumatano wakati wa kusikizwa kwa kesi ya ufisadi wa... Na CHARLES WASONGA |
WANASIASA na watu ambao majina yao yatawekwa katika orodha ya aibu ya Tume ya Uwiano na Utangamano ya Kitaifa (NCIC)... BENSON MATHEKA na SIMON CIURI |
Masaibu ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko yaliendelea kuongezeka jana alipozuiliwa rumande baada... Na RICHARD MUNGUTI |
MASAIBU ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Gidion Kioko yameongezeka baada ya kusukumwa ndani hadi... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA SAMMY WAWERU MSANII tajika wa nyimbo Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh huenda ametengana na mpenzi wake mwanasiasa Karen Nyamu. Hii ni kutokana na video iliyochipuka ambayo anaskika akisema “nilikuwa kwenye ndoa ya mitara, sasa niko singo”. Samidoh amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Seneta Maalum Karen Nyamu, na wamejaaliwa kupata watoto wawili. Msanii huyo wa nyimbo za Agikuyu, alifichua kuachana na Karen kupitia video ya mbashara ya Tiktok (live) ambapo alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake. Wakati wa mafichuzi hayo, alionekana kuwa kwenye eneo la burudani alikoandamana na msichana ambaye hakuweka wazi endapo ndiye mchumba wake mpya. “Ati hongera kwa kuwa na mpenzi mpya…” Samidoh akasoma mojawapo ya jumbe zilizotumwa na mashabiki wake. Alijibu, “Si wewe pekee ulishushwa madaraka kutoka kiwango cha hadhi hadi dereva wangu…Nilikuwa kwenye ndoa ya mitara ila sasa niko singo”. Mfuasi huyo aliendelea kumdadisi, akitaka kujua iwapo Samidoh anafahamu kuhusu ukurasa wa kimitandao unaohusishwa na mchumba wake – Karen Nyamu Fun Page. Kwa ucheshi, mwimbaji huyo wa kibao tajika cha Kairetu Gakwa (Binti yangu) na Ndiri Mutwe Mwega (Sina kichwa kizuri) alisema kwa sasa anajishughulisha na biashara. “Kwa sasa, ninajishughulisha na masuala biashara. Ikiwa si mradi au biashara, ishi na mama yako,” alielezea. Shabiki wake alimkejeli akitaka kujua aliko nina yake, isijulikane ikiwa alimaanisha mama yake mzazi au mpenzi wake. “Ameoleka na kwa sasa anafurahia fungate (honeymoon),” Samidoh alidokeza. Kidosho aliyeandamana naye alitambua shabiki huyo kama Shabaan, akisema kwamba yeye ni mchochezi. “Wee acha hiyo, unajua Shabaan wewe ni mchochezi sana… (Yuko hapa (akimaanisha Karen Nyamu),” mwanadada huyo alisema. Naye Samidoh aliendelea, “Tunataka Karen, naona hivo ndivo mchango safuni unasema…Naona, lakini sasa yuko online kweli?” Kipusa aliyeandamana naye, alijibu, “Yuko online, mjaribu”. Aidha, shabiki wa Samidoh alitaka Karen Nyamu ajumuishwe kwenye mazungumzo hayo ya mbashara Tiktok. Kilichoshangaza zaidi na kuashiria utengano wa Samidoh na Karen, ni kudai kwamba alimbloki mtandaoni na angeweza kushiriki endapo atamuondoa alikomuweka. “Yuko kwenye orodha ya kublokiwa, sasa hiyo ndio shida. Labda nisitishe mazungumzo haya ya moja kwa moja ili nimuondoa aweze kujumuika nasi,” Samidoh alifafanua. Mahusiano kati ya Samidoh na Karen, ndiyo yalichangia kuachana na mkewe, Edday Nderitu ambaye alihamia Amerika Mei 2023. Edday alikuwa ameonya msanii huyo mapema 2023, akisisitiza kwamba hakuwa tayari kuwa kwenye ndoa ya mitara. Samidoh na Edday wana watoto watatu pamoja. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |

You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MUNGUTI NAIROBI, KENYA RAIA wa Rwanda Desire Muhinyuza atasherehekea Mwaka Mpya 2024 akiwa na amani na utulivu moyoni, baada ya Serikali ya Kenya kuamuru arudishiwe Dola 2.6 milioni (sawa na Sh400 milioni) zilizokuwa zimetwaliwa na Polisi kufuatia mzozo wa umiliki wa kampuni ya biashara ya kimtandao kati yake na mfanyabiashara wa humu nchini Bw Kirimi Koome. Hatua hii ya serikali ni muhimu katika kuimarisha imani ya wawekezaji wanaotoroka nchini mara baada ya kulaghaiwa na baadhi ya Wakenya. Akiamuru Bw Muhinyuza akabidhiwe kitita hicho, hakimu mwandamizi katika mahakama ya Milimani, Nairobi Bi Dolphina Alego alisema Mahakama Kuu mnamo Desemba 27, 2023, ilimtambua mwekezaji huyo kuwa ndiye mwenye kampuni ya Stay Online Limited (SOL) aliyokuwa amenyang’anywa na Bw Koome kwa njia ya ujanja na ufisadi. Bi Alego alisema Jaji Alfred Mabeya, ambaye ni mkuu wa kitengo cha biashara katika Mahakama Kuu, alimtambua Bw Muhinyuza kuwa ndiye mmiliki wa SOL, aliyokuwa amelaghaiwa na Bw Koome mnamo Aprili 14, 2023. Jaji Mabeya alisema katika uamuzi huo wa kihistoria kwamba Bw Koome alitumia ukora na ulaghai kujisingizia na kujitambua kuwa mmiliki wa SOL ilhali alikuwa ameteuliwa na Bw Muhinyuza aiandikishe kwa niaba yake. “Bw Koome aliteuliwa na Bw Muhinyuza aandikishe SOL, Kenya kwa niaba yake, lakini akajisingizia kuwa yake na kupotosha idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya Mwanasheria Mkuu,” Bi Alego alisema. Punde tu baada ya kuandikisha SOL, Kenya wafanyabiashara kutoka Canada, Estonia, Zambia, Tanzania, Uganda, na Kenya waliwekeza zaidi ya Dola 2.6 milioni (Sh400 milioni) katika biashara hiyo ya jukwa la mtandaoni. Kuona kwamba amepokonywa kampuni ya SOL, Bw Muhinyuza alilalamika kwa polisi kwamba ametapeliwa kampuni na pesa na Bw Koome ndipo, idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) ikafika kortini na kupata agizo la kutwaa pesa hizo sizipotee. Na wakati huo huo Bw Muhinyuza akalalamikia idara ya usajili wa kampuni katika afisi ya mwanasheria mkuu kwamba Bw Koome alificha ukweli kuhusu umiliki wa SOL. Pia Bw Muhinyuza kupitia mawakili Danstan Omari, Shadrack Wambui, Sophie Nekesa, Ronald Momanyi na Aranga Omaiyo alimshtaki Bw Koome katika mahakama kuu akiomba ashurutishwe arudishe kampuni na pesa za wateja walioekeza katika SOL, Kenya. Baada ya kutathmini ushahidi uliowasilishwa na Bw Omari, Jaji Mabeya alifikia uamuzi kwamba SOL ni yake Bw Muhinyuza. Alisema mwekezaji huyo aliekeza USD ($)129,000 katika SOL na Bw Koome “hakutoa hata senti moja kufanikisha biashara na usajili wake.” Jaji huyo alimwagiza Bw Koome anayeshtakiwa mbele hakimu mkazi Bw Ben Mark Ekhubi kwa kula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi cha Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000 arudishe pesa hizo. Ijumaa ,viongozi wa mashtaka Bi Dorcus Rugut na James Gachoka walisema ijapokuwa Bw Koome anadai pesa hizo ni zake “hana mamlaka yoyote juu ya pesa hizo.” Bi Rugut alisema Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Igonga ameamuru polisi wamrudishie Bw Muhinyuza kiasi hicho Dola 2.6 milioni. Bi Alego alisema serikali imeagiza pesa hizo zirudishwe kwa mwekezaji huyo aendelee na biashara na kubuni ajira kwa wakenya. Kabla ya polisi kuagizwa kurudisha pesa hizo Bw Koome alipinga ombi hilo akisema “apewe muda wa wiki mbili atafute wakili awasilishe ombi la kuzuia kutwaliwa kwa pesa hizo na Muhinyuza.” Bw Koome alisema : “nimewatimua kazini mawakili Cliff Ombeta, Jackson Omwanza na hivyo nahitaji muda wa kumtafuta wakili mwingine kwa vile sielewi ombi hili la DPP na madhara yake katika kesi hii inayonikabili.” Mahakama iliombwa na wakili Danstan Omari isitilie maanani ombi la Bw Koome kwa vile “pesa anazodai sio zake.” Bi Rugut alisema DPP hapingi pesa hizo zilizokuwa zimezuiliwa kama ushahidi katika kesi inayomkabili Bw Koome. Bi Rugut alisema Desemba 27, 2023, Bw Koome hajakata rufaa kupinga uamuzi wa kumng’oa katika kampuni ya SOL na agizo la kulipa fidia na kurudishia Muhinyuza Dola 100,000 alizomdanganya zilikuwa za kulipia kodi biashara ya SOL lakini “akazitia kibindoni.” Bi Alego alielezwa kesi inayomkabili Bw Koome ni kwamba alikula njama za kumlaghai Bw Muhinyuza kiasi Dola 2.6 milioni na wizi wa Dola 100,000. Mahakama ilikubalia ombi la DPP na kuagiza pesa hizo arudishiwe Muhinyuza. Sasa Bw Koome atapambana na hali yake na kesi ya ufisadi inayomkabili. Kesi inayomkabili Bw Koome itaanza kusikilizwa Februari 9, 2023. Alikana mashtaka manne ya ufisadi na wizi na yuko nje kwa dhamana ya pesa taslimu Sh500,000 You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

It looks like nothing was found at this location. Maybe try one of the links below or a search? Try looking in the monthly archives. 🙂 © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

WYCLIFF KIPSANG na BARNABAS BII KUONGEZEKA kwa umaarufu wa kisiasa wa Seneta Gideon Moi wa Baringo eneo la Rift Valley kumemlazimu Naibu Rais William Ruto kurudi katika ngome yake ya kisiasa kupambana na hali hiyo. Bw Moi amekuwa akiendeleza siasa mashinani kupitia kwa wanasiasa, wazee na mabwenyenye wa Rift Valley, hali ambayo imempa ushawishi mkubwa siku za karibuni katika jamii ya Kalenjin. Duru zilisema Bw Moi na washirika wake walichukua fursa ya Dkt Ruto kutokuwepo nyumbani kufuta umaaruru wake Rift Valley. Baada ya kugundua mambo yamemharibikia nyumbani, Dkt Ruto ameanza msururu wa ziara Rift Valley na tayari amezuru kaunti za Nandi na Uasin Gishu mara mbili ndani ya wiki moja katika juhudi za kubadilisha mkondo wa upepo. Dkt Ruto ametumia muda mwingi kuzuru maeneo ya Mlima Kenya, Pwani, Magharibi na sehemu za Nyanza akiongoza kundi la Tanga Tanga kujipigia debe kwa ajili ya 2022 na hajakuwa akionekana sana Rift Valley. Uasi dhidi yake umeongezeka baada ya baadhi ya wanasiasa na mabwenyenye waliokuwa wakimuunga mkono kuonekana kuhamia kambi ya Bw Moi ambaye ni mwenyekiti wa Kanu. Hatua ya Chama cha Mashinani (CCM) cha aliyekuwa Gavana wa Bomet Isaac Ruto kuegemea upande wa Bw Moi pia imekuwa pigo kwa Naibu Rais. Cha kumtia wasiwasi zaidi ni kuwa Bw Moi amekuwa akikutana na wanasiasa pamoja na viongozi wenye ushawishi kutoka eneo la Sugoi, ambako ni nyumbani kwa Naibu Rais. Wiki iliyopita, Bw Moi alikutana na viongozi kadhaa wa Bonde la Ufa katika eneo la Kabarak katika juhudi za kujitafutia uungwaji mkono kabla ya kinyang’anyiro cha urais cha 2022. Miongoni mwa waliokutana na Bw Moi ni Gavana wa Elgeyo Marakwet Alex Tolgos, ambaye amekuwa akirushiana cheche za maneno na Seneta wa kaunti hiyo Kipchumba Murkomen ambaye ni mwandani mkuu wa Naibu wa Rais. Japo Bw Tolgos anasisitiza kuwa angali ndani ya chama cha Jubilee na anaheshimu Rais Uhuru Kenyatta na Dkt Ruto, amekuwa akimmiminia sifa tele Seneta Moi. “Napenda namna Gideon Moi anaendesha mambo yake. Anapenda kila mtu na wala hatumii matusi; ana tabia sawa na mimi,” Gavana Tolgos aliambia Taifa Leo. Wengine waliohudhuria kikao cha Kabarak ni wabunge Sila Tiren (Moiben), Wilson Sossion (Kuteuliwa) na Katibu Mkuu wa Kanu Nick Salat. Wengine ni wabunge wa zamani Zakayo Cheruiyot, Musa Sirma, Frankline Bett, Bw Isaac Ruto, mwanasiasa Zedekiah Bundotich maarufu Buzeki na mbunge wa Tiaty William Kamket. Kushuka kwa umaarufu wa Naibu Rais katika ngome yake ndilo pigo la majuzi kabisa kumkabili kwenye safari yake ya kujiimarisha kwa ajili ya kuwania urais 2022. Tayari kundi la wanasiasa wanaomuunga mkono la Tanga Tanga limeonekana kutuliza siasa baada ya kukabiliwa vikali na maafisa wa serikali akiwemo Rais Uhuru Kenyatta mwenyewe. Umaarufu wake pia umefifia Pwani ambako mwaka jana alifanya kampeni kali za kushawishi wabunge wa ODM kumuunga mkono, lakini sasa wametulia. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na AFP WAKIMBIZI 200,000 kutoka Burundi wamepewa makataa ya mwezi mmoja kuondoka Tanzania la sivyo watarejeshwa kwao kwa nguvu. “Kwa sasa kuna amani nchini Burundi, kwa hivyo wakimbizi wote wanaoishi humu nchini wanatakiwa kurejea kwao kwa hiari kufikia Oktoba 1. Baada ya makataa hayo tutawarejesha kwao kwa nguvu iwe wanataka au la,” akasema waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola. Raia hao wa Burundi walitoroka nchi yao kufuatia machafuko yaliyotokea mnamo 2015 wakati wa maandamano ya kupinga Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Baada ya miezi mitatu, serikali iliandaa kura ya maamuzi na kubadili katiba kumwezesha Rais Nkurunziza kusalia mamlakani hadi 2034. Wakimbizi hao wanaishi katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli kusini-magharibi mwa mkoa wa Kigoma. Mwaka jana, serikali ya Tanzania na Burundi ziliafikiana kuwa zitakuwa zinarejesha nyumbani wakimbizi 2,000 kila wiki. Lakini Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) lilipuuza maafikiano hayo. Shirika la UNCHR limeshikilia kuwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi, unapiga marufuku kurejesha kwa nguvu wakimbizi katika mataifa ambayo wametoroka. Ijumaa iliyopita, Waziri Lugola na mwenzake wa Burundi Pascal Barandagiye walitembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta ambapo alitangaza mpango wa kuwarejesha makwao. Wakati wa ziara hiyo, waziri Lugola alisema serikali haitakubali mpango huo kutatizwa na mashirika ya kimataifa au wageni. Serikali ya Burundi tayari imeshutumu UNCHR kwa kuwa kikwazo kwenye mchakato wa kuwarejesha nyumbani raia wake walioko katika nchi jirani ya Tanzania. Barandagiye wiki iliyopita alisema kuwa shirika la UNHCR ndilo linatatiza mpango huo na ‘linalenga kuzua uhasama baina ya serikali za Tanzania na Burundi’. “Shirika la UNCHR lilipoulizwa na serikali ya Burundi kwa nini wakimbizi wanaorejea nchini ni idadi ndogo, walijibu kuwa hao ndio serikali ya Tanzania iliyoweza kuwaorodhesha. Na serikali ya Tanzania ikiulizwa inasema kuwa serikali ya Burundi imependelea hivyo kwani haina uwezo wa kuwapokea. Hivyo tumegundua UNHCR inalenga kuzua uhasama baina ya serikali hizi mbili. Na ni kikwazo kwa mchakato wa kurejesha wakimbizi nchini.” akasema Barandagiye. Baadhi ya wakimbizi wamepinga mpango wa kurejeshwa makwao huku wakisema kuwa watahatarisha maisha yao. Kulingana na wakimbizi hao, serikali ya Nkurunziza ingali inaendeleza visa vya utekaji nyara na dhuluma. “Watu wamekuwa wakitekwa nyara na kisha miili yao kupatikana imetupwa misituni. Mbona wanataka turejee nyumbani kuuawa?” akasema mmoja wa wakimbizi hao. Msemaji wa UNHCR Dana Hughes alitaka Tanzania na Burundi kuheshimu mkataba wa kimataifa kuhusu hifadhi kwa wakimbizi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na RICHARD MUNGUTI SENETA wa Meru, Mithika Linturi Jumatano aliendelea kuanikwa katika kesi ya talaka inayoendelea kati yake na Maryanne Kitany. Mahakama iliambiwa kuwa mjakazi wao alifariki muda mfupi baada ya kupiga simu na kumweleza Bi Kitany kwamba Seneta Linturi alikuwa akiwapeleka wanawake wengine nyumbani kwao Igembe, Kaunti ya Meru. “Mjakazi wangu aliyekuwa akiwatunza watoto nyumbani Meru alinipigia simu akitaka kuzugumza nami. Nilimweleza nitaenda kumtembelea wikendi hiyo kwa vile Bw Linturi alikuwa anasafiri hadi Uswizi. Usiku huo ndio mjakazi wangu alifariki. Sikuenda kumuona kwa sababu alifariki,” alisema Bi Kitany. Akitoa ushahidi, Bi Kitany alisema sababu kuu zilizomfanya kuwasilisha kesi hiyo ya talaka ni Bw Linturi kutisha kumuua pamoja na kughushi hatimiliki za mashamba ya Kitany pamoja na kupokea mikopo ya mamilioni ya pesa kutoka benki kadhaa bila kumhusisha. Alisema Bw Linturi alimfukuza yeye na watoto katika makazi yao ya Riverside jijini Nairobi kisha akapiga ripoti kwa polisi kuwa magaidi walikuwa wanaishi kwake. “Bw Linturi alisafirisha wahuni kwa basi wakiwa na mbwa na panga kututimua kutoka kwa nyumba yetu Nairobi. Nimemsaidia kujenga makazi yetu na ya wazazi wake Meru,” alisema Bi Kitany. “Mume wangu Bw Mithika alisusia majukumu ya mume, alitoroka makazi yetu ya kifahari ya Nairobi na kujificha Meru. Alidai watu wangu walifanya njama ya kuiba kampuni zake,” Bi Kitany alimweleza Hakimu Mkuu Peter Gesora. Mahakama ilifahamishwa kuwa kila wakati Bw Linturi alipoulizwa na mkewe sababu ya kutotekeleza majukumu ya mume alikuwa akitoroka na kuishi katika hoteli jijini. Bi Kitany alisema Bw Linturi alimchapa wakiwa nyumbani kwao Meru na kwamba alikuwa akimnyima haki ya ndoa. Hakimu Gesora aliamua kuwa vikao vya kesi hiyo sasa vitasikizwa faraghani ili kutoa nafasi ya kueleza kwa undani masuala yaliyovuruga ndoa yao. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA SHABAN MAKOKHA WANDANI wa kiongozi wa ODM Raila Odinga katika eneo la Magharibi wamewaonya wenzao katika kundi la Tangatanga wanaomuunga mkono Naibu Rais William Ruto kujitayarisha kwa kinyang’anyiro kikali 2022. Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na Seneta Cleophas Malala waliwaeleza wabunge kutoka eneo hilo wanaompigia debe Dkt Ruto kwamba, watajutia uamuzi wao baada ya kuadhibiwa na wapigakura ambao hawavutiwi kwa vyovyote na ziara wanazofanya kila wikendi katika kaunti za eneo hilo. “Magharibi ni nyumbani kwa muungano wa Nasa ambao bado ungali hai. Wenzetu wa Tangatanga ambao wana mazoea ya kukita kambi hapa kila wikendi wanafaa kufahamu hawatapata uungwaji mkono wowote; tutawakabili. Lazima waheshimu viongozi wa hapa wakati wa ziara zao,” akasema Bw Oparanya. Mwenyekiti huyo wa Baraza la Magavana Nchini (COG) aliwaomba Wakenya kuwa na subira kuhusu kura ya maamuzi akisema Rais Uhuru Kenyatta na Bw Odinga wapo kwenye mchakato wa kuleta mageuzi makubwa katika siasa za Kenya. “Msihadaike kuunga Punguza Mizigo kwa sababu kuna mambo mengi yanayofaa kushughulikiwa ambayo hayapo kwenye mswada huo unaodhaminiwa na kiongozi wa Third Way Alliance. Tulieni hadi ripoti ya kamati ya maridhiano ya BBI itolewe,” akaongeza Bw Oparanya. Gavana huyo ambaye pia aliwahi kuhudumu kama mbunge wa Butere alisema ni ripoti ya BBI pekee itakayotoa mwanga wa mabadiliko na kusafisha siasa za nchi. Kwa upande wake, Bw Malala ambaye ni Naibu Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Seneti alisema, Nasa haijajiunga na Jubilee ila inashirikiana na Rais Kenyatta kufuatia muafaka kati yake na Bw Odinga, maarufu kama Handsheki, mnamo Machi 2018. “Kundi la Tangatanga linafaa kuzinduka na kufahamu Nasa haipo ndani ya Jubilee. Wakati unakuja ambapo watafahamu msimamo wetu,” akasema Bw Malala. Akizungumza katika eneo la Kanyumba, Kaunti ya Siaya, seneta huyo alifichua kwamba vurugu zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi wenye utata wa 2017 zilitishia kusambaratisha taifa hili ndiposa vigogo wengine wa Nasa walisalimu amri na kuamua kuendesha siasa za kimyakimya ili ukuuaji wa uchumi unaoshuhudiwa usitatizwe. Bw Malala alitabiri kwamba kivumbi cha kugombea Urais 2022 kitakuwa kikali na akawataka wanaomvumisha Dkt Ruto Magharibi kuwa tayari kutemwa na wapiga kura debeni. Huku Bw Oparanya akishikilia kwamba atawania urais, Bw Malala hakufichua kiongozi atakayemuunga mkono wakati wa uchaguzi huo. Naibu Rais amekuwa akishutumiwa na wandani wa Bw Odinga na kundi la Kieleweke kwa kuendesha kampeni za mapema kinyume na agizo la Rais Kenyatta. Ingawa alinukuliwa mara kadhaa akiapa kumuunga mkono Dkt Ruto mnamo 2022 katika kipindi cha kwanza cha utawala wake, Rais Kenyatta amesalia kimya huku ushirikiano wake na Bw Odinga ukifasiriwa na baadhi ya viongozi kama njia ya kuzima nia ya naibu wake kutwaa uongozi kwenye uchaguzi huo. Naibu Rais amepata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge Ben Washiali (Mumias Mashariki), Benard Washiali (Ikolomani), Emmanuel Wangwe (Navakholo), Dan Wanyama (Webuye Mashariki), Malulu Injendi (Malava), Charles Gimose (Hamisi) Dismus Baraza (Kimilili) na John Waluke (Sirisia). Aliyekuwa Seneta wa Kakamega Bonny Khalwale na aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa pia wamekuwa wakimkaribisha Dkt Ruto katika eneo la Magharibi ambalo ni ngome ya Bw Odinga. Kinara wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetang’ula pia siku za nyuma waliwaonya wabunge wanaomshabikia Dkt Ruto wakiwataka wawe tayari kushindwa 2022 wakikosa kuunga mkono mwaniaji kutoka jamii ya Waluhya. Ingawa Mabw Mudavadi na Wetang’ula walieleza nia ya kuunganisha vyama vyao kama njia ya kuhakikisha kura za jamii ya Waluhya zinaelekezwa kwenye kikapu kimoja, juhudi hizo bado hazijafanikiwa huku kila mmoja wao akionekana kuvumisha azima yake ya kumrithi Rais Kenyatta atakapostaafu 2022. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

Na MASHIRIKA SUDAN huenda ikaanza kupokea uwekezaji kutoka nchi za kigeni pamoja na ufadhili wa kifedha huku Waziri Mkuu mpya nchini humo Abdalla Hamdok, akichukua hatua za kuhakikisha taifa lake kunaondolewa kwenye orodha ya Washington kuhusu mataifa yanayofadhili ugaidi. Hamdok alisema amezungumza na maafisa wa Amerika kuhusu kuiondoa Sudan kama mojawapo ya mataifa yaliyoorodheshwa kama wafadhili wakuu wa shughuli za kigaidi. “Huku Sudan ikianza ukurasa mpya, kuondoka katika orodha ya Amerika kuhusu ufadhili wa ugaidi ndilo jambo ‘kuu’ zaidi tunaloweza kufanyia taifa hili,” Hamdok alieleza vyombo vya habari Jumapili, akisema kwamba taifa la Sudan si tishio kwa yeyote ulimwenguni. Haya yamejiri siku chache tu baada ya kiongozi huyo kuchukua usukani wa serikali ya mpito nchini humo inayokumbwa na utata kuhusu utawala wa uraia na jeshi. Uteuzi wake rasmi wiki iliyopita ulifuatia maandamano makubwa yaliyosababisha kung’atuliwa mamlakani kijeshi mnamo Aprili, kwa Rais Omar al-Bashir aliyetawala kimabavu kwa muda mrefu. Baraza kuu linalojumuisha raia sita na wanajeshi watano linatazamiwa kutawala nchi hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu hadi uchaguzi utakapofanyika. Kulingana na Hamdok, hatua ya kuiondoa Sudan kwenye orodha hiyo itafungua milango kwa uwekezaji wa kigeni na kuruhusu taifa hilo kupokea msaada unaohitajika zaidi wa Hazina ya Kimataifa kuhusu Fedha na ufadhili wa Benki ya Ulimwengu. Tangu 1993 Amerika iliiorodhesha Sudan kama taifa linalofadhili “ugaidi” mnamo 1993, na ikadumu katika hali hiyo katika utawala wote wa al-Bashir. Kama mojawapo ya hatua za mwisho za utawala wa Obama, Amerika ilianza mchakato rasmi wa kuiondoa Sudan katika orodha hiyo mnamo Januari 2017, huku ikifutilia mbali vikwazo vya kibiashara na kiuchumi mnamo Oktoba. ‘Tunafahamu na kuelewa kwamba, kuna mchakato katika serikali pamoja na Congress,’ alisema Hamdok, akiongeza kuwa anatumai itafanyika hivi karibuni kwa kuwa “ina matokeo muhimu mno katika hali yetu.” ‘Kwa miaka 30 tulitengwa. Tulichukuliwa kama taifa lisilohitajika. Tunataka kueleza ulimwengu kwamba tunaondoka kwenye vikwazo, masuala ya adhabu na mambo hayo yote na kuwa Sudan inayorejea katika hali ya mataifa ya kawaida,” alisema. Sudan ina deni la karibu Sh6.2 bilioni ambapo Hamdok alisema riba ya deni hilo ni Sh3.1 bilioni.Mkataba wa kugawana mamlaka kati ya viongozi wa maandamano na Baraza la Mpito la Kijeshi Sudan, (TMC) ulitiwa sahihi mapema mwezi huu. Jeshi lilimfurusha al-Bashir mnamo Aprili kufuatia miezi kadha ya maandamano makubwa lakini waandamanaji waliendelea kufurika barabarani wakihofia jeshi huenda likakatalia mamlakani na kudai uhamishaji mara moja katika serikali ya kiraia. Mkataba wa kugawana mamlaka kati ya viongozi wa maandamano na TMC ulitiwa sahihi mapema mwezi huu na kumaliza kipindi cha miezi kadha cha taharuki na ghasia za kisiasa. Imetafsiriwa na Mary Wangari You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |