input
stringlengths
5
25.1k
label
stringclasses
6 values
NA JESSCA NANGAWE STAA wa Bongo    Fleva, Snura Mushi, amewang’ata sikio wachezaji wa timu ya Simba kuelekeza nguvu zao kwenye ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Snura ambaye ni shabiki mkubwa wa timu hiyo, ameeleza hisia zake kwa kikosi hicho baada ya     kushindwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Simba iliondolewa kwenye michuano hiyo na timu ya Al Masry ya Misri baada ya kutoka sare ya  2-2 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushindwa kuifunga timu hiyo katika mchezo wa ugenini. Akizungumza na MTANZANIA jana, Snura aliwapa moyo wachezaji hao huku akiamini ubingwa ndio utawapunguzia machungu. “Yale ni mashindano na lazima tukubaliane na matokeo, mimi kama shabiki wao mkubwa nimesikitika kushindwa kusonga mbele lakini nashukuru vijana walipigana kiume, kazi iliyobaki wanatakiwa kutusahaulisha machungu kwa kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu,”    alisema Snura. Aliongeza kuwa kutokana na kiwango cha wachezaji wa Simba ni dhahiri ubingwa kwao hauzuiliki huku akiwataka kuongeza umakini kwa kuwa wapinzani wao nao wapo kwenye mbio hizo
BURUDANI
Mwashuiya, winga chipukizi aliyesajiliwa na Yanga akitokea Kimondo ya Mbeya alionesha kiwango bora kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda na kufanya mashabiki wa klabu hiyo kumlinganisha na gwiji wa zamani wa klabu hiyo Edibily Lunyamila.Hata hivyo, Pluijm alitoa mwito kwa mashabiki wa soka kuacha kumlinganisha winga huyo na mshambuliaji yeyote aliyepata mafanikio iwe ndani ama nje ya nchi kwani bado ana safari ndefu.“Nilikuwa sijawahi kumsikia Edibily Lunyamila, nimeanza kumsikia baada ya Mwashuiya kuonesha kiwango bora, wananiambia aliwahi kucheza Yanga, lakini nasema ni mapema mno kumlinganisha na mchezaji yeyote aliyefanikiwa kisoka iwe wa ndani ama wa nje ya nchi. “Bado ni kijana mdogo na wote tunatakiwa kumlinda na kumuunga mkono, ana safari ndefu kuthibitisha uwezo wake,” alisema Pluijm.Alisema kwamba Mwashuiya ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee kwani ana hamasa ya ushindi na hali ya kutaka kushinda muda wote lakini bado ana nafasi zaidi ya kubadilika kimbinu ili awe mchezaji mahiri.
MICHEZO
WANAFUNZI 214 wa shule za msingi na sekondari mkoani Kilimanjaro, wamekatishwa masomo kutoka na kupewa ujauzito kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu.Mkuu wa Mkoa, Anna Mghwira ameyasema hayo wakati akizungumzia tatizo la mimba shuleni kwa mkoa huo na hatua zinazochukuliwa kudhibiti hali hiyo.“Mathalani mwezi Septemba mwaka huu watoto wapatao 60 wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Hai walibainika kujihusisha na masuala ya ngono jambo ambalo ni kichocheo kikubwa cha kuwapo kwa mimba mashuleni,” amesema.Amesema kutokana na hali hiyo, Bodi ya Shule ya Hai, ilifanya maamuzi ikiwemo kuwasimamisha masomo baadhi ya wanafunzi wakaidi zaidi na wengine wakihamishiwa shule nyingine.Mghwira amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa wataalamu wa mkoa, moja ya sababu ya mimba mashuleni ni kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii.“Tatizo la mimba mashuleni linachangiwa zaidi na kuporomoka kwa maadili na baadhi ya wazazi/walezi kutotimiza wajibu ama majukumu yao katika malezi ya watoto wao wa kiume na wakike,” amesema.Mkuu wa Mkoa amesema, miongoni mwa jitihada zilizofanyika katika kukabiliana na vitendo hivyo ni ushirikishwaji wa wadau wa elimu katika kupanga mikakati ya kudhibiti matukio ya mimba mashuleni.Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Moshi, Maulid Meshak na Mwanaima Msangi, walisema mimba mashuleni zinaweza kupungua iwapo wananchi watajenga mabweni katika shule ambazo wanafunzi hutembea umbali mrefu kwenda shule.“Uhamasishaji ufanyike ili yajengwe mabweni ya kutosha kwa wanafunzi wanaoishi mbali na zilipo shule, kinyume na hapo mimba zitaendelea kuwepo” amesema Msangi.Wananchi hao walitaka kuwapo kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu hatua zinazochukuliwa kwa watu wanaopatikana na hatia ya kuwapa wanafunzi mimba ili iwe fundisho kwa wengine.
KITAIFA
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili -Mlonganzila jijini Dar es Salaam, imewahakikishia Watanzania kuwa huduma zinazotolewa hospitalini hapo, zimeboreshwa. Pia imesema wagonjwa wanaotibiwa hapo, wameongezeka katika makundi yote.Imesema wagonjwa wa nje, wameongezeka kutoka 17,115 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba 2018 kufikia wagonjwa 25,493 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019 ambalo ni ongezeko la asilimia 48.8.Aidha, wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa wameongezeka kutoka 1,459 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba 2018 na kufikia wagonjwa 2,795 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, ambalo ni ongezeko la asilimia 91.6. Aidha, wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa wameongezeka kutoka 1,459 katika kipindi cha robo mwaka cha Julai hadi Septemba 2018 na kufikia wagonjwa 2,795 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, ambalo ni ongezeko la asilimia 91.6.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, akitoa ufafanuzi tuhuma zinazosambaa mitandaoni kwamba wagonjwa wengi wanapoteza maisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila (MNH-Mloganzila).Profesa Museru alisema katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2019, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH - Upanga) ililaza wagonjwa 17,230 na kati ya hao vifo vilikua 1,673, ambayo ni asilimia 9.7.Alisema hivyo basi takwimu kati ya MHN-Mlongazila na MNH- Upanga za asilimia ya wagonjwa waliofariki dunia hazitofautiani sana, ambapo MNH-Upanga ni asilimia 9.7 wakati MNH-Mloganzila ni asilimia 10.4 katika robo ya Julai hadi Septemba, 2019.“Hatua hii inaonyesha juhudi ambazo zinafanyika za kuboresha utoaji wa huduma katika MNHMloganzila zinazaa matunda,” alisema.Kuhusu tuhuma kuwa madaktari wanaotoa huduma MNHMloganzila ni wanafunzi waliopo katika majaribio, alisema si za kweli, kwa kuwa hospitali hiyo ina madaktari bingwa 52, madaktari wa kawaida 50 na kwa sasa ina madaktari tarajali 53.“Licha ya madaktari bingwa hawa walioajiriwa MNH-Mloganzila kutoa huduma, lakini pia wanashirikiana na madaktari bingwa kutoka MNH-Upanga katika kutoa huduma hapa MNH-Mloganzila, vilevile hospitali hii ina madaktari wawili waliobobea wenye hadhi ya Profesa kutoka Korea, nao wapo wanatoa huduma,”alisema.Alisema madaktari ambao wapo mafunzoni, hawafanyi kazi bila usimamizi kwani hospitali imeweka utaratibu wa kila mgonjwa anayefika kupata huduma, kuonwa na daktari bingwa kwa ajili ya maamuzi.Alisema uongozi wa hospitali unafanyia kazi tuhuma na malalamiko yaliyotolewa juu ya utoaji huduma katika taarifa hiyo ya kwenye mitandao. Alieleza wananchi kwamba tangu MNH, ipewe dhamana ya kusimamia hospitali hiyo ya Mloganzila, uongozi umetatua changamoto zilizokuwepo katika utoaji huduma na kwa kiasi kikubwa kuna mafanikio, ambayo yanaonesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa na pia wagonjwa ambao wametibiwa, wameshuhudia na kuridhika na utoaji wa huduma zake.“Tunawahakikishia Watanzania kuwa huduma zinazotolewa na MNH-Mloganzila zimeboreshwa. Tunawakaribisha Watanzania wenye jukumu la kuelimisha jamii, waje kuzungumza na wataalam na waone jinsi huduma zinavyotolewa ili waweze kutoa taarifa sahihi kwa jamii” alisema Profesa Museru.
KITAIFA
Na ASHA BANI BENKI ya Biashara Afrika (CBA) Tanzania Limited imeungana na Serikali katika kuhakikisha inapambana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona. Katika hilo, CBA imetoa msaada wa matanki ya kuwekea maji yenye thamani ya Sh milioni 10 kwa hospitali kubwa nne za jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuunga mkono mapambano ya ugonjwa huo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa Hospitali ya Mwananyamala, Amana, Lugalo na Sinza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CBA, Gift Shoko alisema hiyo ni hatua ya awali ya kuunga mkono Serikali na jamii. “Lengo la kufanya hivi ni kuonyesha jinsi gani benki inaendelea kujali jamii na watu wake, inajali wateja na pia kushirikiana na Serikali kwani pasipo kujilinda ugonjwa huu ni hatari pia,” alisema Shoko. Aliongeza kuwa mchango huo ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na CBA katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid–19 nchini. “CBA imeweka nia thabiti ya kusaidia hospitali kwa kugawa vifaa vinavyohitajika kutakasia mikono ili watu waweze kunawa mikono kama njia muhimu ya kuzuia maambukizi. “Mara baada ya kuona ongezeko la mahitaji ya kunawa mikono, CBA ilianza mchakato wa kuandaa matenki ya kuhifadhia maji ili kuwezesha watu kunawa mikono wanapokuwa hospitalini, maeneo ambayo ni muhimu kwa afya ya wakazi wa Dar es Salaam. “Kama tunavyojua, virusi vya corona pia huenea kwa kugusa maeneo yaliyo na maambukizi, hivyo tumehakikisha kuwa matenki hayo yana pedali za miguu ili kuwakinga zaidi watumiaji wa matenki hayo,” alisema Shoko. Alisema CBA inatoa elimu kupitia barua-pepe, ujumbe mfupi wa simu, mabango katika maeneo mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii (Facebook na Twitter) ili kutoa taarifa sahihi kuhusu Covid-19 na jinsi ya kulinda, kuzuia maambukizi na kuchukua hatua mbalimbali. “CBA imeweka msisitizo mkubwa kwenye usalama wa wafanyakazi na wateja wetu kwa kuweka vitakasa mikono katika njia zote za kuingia benki na katika vyumba vyote kwa matumizi ya wateja na wafanyakazi,” alisema Shoko. 
AFYA
MARAIS Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake Paul Kagame wa Rwanda ambao katika siku za hivi karibuni nchi zao zimeripotiwa kutokuwa na uhusiano nzuri, wamekutana na kuzungumza.Wamekutana wakati wa mkutano wa kujadili changamoto ya ulinzi na usalama katika eneo la nchi za Maziwa Makuu uliofanyika Luanda, Angola. Walikuwa sehemu ya viongozi wa mataifa manne waliokutana kujadili hali ya usalama katika nchi zao. Mbali ya Rwanda na Uganda, mataifa mengine yaliyoshiriki ni wenyeji Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC).Lakini kivutio kikubwa kilikuwa ushiriki wa Kagame na Museveni ambao walionekana kuwa wamoja na kuzungumza mara kadhaa, jambo linaloonekana huenda likarudisha ukaribu baina ya nchi zao.Viongozi wa mataifa hayo manne ambao walihudhuria mkutano huo ni pamoja na Felix Tshisekedi (DRC), Joao Lourenço (Angola), Kagame na Museveni. Biashara kati ya Rwanda na Uganda imekuwa katika wakati mgumu kutokana na kufungwa kwa mipaka ya nchi hizo mara kwa mara kutokana na hali tete ya usalama katika mipaka ya nchi hizo ambayo kuna wakati ilifungwaa, hivyo kuathiri biashara na safari binafsi za watu wa mataifa hayo.Kukutana kwa viongozi hao kumeleta matumaini mapya juu ya kurudishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, kirafiki na kindugu kwa nchi hizo mbili ambazo pia ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
KITAIFA
KIWANDA cha kukausha matunda na viungo cha kampuni ya ELVEN Agri Co Limited kimepanga kuingia katika soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanya biashara kwa kiwango cha juu.Kiwanda hicho kinachofanya biashara hivi sasa katika baadhi ya nchi za SADC ikiwamo Tanzania, Zambia na Botswana, soko lake kubwa lipo Japan, Australia na nchi za Ulaya.Meneja wa Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Brij Kumari, alisema lengo la kiwanda ni kushirikiana na serikali kuzalisha ajira, chakula bora na kufanya biashara yenye viwango katika nchi mbalimbali. Alikuwa akiwasilisha mada kwa ujumbe wa SADC; ambao walikuwa washiriki wa maonesho ya nne ya viwanda yaliyohitimishwa wiki iliyopita.Washiriki hao kutoka nchi 16 za jumuiya, walitembelea viwanda mbalimbali kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua katika kutekeleza sera ya viwanda.“Sasa hivi kutokana na hamasa tunayoipata kutoka serikalini, tumejipanga kupeleka bidhaa zetu katika nchi za SADC, tunaomba ushirikiano wenu kupata ushauri na mawazo mapya ili tuweze kuifikia lengo kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kumari.
KITAIFA
Kuanzia sasa, kwa kuzingatia Muswada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, walimu wote nchini watasajiliwa na itabidi wawe na leseni za kufundishia.Muswada huo uliowasilishwa bungeni jana umependekeza kuwa, mwanataaluma atakayekiuka masharti masharti yatakayowekwa kwa mujibu wa sheria hiyo atatozwa faini si chini ya shilingi milioni tatu au kifungo jela cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imependekeza kuwa, kuwe na ukomo wa adhabu ya fedha kwa kuwa kusema tu si chini ya shilingi milioni tatu kunatoa mwanya kwa muhusika kutozwa zaidi ya kiasi kilichotajwa.Bunge limeelezwa kuwa, Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania itakuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuinua kiwango cha utaalamu wa ualimu ili kuhakikisha walimu wanakuwa na viwango vinavyostahili vya kitaaluma na wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya ualimu. Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekonolojia,Profesa Joyce Ndalichako ametaja walengwa wa bodi hiyo kuwa ni mtu yeyote aliyefuzu mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu au chuo kikuu kinachotambuliwa na mamlaka husika katika ngazi astashahada, stashahada na shahada.Kwa mujibu wa Waziri Ndalichako, mlengwa wa bodi hiyo atakuwa anafundisha katika shule ya awali, shule ya msingi, shule ya sekondari, chuo cha ualimu, au chuo au kituo rasmi cha elimu ya watu wazima.Bodi hiyo itaweka viwango vya utaalamu wa ualimu, itasimamia maadili ya utaalamu wa ualimu na kufanya tafiti kuhusiana na utaalamu wa ualimu ili kuboresha tasnia hiyo.Bunge limeelezwa kuwa, bodi hiyo itawezesha na kusimamia utoaji wa mafunzo kwa walimu na kusikiliza mashauri dhidi ya mwalimu yanayohusiana na uvunjifu wa Kanuni za Maadili ya Utaalamu wa Ualimu na kutoa uamuzi.
KITAIFA
WANAWAKE wa Tanzania jana waliungana na wanawake wenzao duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, huku Rais John Magufuli akiwashukuru kwa mchango mkubwa kwa Taifa.Rais Magufuli amesema serikali inatambua na kuthamini juhudi zao mbalimbali na kwamba anawatakia heri ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka duniani kote. Alisema hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana, baada ya kuagana na mgeni wake, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Alisema hayo alipowasalimia wananchi wa Dar es Salaam, waliojitokeza kumuaga Kagame, ambao wengi wao walikuwa ni wanawake. Katika salamu hizo, Rais Magufuli alisema anawashukuru wanawake wote nchini kwa mchango wao mkubwa kwa Taifa na kwamba serikali inatambua na kuthamini juhudi zao mbalimbali. “Mungu awabariki sana akina mama, mnafanya kazi nzuri kwa ajili ya Taifa hili, endeleeni kuimarisha umoja wa Watanzania wote, serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na akina mama, endeleeni kutembea kifua mbele, Mungu atawalinda.“Na mimi sasa hivi naondoka kwenda kumuona mama yangu hospitalini katika siku yake hii, pia natoa shukrani nyingi kwenu na kwa viongozi wa mkoa na wilaya kwa jinsi mnavyojitolea kuwapokea na kuwaaga vizuri wageni wetu,” alisisitiza Rais Magufuli. Mkoani Dar es Salaam, wasichana 100 waliomaliza kidato cha nne mwaka jana na kufaulu masomo ya Sayansi, wamepata ofa ya kusomeshwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Makonda alitoa ofa hiyo ikiwa ni Siku ya Wanawake Duniani, yenye kaulimbiu ‘Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu’ ambako alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho kwenye Ukumbi wa Mlimani City.“Wasichana 100 waliofanya vizuri kidato cha nne masomo ya Sayansi ofisi yangu itawasomesha, wameonesha nia, hivyo ni lazima tuwashike mkono, tutawalipia ada na mahitaji yote muhimu ya shule,” alisema Makonda. Alisema ameamua kutoa upendeleo kwa watoto wa kike, kwa kuwa wamezungukwa na changamoto nyingi, ikiwemo za mfumo dume katika taifa.“Mtoto wa kike mbali na changamoto za mfumo dume, pia kuna changamoto za manyang’au kama dereva wa bodaboda, bajaji, makondakta na madereva, na baadhi ya walimu wasio na weledi ambao wamekuwa wakiwalaghai na kuwabebesha mimba” alisema. Katika hatua nyingine, Makonda alisema watoto 1,900 wamepata baba zao na wanawalea, ambao awali walitelekezwa na ofisi yake kuanzisha mchakato wa wakazi waliotelekezwa na wenza wao kufika ofisini kwake.Aliwahakikishia akinamama wote na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa hatokubali watoto waliowabeba matumboni mwao miezi tisa na kuwalea kwa tabu, wafe kwa matumizi ya dawa ya kulevya. ‘Naomba tuungane na Mheshimiwa Rais wetu Magufuli kuhakikisha tunashinda dhidi ya wauaji na wanyonyaji wanaofanya biashara haramu ya dawa za kulevya, kama uliweza kumtunza tumboni miezi tisa basi usikubali mtoto wa mwingine akakatisha matumaini yako, mlinde mwanao ili ule matunda ya uzao wako,” alisisitiza.Mke wa wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein amesema Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, yamewakomboa wanawake na kufungua milango ya fursa mbali mbali ikiwemo za uongozi na elimu. Mama Mwanamwema alisema hayo Gombani kisiwani Pemba wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, akieleza kuwa katika awamu mbali mbali wanawake wamepewa fursa za uongozi wa juu. Kwa mfano, alisema katika Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, wanawake wameshika nafasi za juu za uwaziri katika wizara nyeti zinazoigusa jamii moja kwa moja.Aidha, alisema mawaziri hao wameonesha uwezo mkubwa katika kuziongoza wizara hizo kiasi ya jamii yenyewe kuthibitisha kwamba wanawake wakipewa nafasi za uongozi wanaweza. “Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa nafasi nyingi kwa wanawake katika ngazi ya maamuzi ambapo kwa sasa wapo mawaziri watano walioshika nafasi nyeti za uongozi,” alisema.Aidha, alisema nafasi hizo zipo kwa upande wa vyombo vya maamuzi ikiwemo Mahakama ambako wanawake wanashikilia nafasi hizo ikiwemo majaji. Aliwataka wanawake kupambana na vitendo vya udhalilishaji na kutoa taarifa hizo katika vyombo vya sheria kwa ajili ya uamuzi sahihi. Mapema Waziri wa Uwezeshaji, Wanawake na Watoto, Mauldline Castico aliwataka wanawake kusimamia malezi ya watoto kwa lengo la kujenga Taifa bora la baadaye lenye maadili mazuri.Alisema viongozi wazuri watapatikana kwa kuwepo watoto waliofunzwa na kulelewa katika maadili bora huku wakipata fursa zote muhimu ikiwemo elimu. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, Gaudensia Kabaka aliwataka wanawake kamwe wasikae nyuma na wasimame kidete kuhakikisha wanapata haki na fursa zote ambazo zimo katika Katiba ya Tanzania. “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia mikataba ya kimataifa pamoja na malengo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa ambayo yanasisitiza usawa wa kijinsia kwa jamii ya wanawake,” alisema.Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amewataka wanawake kudumisha upendo na umoja katika kushiriki shughuli za maendeleo nchini kwa kushikamana pamoja bila kujitenga.Akihutubia katika Viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mavunde alibainisha miongoni mwa changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wanawake ni kukosekana kwa umoja, upendo na ushirikiano ambao unawaga katika makundi na kusababisha wanawake kutokuwa na maendeleo ya pamoja. “Niseme ukweli japokuwa hamtaupenda kwa leo, miongoni mwa sababu zinazowakwamisha katika kuendelea ni tabia ya chuki miongoni mwenu, umbeya na makundi yasiyoleta tija za kimaendeleo,” alieleza Mavunde.Alisema wanawake wanapaswa kubadili mitazamo na tabia zinazowagawa na kuondoa upendo kati yao na kujikuta wanajitenga hivyo, kupunguza nguvu kazi ya pamoja katika uzalishaji na kuchangia kusuasua kwa maendeleo yao. Aidha, Mavunde alieleza kuwa, kwa kuzingatia mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo nchini ni vyema wakaishi kwa upendo na umoja ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania ya viwanda.“Kimsingi wanawake ni nguzo imara inayotegemewa na Taifa kwa kuzingatia uthubutu na namna Mungu alivyowapa roho ya kuvumilia na kuwaamini katika utendaji wenye uadilifu,” alisisitiza Mavunde. Nao wanawake walionufaika na mikopo ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wametakiwa kuirejesha kwa wakati ili fedha hizo zivinufaishe vikundi vingi katika kujiletea maendelea kama ilivyokusudiwa. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Janet Kayanda katika katika Uwanja wa Chipukizi Manispaa ya Tabora, akisema fedha zinazotolewa na halmashauri sio sadaka na wala sio ruzuku ya serikali kwao, bali zinatakiwa kurejesha ili zikopeshwe kwa wengine.Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora kuanza utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ya kutaka kiwango cha mikopo kiwe kikubwa ambacho kitaleta tija kwa vikundi. Mwanri alisema kutokana na agizo kiwango cha mikopo kwa vikundi ni lazima kianzie Sh milioni 15 ili wahusika wazalishe bidhaa bora, badala ya kutoa fedha kidogo, ambazo zinaiishia kwa wanakundi kugawana. Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewaagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri, manispaa na majiji nchini kuhakikisha wanatoa mikopo yenye tija kwa wanawake.Akihutubia kwenye Viwanja vya Mlabo katika Kata ya Kisesa wilayani Magu Mkoa wa Mwanza, alisema “Lazima tuihusishe mikopo hiyo na juhudi zinazochukuliwa na Rais Magufuli za kujenga uchumi wa viwanda.” Alisema serikali haitamvumilia mkurugenzi yeyote atakayebainika kutoa mikopo ambayo haina tija kwa mwanamke.Alisema juhudi za serikali katika kuboresha maisha ya mwanamke zinalenga kuhakikisha kila mwanamke anapata mkopo utakaomuwezesha kujiwezesha kiuchumi na kwenye shughuli zake za maendeleo. Aliongeza kuwa serikali imekuwa ikifanya kazi bila kuchoka ili kuhakikisha kuwa vita dhidi ya ukatili kwa mwanamke vinakomeshwa kwa kuendelea kuweka sera na marekebisho ya sheria mbalimbali ili kuzuia mifumo yote ya ukandamizaji kwa mwanamke hapa nchini.
KITAIFA
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwaongoza wapenzi na wanachama wa Klabu ya Yanga kwenye tukio la uchangiaji wa timu hiyo utakaofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Wakati huo huo, wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba, Juma Nature pia wanatarajiwa kuwa miongoni mwa wasanii 15 watakaotumbuiza kwenye tukio hilo kubwa linalotayarajiwa kuiwezesha Yanga kuendeshwa kisasa.Akizungumza mapema leo, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya kuhamasisha uchangishaji Dk David Ruhago alisema kuwa tukio hilo ’Kubwa kuliko’ linatarajiwa kuwakutanisha wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kwa lengo la kuchangisha fedha ambazo zitaisaidia timu hiyo kusajili na kuendesha klabu kisasa.“Ninawaomba wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwenye tukio hilo ikiwa ni pamoja na kununua tiketi kuweza kuichangia timu hiyo ili waweze kufikia malengo walinayotarajia kuyafikia.“Dk Kikwete anatarajiwa kutuongoza hivyo mnapaswa kujitokeza  siku hiyo,”alisema na kuongeza kuwa mashabiki wamerahisishiwa kununua tiketi na kwamba kwa sasa zinazopatika kwenye simu.Aidha kiongozi huyo alisema kuwa tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kama; klabuni Yanga, Dar Live, Total Petrol Azikiwe Posta, Vunjabei Sinza, Robi One Kinondoni na sehemu nyinginezo.
MICHEZO
 BEATRICE KAIZA MARA kadhaa tumeona mastaa wanapofika kwenye vilele vya umaarufu kinachofuata ni kuanguka au kupoteza kabisa nafasi walizonazo, ila sio kwa Wema Sepetu a.k.a Tanzania Sweetheart. Mrembo huyo amefanikiwa kubaki katika kilele cha umaarufu tangu alipoukwaa ustaa kwenye mashindano ya urembo 2006, kisha kujitupa kwenye uingizaji anaoufanya kwa mafanikio mpaka sasa. Juzi kati aliibuka na kipindi chake, Cook With Wema Sepetu kinachopatikana kwenye App na chaneli yake ya YouTube japo kuwa hata akiwa kimya, jina lake halijawahi kukauka kwenye midomo ya wajumbe (mashabiki). Alhamisi wiki hii, Wema Sepetu alitangaza kurudi upya kwenye ulimwengu wa filamu akiwa mhusika mkuu katika tamthilia mpya ya Karma, inayoanza kuruka leo kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo (DSTV). Baada ya kufanya mazungumzo na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Swaggaz tulimvuta pembeni na kuzungumza naye mengi kuhusu kazi na maisha yake binafsi yanayowavutia mashabiki wengi. Swaggaz: Hujaonekana kwa muda mrefu kwenye filamu, umekuja na zawadi gani kwa mashabiki? Wema Sepetu: Kwa sasa nitakuwa naonekana kwenye tamthilia ya Karma ambayo itakuwa inaonekana kila siku za Jumamosi na Jumapili kwa saa nzima kuanzia kesho kutwa (leo). Swaggaz: Karma ni tamthilia yenye maudhui gani? Wema Sepetu: Kwenye Karma ni tamthilia yenye uhondo wa kusisimua, ndani yake kuna siasa, pesa, visasi na mapenzi, ndio vitu vinne tunavyokwenda kushuhudia kwenye tamthilia hii ambayo inakuja kukonga nyoyo za wapenzi wangu. Na Karma ni neno la kituruki lenye maana ya utu na kama utafanya ubaya utalipwa kwa ubaya siwezi kuongea sana mashabiki zangu wakae karibu na Dstv ili kujionea wenyewe uhondo wa tamthilia hii. Swaggaz: Unafanya kazi na wanamitindo wengi ila kwanini ukitengenezewa vazi na Martin Kadinda huwa anafunika zaidi? Wema Sepetu: (anacheka) Yaani Martin ni kila kitu kwangu kwenye mambo ya mavazi na hajawahi kukosea ndio maana akinitengenezea nguo lazima nifunike. Mfano ni siku ile ya uzinduzi wa EP ya Zuchu nilishangaa wengi walinipongeza kwa kupendeza, inatokea tuu, si unajua watu na nyota zetu, huwezi kuamini kuwa hata nguo zilikuja nikiwa ‘location’ na nilizivalia nikiwa huko huko, binafsi sijawahi kupania sherehe jamani. Swaggaz: Na kwanini hivi karibuni umekuwa ukipenda zaidi pendeza kwa kuvaa mavazi meupe? Wema Sepetu: Na bado watu watengemee kuniona na nguo nyeupe tena na tena, nimejikuta tu napenda rangi hii nyeupe kwa sababu nimeona inanipendeza na kwa ushauri ambayo Kadinda ananipa. Swaggaz: Ulipokuwa mnene ulikuwa huonekani kwenye uigizaji ila ulipopungua umepata nafasi ya kuigiza tamthilia mbili mfululizo, We Men na Karma, je wembamba ndio siri ya mafanikio yake kwenye uigizaji kwa kwasa? Wema Sepetu: Ndio, yaani sasa hivi ni kazi kwenda mbele, nafanya kipindi changu cha Cook With Wema Sepetu, matangazo ya biashara, tamthilia nk, kila kitu nafanya kwa sababu najiona mwepesi na ninaupenda sana mwili wangu wa sasa. Swaggaz: Umebadilika kwa kuweka usiri mahusiano yako ya mapenzi, unaifurahia hiyo hali? Wema Sepetu: Nayafurahia sana mapenzi yangu ya sasa ya kuweka ‘private’ mahusiano, ni watu wachache ndio wanamjua mpenzi wangu hadi pale ambapo nitaolewa na ni hivi karibuni tu, Inshallah. Swaggaz: Haya mama asante kwa muda wako. Wema Sepetu: Thank you, shukrani.
BURUDANI
BARCELONA, HISPANIA MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, huenda akafungiwa michezo minne au 12 endapo atakutwa na hatia ya kumsukuma mwamuzi, Ricardo De Burgos, katika mchezo dhidi ya Barcelona. Kwenye mchezo huo wa Super Cup ya Hispania uliochezwa Uwanja wa Nou Camp, Madrid ilishinda mabao 3-1 huku Ronaldo akitolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu. Kwa mujibu wa sheria za soka la Hispania, mchezaji anaweza kufungiwa kuanzia michezo minne hadi 12 ikithibitika amemsukuma mwamuzi. Kifungu cha 96 cha sheria ya soka la Hispania, kinasema kuwa mchezaji akimsukuma, kumtingisha, kumbeba mwamuzi katika hali ya kuashiria vurugu atafungiwa michezo minne au 12. Ronaldo, aliyeingia kama mchezaji wa akiba, alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga, lakini alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake akiwa anashangilia bao lake. Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya njano kwa kujiangusha na akaondolewa uwanjani kwa kuoneshwa kadi nyekundu. Mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, aliamini kwamba alitakiwa kupewa penalti baada ya kuanguka alipokabiliwa na Samuel Umtiti na alionekana kumsukuma mwamuzi baada kuoneshwa kadi nyekundu. Katika mchezo huo beki wa Barcelona, Gerard Pique, alijifunga kupitia krosi iliyochongwa na Marcelo Junior, kabla ya Lionel Messi kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti. Barcelona walionekana kutatizika bila Neymar ambaye amehamia timu ya  Paris Saint Germain (PSG) kwa rekodi ya dunia ya pauni milioni 200. Madrid wanatarajia kuwa wenyeji wa Barcelona katika mechi ya marudiano itakayochezwa kesho saa 6:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Barcelona walimchezesha Gerard Deulofeu safu ya ushambuliaji pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez. Katika ripoti ya mwamuzi huyo alidai kwamba alisukumwa na Ronaldo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kitendo ambacho kiliashiria hakukubaliana na hatua hiyo. Kitendo kama hicho kilitokea Aprili mwaka huu kwa mshambuliaji wa Las Palmas, Marko Livaja, ambaye alifungiwa michezo mitano, mchezo mmoja wa kadi nyekundu na minne kama adhabu. Adhabu aliyopata Livaja ilitokana na sheria ya Ligi ya La Liga  ambapo kutokana na kutodhamiria kitendo hicho aliadhibiwa  kifungo cha michezo minne
KIMATAIFA
Ashura Kazinja-Morogoro MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, amewataka wananchi mkoani hapa kuhakikisha kila mtoto chini ya miaka mitano anasajiliwa kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na kupewa cheti cha kuzaliwa. Alitoa rai hiyo jana kwenye ufunguzi wa kampeni ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio chini ya miaka mitano.  Aliwataka viongozi  wa mkoani humo kuhakikisha wasajili hawaweki urasimu wa aina yoyote kama kudai fedha kwa wananchi ili huduma hiyo isigeuzwa mradi wa kujipatia kipato kwa mtu binafsi.  “Wananchi wa Morogoro tubadilike na kujenga utamaduni wa kufuata mambo muhimu mapema, tuchukue nyaraka zetu zote muhimu za utambulisho ikiwemo vyeti vya kuzaliwa watoto mapema na kuzitunza vizuri ili tuepuke kuwa watu wa matukio” alisema Sanare. Naye Mtendaji Mkuu RITA, Emmy Hudson, alisema hali ya usajili nchini na utunzaji wa kumbukumbu bado hauridhishi, hivyo kusababisha Serikali kukosa takwimu muhimu kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya taifa kama vile afya, elimu na maendeleo ya jamii. “Bila kujua idadi ya wananchi ambao inao serikali haiwezi kutoa huduma kwa ufanisi, lakini maswala ya utawala bora hayawezi kufanikiwa, pia kwa mwananchi mmoja mmoja nyaraka hii ni muhimu kama utambulisho na katika upatikanaji wa haki na huduma mbalimbali” alisema Hudson. Alisema nyaraka hizo zinamsaidia mwananchi kupata haki ya urithi, kupata ajira na huduma nyingine za matibabu na kwamba bila cheti hicho mtu hawezi kupata bima ya afya wala kugaiwa urithi kwani lazima utambuliwe kwa majina na vinasaba. Alisema kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya mwaka 2012 ni asilimia 13.4 tu ya wananchi wa Tanzania bara ndio walikuwa wamesajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa na hivyo kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi yenye viwango vya chini kabisa vya usajili Afrika. Alisema katika tathmini iliyofanyika katika maeneo mbalimbali nchini, sababu zinazosababisha wananchi wengi kutosajiliwa na kupata vyeti kwa wakati ni pamoja na umbali toka makazi ya wananchi mpaka ofisi za wakuu wa wilaya, uelewa mdogo wa umuhimu wa cheti cha kuzaliwa, ada ya cheti na nyinginezo ambazo tayari zimeshafanyiwa kazi. Kwa upande wake  Mwenyekiti Halmashauri ya Morogoro, Kibena Kingo, alisema mtoto anapozaliwa hospitali anapewa kadi ili imsaidie katika usajili, lakini muda unapokuwa mrefu akisubiri kupata pesa 10,000 au 20,000 ya usajili kadi inapotea na kumbukumbu muhimu za mtoto pia. “Kubwa kabisa ambalo nimelipenda mbali na kupeleka huduma karibu na jamii ni kuondosha ada ya usajili, nayo pia ilikuwa kwa wananchi wengine ni shida mtu alikuwa anaona kutoa 20,000 au 10,000 kusajili anaona bora abaki na mtoto” alisema kibena. 
AFYA
Mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yapatikana katika kijiji cha Kambini Kichokochwe kanda ya Mashariki ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kufatia mafunzo ya Mradi wa uwajibikaji Zanzibar (PAZA),Promoting Accountability in Zanzibar.Mabadiliko hayo ambayo yameeonekana katika Nyanja za kielimu ni baada ya wananchi wa kijiji hicho kupatiwa Elimu ya uwajibikaji na kuzungumza changamoto zinazowakabili ndani ya jamii yao na hata nje ambapo mabadiliko chanya yamepatikata ndani ya sekta ya Elimu.Bw,Bakar Suleiman Juma wa Kambini Kichokochwe amefahamisha kuwa kijijini kwao mbali ya mambo mengi yaliyofanywa kupitia mradi huo wa PAZA ni kupata walimu katika skuli ya Kojani ambapo walimu wawili wameajiriwa na Wizara ya Elimu huku walimu tisa wakiwemo nane wa msingi hivi sasa wanalipwa posho na Halmashauri ya Wilaya ya Wete huku mwalimu mmoja wa Sekondari akilipwa posho na Wizara ya Elimu.Amesema” sisi tuliona suala la elimu ni muhimu ila haliwezekani pasipo walimu hivyo hayo yote yamekuja baada ya kupata Elimu na kutafutia ufumbuzi changamoto zetu kwa kupita njia sahihi tulizoelekezwa na mradi huu muhimu wa PAZA”Alifafanua Bw Bakar Nae bi Fatma Saidi,Ameongeza mbali ya suala la elimu pia PAZA umewapatia kisima cha maji safi na salama ambapo hapo awali wanawake kama wahanga wa tatizo hilo maji kambini kichokochwe yalikuwa ni ndoto na sasa kisima hicho kinawanufaisha wanakijiji na kuwarahisishia katka shughuli mbalimbali za maendeleo.Aidha Bi Asha Juma amesema mradi huo ni mkombozi mkubwa kijijini kwao kwani kipindi cha mvua zilizopita mwaka jana nyumba zao zilianguka kwa kuingia maji hali ambayo sasa kumejemgwa vizuizi (slops) ambazo zinazuia maji kupita ndani na kubomoa wakati wananchi waliojenga pembeni mwa barabara walikuwa wanakaa roho juu kila kipindi cha mvua kinapokuja kwa kuhofu kuingiliwa na maji ndani ya nyumba.“Hatuachi kuondoa shukrani kwa mradi huu umetusaidia mambo mengi ambayo yalizorotesha maendeleo kijijini kwetu ila sasa tunasema Alhamdulillah uwajibikaji umepatikana ikiwemo kpata haki za kisheria kama vitambulisho vya Mzanzibar na vyeti vya kuzaliwa”Alishukuru bi Asha.Mradi wa Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) Promoting Accountability in Zanzibar ,umesimamiwa kwa mashirikiano ya jumla ya jumuiya tatu,ikiwemo ya uhifadhi wa mali asili Pemba NGANEREKO, jumuiya ya waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar Wahamaza na TAMWA.
KITAIFA
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda, Obure Pius; vijana sasa wanafanya kazi kwa uhuru na malengo ya kimaendeleo.Anasema kabla ya busara za Airo na Kiboye, waendesha bodaboda walikuwa wanakamuliwa kiasi hicho cha fedha hata kama pikipiki iko kwa fundi.Uamuzi wa Airo na Mwenyekiti huyo wa CCM, umekuja mwezi mmoja baada ya vijana zaidi ya 100 wa Shirati kufanya vurugu na kutaka kumshambulia wakala wa kutoza ushuru, Roja Okuku aliyesalimisha maisha yake kwa kukimbilia Kituo cha Polisi Shirati.
UCHUMI
Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya klabu ya Yanga na mchezaji wake Bernad Morrison raia wa Ghana hatimaye leo kiungo huyo ametambuliswa rasmi kwa watani wao wa jadi Simba SC ikiwa bado kuna kesi ya kimkataba baina ya Morrison na Yanga Hapo awali iliezwa kuwa Morrison ni mali ya Yanga na amesiani kandarasi ya miaka miwili na klabu hiyo kabla ya kugoma kushiriki mazoezi ya timu hiyo ikiwa kwenye hatua za mwisho za kujinda na michezo ya kumalizia ligi. Simba imemtambulisha Morrison ikiwa ni baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu juu ya usajili wa mchezaji huyo alishindwa kufikia makubaliano na Yanga. MORRISON IS RED 🔴 #NguvuMoja A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania) on Aug 8, 2020 at 4:02am PDT
MICHEZO
NA MSHAMU NGOJWIKE, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, Simba leo wanatarajia kushuka dimbani kutupa karata yao ya kwanza kwa kuvaana na timu ya Jamhuri ya Pemba katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Amaan. Simba ambao wamepangwa Kundi A la michuano hiyo wataingia uwanjani saa 2:15 usiku kuwakabili wapinzani wao ikiwa ni baada ya mchezo wa awali wa JKU dhidi ya URA ya Uganda kupigwa kwenye uwanja huo jioni. Kocha Mkuu wa Simba Mwingereza, Dylan Kerr ambaye atakinoa kikosi hicho kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Mapinduzi, amesema matokeo ya ushindi yatatokana na jitihada za wachezaji wake uwanjani kwani tayari amewapa majukumu. Alisema anaamini michuano ya mwaka huu itakuwa migumu kutokana na ubora wa timu zinazoshiriki lakini wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza historia ya kulitwaa kombe hilo. “Mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zinazoshiri, kwa upande wetu tumejipanga kwa matokeo mazuri ili kuendeleza historia ya kufanya vizuri kwenye michuano hii,” alisema. Simba inajitupa uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 iliopata dhidi ya Ndanda FC Ijumaa iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Wekundu hao wa Msimbazi wamekuwa na historia nzuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa mara tatu wakifuatiwa na Azam FC waliochukua mara mbili huku Yanga, Miembeni, Mtibwa Sugar na KCCA wakilinyakua mara moja. Simba walifanikiwa kutwaa taji hili mwaka jana baada ya kuifunga Mtibwa kwa mikwaju ya penalti 4-3. Beki tegemeo wa Simba, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, ataikosa michuano ya Kombe la Mapinduzi kutokana na kupata majeraha yatakayomfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili. Kutokana na kukosekana beki huyo, Kerr atalazimika kumtumia Emery Nimubona upande wa kulia ambaye alionyesha kandanda safi wakati timu hiyo ilipocheza na Ndanda wiki iliyopita. Kiungo Jonas Mkude aliyekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria uliomsababisha kukosa mchezo uliopita dhidi ya Ndanda, aliondoka na kikosi cha Simba kilichosafiri kwenda Zanzibar.
MICHEZO
Erick Mugisha -Dar esw salaam MFANYABIASHARA ambaye ni Mkazi wa Tandale kwa Tumbo, Ally Makwaya (40) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto. Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Saada Mohamed,  akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mwamini Kazema, alidai Januari 7, 2018 eneo la Tandale kwa Tumbo wilayani Kinondoni,  Dar es Salaam mtuhumiwa alikutwa na silaha yenye namba za usajili Uc 49351998 aina ya AK 47. “Upelelezi wa shauri hili haujakamilika na tunaomba mahakama yako kutoa tarehe nyingine kwa kutajwa na kukamilisha upelelezi,” alidai Saada. Hakimu Kazema alisema mshtakiwa hataruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo hadi shauri lake litakapohamishiwa Mahakama Kuu. Alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, mdhamini mmoja awe anafanya kazi taasisi inayotambulika kisheria,  barua za utambulisho na nakala ya kitambulisho cha taifa. Hata hivyo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Desemba 12. Wakati huo huo, watu wawili wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha. Waliofikishwa mahakamani hapo ni Christopher Douglas (24), mkazi wa Mbezi Kimara na Gadi Daudi (27), mkazi wa Makoka Mwisho. Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Doroce Massawe  akiwasomea washtakiwa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu John Chacha, alidai Novemba 26, 2018 eneo la Mwananyamala wilayani Kinondoni, Dar es Salaam waliiba simu aina ya Samsung Note 4 yenye thamani ya Sh 200,000 fedha taslimu Sh 20,000 na vitenge nane vyenye thamani ya Sh 95,000 mali ya Omary Kibalati,  kabla na baada walimtishia kwa panga ili kujipatia mali hizo. Washtakiwa wote walikana kutenda kosa na Massawe alidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba mahakama tarehe nyingine kwa kuanza hoja za awali. Hakimu Chacha alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za kosa washtakiwa hawatakuwa na dhamana, watakuwa wakitokea rumande hadi mwisho na kesi itakuja kwa kuanza hoja za awali Desemba 12.
KITAIFA
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa habari wa BMT, Najaha Bakari jana muda wa kuchukua na kurudisha fomu umeongezwa hadi Julai 31 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 29 badala ya Agosti 15 mwaka huu.Alisema fomu za maombi zitaendelea kutolewa katika ofisi za BMT ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi huo.Pia alisema sifa za wagombea ziambatanishwe katika fomu ya maombi na malipo ya fomu yafanyike katika Benki ya NMB kwa jina la akaunti National Sports Council of Tanzania akaunti namba 20401100013.Aidha baraza limetoa mwito kwa wale wote wenye sifa wapenda michezo wa mpira wa mikono na nia ya kuendeleza mchezo huo kujitokeza kuchukua fomu ili Tanzania isonge mbele kimichezo.
MICHEZO
Ramadhan Hassan-Dodoma JUMLA ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii. “Katika kipindi hiki, matarajio yalikuwa ni wajawazito 1,100,000 wangejifungua, hata hivyo takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 walijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma,” alisema Ummy. Kwa upande wa mahudhurio ya kliniki, alisema kuwa jumla ya wajawazito 797,803 sawa na asilimia 73 ya walengwa walifanya mahudhurio ya kliniki manne na zaidi kama mwongozo ulivyoelekeza. Aidha, alisema kuwa asilimia 87.4 ya wajawazito sawa na kina mama 886,810 walipatiwa dawa za kukinga malaria na jumla ya 2,844,174 sawa na asilimia 84.6 walipewa dawa ya kuzuia upungufu wa damu (FEFOL). Hata hivyo Ummy alisema kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, ilihakikisha dawa muhimu za kuzuia na kutibu kifafa cha mimba na kukinga na kutibu kupoteza damu baada ya kujifungua, kutibu magonjwa kwa watoto chini ya miaka mitano uliimarika kwa zaidi ya asilimia 85.
AFYA
MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi amesema viongozi wa Morogoro watakuwa wasemaji rasmi wa tukio la moto lililosababisha vifo vya watu 64 na kujeruhi wengine 70.Ametoa wito kwa Watanzania kuungana na wakazi wa Morogoro kuomboleza vifo hivyo na kuwaombea majeruhi ili wapate tiba wapone haraka.Akizungumza kupitia Kituo cha Televisheni cha TBC1 jana, Dk Abbasi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), alitoa wito pia kwa watu kutoa msaada kuhakikisha miili ya waliokufa inatambuliwa na ndugu zao na kuhifadhiwa na majeruhi wanapata tiba ili wapone na kurudi katika hali zao kiafya.Dk Abbasi alisisitiza pia vyombo vya habari kuandika na kutumia picha za tukio hilo kwa weledi, maadili na watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia utu na maadili wakati wanapopiga picha za matukio kama hayo na kuacha kusambaza hovyo kwani sio jambo zuri.Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari zinapototea ajali waache kukimbilia kwenye maeneo hayo na badala yake wanapaswa kukaa mbali na kuongeza kuwa anaamini Watanzania wana elimu ya kutosha kuhusu matukio hayo kwani si la kwanza, ila jambo la msingi ni kujifunza kukaa mbali ili kuepusha majanga kama hayo.
KITAIFA
NA FLORENCE SANAWA – MTWARA JESHI la Polisi Mkoa wa Mtwara limezuia mkutano wa ndani wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kupokea barua kutoka kwa uongozi wa CUF Wilaya ya Mtwara wakiwaomba kuchukua hatua hiyo kutokana na hofu ya kutokea uvunjifu wa amani. Mkutano huo uliokuwa ufanyike jana, uliitishwa na Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVICUF) na kuongozwa na Maalim Seif ambaye yuko mkoani hapa kwa ziara ya siku mbili. Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Maalim Seif alitarajiwa kuzungumzia hali ya siasa nchini chini ya utawala wa mwaka mmoja wa Rais Dk. John Magufuli. Ziara ya Maalim Seif ni ya kwanza mkoani hapa tangu chama hicho kikumbwe na mgogoro ambao msingi wake umesababishwa na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kumrudisha Profesa Ibrahim Lipumba katika nafasi yake ya uenyekiti. Kitendo cha mkutano huo kuzuiliwa na polisi ambao walizingira eneo la Ukumbi wa Chuo cha SAUT ulipotakiwa kufanyika wakiwa na gari la maji ya kuwasha na kuimarisha ulinzi, kumesababisha JUVCUF mkoani hapa kulilamikia Jeshi la Polisi kwamba linatumika kisiasa na kuwahujumu. Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya jeshi hilo kuzuia mkutano huo, Maalim Seif, alisema Katibu wa Wilaya wa CUF hana mamlaka ya kumzuia yeye kufanya mkutano au kuzuia mkutano wake wa kuangalia miradi ya maendeleo ndani ya chama chao. “Hiki ni kioja cha mwaka, sijawahi kuona mahali popote duniani kikitokea, hii haiwezi kuwa ni uongozi wa CUF wilaya kwa kuwa hawana uwezo wa kuzuia mkutano huu, hapa Serikali imehusika  kukwamisha huu mkutano,” alisema Maalim Seif. Pia alisema kitendo cha polisi kuzuia mkutano huo ni moja ya njama iliyofanywa na Serikali ya kuukwamisha jambo alilosema kuwa ni ukandamizaji wa demokrasia. Alisema chama chao kilifuata taratibu zote wakati wa maandalizi ya mkutano huo, kuanzia ngazi za juu hadi mkoa na ungefanyika kwa kufuata taratibu zote za kisheria pasipo uvunjifu wowote wa amani. “Katibu wa CUF wilaya hana mamlaka ya kuandika barua kwa polisi ili kumzuia katibu mkuu wa Taifa asifanye mkutano, inashangaza, yaani hao watu wamefikia hatua hadi kwenda katika Ukumbi wa Chuo cha SAUT ambao nilitarajia kufanya mkutano wangu na kuzuia eti kwa sababu kuna viashiria vya vurugu jambo ambalo sio kweli,” alisema Maalim Seif. Baada ya mkutano huo kuzuiliwa, Maalim Seif na uongozi wa chama hicho walikwenda mkoani Lindi kuendelea na mkutano mwingine na kueleza kuwa viongozi wa mkoa huo wana msimamo mmoja, hivyo utafanyika. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Thobias Sedoyeka, alisema walipokea barua kutoka kwa uongozi wa CUF Wilaya ya Mtwara wakiwaomba wazuie mkutano huo. Sedoyeka alisema taarifa hiyo ya CUF Wilaya ilionyesha kuwa kuna viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kutokea katika mkutano huo ndiyo maana wakalazimika kuuzuia. “Tulilazimika kuzuia mkutano huo na endapo watakaa chini na kupanga taratibu zao vizuri, hatuna tatizo na tutaruhusu kuendelea na taratibu zao. Tumelazimika kuzuia kuhofia uvunjifu wa amani kama barua ya CUF Wilaya ya Mtwara ilivyojieleza,” alisema Sedoyeka. Naye Mwenyekiti wa JUVICUF Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga mkaani Lindi, Hamidu Bobali, aliwataka wafuasi wa chama hicho kujiongeza baada ya polisi kuzuia mkutano huo kisha waamue kufanya uamuzi sahihi. Mkutano huo umezuiliwa wakati mwezi uliopita viongozi wa chama hicho Wilaya ya Mtwara walimpokea Profesa Lipumba aliyefanya ziara ya siku mbili mkoani hapa na kufanikiwa kufanya mkutano bila zuio lolote la polisi.
KITAIFA
Ilijipatia bao hilo dakika ya 46 mfungaji akiwa Bakar Thani baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Polisi. Polisi wapo nafasi ya pili kutoka mkiani wakiwa na pointi 14, huku ligi hiyo bado ikiongozwa na JKU yenye pointi 51, wakati Mafunzo ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 40.Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo juzi mapema kwenye uwanja huo, Miembeni na Mafunzo zilitoka sare ya bila kufungana. Wakati huo huo, timu ya soka ya Miembeni City imevuna pointi tatu za bure baada ya timu ya FC Lion kushindwa kutokea uwanjani katika Ligi Daraja la Pili Taifa.Kwa mujibu wa Kamishina wa mchezo huo, Ramadhan Nassor waamuzi wote walifika uwanjani kwa wakati na timu ya Miembeni kuwasili kwa wakati na kufanyiwa taratibu zote za mchezo. Alisema mara baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, waamuzi walisubiri timu pinzani lakini walishindwa kutokea.
MICHEZO
Mwadui inatarajiwa kucheza na Azam katika mchezo utakaochezwa kesho Shinyanga.Akizungumza na gazeti hili Kocha Mkuu wa Mwadui, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ alisema kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo.“Sisi tumejipanga kushinda, kwani Azam, Simba na Yanga ni akina nani wasifungwe, tutawaadabisha kwa kuwa kikosi changu kipo vizuri kwa mapambano,” alisema.Kihwelu tayari aliiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika mchezo wa pili wa ligi baada ya kuifunga Africans Sport ya Tanga.Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Toto African ya Mwanza walipoteza.Kocha huyo alisema bado ana nafasi ya kufanya mapinduzi katika michezo ijayo na kufikisha hatma yake ya kutwaa ubingwa. Alisema haijalishi kuona kuwa timu kongwe za Simba, Yanga na Azam kuanza vyema kwani wanaweza wakachemka baadaye na wao wakapnda.
MICHEZO
KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR MUUGUZI Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mwanamvua Said Nassor, amesema wajawazito kukimbilia kwa wakunga wa jadi na kutumia miti shamba, ni baadhi ya sababu ya vifo vingi vyao na watoto. Kutoka na hali hiyo, amewahimiza wajawazito kujifungulia hospitalini kwani licha ya Serikali kuimarisha huduma za afya, bado wapo wanaoendelea kujifungua kwa wakunga wa jadi na wanapopata matatizo ndipo hukimbilia hospitali. Akizungumza na MTANZANIA jana ofisini kwake Kivunge, Dk. Mwanamvua alisema sababu nyingine zinazosababisha vifo vya wajawazito ni utapiamlo na kifafa cha mimba. Alisema mwaka jana hadi Juni mwaka huu, watoto wasiopungua 30 walipoteza maisha katika hospitali hiyo, kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mama zao kujaribu kujifungua kwa wakunga wa jadi. “Tatizo ni wajawazito kujifungua nyumbani, licha ya kuendelea kutoa elimu na Serikali kujitahidi kuimarisha huduma za afya, wapo wanaoendelea kujifungua huko,” alisema Dk. Mwanamvua. Alisema asilimia 90 ya wanawake hubeba mimba wakiwa na umri mdogo na kutumia vyakula visivyo na lishe, jambo linalochangia matatizo kwao na watoto. “Kujifungua nyumbani kuna changamoto nyingi, wajawazito hutoka damu nyingi na hatimaye wanapofikishwa hospitali huwa wamechoka na inakuwa vigumu kuwasaidia, wengine hutumia miti shamba wakiwa wajawazito. “Lakini tutaendelea kutoa elimu juu ya athari ya matumizi ya miti shamba, kwa mfano mti unaoitwa mpambawake watu wanaamini unaongeza damu kwa mjamzito, lakini kitaalamu mti huu unasababisha mkojo kuwa mchafu na kupelekea matatizo wakati wa kujifungua,” alisema. Alieleza kwamba kwa mwezi watoto 10 hadi 15 hupokewa katika hospitali hiyo wakiwa na utapiamlo na upungufu wa damu. Dk. Mwanamvua alisema kutokana na mazingira hayo, mahitaji ya damu salama hospitalini hapo huwa makubwa. Kwa mwezi zaidi ya chupa 30 hutumika kuhudumia wagonjwa, hasa wajawazito na watoto. Alisema katika kuhakikisha matatizo hayo yanapatiwa ufumbuzi, madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo wanatoa elimu kwa wakunga wa jadi, masheha na wajawazito juu ya umuhimu wa kuvitumia vituo vya afya na hospitali kujifungua. Dk. Mwanamvua alisema miongoni mwa juhudi nyingine zinazochukuliwa ni kuelekeza nguvu ya elimu ya afya katika vijiji jirani kama vile Matemwe na Nungwi ambako changamoto inaonekana kuwa kubwa.
AFYA
MASHINDANO ya afya na usafi wa mazingira yanayofanyika kila mwaka tangu 1988, yamechangia kupunguza magonjwa ya kuhara kutoka wagonjwa 1,300,000 katika mwaka 2014 hadi 70,000 katika mwaka 2018.Akizungumza wakati wa kuzindua mashindano hayo jijini hapa jana, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema yameongeza hali ya afya na usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya na katika taasisi. Alisema mashindano hayo, pia yameongeza kazi ya kujenga madampo ya kisasa katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Arusha, Kigoma na Mtwara na na machinjio katika miji mbalimbali nchini.“Kutokana na mshindano hayo, ujenzi wa vyoo bora umeongezeka kutoka asilimia 34.5 mwaka 2014 hadi 55 mwaka 2018, wakati unawaji wa kutumia maji na sabuni umeongezeka kutoka asilimia 11 hadi 19.4 katika kipindi hicho,” alisema. Dk Ndugulile alisema vijiji vinavyotumia vyoo bora kwa asilimia 100 vimeongezeka kutoka 1,300 katika hadi kufikia 4,000, vile vile shule za msingi zinazotumia vyoo bora zimeongezeka kutoka asilimia 38 hadi 89.5.Alisema mashindano ya mwaka huu baada ya kuongeza vipengele viwili vya ofisi ya makatibu tawala wa mikoa na taasisi ya kibenki, yatahusisha makundi 12 ambapo kila kundi litatoa washindi watatu wa kwanza, pili na tatu ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia gari na wengine kupata pikipiki pamoja na zawadi nyingine.Dk Ndugulile alisema katika mashindano ambayo kamati ya kitaifa ya mashindano inajumuisha wajumbe kutoka taasisi, wizara na idara za serikali, yatahusisha halmashauri zote 184 nchini, yakiwemo majiji manne na manispaa 21 na halmashauri za miji 21 nchini.Pia, kutakuwa na mashindano kutafuta kijiji bora, hospitali za rufaa za mikoa, za rufaa za binafsi, hoteli, shule za msingi na sekondari za bweni, shule binafsi za sekondari za bweni pamoja na ofisi za umma. Dk Ndugulile alizipongeza halmashauri za Njombe, Iringa, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro kwa kuongoza katika usafi huo kwa muda mrefu akaomba halmashauri nyingine ziige mfano huo.Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira, Anyitike Mwakitalima alizitaja halmashauri ambazo zimefanya vizuri katika masuala ya usafi kwa miaka mingi iliyopita, kuwa ni pamoja na Iringa, Arusha na Moshi. Mashindano ya mwaka huu ya afya na usafi wa mazingira kwa mwaka 2019 yamezinduliwa rasmi na kilele chake kitakuwa Novemba mwaka huu.
KITAIFA
NEW YORK, Marekani BAADA ya tetesi kwamba msanii wa hip hop nchini Marekani, Curtis Jackson ‘50 Cent’ amefilisika, msanii huyo ameibuka na kuweka wazi baadhi ya vitu anavyojenga kwa sasa akionyesha kwamba bado ana hazina kubwa ya fedha. Hivi karibuni alionyesha nyumba yake mpya ambayo ameijenga barani Afrika lakini hajasema iko nchi gani. Kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo amesema alitangaza kufilisika akiwa na lengo la kujiimarisha kibiashara kwa kujilinda na waovu. “Bado nipo vizuri katika biashara, sijafilisika kama watu wanavyodhani ila nilifanya hivyo kwa ajili ya kujilinda katika biashara zangu,” alisema 50 Cent ambaye anahisa nyingi katika makampuni mbalimbali ya mavazi, vinywaji, ngumi na uchimbaji madini.  
BURUDANI
SERIKALI ya Msumbiji imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa ya watu wapatao 200 walipoteza maisha kutokana na kimbunga na mafuriko kilichoikumba pia Zimbabwe na Malawi.Kimbunga hicho kijulikanacho kama Idai, kimeacha maelfu ya watu bila makazi na kimeharibu miundombinu zikiwamo nyumba, shule, hospitali, viwanja vya ndege, michezo, reli na barabara. Katika taarifa yake kupitia televisheni, Rais Filipe Nyusi alisema takribani watu 200 wamekufa huku miili zaidi ikiwa haijaonekana. Alipotembelea maeneo mbalimbali juzi, alisema idadi ya waliokufa inaweza kufikia watu 1,000.Kwa mujibu wa serikali, watu wapatao 600,000 wameathiriwa huku wengine 100,000 wakihitaji msaada wa dharura mjini Beira. Mfanyakazi wa kitengo cha misaada cha Shirika la Umoja wa Mataifa aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwamba majengo yote katika mji wa Beira wenye watu wapatao 500,000 yameharibiwa.Kwa upande wa Zimbabwe, taarifa zinasema watu 98 wamepoteza maisha. Rais Emmerson Mnangagwa alilazimika kukatisha ziara yake katika Falme za Kiarabu (UAE) na kurejea nyumbani. Nchini Malawi, kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 122.
KITAIFA
SWAGGAZ RIPOTA KAMPUNI kongwe ya uandaaji filamu nchini Marekani, Disney ,inatarajia kufyatua sinema yake mpya, The Lion King, Julai 19 mwaka huu kwenye majumba ya filamu baada ya Jumatano wiki hii kuzinduliwa huko Hollywood. Gumzo kubwa ni hatua ya staa wa muziki, Beyonce Knowles Carter, kutumia maneno ya lugha ya Kiswahili katika wimbo wake Spirit ambao upo kama ‘soundtrack’ kwenye filamu hiyo. Mwanzoni kabisa mwa ngoma hiyo yenye dakika 4:37, yanasikika maneno ya Kiswahili sanifu yakisema: ‘Uishi kwa muda mrefu mfalme (Uishi kwa uishi kwa) Uishi kwa muda mrefu mfalme (Uishi kwa, uishi kwa),” kisha Queen B, anaendelea kuimba Kingereza. Unaweza kuona ni jinsi gani lugha ya Kiswahili inakua kwa kasi na imekuwa na nafasi kubwa kwenye sanaa ulimwenguni kote kiasi cha kutokuwa ajabu tena kuisikia kwenye filamu na nyimbo za wasanii wakubwa. Ukiacha hili la Beyonce, miaka kadhaa nyuma hata Michael Jackson kwenye Liberian Girl, Omario, Nas na wengino waliwahi kuimba Kiswahili katika ngoma zao, hivyo inatupa tafsiri kuwa tunahitaji kuwekeza zaidi kwenye lugha hii. Inatarajiwa kusikia maneno mengi ya Kiswahili yakitumika katika filamu ya The Lion King maana ndani yake kuna mhusika mmoja anaitwa Simba, jina la Kiswahili la mnyama ila jambo la ajabu utaona aliyeingiza sauti yenye maneno ya Kiswahili kwenye wimbo, Spirit siyo Mtanzania wakati Bongo tuna wataalamu wa lugha hii tamu. Disney, wanasema wimbo huo unapatikana kwenye albamu ambayo imeandaliwa na Beyonce mwenyewe kama ‘soundtrack’ ya filamu ya The Lion King, ambayo imebeba kisa kisa cha simba mdogo anayetafuta namna ya kuwa mfalme na kuigizwa na mastaa wengi akiwamo Beyonce, Chaldish Gambino, Seth Rogen, Chiwetel Ejiofor, Billy Eichner na Keegan Michael. Intro Uishi kwa muda mrefu mfalme (Uishi kwa uishi kwa) Uishi kwa muda mrefu mfalme (Uishi kwa, uishi kwa) Verse Yeah, yeah, and the wind is talkin’ Yeah, yeah, for the very first time With a melody that pulls you towards it Paintin’ pictures of paradise Chorus Sayin’ rise up To the light in the sky, yeah Watch the light lift your heart up Burn your flame through the night, woah Chorus Spirit, watch the heavens open (Open) Yeah Spirit, can you hear it callin’? (Callin’) Yeah Verse Yeah, yeah, and the water’s crashin’ Trying to keep your head up high While you’re trembling, that’s when the magic happens And the stars gather by, by your side Chorus Sayin’ rise up To the light in the sky, yeah Let the light lift your heart up Burn your flame through the night, yeah Chorus Spirit, watch the heavens open (Open) Yeah Spirit, can you hear it callin’? (Callin’) Yeah Chorus Your destiny is comin’ close Stand up and fi-i-ight Bridge So go into that far off land And be one with the Great I Am, I Am A boy becomes a man, woah Chorus Spirit, watch the heavens open (Open) Yeah Spirit, can you hear it callin’? (Callin’) Yeah Spirit, yeah, watch the heavens open, open Yeah Spirit, spirit, can you hear it callin’? (Callin’) Yeah Outro So go into a far off land.
BURUDANI
Na WAANDISHI WETU MAMA mmoja mwenye asili ya Zanzibar mapema wiki hii amehukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela kwa kosa la kudanganya kuwa amekufa, ili aweze kujipatia pauni 140,000 za Uingereza kutoka shirika la bima la nchi hiyo. Kiasi hicho cha fedha ni sawa na Sh 405,749,400 za Tanzania iwapo kitabadilishwa kwa sasa, ambapo pauni moja ni sawa na Sh 2,800 za Tanzania. Mama huyo, aitwaye Arafa Nassib, mwenye umri wa miaka 48, anatuhumiwa kupanga njama hizo akishirikiana na mtoto wake wa kiume, Adil Kasim, mwenye miaka 18 na mtu mwingine wa tatu aliyetajwa kwa jina la Yusuf Abdullah, mwenye umri wa miaka 24. Daily Mail limeandika kuwa, mama huyo alikuwa na madeni makubwa yaliyotokana na kukopa samani za gharama kutoka katika makampuni ya BrightHouse na PerfectHome. Inaelezwa, samani hizo alizoziweka kwenye ghorofa alilopanga huko Walsall, West Midlands, alishindwa kulipa na hivyo kuamua kushirikiana na mtoto wake huyo, Kasim, kudai kuwa aliuawa kwa ajali ya barabarani wakati akiwa amekwenda Zanzibar, ili kijana wake huyo aweze kuidhinishiwa malipo ya bima ya maisha ya pauni 140,000. Inaelezwa fedha hizo ziliombwa na Kasim katika Mamlaka ya Wajane (Scottish Widows) kati ya Machi na Desemba, mwaka jana. Nassib, Kasim na Abdullah walikuwa nje kwa dhamana hadi Julai 12, wiki hii, siku iliyotolewa hukumu. Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na Daily Mail, mama huyo pamoja na mtoto wake mashtaka yao yalifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Birmingham Aprili, mwaka huu, baada ya kufanyika uchunguzi dhidi madai ya kifo chake. Taarifa zinaeleza kuwa, mama huyo na mtoto wake, Kasim na Abdullah, wote ni wakazi wa kitongoji chenye viwanda cha Walsall, kilichoko katika mji wa West Midlands, nchini Uingereza. Kitongoji cha Walsall kipo umbali wa maili nane kaskazini magharibi mwa jiji la Birmingham na maili sita mashariki mwa jiji la Wolverhampton. Katika taarifa ya kuthibitisha mashtaka hayo, Jeshi la Polisi nchini Uingereza lilisema mama huyo alikamatwa Februari, wakati akirejea nchini Uingereza, akitokea nchini Canada alikokuwa amekwenda kwa siri. Kesi hiyo ilikuwa inapelelezwa na Kitengo cha Bima cha Jeshi la Polisi cha jijini London, ambacho kilifanya uchunguzi mapema Novemba, mwaka jana na kubaini kuwa Arafa hakufariki dunia kama ilivyodanganywa mamlaka ya bima. MTANZANIA Jumamosi lilimtafuta baba mdogo aliyemlea Arafa aitwaye Haji Nassib, ambaye anaishi visiwani Zanzibar na kukiri kuwa hata yeye amezisikia taarifa hizo. Haji aliliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa, alitumiwa taarifa hizo kupitia mtandao wa WhatsApp, ingawa hajapata taarifa rasmi. “Sina taarifa zozote rasmi zaidi ya kupata habari kwenye WhatsApp kuwa tayari wamehukumiwa, huku nyumbani hawajui na hawajui alidanganya vipi, huku Zanzibar wanajua yupo hai,” alisema Haji. Anasema kabla ya hukumu hiyo alisikia Polisi kutoka nchini Uingereza walifika Zanzibar kuchunguza tuhuma hizo. Ingawa Haji anasema hajui Polisi hao wa Uingereza walifika lini, lakini anasisitiza kuwa hawakufika nyumbani kwake. Haji alisema wao kama familia bado hawana taarifa rasmi na kwamba wakizipata watajua nini wafanye. “Hatuna taarifa rasmi na sijui nini cha kufanya, huyo Arafa ana watoto wawili, mmoja ndio huyo aliyekamatwa naye…pia ana dada yake ambaye anaishi huko huko Uingereza na sijapata taarifa kutoka kwa hao wote,” alisema Haji. Akimwelezea Arafa, baba yake mdogo huyo alisema aliondoka Zanzibar miaka ya 90 na kuhamia Uingereza. Alisema hafahamu kama Arafa ana uraia wa kudumu nchini humo. Akitoa hukumu dhidi ya Arafa, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Birmingham, William Edis, alisema; “Ulikuwa ni mwanzo wa kumaliza uongo mwingi mwingi”. Alilielezea tukio hilo kama ni mpango uliopangwa kisasa, kwa uangalifu ambao umekaribia kufanya kazi. “Ikiwa Tanzania haijawa katika orodha ya nchi hatari kwa udanganyifu wa bima, ni busara kuchukua hatua,” alisema hakimu huyo na kuongeza; “Uaminifu katika mchakato wa madai ya bima ni muhimu, labda mfumo wote wa bima upo hatarini”.
KITAIFA
    NA AZIZA MASOUD, MZAZI ana nafasi kubwa ya kumfundisha mtoto mambo mbalimbali ambayo yatakuwa  yakimuonyesha njia katika maisha yake. Yapo mambo ambayo yatambadilisha kitabia na kumjenga kwa wakati huo, pia yapo ambayo yatamsaidia kuwa sawa katika maisha yake ya baadaye. Taratibu mbalimbali, zikiwamo za mtu kujua kutunza fedha ama kujiwekea akiba hutokana na mazoea na tabia aliyofunzwa ama kuoneshwa akiwa mtoto. Mazoea hutokana na mafunzo anayoyapata kutoka kwa mzazi akiwa mdogo, mtoto kuanzia miaka saba mpaka 11 anakuwa katika nafasi nzuri kumfundisha jinsi ya kuhifadhi fedha. Ili uweze kumsaidia mtoto kuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi fedha mbali na kumfungulia akaunti ya benki ambayo atakuwa anaifahamu, pia unaweza kumwelekeza utaratibu mbadala ambao utamfanya ahifadhi fedha zake ndogondogo. Hakikisha mtoto anakuwa na chombo maalumu ambacho atatumia kuhifadhi fedha ambazo unampa kwa ajili ya matumizi yake ya kila siku, huku ukimsisitiza zitakuja kumsaidia wakati ujao. Anza kwakumfanyia majaribio  wa kumpa fedha mfululizo,mfano pamoja na kwamba umemuwekea utaratibu wa kumpa fedha za shule  siku moja jaribu kumnyima  huku ukimsisitiza  kuwa atumie fedha ya akiba aliyonayo. Kufanya hivyo kutamfanya kuwa makini katika kuhifadhi fedha, kwakuwa atafahamu kuwa ipo siku atahitaji kuitumia. Mwelekeze jinsi ya kuficha katika sehemu salama ambayo hataisahau wala hakuna mtu yeyote ambayo ataiona. Ili kumpa hamasa ya kuendelea kuzihifadhi fedha inapofika muda fulani zitakapokuwa nyingi mshauri akanunue kitu kikubwa ambacho anakipenda na kupitia fedha ndogo anazopewa kwa siku hawezi kukinunua. Lengo la kumfundisha vitu hivyo siyo kwamba unamwelekeza mtoto awe mchoyo, isipokuwa unamfundisha kujua thamani ya fedha. Pia inaelezwa kuwa, mtoto yeyote anayefundishwa kutunza fedha anakuwa na matumizi mazuri ukubwani. Mbali na hilo, mtoto pia unamfundisha mtoto kuishi kwa malengo, kwakuwa endapo atazoea utaratibu huo atakuwa na uwezo wa kujipangia kununua vitu ambavyo havina gharama kubwa  kama mpira wa kuchezea na vingine. Kumfundisha kuishi katika maisha hayo kutamfanya mtoto awe na heshima na fedha, pia atakuwa makini katika matumizi yake ya kila siku.
AFYA
Na Mary Mwita-Namanga UHUSIANO  kati ya Tanzania na Kenya umeanza kuingia dosari baada ya uongozi wa Kaunti ya Kajiado kuwamuru Watanzania zaidi ya 500 wanaoishi kwenye mpaka wa Namanga  kuondoka katika eneo hilo. Hatua hiyo ya Kaunti ya Kajado  kuwafukuza Watanzania hao imetokana na Serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Uhamiaji kudhibiti raia wa Kenya waliokuwa wakiingia nchini holela kupitia mpaka wa Namanga wilayani Longido Mkoa wa Arusha. Uamuzi huo wa Kenya unatajwa kuathiri uhusiano wa  jamii za   pande mbili za nchi hizo uliojengewa kwa zaidi ya miaka 60 ambako wananchi wamekuwa wakipita kwenda kila upande  kununua bidhaa bila kuzuiwa. Baadhi ya Watanzania waliofukuzwa   Kenya  walisema  uamuzi huo wa Kaunti ya Kajiado, umewasababishia hasara kutokana na uwekezaji waliofanya nchini humo. Shedrack Tlway  ambaye   amefukuzwa Kenya na kuacha mali zake, alisema kwa sasa amepoteza mwelekeo kwa kuwa shughuli zake za biashara alikuwa akizifanya Namanga upande wa Kenya. Naye John Bakari alidai hatua ya kufukuzwa   Kenya imemfanya aishi kama ndege asiyekuwa na makazi ya kueleweka kwa sababu  kwa sasa amezuiwa kuishi   pande mbili za Kenya na Tanzania. “Hata  Rais Moi (Daniel Arap) wakati anamaliza muda wa uongozi wake alipita barabara hii ya Namanga na kusimama na kutoa salamu kwa wananchi wote wa mpaka huu. “Alitoa zawadi ya ng’ombe 10 upande wa Namanga Tanzania na Kenya kama ishara ya kudumisha uhusiano baina ya pande zote mbili. “Kwa hali hii ninaziomba Serikali zote mbili zitafakari uamuzi huu kama njia ya kudumisha umoja. “Kwa kweli mimi sijui niende wapi, sikujua kama nitakosa makazi kwa kufukuzwa… wanangu ambao ni wakenya wamenikataa, Tanzania pia nimekataliwa na kunyang’anywa vibali vyote, Mwenyezi Mungu nisaidie,” alisema Bakari. Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, alisema akiwa kiongozi na mwakilishi wa Rais Dk. John Magufuli anatekeleza sheria za nchi. Aliwataka wananchi wanaotaka kuishi nchi yoyote   wafuate sheria za nchi husika na si vinginevyo. “Ikiwa wazazi wanataka watoto wao wasome   Kenya wafuate sheria za Kenya na Wakenya wakitaka kuingia Tanzania wafuate sheria za Tanzania. Huu ndiyo utaratibu na si vinginevyo,” alisema DC Chongolo. Nao raia wa Kenya ambao walizungumza na mwandishi wa habari   kwa nyakati tofauti, walisema hatua ya kufukuzwa kwa Watanzania nchini humo imetokana na Serikali ya Tanzania  kuwafukuza wananchi wa nchi hiyo Machi mwaka huu. Wahome Wafula, alisema   anashangazwa na viongozi wa Tanzania kuondoa uhusiano ambao umejengwa na waasisi wa mataifa hayo kwa miaka zaidi ya 60 kabla na baada ya Uhuru wa nchi hizo. “Mimi naona   hatua ya viongozi wa Kenya  kuwafukuza Watanzania ni sahihi kabisa na ikiwezekana  uhusiano ufe kwa kuwa viongozi wao ndiyo wametaka iwe  hivyo,” alisema wafula. Gazeti hili lilimtafuta Gavana wa Kaunti ya Kajiado, David Nkedianye  kupata ufafanuzi wa uamuzi huo lakini simu yake iliita bila kupokewa hadi tunakwenda mitamboni.
KITAIFA
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, amewageukia mawaziri ambao kwa sasa wanajipitisha kutaka urais mwaka 2020. Amesema watu hao hivi sasa wameanza kujipitisha kutaka kumrithi Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya muda na kwa hatua hiyo huenda wakapoteza sifa. Kauli hiyo aliitoa juzi Ikulu Dar es Salaam, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Kwa mujibu wa chanzo chetu, Dk. Magufuli aliwaonya makada hao wanaoanza kujipitisha kutaka urais wa Zanzibar kabla ya muda, huku akitaka Dk. Shein aachwe afanye kazi. “Rais Magufuli alikuwa mkali sana, hasa ilipoletwa ajenda ya hali ya kisiasa Zanzibar, ambayo ilikuwa ikiangazia uchaguzi wa marudio na wana CCM waliosaliti chama. “Alisema hivi sasa wapo mawaziri ndani ya CCM wameanza kujipitisha kutaka kumrithi Dk. Shein kabla ya wakati wake na akawaonya kuwa wamuache afanye kazi muda wake,” kilisema chanzo chetu. Chanzo hicho kilisema kutokana na hali hiyo, Dk. Magufuli alisema kuwa ili mtu awe rais ni lazima apitie taratibu zinazokubalika na chama na si vinginevyo. Mawaziri na vigogo kadhaa wanatajwa na wana CCM kwamba huenda wakajitosa katika kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar mwaka 2020 wakiwamo Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni na Waziri wa Miundombinu wa Zanzibar, Balozi Ali Abeid Karume. Nahodha alikuwa mmoja wa vigogo waliojitosa mwaka 2010 kuwania kuteuliwa kuwa mgombea urais, lakini alikuwa mshindi wa tatu akipata kura 33, nyuma ya Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyepata kura 54 na Dk. Shein aliyeibuka mshindi kwa kura 117.   MATOKEO UCHAGUZI PEMBA Mbali na hilo, pia katika ajenda hiyo ya hali ya kisiasa Zanzibar, iliwasilishwa taarifa ya namna chama hicho tawala kinavyoteswa na matokeo ya uchaguzi wa wabunge na wawakilishi kwa majimbo ya Pemba. Kutokana na hali hiyo, juzi NEC iliagiza kuundwa kamati maalumu ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa 2015. Wakati hayo yakiendelea, leo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Shein, anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati Maalumu ya NEC. Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar – Idara ya Itikadi na Uenezi, Waride Bakar Jabu, ilisema kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi. Alisema kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili mapendekezo ya wanachama wa CCM, wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani. “Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya NEC, ambacho kimefanyika leo (jana) chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa agenda za kikao hicho,” alisema Waride katika taarifa yake.
KITAIFA
NA FARAJA MASINDE-DARA ES SALAAM POLISI watatu wanaokabililiwa na mashtaka matano ya kuomba na kupokea rushwa  wanatarajiwa kusomewa maelezo ya awali, Agosti 22, mwaka huu. Hatua hiyo ilifikiwa Ijumaa iliyopita baada ya upande wa mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuiambia Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika. Washtakiwa hao  ni Askari PF 20078  Mathias Nkayaga(31) ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi na mkazi wa Mbezi Mwisho, F 919  D/ Sajenti  Philbert Nemes (39) mkazi wa Kambi ya Polisi Kurasini na  F 3539 Koplo Emmanuel Ndosi ( 37) mkazi wa Survey Mlalakuwa. Wakili kutoka Takukuru, Devotha Mihayo alisema  upelelezi umekamilika wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 22, mwaka huu  kwa ajili ya kusomewa hoja za awali kwa washtakiwa hao. Mihayo  alidai  , washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Februari  27, mwaka huu  katika Kituo cha Polisi  Oysterbay,   Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam. Alidai siku ya tukio, washtakiwa waliomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa mfanyabiashara, Juhudi Kyando kama kishawishi cha kuzuia uchunguzi kuhusu tuhuma za kusafirisha meno ya tembo. Katika shtaka la pili ilidaiwa katika Kituo cha Mabasi cha Fire (Faya)   Wilaya ya Ilala, washtakiwa walipokea Sh milioni nane kama sehemu ya malipo ya Sh  milioni 25 walizoomba kwa mlalamikaji. Mihayo alidai katika shtaka la tatu, katika Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Dar es Salaam, washtakiwa walijipatia Sh milioni 10  kama sehemu ya malipo ya Sh milioni 25 walizomuomba mlalamikaji,huku shtaka la nne ni kujipatia Sh milioni saba. Wakili huyo  alidai  katika shtaka la tano, Februari 28, mwaka huu katika eneo la Tabata Bima, washtakiwa hao walijipatia Sh milioni moja kutoka kwa Kyando  kama sehemu ya malipo ya Sh milioni 25 walizoomba.
KITAIFA
Uchambuzi wa Sebastien Satigui Kufuatia tathmini ya miezi 43, Mamlaka ya Usimamizi waChakula na Dawa nchini Marekani (FDA) mnamo Julai 7 iliagiza uuzaji wa IQOS nchini humo, Philip Morris International’s (PMI) mfumo wa joto wa tumbaku, kama bidhaailiyorekebishwa ya tumbaku. Uamuzi huu wa FDA (Marekani) unaashiria mara ya kwanza kwa shirika hilo kutoa agizo la uuzaji la MRTP(Modified Risk Tobacco Product) mbadala wa sigara wa elektroniki. Mamlakailigundua IQOS kuwa “inafaa kukuza afya ya umma nainatarajiwa kuongeza faida kwenye afya ya watu kwa ujumla.” Wakati FDA haikubali IQOS, uamuzi wake ulifuatilia hakiki yakisayansi ya ukurasa zaidi ya milioni 1 wa ushahidiuliowasilishwa na PMI na uliozingatia tafiti huru. Mamlaka hiyo iliongezea kwamba bidhaa za tumbaku ambazohaziwezi kuwaka kama IQOS hutofautiana na sigara nyinginehivyo kupunguza uwezekano wa mwili kupata kemikalihatarishi. Hii inaambatana na hitimisho la mapema la vyombo vyakisheria na kisayansi, nchini Uingereza, Ujerumani, naUholanzi, ambazo zimegundua kuwa bidhaa hiyo hutoa viwangovya chini vya sumu hatarishi ukilinganisha na sigara kali. Utafiti huo unatambua teknolojia ya kupunguza athari ya”kutokuwasha-moto”, ambayo huwapa wavuta sigara nikotini, huku ikipunguza sana hatari zinazohusiana na muwako wasigara ya kawaida. Kwa kuzingatia kuwa uvutaji wa sigara unaua watu zaidi yamilioni saba ulimwenguni kila mwaka, uamuzi wa USDA unafungua fursa ya afya ya umma katika mapambano dhidi yajanga la tumbaku ulimwenguni. Hii ni katika kuhimiza uhamajiwa haraka kutoka kwa sigara kali kwenda kwa njia mbadalakama IQOS – kwa watu wazima wanaovuta sigara ambaowameshindwa au hawataki kuacha – inaweza kuokoa maisha. Uvutaji wa sigara unakua haraka barani Afrika na vifo vinazidikuongezeka. Wakati viwango vya sigara vimepungua katika nchitajiri, viwango hivyo vimekua katika mataifa masikini. Katikakusini mwa Jangwa la Sahara, matumizi ya sigara yaliongezekakwa zaidi ya asilimia 50 kati ya 1980 na 2016. Kati ya vifo vyawatu wazima katika nchi za Kiafrika, vifo hivyo vinasababishwana moshi wa pembeni. Zaidi ya asilimia 60 ni kati ya wanawakeambao wanaishi na hufanya kazi na wavutaji sigara. Masomo sita ya kujifunza kutoka kwa uamuzi wa USFDA namamlaka kama hiyo ya udhibiti huko Ulaya.1. Mbinu thabiti ya kudhibiti tumbaku, ambayo inashutumubidhaa zote za tumbaku kama moja ya kisababishi cha athari kwa afya ya umma, ina nafasi ndogo ya kupunguzamadhara ya sigara katika ulimwengu wa leo;2. Mamlaka za udhibiti zinazotegemea utafiti unaotambuateknolojia mpya za kupunguza madhara zinaweza kusaidiakuunda sera madhubuti za umma kupunguza hatari zakuvuta sigara;3. Sekta ya tumbaku lazima iende haraka katika kukomeshautengenezaji na kuuza sigara za kawaida;4. Inapaswa kupunguza gharama ya bidhaa zinazopunguzahatari na kurahisisha upatikana wake kwa wavutaji sigarawatu wazima barani Afrika;5. Nchi zinapaswa kuzingatia kupunguza uharibifu katika safuyao ya hatua za kudhibiti tumbaku na kushirikisha tasnia yatumbaku ili kupata njia bora za kufanya bidhaa mpyazipatikane kwa watu wazima wanaovuta sigara hawafai au hawataki kuacha, ikijumuisha ushuru kwenye sigara zakawaida, wakati kuzipunguza kwa kiasi kikubwa kwenyebidhaa zilizopunguzwa hatari;6. Katika Afrika nzima, ambapo umri wa wastani ni chini yamiaka 25, hatua madhubuti lazima zifanywe ili kuwalindavijana wenye umri wa chini kutoka kwa kupata bidhaampya, kwa kuzingatia kwamba wameonyeshwa mbadalabora lakini ambao sio kwamba hauna hatari kabisa. Katika ulimwengu mzuri, wanadamu wangeepuka vitu vyotevisivyo vya lazima ambavyo vina athari mbaya kwa afya zao. Kwa bahati mbaya, sivyo ilivyo na labda hautawahi kuwa hivyo. Inahitaji ujasiri na utashi wa kisiasa, lakini ni muhimu kwamamlaka za afya ya umma kuchukua hatua za kupunguza hatarikwa wavutaji zaidi ya bilioni moja ulimwenguni.
AFYA
NA THERESIA GASPER MSANII wa kizazi kipya nchini, Khery Sameer ‘Mr Blue’, amewaeleza wasanii wenzake ambao hawajaolewa na wale wasiooa kwamba ndoa ina neema kubwa kimuziki hivyo watimize jambo hilo mapema. “Inasikitisha vijana wengi wake kwa waume waliofikisha umri wa kuoa na wale wa kuolewa wanakwepa kutimiza ndoa wakihofu kupotea kimuziki lakini nawaeleza kwamba ndoa ina uhusiano mzuri na mafanikio ndiyo maana wengi waliooana wanafanya vizuri katika mambo yao,” alieleza Mr Blue. “Nawashauri wasanii ambao muda wa kuoa umefika waoe ili wajiongezee heshima na kuzidi kukubalika katika jamii kwa kuwa ile dhana ya kuonekana wahuni itapotea na pia fursa mbalimbali na heshima dhidi yao zitafunguka,” alisema. Msanii huyo licha ya kuoa kwa sasa anaendelea vema na muziki wake huku akiwaomba waendelee kuupenda muziki mzuri unaotolewa naye kwa ajili yao kwa kuwa amejipanga mwakani kuendelea na nyimbo nzuri kwa ajili yao huku akiendelea kuboresha ndoa yake iwe mfano wa kuigwa.
BURUDANI
Akizungumza na gazeti hili, Mgosi alisema hatua waliyofikia Yanga ni nzuri na kuwataka wachezaji kuitumia vizuri nafasi hiyo, kwa ajili ya kujitangaza wao binafsi na Tanzania iweze kutambulika kimataifa.“Nawapongeza kwa juhudi zao na walistahili, tangu mwanzo walipokuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa walionesha wamejiandaa, kitu cha msingi kwao wasibweteke, wajipange kuhakikisha wanafanya vizuri hatua ya makundi ikiwezekana wafike fainali,” alisema Mgosi.Alisema hajawahi kushiriki michuano hiyo, lakini anatambua ugumu uliopo na kuwataka Yanga kujizatiti ili kuendana na ushindani.Alisema kama michuano hiyo wataitumia vizuri, itawasaidia kukiimarisha kikosi chao na kuwapa uzoefu mkubwa kuendelea kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu msimu ujao na michuano mingine ya kimataifa ambayo watashiriki.
MICHEZO
Na Waandishi Wetu RAIS Dk. John Magufuli, amewakosoa baadhi ya watendaji wa Serikali waliombeza aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wakati wa sakata la kashfa ya Escrow. Rais Magufuli alisema Kafulila ameonesha uzalendo mkubwa ambao hauwezi kusahaulika katika historia ya Tanzania na kumpongeza kwa hatua yake ya kujitoa muhanga kutetea rasilimali za Watanzania. Akizungumza na wananchi wa Kata ya  Nguruka jana katika uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilaya ya Uvinza alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua ubadhirifu uliofanywa na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL. Alisema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwa sababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa. “Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea kumpongeza maisha yangu yote” alisema. Rais Magufuli alisema maendeleo hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea fedha za umma zilizo kuwa zikiibwa na mafisadi wachache na kujinufaisha wao wenyewe. “Ninajua Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu walikuita tumbili mimi najua  wewe sio tumbili, wao ndiyo matumbili. “Kafulila wewe hongera alisimamia wizi tuliokuwa tunafanyiziwa IPTL. Ni wizi wa ajabu na wengine wakamtisha kumpeleka mahakamani, wakamtukana weee! Na wengine wakamwita tumbili, sasa tumbili amefanya kazi kubwa kwa ajili ya Watanzania. “Tunahitaji wazalendo katika nchi hii, nchi hii ilikosa uzalendo ikawa na watu watafutaji, ukimchagua kiongozi anatafuta pesa yake badala ya kwenda kuongoza kwa ajili ya watu ambao ni masikini. “Tulikosa uzalendo wa utanzania, tukashindwa kumwogopa Mungu kwamba mali ni za muda tu baadae tutaziacha na kwenda kwenye shimo moja tu (kaburini) tutakapozikwa kule kaburini. Ninawaomba Watanzania tujenge uzalendo. “Kafulila wewe najua ni wa chama kingine, lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi ya nchi, kwa hiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza. Kitu ulichokifanya kwa taifa ni kikubwa naomba nikupongeze kwa hilo,” alisema. Alisema kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala siasa za uchochezi, hivyo atahakikisha kuwa wananchi hawateseki na wale ambao wameiba fedha za Serikali wanazirudisha bila kujali nyadhifa walizonazo ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo. Rais Magufuli aliwaahidi wananchi wa Nguruka kuwa atahakikisha anatatua kero ya maji na umeme katika kata yao, wakati katika suala la umeme atamtuma Waziri wa Nishati na Madini ili aweze kutatua tatizo hilo na kuwasaidia. Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Nguruka uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 2, ambao unatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu. Kafulila Akizungumza na MTANZANIA jana, Kafulila ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia (NCCR- Mageuzi), alimshukuru Rais Magufuli kwa kutambua kazi aliyokuwa akiifanya na sasa imeanza kuleta matokeo mazuri. “Kwa kweli nafarijika na inanipa moyo wa kizalendo zaidi ninapoona Rais anaunga mkono sakata la Escrow ambalo mimi ndo nililiibua wakati nikiwa mbunge japo nilipitia kwenye kipindi kigumu. “Nimefarijika sana mkuu wa nchi kuguswa na kutambua mchango wangu  katika vita hatari ya ufisadi wa IPTL / ESCROW, natambua kwenye vita hii hakuna chama. “Niliteseka sana ndani na nje ya jimbo kutokana na vita hii, zilifanyika kila hila na njama lakini Namshukuru Mungu kuwa upande wangu hata nimebaki hai,’’alieleza Kafulila. Aliendelea kueleza.  “Ukweli nimefarijika sana kuona mkuu wa nchi amelizungumzia jambo hili jimboni kwa wananchi walionipenda sana amezungumzia kwa hisia na uzito wa kutosha binafsi kwenye vita ya ufisadi nchini ninamuunga mkono Rais ,”alieleza Kafulila. Kafulila alimshauri Rais ajenge mfumo wa taasisi imara za uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka katika eneo hilo ili kuhakikisha vita hiyo inakuwa ya mafanikio makubwa. Msuguano   Kafulila alipoibua sakata hilo alipata upinzani mkubwa  ndani na nje ya Bunge, ambapo kulikuwa na mvutano mkali kati yake na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, wanasiasa na watendaji wengine wa Serikali waliohusishwa na sakata hilo.   Wakati Bunge likiwa linaendelea mwaka 2014 katika hali isiyokuwa ya kawaida  kuliibuka na mvutano mkali baada ya Kafulila kuomba mwongozo juu ya ESCROW na wizi uliofanyika. Werema wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipotakiwa kutoa maelezo, kwanza alianza kushambulia vielelezo vya Kafulila kuwa ni vipeperushi visivyokuwa na maana hali hiyo ilipelekea Mbunge wa Ubungo wakati huo, John Mnyika (Chadema) kudai kuhusu utaratibu lakini mwenyekiti  wakati huo Mussa Zungu alipotezea. AG aliendelea  kumtaka Kafulila wakutane nje kama anamambo mengine ila bungeni kunautaratibu wake (walikuwa wakimwingilia wakati anazungumza wakionesha kutokubaliana naye). Majibishano yalipozidi Werema alipandwa na hasira alisema. “Kafulila wewe ni sawa na tumbili asiyeweza kuamua mambo ya msituni,” alisema na baadae Kafulila aliposimama naye alimwita Werema mwizi.   Kutokana na mvutano huo Werema alionesha dalili za kutaka kumfuata Kafulila akampige, lakini baadhi ya mawaziri walimzuia na kumsihi atulize hasira. Baada ya Bunge kuahirishwa wakiwa nje Jaji Werema alilalamika hadharani kuhusu Kafulila kumwita mwizi ndani ya Bunge na ndipo jaji huyo alipotaka kumvamia tena Kafulila. “Mimi nakwambia Kafulila nitakukata kichwa, we subiri tu labda ukiniomba msamaha” alisema Werema kwa sauti ya hasira. Kutokana na maneno hayo Kafulila naye alijibu. “Huwezi kunikata kichwa, huwezi, yaani uniue, hapana huwezi tena nakwambia huwezi,” alisema Kafulila. Ampongeza Sakaya Wakati huo huo akiwa mkoani Tabora, Rais Dk. Magufuli amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF), kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo licha ya kuwa anatoka chama cha upinzani. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana wilayani Kaliua mkoani Tabora alipokua akizindua barabara ya Kaliua-Kazilabwa yenye urefu wa kilomita 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Chico ya China. Dk. Magufuli alisema kuwa ni heri kuwa na mbunge wa upinzani anayetekeleza mambo ya Chama Cha Mapinduzi  kuliko kuwa na mbunge wa CCM anayetekeleza ya upinzani kwani huo ni usaliti mkubwa kwa chama. “Nasema haya kwa sababu nafahamu hata wakati wa kampeni niliyashudia haya, ndiyo maana nasema ni bora kuwa na mbunge wa CUF, Chadema anayetekeleza mambo ya CCM kuliko wa CCM anayetekeleza mambo ya vyama vingine. “Najua mwili wake wote na akili yake yote ni CUF lakini damu yake ni CCM” alisema Dk. Magufuli. Akizunguzia ujenzi wa barabara hiyo Dk. Magufuli alisema imejengwa kwa fedha za Serikali bila mfadhili kuchangia, ambapo aliwataka wananchi kutozidisha uzito wa mizigo na kuchimba mchangan kado ya barabara ili idumu kwa muda mrefu. Aliutaka Wakala wa Barabara (Tanroads) kubomoa nyumba zote zitakazojengwa katika hifadhi ya barabara bila kutoa taarifa. “Kuna zoezi litaanza hivi karibuni la kubomoa nyumba ziliopo kando ya reli, hakikisheni zote zinaondoka, tunaaza kujenga reli ya kisasa lazima nyumba zote ziondoke kupisha ujenzi, najua wapo viongozi wengine wa CCM wanapitishapitisha maneno wa kubomoa anzeni na za hao wa CCM” alisema Dk, Magufuli. Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 56 umegharimu zaidi ya sh bilioni 61.9 ambazo ni pamoja na gharama za ujenzi, usimamizi na fidia kwa wananchi waliopisha utekelezaji wa mradi huo. Wakati huo huo Dk. Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Kaliua hadi Urambo yenye urefu wa kilomita 28 kwa kiwango cha lami ndani ya mwezi mmoja kutoka sasa. “Tafuteni mkandarasi kama hamjampata ndani ya mwezi mmoja apatikane msaini mkataba, pesa zipo hata mkitaka kesho njooni mchukue” alisema. Akizungumzia kero zinazowakabili wakulima wa tumbaku Dk. Magufuli alisema suala hilo amemwachia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alishughulikie na kisha kumpelekea taarifa. Alizitaka mamlaka husika kutotumia nguvu kubwa kuwaondoa waliovamia misitu badala yake wawaeleweshwe ili watafahamu madhara ya uharibifu wa mazingira. Kuhusu suala la mimba shuleni, Rais Magufuli aliwataka wanaume wanaowapatia wanafunzi ujauzito kujiandaa kwenda jela miaka 30 ili wakatumie nguvu zao kuzalisha wakiwa gerezani. Habari hii imeandaliwa na Editha Karlo, Kigoma, Leonard Mang’oha na Asha Bani, Dar Mwisho
KITAIFA
Chanzo cha picha, Getty Images Kuanzia hali ya joto na ukungu wa akili hadi maumivu ya viungo na kukosa usingizi. Kuna dalili nyingi zinazoambatana na ukoma wa hedhi na kipindi cha mpito hadi hatua hii ya maisha ya uzazi ya mwanamke. Lakini kwa wanawake ambao wanakabiliwa na baadhi ya dalili hizi na wanaona kuwa inasababisha kuzorota kwa ubora wa maisha yao, kuna chaguo la tiba ya uingizwaji wa homoni (pia inaitwa tiba ya homoni au tiba ya uingizwaji wa homoni). Ikiwa unazingatia mbadala huu, hapa kuna mwongozo wa baadhi ya maswali ya msingi ili kukusaidia kuelewa ni mambo gani ya kuzingatia. Wakati hedhi inapokaribia kukoma, viwango vya estrojeni hubadilika-badilika na kupungua kwa baadhi ya wanawake. Estrojeni zina kazi nyingi: husaidia kudhibiti mzunguko wa hedhi, huchangia kutengeneza mifupa yenye nguvu na huathiri joto la ngozi. Chanzo cha picha, Getty Images Viwango vya estrojeni vinapoyumba, dalili mbalimbali kama vile mwili kupata joto kali, kutokwa na jasho usiku, wasiwasi, na maumivu ya viungo vinaweza kutokea. Tiba ya homoni huongeza viwango vya estrojeni katika mwili wa mwanamke na inaweza kusaidia kupunguza dalili hizi. Wanawake wanaofanya tiba hii kwa kawaida haiwachukui milele, ili tu kupunguza dalili hizo katika kipindi cha mpito wa kukoma hedhi na wengi wanasema imefanya tofauti kubwa kwa ustawi wao. Tiba ya uingizwaji wa homoni pia inaweza kuwa na faida zingine, kama vile kuzuia udhaifu wa mfupa na kuvunjika. Kwa wanawake walio chini ya miaka 60, inaweza pia kutoa ulinzi fulani dhidi ya ugonjwa wa moyo. Huenda umesikia kuhusu manufaa mengine yanayoweza kutokea, kama vile kulinda afya ya ubongo na kuboresha ngozi na nywele, lakini hadi sasa ushahidi wa faida hizo ni mdogo. Matibabu huja katika maumbo na ukubwa tofautitofauti, kuanzia vidonge na hadi jeli na pete. Kiambatanisho kikuu ni estrojeni, lakini moja ya aina za kawaida ni tiba ya mchanganyiko, ambayo estrojeni hutolewa pamoja na toleo la synthetic la progesterone ya homoni. Kuongeza progesterone husaidia kulinda ukuta wa tumbo la uzazi, kwani estrojeni pekee inaweza wakati mwingine kuongeza hatari ya saratani ya mfuko wa uzazi. Aina bora ya tiba hutofautiana kati ya mtu na mtu na inategemea dalili na mtindo wa maisha. Kwa ujumla, anza na kipimo cha chini kabisa. Tiba nyingi za homoni huathiri mwili mzima. Lakini baadhi kama Gina 10, inapatikana kwenye maduka ya dawa nchini Uingereza hutumiwa katika uke tu, ili kupunguza dalili katika sehemu hiyo ya mwili. Chanzo cha picha, Getty Images Hii inapunguza kiwango cha estrojeni kufyonzwa na sehemu nyingine za mwili, lakini inamaanisha kuwa matibabu haya hayaondoi dalili zingine kama vile mwili kuwaka moto. Inaweza kuchukua hadi miezi mitatu kabla yakuhisi athari kamili na kipimo na aina ya tiba ya homoni inaweza kuhitaji kurekebishwa au kubadilishwa. Wataalamu wengi wanapendekeza kuanza tiba ya uingizwaji wa homoni kwa dalili ya kwanza za kukoma hedhi. Ushahidi ni mdogo linapokuja suala la kuanza baada ya miaka 60, ingawa baadhi ya wanawake hupata nafuu kutokana na dalili zinazoendelea. Hakuna kikomo kwa muda wa kuitumia. Baadhi wanaunga mkono wazo la kuendelea na matibabu kwa miaka mingi, lakini Wakala wa Udhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya wa Uingereza unapendekeza itumike kwa kipimo cha chini kabisa na kwa muda mfupi iwezekanavyo. Ingawa tiba hii imekuwa na habari vibaya hapo awali, faida zake zinadhaniwa kuzidi hatari zake. Tafiti mbili zilizochapishwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 zilisema kuwa na madhara zaidi kuliko faida. Hii ilipata matangazo mkubwa na matumizi yake yalipunguzwa. Chanzo cha picha, Getty Images Wengine huendelea kuwa waangalifu, licha ya uthibitisho unaoongezeka kwamba matibabu yanaweza kusaidia. Aina fulani za matibabu yamehusishwa na hatari iliyoongezeka kidogo ya saratani. Mchanganyiko, kwa mfano, unaweza kuhusishwa na hatari ndogo ya kuongezeka kwa saratani ya matiti. Kuna hatari ndogo ya kuganda kwa damu wakati wa kutumia dawa hii. Walakini, pia inategemea mambo mengine, kama vile sigara, uzito na umri. Hatari ni ndogo ikiwa unatumia vipande vya kwenye ngozi au jeli badala ya vidonge. Hatari ya kuganda kwa damu ni ndogo sana kuliko ile ya kuchukua vidonge vya kudhibiti uzazi au kupata mimba. Madhara mengi yanaonekana ndani ya miezi mitatu baada ya kuanza matibabu. - Matiti kuuma - maumivu ya kichwa - kichefuchefu - Ugumu wa kusaga chakula - maumivu ya tumbo - kutokwa na damu ukeni Ni kawaida kuongezeka uzito unapokaribia kukoma hedhi, lakini hakuna ushahidi kwamba tiba ya homoni ndiyo sababu. Inaweza kuwa haifai katika kesi hizi: - Ikiwa umekuwa na saratani ya matiti, saratani ya mfuko wa uzazi - Shinikizo la damu lisilotibiwa - Ugonjwa wa ini - Au wewe ni mjamzito Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kukusaidia kulala vizuri, kupunguza mwili kuwaka moto na kuboresha hisia zako. Kula lishe bora, kupunguza unywaji wa kahawa, pombe, vyakula vyenye viungo, na kuacha kuvuta sigara kunaweza pia kusaidia kupunguza joto. Chanzo cha picha, Getty Images Mazoezi ya viungo, kupanda mlima, kutembea haraka haraka au kucheza tenisi pia huchangia kuimarisha mifupa. Dawa zingine kama Tibolone, ambayo hufanya kazi kwa kuiga shughuli ya estrojeni na progesterone, au dawamfadhaiko fulani zinaweza kusaidia. Lakini pia zinaweza kuwa na madhara. Huenda umesikia kuhusu homoni zinazofanana kibiolojia. Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza, kwa mfano, haipendekezi kwa sababu hazijadhibitiwa na usalama wake hauko wazi.
AFYA
Na MWANDISHI WETU SHANGWE za tamasha la Tigo Fiesta zitakuwa zikirindima Tabora leo kwa wakazi wake kupata burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali watakaopanda jukwaani. Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wamejipanga kutoa burudani ya uhakika katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, ili kuwaridhisha mashabiki wao ambao wana kiu ya kuwaona wakiimba nyimbo kwa kuwashuhudia tofauti na kuwasikiliza redioni au kuwashuhudia kwenye runinga. Wasanii ambao wako mkoani hapa tayari kwa ajili ya kuwapa mashabiki wao burudani katika tamasha hilo la Tigo Fiesta ni pamoja na Chege, Ney wa Mitego, Nandy, Maua Sama, Darassa, Rostam, Mr Blue, Young Dee, Aslay, Jux, Msami na Ben Pol. Wasanii Roma Mkatoliki na Stamina wamekuwa wakiwapagawisha mashabiki wa tamasha hilo kutokana na kuwateka kihisia kupitia wimbo wao wa pamoja uitwao ‘Hivi ama vile’. Pia Chege atakuwa kivutio katika Tigo Fiesta na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya watakuwa na shauku ya kutaka kumshuhudia akiimba nyimbo zake mbalimbali, ikiwamo ile mpya ya ‘Runtown’ sambamba na ule wa ‘Kelele za Chura’ aliyomshirikisha mwanadada Nandy, ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaokuwapo katika tamasha hilo. Kwa upande wa Ney wa Mitego, anatarajiwa kuwapagawisha wakazi wa Tabora akiwa na wimbo wake wa ‘Wapo’ na nyinginezo. Nandy, ambaye ameonekana kuliteka jukwaa katika Tigo Fiesta tangu ilipozinduliwa jijini Arusha, naye anasubiriwa kwa hamu kutoa burudani akiwa na wimbo wake wa ‘Wasikudanganye’, Nagusagusa na nyinginezo. Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe, alisema mwaka huu wameamua kudhamini Fiesta ili kusaidia vipaji vya wasanii na kuwaletea wateja wao burudani pamoja na kuwapatia vifurushi wanaponunua tiketi za Tigo Fiesta kwa Tigopesa. Kauli mbiu ya Tigo Fiesta mwaka huu ni ‘Tumekusoma’ na kwamba baada ya wasanii hao kuuwasha moto Tabora, burudani hiyo itaendelea katika mikoa Dodoma, Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na kuhitimishwa jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta, Sebastian Maganga, alisema kuwa, Tigo Fiesta ni burudani ya kipekee ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba mashabiki wamefurahia burudani Arusha na wataendelea kufurahia zaidi katika mikoa mingine. “Tutawaletea wasanii wenye hadhi kulingana na mapendekezo ya mashabiki husika wa mkoa huo, tena wale waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi,” alisema.  
BURUDANI
Na NORA DAMIAN-RUFIJI WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemsimamisha kazi Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Rufiji, John Hangi kutokana na utovu wa nidhamu. Hatua hiyo inafuatia baada ya Lukuvi kufanya ziara jana katika baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo lakini ofisa huyo hakuwepo huku waziri huyo akidai amekuwa akimkwepa mara kwa mara. Akizungumza kwa nyakati tofauti jana katika Wilaya za Rufiji na Kibiti, aliwataka watendaji wa ardhi kufanya kazi kwa weledi ku- tatua kero za wananchi. “Hangi asikanyage ofisi ya Rufiji, hii ni mara ya tatu ananikwepa, nitashangaa sana kanali (Mkuu wa Wilaya ya Rufiji) kama huyu mtu asiyekuwa na adabu anakaa ofisini. “Na kama kuna mtu mwingine ambaye anampenda sana ampeleke huko anakotaka,” alisema Lukuvi. Mkuu wa Wilaya hiyo Luteni Kanali Patrick Sawala, alimu- hakikishia Waziri Lukuvi kuwa atatekeleza maagizo hayo. “Hangi kuanzia sasa hivi asikanyage ofisini, kama kuna mtu wake amfikishie salamu, nikimkuta huko lake langu, hayo ni maelekezo,” alisema Luteni Kanali Sawala. MGOGORO WA NGULAKULA, MIWAGA Akiwa katika Kijiji cha Ngulakula, Lukuvi aliagiza ekari 23,000 ambazo mwekezaji hajaziendeleza zirudishwe kwa wananchi. Kumbukumbu zinaonyesha mwekezaji alimilikishwa na kijiji hicho ekari 29,168 na kati ya hizo zilizoendelezwa ni 6,000 tu. Waziri huyo pia aliagiza kufanyika kwa uchunguzi na iwapo wananchi hao hawakulipwa fidia kwa wakati waongezewe malipo kwa asilimia saba. “Watu wote waliochukua ardhi halafu hawaiendelezi irudi mikononi mwa wananchi. Shughulikeni na ekari alizolipia fidia na zile ambazo hazijafidiwa kuanzia sasa ziko chini ya serikali ya kijiji. “Unawekezaje ekari zote hata kodi ulipi, kwani ulizaliwa nayo, si umeikututa tulikutunzia sasa lazima ulipe kodi ya ardhi, usifikiri kulipa fidia peke yake ndiyo unahalalisha kukaa na ardhi…sitaki kumpa maumivu mara mbili lakini leo ningeweza hata kunyang’anya hizo 6,000,” alisema Lukuvi. Awali mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho, Abdallah Kirungi, alisema kabla ya kumpatia mwekezaji ardhi hiyo walimweleza changamoto lakini kilichotekelezwa ni ujenzi wa nyumba ya mwal- imu na ununuzi wa trekta. “Visima vimechimbwa hakuna maji na msikiti haujajengwa,” alisema Kirungi. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, alisema hadi kufikia mwaka 2017 mwekezaji alikuwa amelipa fidia ya Sh milioni 515.8 na kati ya hizo Sh milioni 354 ni kwa Kijiji cha Ngulakula na Sh milioni 161 Kijiji cha Miwaga huku wakiendelea kudai Sh bilioni 1.9. Naye Mwekezaji Shiraz Jaffary wa Kampuni ya Carbon Planning, alijitetea kuwa changamoto za miundombinu ya barabara na maji ndizo zimechangia kushindwa kuendeleza eneo lote. MGOGORO WA MCHUKWI B, MKUPUKA Akiwa katika Vijiji vya Mkupuka na Mchukwi B vyenye changamoto ya mipaka, alisema ataunda timu maalumu kutoka wizarani kuhakiki mipaka na kuchunguza fidia zilizolipwa kwa wananchi. Pia alimuagiza mwekezaji kusimamisha shughuli zake hadi uchunguzi huo utakapokamilika. “Kuna changamoto ya mpaka kati ya Mchukwi B na Mkupuka kwa sababu maeneo yanayotakiwa kuendelezwa Mchukwi B wananchi wa Mkupuka wanaamini ni yao,” alisema Lukuvi. Mwakilishi wa Mwekezaji Daud Brothers & Family, Ibrahim Manzool, alisema waliomba ekari zaidi ya 1,531 katika Kijiji cha Mkupuka na hadi sasa wameshalipa fidia ya Sh milioni 143. Hata hivyo alisema walipoanza kusafisha ekari 500 waliambiwa baadhi ya maeneo ni ya Mchukwi B hatua iliyosababisha kuwapo kwa mgogoro.
KITAIFA
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM KIKOSI cha timu ya soka ya Azam FC leo kitakuwa katika kibarua kigumu ugenini kitakapovaana na wenyeji wao, maafande wa Tanzania Prisons, katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ni wa kiporo, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, kutokana na historia ya timu hizo kila zinapokutana. Mara nyingi Prisons imekuwa ikiutumia vyema uwanja wake wa nyumbani, ambao katika msimu huu iliweza kuichapa Simba bao 1-0 na baadaye kulazimisha sare ya mabao 2-2 na Yanga. Rekodi ya timu hizo inaonyesha kuwa zimekutana mara 11 katika mechi mbalimbali za ligi, ambapo wametoka sare mara tano, huku kila timu ikifanikiwa kushinda michezo mitatu. Azam hawajafanikiwa kushinda mechi hata moja wakicheza Uwanja wa Sokoine, kutokana na kufungwa mara mbili na kupata sare tatu, jambo linalowafanya wauchukulie kwa uzito wa hali ya juu mchezo huo ambao utawawezesha kurudi kileleni. Jumla ya mabao 20 yamefungwa na timu hizo katika mechi zote 11 walizokutana na kila timu imefunga mabao 10, jambo linaloweza kuongeza ushindani kwa kila mmoja kutaka kumzidi mwenzake. Lakini Azam, waliopania kuwashusha wapinzani wao Yanga kileleni, wataingia uwanjani kwa kujiamini zaidi kutokana na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-2 waliopata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Prisons, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex. Katika mchezo uliopita, Azam ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja huo, hali inayoweza kuwaongezea morali ya kutaka kuendeleza wimbi la ushindi na kurejea kileleni. Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stewart Hall, alisema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha Prisons, ambacho msimu huu kiwamezidi maarifa Mbeya City. Alisema wana nafasi ya kupata ushindi kama wachezaji watacheza vizuri, huku akidai wataingia uwanjani kucheza kwa nguvu zote na kujitahidi kumiliki mpira kwa muda wote ili kuwanyima nafasi Prisons. Kocha huyo raia wa Uingereza alidai kuwa amebaini kuwa wapinzani wake wanatumia nguvu sana, ikiwemo kubebwa na maumbile ya wachezaji wake ambayo ni makubwa na warefu.
MICHEZO
Na JUDITH MHINA – MAELEZO HIVI karibuni Sekretarieti ya Ajira kupitia kwa Ofisa Mawasiliano na Msemaji wake, Riziki Abraham, alipokutana na waandishi wa habari, alisema Serikali imetoa ajira 52,000, lakini waombaji wengi wa ajira walishindwa kuitwa kwenye usaili baada ya kushindwa kukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mchakato wa kuomba ajira husika. Wakati umefika sasa wa kukubali kuwa changamoto hii ipo, ni kubwa na inahitaji mkakati wa dhati ili kuweza kuinua uelewa na ufahamu wa jinsi ya kuwawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nje na ndani ya nchi kuweza kuomba ajira. Watanzania tuichukue changamoto hii kuwa fursa kwa vyuo vyetu mbalimbali kuona uwezekano wa kuweka japo kwa muda mfupi kutoa mafunzo ya kuomba ajira, unatakiwa kufanya nini unapoomba ajira na kwa kiasi gani unatakiwa kuwa makini katika kufuata masharti yaliyowekwa katika kuomba ajira husika. Hii ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kuandika wasifu wake binafsi kama kielelezo cha kuthibitisha yeye ni nani na amepitia katika shule na vyuo gani mpaka hapo alipo. Aidha, ana uzoefu wa taaluma gani kutokana na shule na vyuo alivyosoma, ikiwamo kufanya kazi za majaribio katika maeneo mbalimbali wakati akiwa mwanafunzi au mwanachuo. Vilevile, shule zetu za sekondari na za msingi ni muhimu kuanza mazoezi ya kuandika barua ya maombi ya kazi tangu elimu ya awali, ili unapofika elimu ya juu kama Vyuo inamrahisishia Mhadhiri kuwapitisha kama kuwakumbusha umuhimu wa kuandika barua ya maombi ya kazi kwa makini. Ukilinganisha nafasi zilizotolewa na serikali 52,000 walioomba 56,815, walioitwa kwenye usaili, 29,674 na kuacha nafasi 22,326 ambao nao walitakiwa waitwe kwenye usaili kushindikana. Aidha, sababu za msingi zilizotolewa na Sekretarieti ya Tume ya ajira za kutochaguliwa kwa wanavyuo hao ni kutofuata masharti yaliyowekwa kwenye taratibu za kuomba ajira. Riziki amesema jumla ya maombi yaliyopokelewa kupitia njia ya uwasilishaji wa kielektroniki ni 56,815 na baada ya kufanyiwa kazi waliokidhi vigezo kwa mujibu wa sifa zilizokuwa zimeainishwa kwenye matangazo ya ajira husika, waombaji 29,674 waliitwa kwa ajili ya usaili. Sababu nyingine zilizoainishwa ni baadhi ya waombaji ajira kutofahamu namna ya kuandika barua ya maombi ya kazi, kutothibitisha nyaraka zao, hususan kwa wale waliosoma nje ya nchi, kutozingatia masharti kwa ujumla, ikiwepo kuwasilisha nyaraka pungufu, kudanganya kutoa wasifu usio wa kweli. Hata hivyo, baadhi ya waombaji wamewasilisha picha katika mfumo tofauti na bila kujali mandhari na mavazi waliyovaa, kupakia vyeti visivyohitajika katika maombi kama vile transcript, result slip na kuandika wadhamini wachache ambao si wahusika. Riziki amesema: “Mpaka sasa Sekretarieti ya Ajira imepata vibali vya kazi 239, kati ya hivyo baadhi vimefanyiwa mchakato, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Chuo cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)”. Vijana tuchangamkie ajira zinazotolewa, kwa kuwa kumekuwa na tabia ya kulaumu serikali kuwa haitoi ajira, lakini tuzingatie masharti yote pamoja na vigezo vilivyoainishwa ili tuweze kupata fursa hizo.
KITAIFA
NA HUSSEIN OMAR, DAR ES SALAAM KOCHA msaidizi wa Simba Mganda,  Jackson Mayanja, amesema anakabiliwa na shughuli nzito kuhakikisha anaipatia timu hiyo mafanikio katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Mayanja aliyekabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi hicho wiki iliyopita baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Dylan Kerr, juzi aliiongoza Simba kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza na MTANZANIA juzi, Mayanja alikiri kuwa amekuta mapungufu makubwa kwenye kikosi hicho ambacho kinawania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Alisema wachezaji wengi waliosajiliwa kuichezea Simba wamejaliwa vipaji vya soka tofauti na timu nyingine za Ligi Kuu, lakini hawana uwezo wa kuzimudu dakika tisini za mchezo kutokana na kukosa stamina. Alisema wachezaji wake wana uwezo wa kucheza dakika 45 za kipindi cha kwanza, lakini wanaporudi uwanjani wanachoka haraka na kuwapa wapinzani nafasi za kutengeneza mashambulizi. “Tumeshinda lakini siwezi kusema kwamba ndio tumemaliza ligi au timu imepata mkombozi kwani bado tuna kazi kubwa mbele ya kufanya kiufundi hasa tatizo la pumzi,” alisema. Mayanja aliyetimka Coastal Union na kutua Simba, alisema kwa kipindi hiki ambacho amepewa majukumu ya timu hiyo atahakikisha anatumia uwezo wake na kupambana kwa kila hali ili kupata ushindi. “Ni vigumu kusema nianze kuwapa wachezaji mazoezi ya stamina wakati ligi inaendelea na tayari imeshika kasi,” alisema. Kwa matokeo ya juzi, Simba imeendelea kubaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imefikisha pointi 30 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 36 sawa na Azam waliopo nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
MICHEZO
Na WAANDISHI WETU-SINGIDA/DAR CHAMA Cha Mapinduzi  (CCM), Mkoa wa Singida, kimepiga kambi katika Jimbo la Singida Kaskazini, ambalo lilikuwa linaongozwa na Lazaro Nyalandu. Nyalandu alitangaza kujiuzulu uanachama wa CCM, hivyo kupoteza ubunge wake Oktoba 30, mwaka huu, kwa kile alichodai chama hicho kimepoteza mwelekeo. Jana viongozi wa CCM Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mwenyekiti Martha Mlata, walilazimika kuitisha Mkutano Mkuu Maalumu wa jimbo ili kueleza kilichojiri baada ya kujiuzulu kwa Nyalandu. Viongozi wengine walioambatana na Mlata, ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Elias Tarimo, Katibu wa CCM wa Mkoa, Jamsom Mhagama na Mbunge wa Viti Maalumu, Aysha-Rose Matembe. Akizungumza katika mkutano huo, Mlata alianza kwa kumshambulia Nyalandu kutokana na uamuzi wake wa kujiuzulu na kusema kiongozi huyo si mwaminifu kwa chama na wapigakura wa jimbo hilo. Katika mkutano huo uliofanyika Kijiji cha Ilongero, uliotanguliwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya jimbo, wana CCM wengi waliokusanyika walionekana wamepigwa butwaa kutokana na mbunge wao kujiuzulu na kukihama chama chao. Mlata alisema Nyalandu alianza kuwa shida tangu alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, aliposhindwa kufanya kazi za ubunge jimboni kwake. “Kwahiyo akawa mzigo jimboni kutokana na kutofika na akifika, anasimama jukwaani dakika mbili halafu anashuka huku kukiwa hakuna cha maana alichokiongea. Na hata alipokuwa jimboni, hakuweza kuwatetea wananchi wake na hatimaye akawa bubu kabisa,” alisema. Mlata alidai kuwa katika kipindi chote cha ubunge, Nyalandu hakuwahi kushinda kwa kupigiwa kura na wananchi zaidi ya kuhonga wapigakura na shughuli zote za ubunge zilikuwa zikifanywa na wasaidizi wake watatu na yeye anafika jimboni ikiwa zimebakia siku saba za uchaguzi. Mwenyekiti huyo wa CCM alidai kuwa Nyalandu aligeuza jimbo hilo kuwa kitega uchumi chake na kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita aliwaaibisha wafadhili wake raia wa kizungu. “Wafadhili zaidi ya 20 walifika katika jimbo hili kuangalia wanafunzi ambao alikuwa akidai anawasomesha na kufika hapo hawakuona mwanafunzi hata mmoja,” alidai. Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Matembe, alisema katika uchaguzi mdogo unaokuja ni lazima wana CCM na wananchi kwa ujumla wawe makini kwa kuchagua mtu makini na mwenye dhamira ya kweli ya kuwatumikia. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida ambaye pia alikuwa ni mshauri wake wa karibu tangu anaanza kugombea mwaka 2000, Elia Diga, alisema kuwa hakuwa akifanya kazi ya kumwombea kura mbunge huyo pamoja na kusimamia majukumu yake. Katika mkutano huo, CCM ilimsimamisha pia aliyekuwa Meneja Kampeni wa Nyalandu, Khadija Kisuda, aliyesema kwamba mbunge huyo alikuwa na kazi ya kuwalaghai wananchi na si kufanya kazi waliyomtuma. “Nyalandu siku tatu kabla kutangaza kuachana na CCM, alikuwa jimboni kwenye ziara na alikuja na kundi la vijana ambao aliwaacha hotelini, mara baada ya kumaliza hakurudi tena kwa wale vijana, ghafla kesho yake ndio akatangaza kujiondoa CCM. “Hata hivyo, alipofika jimboni alifanya ziara ya kutembelea jimbo, shule na miradi mbalimbali ya jimboni humo, lakini hakuwa mtu wa furaha kwa kuwa alionekana kuwa na wasiwasi muda wote tofauti na ambavyo tumemzoea akiwa anafanya ziara zake. “Na akiwa katika mkutano wake wa hadhara, alitangaza kufanya mkutano mwingine mkubwa hapo baadaye kwa ajili ya kufanya tathmini, lakini ndio hakutokeza tena na wale vijana aliokuwa amekuja nao aliwaacha palepale hotelini,’’ alisema.   HALI YA WANACHAMA Wanachama wengi walionekana kupatwa na mshtuko kutokana na kueleza kuwa tukio hilo ni la kushtukiza kwa kuwa walizunguka naye katika kampeni ya kukagua jimbo. Mmoja wa wanachama hao alisema kuwa baada ya kukagua jimbo, Nyalandu alihudhuria mkutano wa dini uliokuwa ukiongozwa na Mchungaji Engon. “Hatuwezi kuamini kilichotokea kwa kuwa alifanya ziara yake kama kawaida na baada ya hapo akahudhuria mkutano wa Mchungaji Engon, lakini pia si yule Nyalandu ambaye tunamfamu siku zote, alikuwa ni kama mtu ambaye alipatwa na kitu kutokana na kuwa na hali ya wasiwasi mkubwa,’’ alisema.   NYALANDU ATOA BARUA Siku moja baada ya Ofisi ya Bunge kutoa taarifa kwa umma, kwamba Spika wa Bunge, Job Ndugai hajapokea barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, mwanasiasa huyo ameweka hadharani barua yake aliyomwandikia kiongozi huyo wa Bunge. Nyalandu ambaye alijivua uanachama wa CCM mapema wiki hii, aliweka hadharani barua hiyo jana, ambayo alimwandikia Spika siku aliyotangaza kujiuzulu Oktoba 30, mwaka huu. Katika barua yake hiyo kwa Spika, Nyalandu alisema: “Itakumbukwa kwamba nilichaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia bungeni nikiwa Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM tangu mwaka 2000 na kuchaguliwa mfululizo kuwakilisha wananchi wa jimbo hilo, kazi ambayo nimeifanya kwa mapenzi makubwa, dhamira thabiti na moyo wa ukunjufu. “Kwa barua hii, napenda kukujulisha kuwa kama nilivyotangaza muda mfupi uliopita kupitia mkutano wangu na wanahabari, nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge wa Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM kuanzia leo Oktoba 30, 2017. “Nachukua nafasi hii kukushukuru wewe pamoja na wabunge wenzangu wote wa CCM kwa muda wote ambao tumefanya kazi kwa pamoja kupitia kamati ya wabunge wote wa CCM. “Aidha nawashukuru maspika waliotangulia ambao nilipata fursa ya kuwa chini ya uongozi wao bungeni, kuanzia na Pius Msekwa, Samuel Sitta (Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) na Anne Makinda,” alisema.
KITAIFA
WAKATI Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri akikabidhi uniti 100 za damu salama kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam majeruhi mmoja amefariki usiku wa kuamkia leo Jumamosi.Hii ina maana kuwa waliofariki kutokana na ajali ya lori la mafuta ya petroli iliyotokea wiki iliyopita, Agosti 10, 2019, eneo la Msamvu mkoani Morogoro hadi kufikia leo Jumamosi Agosti 17, 2019 kufikia 94.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha akitoa tarifa jana alisema kwa sasa wamesalia majeruhi 20 kati ya 46 waliopokelewa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.Alisema majeruhi wote wapo chumba cha uangalizi maalum ( ICU) chini ya jopo la Madaktari wa Muhimbili na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutoka Lugalo, Dar es Salaam.Alisema mbali na vifo hivyo, majeruhi waliolazwa hospitali ya Morogoro wameongezeka kutoka 16 hadi 17 baada ya mmoja aliyekuwa ameruhusiwa nyumbani kurejea hospitali kutokana na kutojisikia vizuri.Naye Meneja wa Taifa wa Mpango wa Damu Salama, Dk Magdalena Lyimo alikabidi uniti 100, MNH kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri.Alisema uniti hizo 100 zimepatikana baada ya mkuu huyo wa Tabora kuhamasisha wananchi wake kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi wa Moto na wagonjwa wengine wenye huitaji.Alisema mpaka sasa kupitia MNH unit 611 za damu salama zimekusanywa toka zoezi hilo lilipoanza Jumamosi iliyopita Agosti 12. Alisema majeruhi wa moto wanatumia chupa 200 hadi 250 kwa siku na kuwataka Watanzania kuendelea kujitokeza kuchangia damu.
KITAIFA
MWANDISHI WETU-DODOMA MTAKWIMU Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa, amesema matumizi ya teknolojia za kisasa yataleta ufanisi mkubwa katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, hivyo kuipatia nchi takwimu za uhakika zaidi na kwa wakati kuliko sensa zilizopita. Hayo aliyasema jana alipotembelea wilayani Kondoa kukagua maendeleo na ubora wa kazi katika hatua ya awali ya utengaji wa maeneo Mtaa wa Mnarani, ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya sensa ya mwaka 2022. “Lengo letu ni kufanya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa ufanisi mkubwa na nimekuja hapa kukagua na kutathmini ubora wa kazi ya kutenga maeneo katika wilaya yenu,” alisema Dk. Chuwa. Wakati wa ukaguzi huo, Dk. Chuwa alionyeshwa namna maeneo hayo yanavyopimwa na kuwekewa mipaka pamoja na namna taarifa zinavyohifadhiwa katika kishikwambi (tablet) ambazo zitatumika wakati wa kuhesabu watu tofauti na sensa zilizopita ambazo wadadisi walikuwa wakitumia ramani zilizochorwa kwenye karatasi. Katika sensa ya mwaka 2012 kiwango cha watu waliosahaulika kuhesabiwa kilikuwa asilimia tano, ambacho hata hivyo ni cha chini ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika. “Tunataka kile kiwango cha asilimia tano cha waliosahauliwa kuhesabiwa mwaka 2012 kiondoke katika sensa ijayo ili tupate takwimu halisi na kuongeza ufanisi katika upangaji wa mipango yetu ya maendeleo,” alisema Dk. Chuwa. Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Taarifa za Kijiografia katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Benedict Mugambi, alisema kwa kutumia kishikwambi, mdadisi atafanya kazi yake ya kuhesabu watu katika eneo lake tu na hataweza kuingia eneo la mwenzake. “Mdadisi akitoka nje ya eneo lake, kishikwambwi kitamuonyesha alama kuwa anaingia eneo silo, lakini zaidi dodoso halitaweza kufunguka, hivyo hataweza kufanya kazi,” alieleza Mugambi. Awali, akitoa taarifa ya kazi, kiongozi wa timu hiyo, Mrasimu Ramani Jerve Gasto wa NBS, alieleza kuwa hadi sasa vijiji vyote 84 katika Halmashauri ya Kondoa Vijijini tayari vimetengewa maeneo ya kuhesabia watu na taarifa zote muhimu zimeshachukuliwa na kuweka katika ramani. Kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu wilayani Kondoa ilianza Septemba 16, mwaka huuna kushirikisha warasimu ramani kutoka NBS, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) na wataalamu wa mipango miji kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
KITAIFA
Mwandishi Wetu Imeelezwa kuwa si kila mtu anatakiwa kuvaa kifaa cha kuziba uso ‘mask’ (barakoa) ili kujikinga na homa inayosababishwa na virusi vya corona. Akitoa maelekezo kuhusu watu wanaotakiwa kuvaa mask, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa Mlipuko, Dk. Janeth Mghaba amesema kifaa hicho kinavaliwa si zaidi ya saa nne tu na mtu ambaye tayari ana maambukizi kusudi asimuambukize mwingine. Amesema hiyo ni kwa sababu siyo rahisi mtu akakohoa aidha kwa kutumia kiwiko au mkono atakuwa na maji maji na mara nyingi ataweza kumuambukiza mwenzie. “Kwa hiyo yule ambaye ni mgonjwa tu, tunasema kwamba ukijisikia dalili za kukohoa basi wewe vaa mask yako nenda kwenye kituo cha afya karibu au hospitali. “Mask pia zinaweza kuvaliwa kwenye sehemu za msongamano au sehemu zenye watu wengi lakini kwa sababu tayari serikali imeshapiga marufuku hii misongamano, hatutegemei kukuona wewe unavaa mask unapita sehemu ambako hakuna msongamano na wewe ni mzima huna maambukizi,” amesema. Aidha, Dk. Mghaba amebainisha kuwa kuna hatari kubwa ya kuvaa mask kwa sababu watu wengi bado hawajawahi kuuzingatia uvaaji wake. “Mask hizi zinatakiwa kuvaliwa kila baada ya saa nne na kuzibadilisha, usipokuwa na hii tabia ya kuzibadilisha ukakaa nayo siku nzima kwako wewe ni hatari, itakuletea maambukizi mengine zaidi. Kwa hiyo tunashauri matumizi haya ya uvaaji mask yawe yanatumika kwa usahihi,” amesema.  
KITAIFA
MKUTANO wa 13 wa Baraza la tisa la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza Jumatano ambapo jumla ya miswada miwili itasomwa kwa mara ya kwanza huku maswali na majibu 146 yakiulizwa na kujibiwa na mawaziri husika wa wizara.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Raya Issa Mselem alisema marekebisho ya sheria mbalimbali za mwaka 2018 na mambo mengine yanayohusiana na hayo yatajadiliwa.Aidha Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Wakala wa Serikali wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo pamoja na mambo mengine utasomwa. “Kwa mujibu wa ratiba yetu ya kikao cha wiki mbili cha Baraza la Wawakilishi tutakuwa na miswada miwili pamoja na maswali na majibu 146,” alisema.Aidha alisema ripoti za kamati za kudumu za Baraza la Wawakilishi kwa mwaka 2018-2019 zitawasilishwa na wenyeviti wa kamati hizo. Aidha katika kikao hicho mwelekeo wa Mpango wa Taifa wa Uchumi utawasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Mohamed.Katika kikao hicho kamati teule ya kuchunguza majengo ya shule 19 za sekondari zilizojengwa Unguja na Pemba itawasilisha ripoti yake mbele ya wajumbe. Wajumbe katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichopita waliibana serikali na kulitaka Baraza kuchunguza mradi wa ujenzi wa shule 19 zilizojengwa chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ambapo baadhi ya majengo inadaiwa yamejengwa chini ya kiwango.
KITAIFA
BENKI ya KCB imeendelea kuwa sehemu ya wadhamini wa Ligi Kuu Bara baada ya jana kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuidhamini ligi hiyo.Akizungumza wakati wa kutia saini Dar es Salaam jana, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB, Fatma Chiro alisema mkataba huo wa shilingi milioni 420 una lengo la kuimarisha Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya ule wa awali kwisha.Akifafanua zaidi kuhusu udhamini huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Cosmas Kimario alisema wameamua kuongeza mkataba mpya ili kuzisaidia klabu katika kukuza uchumi.Aidha, alisema benki yake inaangalia uwezekano wa kudhamini pia ligi daraja la kwanza, ligi ya wanawake na ligi ya Zanzibar.TFF imeendesha ligi ya wanawake kwa msimu wa pili sasa lakini imekuwa ikisuasua kutokana na kukosa udhamini.Akizungumza baada ya kutia saini, rais wa TFF, Wallace Karia alisema:“Tumekubaliana KCB waongeze mkataba baada ya ule wa awali kumalizika, benki hii ni mdhamini mzuri ambaye uongozi wa TFF umeridhia kufanya nao kazi tena,’’ alisema.
MICHEZO
Mwandishi Wetu, Mwanza Serikali imelifungia Kanisa la Mfalme Zumaridi linalomilikiwa na Dayana Bundala (Mfalme Zumaridi) lililopo eneo la Iseni jijini Mwanza kutokana na kuendesha huduma zake kinyume cha sheria. Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo, Dk. Philis Nyimbi amesema kanisa hilo linaendesha ibada kinyume na sheria na katiba ya nchi huku likidaiwa kutumia usajili wa kanisa jingine la Pentekoste Christian Church of Tanzania (PCCT) ambapo amemtaka msajili wa vyama vya kijamii kuchunguza kanisa hilo. “Kamati na wajumbe wake na vyombo mbalimbali vya dola imejiridhisha pasipo shaka kupitia njia mbalimbali kuona kwamba kanisa hili limekuwa likifanya kazi nje kabisa ya utaratibu kwa mantiki hiyo imeweza kuleta athari kwa watu wengine na Watanzania wengine hivyo tunasitisha shughuli zote zinazoendelea katika kanisa hili hapa. “Kwa maslahi serikali yetu, shughuli hizo zinasitishwa hapa kanisani lakini na mpaka  nyumbani tusione shughuli hizo zikiendelea. “Kiongozi wa kanisa hili mfalme Zumaridi yeye kwa jinsia ni mwanamke lakini sambamba na hilo amekuwa akijiita mfalme wakati yeye ni mfalme lakini pia na ameendelea kupotosha umma kujiita yeye ni Mungu wa dunia,” amesema.
KITAIFA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa mfano katika kuhifadhi, kutunza na kujenga nyumba bora za gharama nafuu kwa ajili ya kuziuza au kuzipangisha kwa wananchi wakiwemo watumishi wa umma.Amelitaka shirika la NHC kuwa mfano kwa taasisi nyingine zinazojishughulisha na ujenzi kwa kujenga nyumba bora na wakati huo kuwapangisha wananchi kwa malipo ya kodi ya mwezi mmoja badala ya utaratibu uliozoeleka wa kupangisha kwa malipo ya kipindi cha miezi sita au mwaka mzima.Lukuvi aliyasema hayo jana alipolitembelea NHC katika mkoa wa Kilimanjaro wakati wa mwisho wa ziara yake ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya za Hai, Moshi na Same mkoani Kilimanjaro.Alisema NHC lazima iwe na mkakati mzuri wa ukarabati nyumba zake na kubainisha kuwa haiwezekani shirika kubwa kama hilo kuwa na nyumba nyingi katika maeneo ya vitovu vya miji, huku nyingi ya nyumba hizo zikiwa zimechoka na kusisitiza kuwa hataki kusikia NHC inakuwa na nyumba za aina hiyo.Alilitaka shirika kujipanga vizuri na kuhakikisha linashirikiana vizuri na ofisi za mikoa na halmashauri kwa lengo la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi na wakati huo kutangaza shughuli zake kwa kuwa NHC ina kampuni yake ya ujenzi iliyosheheni wataalamu wa fani mbalimbali na kuwa na uwezo wa kujenga majengo mbalimbali kama vile shule, hospitali, vituo vya afya na vyuo.Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba alimueleza Lukuvi kuwa NHC katika mkoa huo iko kwenye mazungumzo na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 25 za gharama nafuu, mradi huo utagharimu jumla ya Sh bilioni 1.4 na utachukua miezi 18 mpaka kukamilika.
KITAIFA
Safina Sarwatt – Moshi HOSPITALI ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC), imesema iko kwenye mchakato wa hatua za kuanzisha maabara ya virusi vya korona ili kukabiliana na vizusi hivyo endapo itabainika kuwepo kwa mgonjwa wa korona.  Mkurugenzi wa Mtendaji wa KCMC na Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaria Mwema la Tanzania, Professa  Gilearrd Masenga aliyesema hayo jana, wakati wa ibada ya shukrani ya maadhimisho miaka 49 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo kuelekea miaka 50 . Professa Masenga, alisema hospitali tayari imetenga eneo maalumu kwa ajili kujenga maabara ya virusi vya korona.  Alisema hospitali imejipanga kwa vifaa tiba pamoja na watalaamu kwa ajili ya dharura, endapo itatokea mgonjwa mwenye virusi vya korona kwa kushirikiana timu ya mkoa.  “Tumejipanga kwa vifaa na watalaamu wetu wako tayari muda wote,tunashirikiana na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi  na timu iliyondwa na ofisi ya mkuu wa mkoa, nawaondoa hofu wananchi kwamba tupo vizuri, “alisema professa Masenga.  Alisemakutokana na mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa ambayo inapokea wageni wengi kutoka nje ya nchi kwa sababu za utalii wa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, umeimarisha huduma muda wote. Alisema  hospitali hiyo, ina madaktari na wauguzi wa ngazi mbalimbali, madaktari bingwa 76 ,madaktari wa kawaida 74 na madaktari wasaidizi wanne  na (Clinical officers) 6. Alisema kwa miaka 49, sasa kuelekea jubilee ya miaka 50 ,hospitali   imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika fani ya kitabibu kwa kanda nzima ya kaskazini pamoja na taifa.  “Mafanikio haya yanatokana na jitihada za uongozi na  watumishi vitengo mbalimbali ndani ya hospitali ambao wamekuwa uti wa mgongo katika hatua tunazopiga siku baada ya siku, “alisema.  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo aliipongeza hospitali hiyo kwa hatua kubwa waliyopiga katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi, ambapo aliwataka kuongeza juhudi zaidi  ili kuhakikisha kwamba wanaondoa changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza. 
KITAIFA
BADI MCHOMOLO NA MITANDAO MAVAZI ya mwanamuziki Rihanna na mwanamitindo, Kim Kardashian yamekuwa kivutio na kituko kwa mashabiki wao walipokuwa katika onyesho la Met Gala, huko nchini Marekani. Kim alikuwa karibu muda wote na mume wake mwanamuziki, Kanye West, huku Rihanna akiwa wa mwisho kuingia katika onyesho hilo akionekana mpweke aliyefunikwa vema na gauni lake lililoonekana kama limemkumbatia. Wawili hao walionekana katika onyesho la Met Gala, lililohudhuriwa na wasanii wa fani mbalimbali, lakini hata hivyo hawakujali namna watu walivyokuwa wakiwazungumzia. “Nimeamua kuacha simu yangu nyumbani kwa kuwa nilijua kwamba mashabiki watakuwa na maswali mengi juu ya vazi langu,’’ alisema Kim na kuongeza: “Nikiwa na shida ya kutumia simu nitatumia ya mume wangu, ninaamini kama ningekuja na simu yangu muda mwingi ningekuwa natumia kutokana na ujumbe kutoka kwa mashabiki.”
BURUDANI
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipozungumza kwenye hafla ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya kupima virusi vya Ukimwi kwa wasichana iliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya msingi Kakola wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Alisema wasanii wana nafasi kubwa kupitia shughuli zao za sanaa kuhamasisha na kuelimisha jamii kwa mambo ya msingi ya maendeleo ya nchi, likiwemo kuwahamasisha wasichana wajitokeze kupima afya zao.Alimtaka Msanii wa kizazi kipya Supa Nyota Diva 2014, Hellen George ‘Ruby’ ambaye alitumbuiza katika hafla kuwatafuta wasanii wachanga wa kike nchini kutunga wimbo huo.“Ruby hebu tukutane Dar es Salaam ili tuone ni namna gani tufanye ili wewe na wasanii wenzako wa kike mtunge wimbo maalum utakaotumika kwenye kampeni ya kuhamasisha wasichana kupima afya zao,”, alisema Ummy.“Unajua Ruby akionekana nawasanii wenzake wa kike wakiwa wanaimba kwa kuwahamasisha wasichana na kwasababu watakuwa ni wasanii wa kike wenye umri mdogo wanaolingana na wao watawahamasisha sana wajitokeze kupima afya zao,”alisema.Aidha aliwataka vijana wa kike na kiume nchini badala ya kutumia muda mwingi kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa kutuma ujumbe wa mapenzi, watumie ujumbe katika kuhamasishana kupima afya zao.Kwenye hafla hiyo Ruby ambaye alipanda jukwaani mara kadhaa alikuwa kivutio kikubwa kwa watu waliohudhuria kwenye kampeni hiyo maalumu ya kitaifa ya kuhamasisha wasichana kupima virusivya Ukimwi.
MICHEZO
Khamis Sharif -Kusini Unguja UONGOZI wa Shule ya Sekondari  Paje Wilaya ya Kusini Unguja, umemuhamisha shuleni hapo mwanafunzi wa kiume ambaye anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake. Akithibitisha uhamisho wa mwanafunzi huyo, mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Issa Abdallah Makame alisema kuwa uongozi huo umeridhia hatua hiyo kwa lengo baada ya kuona ukubwa wa tatizo hilo shuleni hapo. Alisema suala la wanafunzi kumpa ujauzito katika mazingira ya shule hiyo ni geni hivyo, uongozi umefanya uamuzi huo mgumu iki kutaka kuona matendo hayo hayajirejei tena kwa wanafunzi shuleni hapo. Alisema kuwa mwanafunzi huyo ambae jina lake limehifandhiwa anasoma kidato cha nne  na tayari ameshapewa taarifa za kutafuta skuli nyengine ili kuendelea na masomo yake mara shule  zitakapofunguliwa. Aidha mkuu huyo wa shule alisema kuwa mwanafunzi huyo anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake ambae anasoma kidato cha tatu shuleni hapo. “Tulichokifanya kwanza ni uchunguzi yakinifu na ndipo tukaamua kukutana na kukubaliana tumpe uhamisho na ulikuwa tumpunzishe moja kwa moja lakini kwa vile karibuni anafanya mtihani ni bora aende akamalizia katika skuli nyingine kwani kuendelea kubakia hapa kutawafanya na wengine kuiga na kuishi kwa woga. “Hii ni hukumu yetu kama shule tu, bila shaka kuna hukumu nyingine ya familia ya mtoto wa wa kike huko sijui itakuwa ipi kwani sio suala rahisi mzazi kufanyiwa mtoto wake kitendo kama hiki kisha wakamuangalia tu,” alisema Mwalimu Abdallah Alisema tukio hilo ni la kwanza kwa wanafunzi kupeana ujauzito lakini wameona ni bora kuchukua hatua haraka ili wengine wasireje. Akizungumzia hilo, Mratibu wa Wanawake wa Shehiya ya Paje, Asya Mussa Dai, alisema kuwa uamuzi waliochukuliwa na uongozi wa shule si mbaya kwani litakuwa fundisho kwa wengine.
KITAIFA
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam wameshauriwa kupunguza uzalishaji na matumizi ya vitu vinavyozalisha taka, zisizokuwa za msingi ili kuepuka kulipa faini na pia kuepusha uchafuzi wa mazingira.Mkuu wa Idara ya Udhibiti Taka na Hifadhi ya Mazingira ya Jiji hilo, Shedrack Maximilian amesema utafiti mdogo uliofanyika umeonesha kati ya asilimia 30 hadi 40 ya taka zinazozalishwa kwenye kaya za wakazi wa jiji, zisingestahili kuwepo.Alisema wananchi watambue kwamba jukumu la kukusanya na kudhibiti taka ni la jamii moja kwa moja kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kuanzia anayeuza kitu hadi wa mwisho anayekitumia.“Jukumu la ukusanyaji wa taka ni la wananchi. Na ni jukumu la wananchi kwa sababu wananchi ndio wanaozalisha taka. Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 ambayo ndio sheria mama imezungumzia vizuri kabisa suala la anayezalisha taka, lazima alipie gharama,” amesema Maximilian.Maximilian alisema baadhi ya vyakula vinavyopikwa kwenye kaya na bidhaa kununuliwa kwenye maduka na masoko, ambavyo havihitajiki kwa wakati husika hubaki na kutupwa hivyo kuwa uchafu.“Mabaki haya ya vitu yakitupwa ovyo yanakuwa uchafu ambao kama haumsumbui mtupaji unasababisha gharama kwa watu wengine au unaisumbua serikali. Ukitupa taka unakamatwa unalipa faini,” alisema.Alisema kwamba wananchi katika kaya zao, wajenge utamaduni wa kuhakikisha wanalipia taka wanazozalisha kama wanavyolipia vocha za simu, maji au umeme kwa sababu kuzalisha taka ni gharama.“Wasipolipia taka wanazozalisha wanafikiri zitatokaje pale walipoziweka zifike sehemu inayostahili. Taka isipotoka ilipotupwa ndio maana utakuta mwisho wa siku inaingia kwenye mtaro na kusababisha athari mbalimbali zikiwemo magonjwa kama dengue, kipindupindu, inachafua vyanzo vya maji,”alisisitiza Maximilian.Aidha, alisema wafanyabiashara wa aina zote, wana jukumu pia la kuhakikisha wanaweka vifaa vya kuhifadhi taka za bidhaa zinazonunuliwa kwenye maeneo yao.Maximilian amesema wakazi wengi wa jiji wanapokuwa kwenye mizunguko au shughuli mbalimbali hutumia bidhaa zinazozalisha taka hivyo ni jukumu lao kuhikikisha hawazitupi hovyo.“Lakini vile vile wanaonunua vitu nao wana jukumu la kuhakikisha taka wanazozalisha wanaziweka panapostahili. Ukinunua kitu kikazalisha taka umezalisha taka wewe. Una jukumu la kuhakikisha hiyo taka unaiweka sehemu inayostahili,” amesema.Alisema manispaa za mkoa wa Dar es Salaam, zimejitahidi kuweka vifaa vya kuweka taka sehemu mbalimbali ingawa bado zinaendelea kuweka kadri uwezo unavyopatikana.
KITAIFA
['Kocha wa Inter Milan Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, kutoka klabu yake ya zamani,Chelsea. (Express)', 'Manchester United ina nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Norway Erling Braut Haaland, 19, ambaye alifunzwa na Ole Gunnar Solskjaer akiwa Molde. (Dagbladet - in Norwegian)', 'United inatarajia kuafikiana na Juventus kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33, kufanya mazoezi na klabu hiyo mwezi ujao kabla ya uhamisho wa Januari. (Tuttosport - in Italian)', 'Mandzukic pia analengwa na klabu za ligi kuu ya soka. (Calciomercato)', 'Newcastle inataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Arsenal na Switzerland Granit Xhaka, 27, kwa mkopo mwezi Januari. (Telegraph)', 'AC Milan ina mpango wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uswiss ambaye kwa sasa hana klabu Zlatan Ibrahimovic, 38, mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa, lakini mpango huo unahitaji kuidhinishwa na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis. (Calciomercato)', 'Wakala wa beki wa Arsenal Mhispania Hector Bellerin anasema mteja wake, 24, haoni "jinsi msimu utakavyoenda"katika uwanja wa Emirates baada ya kupokea ombi la usajili kutoka Italia. (Sky Sport Italia via Football Italia)', 'Liverpool na Napoli ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Genk raia wa Norway Sander Berge, 21, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Dimitri de Conde. (Radio Punto Nuovo, via Goal)', 'Napoli huenda ikampoteza mchezaji wa kimataifa wa Albania Elseid Hysaj, 25, bila chochote mkataba wake utakapokapomalizika msimu ujao, lakini ingelipokea £43m kutoka kwa Chelsea msimu uliopita, anasema wakala wake Mario Giuffredi. (Radio Punto Nuovo via Mail)', 'Frank Lampard atajaribu tena kumjumuisha Shay Given katika kikosi cha wakufunzi wa Chelsea licha ya hofu kuhusu kipa huyo wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25. (Mail)', 'Meneja wa Aston Villa Dean Smith ameidhinisha kuuzwa kwa kipa wa Croatia Lovre Kalinic, 29, mwezi Januari. (Football Insider)', 'Mashabiki 114 wa Manchester City waliosafiri kwenda Kharkiv kushangilia mechi ya Champions League kati ya klabu hiyo na Shakhtar Donetsk msimu huu wametambuliwa rasmi kwa barua ya kibinafsi kutoka kwa Pep Guardiola. (Manchester Evening News)', 'Manchester United inatarajia kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, atarejea uwanjani kushiriki mechi ya Manchester City Disemba 7. (Sun)', "Mshambuliaji mwingine wa zamani wa Chelsea striker, Didier Drogba, 41, anasema alipewa nafasi ''nzuri'' ya ukufunzi katika klabu hiyo lakini alikataa kurejea Stamford Bridge ilikufuatilia azma yake ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka la Ivory Coast FA. (Metro)"]
MICHEZO
Hayo yalisemwa na Waziri wa Biashara, Masoko na Viwanda, Nassor Ahmed Mazrui wakati alipofunga tamasha la biashara hapo katika viwanja vya Maisara mjini hapa.Alisema tamasha hilo linalofanyika katika kipindi cha tatu sasa limekuwa likipata mafanikio siku hadi siku kwa wafanyabiashara kuonesha bidhaa zao wakiwemo wajasiriamali akinamama.Mazrui alisema hiyo ni moja ya fursa nzuri ya kipekee kwa wafanyabiashara kubadilisha mawazo na kuonesha bidhaa zao kwa ajili ya kupanua masoko ya biashara.“Tamasha la maonesho ya biashara ni fursa nzuri kwa wafanyabiashara kuonesha bidhaa zao mbalimbali ambazo watazitumia kwa ajili ya kutafuta soko na wenzao,” alisema.Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda Ali Aboud alisema wamefurahishwa na wizara kuyaendeleza maonesho hayo ambayo yamefungua mlango mzuri wa mashirikiano.Alisema tangu kuanzishwa kwa maonesho hayo yamekuwa yakipata mafanikio siku hadi siku kwa wajasiriamali mbalimbali kuonesha bidhaa zao na kupata soko.“Chama cha wafanyabiashara na wakulima kwa ujumla kimefurahishwa na kuendelezwa kwa maonesho haya ambayo yamefunguwa milango ya mashirikiano na kuitangaza sekta binafsi kupiga hatua kubwa ya maendeleo,” alisema.Aidha aliishauri wizara kuanzia sasa kutenga maeneo maalumu rasmi kwa ajili ya kufanyika maonesho hayo yenye lengo la kutangaza sekta ya biashara na wafanyabiashara kwa ujumla.Tamasha la biashara limehudhuriwa na zaidi ya wafanyabiashara kutoka katika taasisi 162 ikiwemo ziliopo nchini na Tanzania Bara.
UCHUMI
Ramadhan Hassan-Dodoma MSEMAJI Mkuu wa Serikali,Dk.Hassan Abbas  amesema ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa  (SGR) kutoka Dar es Salaam – Morogoro, unaendelea kwa kasi na haujasimama kama ambavyo wanasiasa  wanadai. Alisema mpaka sasa fedha zipo za kutosha kwa ajili ya kumalizia mradi huo. Alisema mwaka huu, Watanzania kwa mara ya kwanza watapanda treni ya umeme. Dk.Abbas, alitoa kauli hiyo  jijini Dodoma jana, alipozungumza na waandishi wa habari. Alisema mradi huo,unaendelea kwa kasi na hakuna sehemu ambayo umesimama.  “Ukisema reli imesimama, ninyi mpo Dodoma nendeni hata Ihumwa nendeni mkaangalie kama kuna eneo mradi umesimama hatuja wahi kukosa fedha, mradi unaendelea.  “Hakuna hoja ya msingi mradi unaendelea kwa awamu zote na tusubirie na kile kipande cha Morogoro, mwaka huu mtapanda treni.Fedha zipo wakati wowote mwaka huu kwa Dar- Moro kipande kile kitakamilika. “Wanasiasa  kusema wanatimiza historia ya kukosoa kama mmoja tulivyomuona anakosoa ndege, lakini anakuja kupanda hiyo hiyo.Sisi hatutasita kuendelea kuchapa kazi. “Licha ya kelele mbalimbali, nipo hapa kuwathibitishia miradi mingi ukiwamo wa  reli tunatekeleza kipande cha Dar – Moro, japo kinasumbua sumbua tupo vizuri kwa asilimia 75. Alisema kipande cha Morogoro – Makutupora- Singida,  kimekamilika kwa asilimia 28, huku changamoto zikiwa ni mvua zinaendelea kunyesha kuwazuia mafundi kuendelea na kazi. Alisema mpaka sasa wametumia Sh trilioni 2.957 kwa ajili ya mradi huo, ambapo alidai gharama ya mradi wote ni Sh trilioni 7. Alisema leo makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, wanatarajia kuanza ziara ya kukagua mradi wa SGR. “Hakuna kilichosimama wala  hakuna ‘tashtiti’ yoyote na kuanzia kesho (leo) tutakuwa na ziara muhimu ya kihistoria kwa makatibu wakuu kukagua mradi huo,”alisema. Kuhusiana na watu wanaobeza miradi ya Serikali, alisema wao wanaendelea kuchapa kazi na siku moja watakuja kuitumia miradi hiyo hiyo. “Siku wakiumwa  tutawatibu, siku wakitaka kupanda ndege tutawakatia tiketi,sisi ni kuchapa kazi tu,”alisema. Alisema Tanzania imekuwa nchi ya 21 duniani kuweka mazingira na kuchagiza biashara ndogondogo. Alisema kwa Afrika, ni ya nne na kwa Afrika Mashariki imekuwa ni ya kwanza. “Wenzetu wanatambua  juhudi tunazofanya, kuna ripoti imetoka kuhusu Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 21 duniani kwa  kuweka mazingira na kuchagiza biashara ndogondogo kwa kupunguza kero mbalimbali,”alisema. Alisema mpaka sasa Serikali imetoa Sh trilioni 1.275 kwa ajili ya  mradi wa kufufua umeme wa Rufiji ambapo gharama za mradi wote ni Sh trilioni 6.5. “Kazi nyingi zinaendelea kwenye mradi huu, sio ndoto na kazi inaendelea, Tunaendelea na utekelezaji,”alisema. Alisema Serikali ya Tanzania imetengeneza   chelezo kubwa katika Ziwa Victoria na mpaka sasa imetoa Sh bilioni 32 kwa ajili ya mradi huo. Mwisho Hatutagiza nguzo za umeme nje-Majaliwa Na Amina Omari,Tanga SERIKALI  imesema haitaagiza nguzo za umeme nje ya nchi kwa sababu wazalishaji wa ndani wamezalisha za kutosha. Kauli hiyo, imetolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alipozindua kiwanda cha kuzalisha nguzo za umeme Muha Traders kilichopo Pongwe. Alisema wakati wa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Serikali itatumia nguzo ambazo zinazolishwa  nchini. “Tunanguzo nyingi,hatuagizi kutoka nje kwani zamani Serikali ilikuwa inapata hasara kuagiza nguzo nje ya nchi,”alisema Waziri Mkuu. Aliwataka watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha wanawasimamia kwa ukaribu wakandarasi wanaosimamia miradi ya REA ili kuhakikisha wanafanyakazi kwa ufanisi. Alisema nia ya Serikali, ni kufikisha umeme maeneo yote ya vijijini na vitongoji ili kutoa fursa kwa wananchi kuitumia huduma hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alisema Serikali imepata Sh milioni  45 kutokana na kodi ya mazao ya nguzo. “Baada ya agizo ulilolitoa la kukusanya kodi katika viwanda vya uzalishaji wa  nguzo, tumebaini deni la Sh milioni 162, tumewekeana utaratibu wa kulipa na mwekezaji,”alisema.
KITAIFA
BABA Mtakatifu, Francis ametoa medani ya heshima iitwayo ‘Medaglia Pontificial’ kwa Bruda Vincent Soreng kwa kutunza, kulinda na kuendeleza mazingira katika shule ya sekondari ya St Peter Claver. Medali ya Medaglia Pontificial ambayo hutolewa na Baba Mtakatifu Francis kwa watu au taasisi zinazojitoa duniani katika kutunza, kulinda na kuendeleza mazingira ilikabidhiwa kwake na Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Amani na Mazingira Duniani. Akizungumza kabla kupokea kwa medali hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St Peter Claver, Padri Buberwa Karongo alisema shule hiyo kupitia juhudi za BrudaVincent aliyezaliwa mwaka 1930 nchini India na wanafunzi iliweza kupanda miti zaidi ya 160,000 katika kipindi cha miaka nane na hivyo kutunukiwa medali ya heshima. “Kupitia medali hii shule imeweza kutambulika duniani kote, hivyo tutaendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi za Serikali ya awamu ya tano kuhusu uhifadhi na uendelezaji wa mazingira ili vizazi vijavyo vikute nchi ikiwa ni kijani na yenye ardhi bora na rutuba za kilimo na kiuchumi.” Naye Simbachawene alisema Serikali inampango wa kuanza kutoa tuzo ya Rais ya Mazingira kwa watu na taasisi ambazo zinatunza mazingira katika nyanja mbalimbali kama vile vyanzo vya maji, upandaji miti na matumizi ya nishati.
KITAIFA
MADRID, HISPANIA MSHAMBULIAJI, Bale akubali yaishe Madrid ameamua kuondoka Real Madrid kwenda kujiunga na Klabu ya China Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu. Vyanzo vilivyo karibu na mshambuliaji huyo raia wa Wales vilithibitisha ripoti kwamba Bale amekubali kuondoka Santiago Bernabeu,  ingawa uhamisho huo bado haujakamilika. Bale amejikuta matatani na kocha wake,  Zinedine Zidane ambaye ameonyesha wazi wazi kutomuhitaji katika kikosi chake. Zidane amekuwa akitamka wazi kuwa Bale kuondoka itakuwa bora kwake, kwani hayupo katika mipango yake ya siku zijazo. Bale ameahidiwa kuwa mchezaji atakayelipwa zaidi duniani akitua China,  kwani atakuwa akilipwa mshahara wa pauni milioni moja kwa wiki(ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni 2 za Tanzania). Licha ya mshambuliaji huyo kutokea benchi kwenye mchezo na kuisadia Real Madrid kushinda kwa penalti 3-2, baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo kujipima nguvu, Zidane alisisitiza hakuna kilichobadilika kwa mchezaji huyo. Bale alijiunga na Madrid  kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi wakati huo ya  pauni milioni  85 kutoka Tottenham  Spurs miaka sita iliyopita, akiipuku rekodi ya Cristiano Ronaldo aliyejiunga na timu hiyo kwa pauni milioni 80, akitokea Manchester United mwaka  2009. Mshambuliaji huyo amebakiza mkataba wa  miaka mitatu na mabingwa wao wa kiistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ameshinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya , taji moja la La Liga, Copa del Rey, mataji matatu ya Uefa Super na matatu ya Klabu Bingwa ya Dunia. Bale amefunga mabao matatu katika michezo minne ya fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo  Real ilishinda taji hilo mwaka  2014, 2016, 2017 na 2018. Moja ya sababu kubwa inayomfanya Bale kushindwa kutema cheche Madrid ni majeraha ya mara kwa mara ambayo yamemsababishia kupata fursa ya kuanza katika michezo 78 tu ya Ligi Kuu kwa misimu yote minne. Msimu uliopita, Bale alifanikiwa kucheza mechi 42 za Real Madrid, huku muda mwingi akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha . Kurudi kwa Zidane katika kikosi cha Real kulitafsiriwa  kama habari mbaya na wakala wa mchezaji huyo, Jonathan Barnett  kwa sababu Mfaransa huyo hakutaka kufanya kazi na Bale kwani wanaume hao wawili hawapikiki chungu kimoja. Bale alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Southampton, akiwa na umri wa miaka 16 kabla ya kuondoka katika klabu hiyo mwaka 2007 na kujiunga na Tottenham  Alitumia misimu sita kwenye klabu hiyo ya  kaskazini mwa London kabla ya kujiunga na Madrid.  Hata hivyo, Bale amekuwa akihusishwa  kurudi katika klabu ya zamani ya Tottenham Spurs, huku pia Manchester United na Bayern Munich zikiwa miongoni mwa timu zilizotamani kumnasa.
MICHEZO
TETEMEKO la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha ritcher 5.1, limetokea katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Mbeya na kuzua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa mji huo.Akizungumzia tetemeko hilo lililotokea jana mchana, Kaimu Mkurugenzi wa wa Idara ya Jiolojia katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini, Maruvuko Msechu aliwaonya wananchi waache kuzua taharuki linapotokea tetemeko, watulie walipo na wasikae karibu na nyumba ndefu na miti mirefu. Mjiolojia Mwandamizi, Gabriel Mbogoni alisema tetemeko hilo lilitokea umbali wa kilomita 40 kutoka Sumbawanga Mjini na kugusa mikoa ya Rukwa, Katavi na Mbeya, kuanzisha saa 6.15 na limedumu kwa dakika tano hivi.Mbogoni alisema tetemeko hilo lililotokea mikoa hiyo, hadi sasa hawajapata taarifa za athari zilizotokea, lakini mara nyingi ya kipimo hicho huwa yanasababisha nyufa katika nyumba tu. Alisema si jambo la ajabu kutokea matetemeko kwenye mikoa iliyopo katika Bonde la Ufa hasa katika mkondo wa magharibi kama ya Mbeya, Rukwa, Kigoma, Katavi na Kagera.“Maeneo yaliyo katika mkondo wa Bonde la Ufa nchini kutokana na mkandamizo na mshikamano wa miamba, husababisha mawimbi ambayo yanakuwa na kasi ya kilomita 13 kwa sekunde moja,” alisema. Alisema historia ya matetemeko katika mkondo huo, inaonesha kwamba kubwa zaidi liliwahi kutokea likiwa na kipimo cha ritcher 7.3 katika mwaka 1970 na halijawahi kutokea tena. Mbogoni alisema, hakuna teknolojia ya kuzuia athari za mawimbi na hakuna teknolojia ya kubaini kuzuia ni majanga ya asili kinachotakiwa ni kuchukua tahadhari.“Wananchi wasishikwe na taharuki, kwani utafiti umebaini kwamba wanaotaharuki ndio wanaoumia kutokana na kasi ya mawimbi ya kilomita 13 kwa sekundu moja,” alisema. Kutokana na kasi hiyo ya mawimbi, mtu akiwa ndani ya nyumba hawezi kukimbia kuwahi kutoka nje, hivyo ni budi asimame kwenye kona ya kuta zinapokutana au chini ya uvungu wa kitanda kwani kwa kukimbia anaweza kuumia au kuangikiwa na nyumba.Kaimu Mkurugenzi wa wa Idara ya Jiolojia katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini, Msechu alisema tetemeko alisema limetokea hadi sasa hakuna athari zilizoripotiwa baada ya kutokea tetemeko hilo. Msechu alisema kama mtu alikuwa wakisafiri kwenye gari anatakiwa kushuka na kusubiri, kwani linapotokea huwa linaweza kuharibu miundombinu ya barabara na kukata hata madaraja.Aliwataka wanatakiwa kukaa mbali na majengo marefu na miti mirefu kwani linapotokea linaweza kuangusha majengo na kusababisha vifo kwa watu walio karibu nayo. Tetemeko hilo lililoanzia umbali wa kilometa kumi ndani ya ardhi, halikuwa kubwa na kusababisha athari kubwa katika mji huo. Mtikisiko wa ardhi ulianza saa sita na dakika kumi na nane mchana wa jana na kudumu kwa sekunde chache ulisababisha hofu kubwa ambapo wananchi waliokuwa ndani ya nyumba zikiwemo ofisi za serikali walikimbia nje wakihofia maisha yao.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Rukwa katika mji wa Sumbawanga, Dk John Lawi alikiri kuwa tetemeko hilo lilisababisha taharuki kwa wagonjwa waliokuwa wakitibiwa pia waliolazwa hospitalini hapo. “ Hata huku hospitalini limetikisha hakika wagonjwa waliingiwa na hofu lakini Mungu ni mkubwa halikusababisha madhara yoyote na hali ya utulivu imerejea na shughuli zinaendelea kama kawaida,” alieleza Dk Lawi.Wakizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kipeta katika Bonde la Ziwa Rukwa walikiri kuwa tetemeko hilo lilipita katika eneo hilo na kusababisha hata wanyama malishoni kuanza kulia na kukimbia ovyo. Hata hivyo, wakazi wa Mji Mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi wameliliambia gazeti hili kuwa tetemeko hilo halikupita wilayani mwao.
KITAIFA
Na MWANDISHI WETU  -DAR ES SALAAM SIKU mbili baada ya kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiuzulu ubunge kwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, umeibuka mkanganyiko kuhusu uamuzi wake huo. Kuibuka kwa mkanganyiko huo, kumekuja baada ya Ofisi ya Bunge kutoa taarifa kwa umma, kwamba Spika wa Bunge, amepokea barua ya kuvuliwa kwa uanachama wa CCM kwa Nyalandu na si ile ya kujiuzulu kwa ubunge kama alivyothibitisha mwanasiasa huyo juzi. Taarifa ya Bunge iliyotolewa jana, ilieleza kwamba Bunge lilipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM ikieleza kwamba tangu Oktoba 30, mwaka huu, kilimvua uanachama Nyalandu, huku mwanasiasa huyo akieleza kuwa barua ya kujiuzulu kwake ameshaiwasilisha kwa Spika. Hata hivyo, baada ya uamuzi huo wa Nyalandu juzi, Spika wa Bunge, Job Ndugai alinukuliwa na kituo kimoja cha redio akisema kuwa bado hajapokea barua ya mwanasiasa huyo kujiuzulu ubunge, huku akimtaka aache kuwashwawashwa. Spika Ndugai, alisema bado anaendelea kumtambua Nyalandu kama mbunge halali na mwenye stahiki zote kwa mujibu wa utaratibu.   KAULI YA POLEPOLE Saa chache baada ya uamuzi huo wa Nyalandu, Katibu wa Itikadi na Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole aliibuka na kutoa video yake akielezea kwamba kuondoka kwa Nyalandu kumewapunguzia kazi za kumjadili kwenye vikao. Polepole alisema kuondoka kwa Nyalandu hakuna jambo kubwa ambalo limetokea, bali ni la kawaida sana na kwamba waliondoka watu wazito na chama kimebaki kama kilivyo, hivyo mwanasiasa huyo si kati ya wazito bali ni mwananchi wa kawaida. “Wapo ambao katika kipindi hiki watashindwa mwendokasi katika kusimamia ajenda za wananchi kifikra na kimatendo, hawa wanatupunguzia kazi ya kuwajadili kwenye vikao vya chama kwa kushindwa kuenenda na mwendokasi tunaoenenda nao katika nafasi zao walizopewa dhamana,” alisema Polepole.   TAARIFA YA BUNGE Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jana, ilisema Spika amepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM ya Oktoba 30, mwaka huu, ikimwarifu kwamba Nyalandu amepoteza sifa za uanachama, hivyo amepoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa chama hicho na ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya chama hicho. Ilisema kwa muda sasa chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume cha misingi, falsafa na itikadi ya CCM. Mbali na hilo, taarifa hiyo pia ilisema kuwa Ofisi ya Spika haijapokea barua kutoka kwa Nyalandu ambayo amekuwa akieleza kuwa amemwandikia Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake tangu Jumatatu wiki hii. “Hivyo, CCM kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Spika kuwa Lazaro Nyalandu  amepoteza sifa za uanachama wa CCM, hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa chama hicho na ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya chama hicho. “Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya CCM, ambacho Lazaro Nyalandu  alipata ubunge  kwa mujibu wa  Ibara  ya 71 (1)(f)  ya Katiba ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania. “Ibara hiyo inatamka kwamba; mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake cha ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge,” ilisema barua hiyo. Kutokana na hilo, barua hiyo ilisema kuwa Nyalandu si mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zinaendelea kuchukuliwa. Hata hivyo barua hiyo haikuweka wazi lini tume hiyo itaarifiwa rasmi kuhusu suala hilo.   MAJIBU YA CCM Alipotafutwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ili atoe ufafanuzi wa suala hilo, simu yake ya mkononi haikupatikana. Alipopigiwa simu Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogolo, alisema yeye si msemaji wa chama, hivyo atafutwe Kinana au Polepole. Polepole alipotafutwa, alisema apigiwe simu baada ya saa moja. Hata hivyo, baada ya muda huo alitafutwa tena, lakini simu yake iliita bila kupokewa.   KATIBA YA CCM Hata hivyo, wakati CCM ikiandika barua ya kumvua uanachama Nyalandu, chama hicho hivi karibuni kilifanya vikao vyake vya ngazi ya juu, lakini haikuwahi kutolewa taarifa ya kuhojiwa au hata kuonywa kwa mwanasiasa huyo, jambo ambalo bado limeendelea kuzua maswali kwa umma. Kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 2005, Ibara ya 14 (4) haki za mwachama ambaye ana makosa kwa mujibu wa utaratibu zimeelezwa wazi. Kwamba mwanachama ana haki ya kujitetea au kutoa maelezo yake mbele ya Kikao cha CCM kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake, pamoja na haki ya kukata rufani ya kwenda katika kikao cha juu zaidi cha CCM kama kipo endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa. Kutokana na hali hiyo ilionekana kuwa bado kuna tatizo katika uamuzi huo wa Spika, ambao umetangazwa kwa umma, huku ufafanuzi wa kina ukiwa bado umekosekana.   MAELEZO YA NYALANDU Jumatatu ya wiki hii, Nyalandu ambaye amekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini tangu mwaka 2000, akiwa mkoani Arusha, alitangaza kujivua nyadhifa zote za CCM na ubunge. “Nimechukua uamuzi huu kutokana na kutoridhishwa kwangu na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania wenzetu. “Pia kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya mihimili ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama), kunakofanya utendaji kazi wa kibunge wa kutunga sheria na kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru ulioainishwa na kuwekwa bayana kikatiba,” alisema. Nyalandu, ambaye amepata kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kabla ya kushika wadhifa wa uwaziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema anaamini kwamba bila Tanzania kupata katiba mpya sasa, hakuna namna yoyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwapo kwa ukomo wa wazi. “Naamini kwamba bila Tanzania kupata katiba mpya sasa, hakuna namna yoyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndiyo chimbuko la uongozi bora wa nchi, na kuonyesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yanatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya watu kwa ajili ya watu. “Mimi naondoka na kukiacha CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya uenyekiti wa UVCCM mkoa, ujumbe wa kamati za siasa wilaya na mkoa, ujumbe wa kamati ya wabunge wote wa CCM na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. “Nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. “Naamini kuwa kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna moja au nyingine, CCM nayo imekuwa chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. “Hivyo basi, kwa dhamira yangu na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya kikatiba, natangaza kukihama CCM leo hii na nitaomba ikiwapendeza wanachama wa Chadema, basi waniruhusu kuingia mlangoni mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na Chadema na Watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kupitia mfumo wa kidemokrasia na uhuru wa mawazo. “Vilevile, nimemua kujiuzulu kiti cha ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. “Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo, ili kwamba sote kama taifa tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. “Ni maombi yangu kwa Mungu kuwa haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za kisiasa na makabila yote nchini uimarike. “Tushindane kisera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu na taifa lililo imara na nchi yenye maadili,” alisema Nyalandu.
KITAIFA
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali haitavumilia mtu anayekwamisha ujenzi wa uchumi wa viwanda ikiwa ni pamoja na kuzalisha au kuingiza nchini bidhaa bandia.Alitoa rai hiyo jana kupitia hotuba ya ufunguzi wa maonesho ya pili ya viwanda mkoani Pwani iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya.“Serikali haitamvumilia yeyote atakayekwamisha ujenzi wa viwanda ikiwa ni pamoja na kuzalisha au kuingiza bidhaa bandia zinazochafua taswira ya viwanda vya ndani,” alisema.Alitaka mamlaka zinazohusika na ubora wa bidhaa kuhakikisha zisizo bora haziingizwi nchini. Alishauri pia wenye viwanda kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazotumiwa zaidi na Watanzania.Alitaka mamlaka za ukaguzi hususani Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Shirika la Viwango (TBS) kuweka sheria, taratibu na kanuni wazi zisiwe kikwazo kwa wawekezaji.“Haiwezekani tukawa tunahamasisha uwekezaji halafu ninyi mkawa kikwazo” alisema na kuwataka kutoa msaada pale panapohitajika, kushirikiana na wadau na kuhakikisha nchi inapiga hatua za haraka katika ujenzi wa viwanda,” alisema.Vile vile aliwataka wawekezaji pia kuwa na tabia ya kufuatilia kuhusu nini wanatakiwa kufanya kwa mujibu wa sheria zilizopo na kutekeleza. Alisema Serikali inafanyia kazi tozo mbalimbali 114 zinaoonekana kero na kwamba tayari serikali imefuta tozo 54 na itandelea kufuta nyingine. Makamu wa Rais aliwahimiza Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini kupanua soko la viwanda na hivyo kuviwezesha kutoa ajira zaidi kwa Watanzania.Aliiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara, kitengo cha masoko kuhamasisha Watanzania kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini na kuhakikisha serikali inatumia bidhaa za ndani katika miradi yake. Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais alisema mwaka jana alitoa maagizo kadhaa ambayo alitaka mkoa umpe mrejesho kuhusu utekelezaji wake.Alitaja maagizo hayo ikiwamo ulinzi wa nafasi za Watanzania kupata ajia zenye staha, kuhakikisha sheria za kazi zinafuatwa na wizara ya kazi kupita mara kwa mara viwandani, kuhakikisha usalama na maslahi ya wafanyakazi yanazingatiwa Maagizo mengine alisema ni kuhakikisha mapato yatokanayo na viwanda yanatumika kuchangia maendeleo ya jamii na kunakuwa na mipango madhubuti ya kulinda ajira kwa wakazi wa Pwani sambamba na kujengwa kwa chuo cha ufundi kuwanoa.Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya viwanda na biashara ambayo ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa, kuboresha bandari, kununua ndege kurahisha usafiri wa watu na mizigo pamoja na kuleta umeme wa uhakika.“Tutaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara kati ya sekta ya umma na binafsi,” alisisitiza Samia.Alipongeza mkoa wa Pwani kwa kufanikisha maonesho ya viwanda na kusema bidhaa nyingi zilizooneshwa ni bora. Halikadhalika aliwapongeza wamiliki wa viwanda kujitokeza na kuwataka ambao hawajajitokeza kufanya hivyo ili bidhaa zao kufahamika kwa wateja.Maonesho hayo yaliyozinduliwa jana yatafungwa Oktoba 23 na keshokutwa Jumamosi kutakuwa na Kongamano la Fursa za Uwekezaji. Makamu wa Rais pia alitoa salamu za Rais John Magufuli akisema alitamani kushiriki kwenye maonesho hayo lakini anatingwa na shughuli mbalimbali za kitaifa.“Rais anawapongeza kwa utayari wenu wa kupokea hivi viwanda na kulinda amani na mazingira yanayowezesha viwanda kufanya vyema... Siku zijazo bila shaka mtatanua wigo na kushirikisha mikoa jirani. Rais anaamini maonesho yatakuwa chachu ya kuvutia wawekezaji zaidi mkoa wa Pwani,” alisema.Akizungumza kama Naibu wa Viwanda na Biashara, Manyanya alisema wizara yake itahakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji zinapatiwa ufumbuzi. “Tutahakikisha katika wizara hakuna visingizio au vichaka vya sheria vinavyoleta usumbufu,” alisema Mayanya.
KITAIFA
MBUNGE wa Karatu, Willy Quamba lo (Chadema) na Mwenyekiti wake wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Jubilate Mnyenye, wametakiwa kuacha kutumia mafuta ya serikali kuwalinda madiwani watatu wa chama hicho wasihamie Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Lootha Sanare mjini Karatu baada ya kupokea umati mkubwa wa watu walienda kuwapokea madiwani wawili wa Chadema waliohama chama hicho na kurudi CCM.Alisema kitendo cha kuwalinda madiwani hao watatu hakina tija kwa kuwa wakiamuwa kuondoka kwa ridhaa yao watafanya hivyo tu bila ya kuzuiwa na kusisitiza kuwa kwa ngome ya Chadema Karatu iliyodumu kwa miaka 25 imetikisika. Mwenyekiti huyo alisema anashangazwa kuona viongozi hao wakikesha mchana na usiku kuwalinda madiwani hao wasifanye maamuzi ya kujiuzulu udiwani ndani ya Chadema kwani wakifanya hivyo baraza la madiwani halitaongozwa tena na chama hicho.Alisema kwa sasa viongozi hao wa Chadema wanakesha usiku milangoni kwa madiwani kuwalinda na mchana wanawachunga katika nyendo zao za kila siku na kusema kuwa kimbunga cha CCM hakizuiliki. Sanare alisema kuwa mlango uko wazi kwa mbunge, mwenyekiti na madiwani kurudi chama tawala kwani nyumbani kwa sasa kumenoga na uamuzi huo unapaswa kufanywa sasa na sio wakati mwingine kwani CCM ya sasa inajali maendeleo ya wanyonge.Alisema Chadema wameingiwa na woga na mshituko kwani wameongoza jimbo hilo na baraza la madiwani kwa miaka 25 na kitendo cha madiwani kung’atuka na kujiunga na CCM kimewashitua na ndio maana wanakesha kuwalinda. Naye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa Arusha, Daniel Awak ambaye ni mkazi wa wilaya ya Karatu alisema kuwa jukumu walilopewa na viongozi wa juu wa CCM ni kutaka Mkoa wa Arusha kuwa na wabunge na madiwani wote wa chama hicho na sio vinginevyo.
KITAIFA
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa kiwango kinachooneshwa na wachezaji wa timu hiyo ni dhahir kuwa timu hiyo haitakuwa na uwezo wa kuifunga timu yao (Yanga).“Kutokana na mazoezi ninayoyaona hapa Zanzibar bado kabisa na zile tano tunazosema mwaka huu ndio zitarudi,” alisema.Simba ipo visiwani hapa kwa kambi ya kujiandaa na Ligi Kuu inayotarajiwa kuaza Septemba.Aidha alisema, usajili wa Hamisi Kiiza Simba hauwasumbui kwani mchezaji huyo kwa sasa hana kiwango kizuri kama alivyokuwa Yanga.“Kwa muziki wa Yanga hasimami mtu si Simba, Azam wala Mtibwa, hivi Kazi Moto (Mwinyi) asimame kwa Niyonzima (Haruna) au kwa mtoto wa Salum Telela wanajidanyanganya tu”, alisema.
MICHEZO
MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewakaribisha wananchi wa mkoa huo, mikoa ya jirani na Tanzania kwa ujumla kuhudhuria katika Jukwaa la Fursa za Biashara mkoani Geita linalofanyika kesho.Kiongozi huyo amesema ana hakika litakuwa na manufaa makubwa kwa mkoa wake. Mkuu wa Mkoa amewaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa, Jukwaa hilo limetanguliwa na maonesho ya bidhaa za wajasiriamali zinazozalishwa Geita.Amesema maonesho hayo yaliyoanza jana katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Geita na kwamba yatamalizika kesho sambamba na Jukwaa la Biashara. Alisema Jukwaa litafanyikia katika ukumbi wa Gedeco unaomilikiwa na Halmashauri hiyo ya Mji wa Geita.Gabriel amesema nia kubwa ya kufanyika kwa Jukwaa na maonesho hayo ni kuwasaidia wajasiriamali wa mkoa wake kutangaza fursa walizo nazo sambamba na kukutana na wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo kujifunza kutoka kwao ili kuweza kupanuka zaidi kibiashara."Wajasiriamali watakapokutana na wadau mbalimbali wa biashara kwenye jukwaa kesho, watakuwa wanaongea lugha moja ya biashara na uwekezaji ili kunyanyua mkoa wa Geita," alisema.Alisema katika jukwaa hilo, ana hakika wajasiriamali wa Geita watapata ujuzi, elimu na hata masoko kwa ajili ya kuboresha shughuli zao."Wajasiriamali wetu watakutana na taasisi za fedha na kujua ni taasisi ipi inaweza kuwasadia kukuza mitaji yao," alisema.Alisema jukwaa hilo pia linausaidia mkoa kutangaza fursa zake kwa Watanzania, fursa ambazo zimekuwa pia zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, hususani vya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).Mkuu wa mkoa ameishukuru TSN kwa kuanzisha majukwaa ya biashara na kuwa tayari kushirikiana na ofisi yake ili kufanikisha Jukwaa la Biashara la kesho.Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah, amesema ana matarajio makubwa kwamba Jukwaa la Biashara la kesho litakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na maandalizi yaliyofanyika na hasa ushirikiano mkubwa uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita.Akielezea kwa nini TSN imeamua kufanya majukwaa ambapo hili ya Geita ni la saba, Tuma amesema ni kutokana na kuona kwamba taasisi hiyo ya serikali ina dhima ya kusaidia na kuleta chachu katika kuboresha biashara na uwekezaji kwa maendeleo ya taifa.Amesema, lengo la majukwaa hayo ni kuibua fursa za biashara na uwekezaji katika maeneo husika.Alisema timu ya TSN imekaa mkoani Geita kwa karibu wiki tatu, imetembea maeneo mbalimbali ya mkoa na kuzungumza na wadau mbalimbali kuhusu maendeleo ya mkoa wa Geita na kisha kusambaza habari za maeneo hayo na kwamba kesho kutakuwa na toleo maalumu la mkoa wa Geita kwenye gazeti hili.Tayari kampuni kadhaa zimejitokeza kudhamini Jukwaa la Geita ikiwa Geita Gold Mine (GGM), Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Maelezo Televisheni, TADB Bank, Benki ya NBC na Busolwa Mining Limited.Wadhamini wengine ni Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Hifadhi ya Jamii (SSRA), Benki ya Azania, Lenny Hotel, Waja General Company Ltd, GF Truck, Air Tanzania Corporation Ltd, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA).Zikiwa zimebaki saa chache Jukwaa kufanyika, wadhamini wanakaribishwa kupitia namba zifuatazo: 0655 332 866, 0712 516 169 au email: advertising@dailynews.co.tz
UCHUMI
NEW YORK, MAREKANI HATIMAYE staa wa filamu na muziki nchini Marekani, Priyanka Chopra, amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Nick Jonas baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miezi miwili. Wawili hao wamekuwa wakionekana wakiwa pamoja kwenye matamasha mbalimbali na kuwafanya mashabiki wabaki na maswali, lakini majibu yake yamepatikana baada ya mrembo huyo kuthibitisha kuvishwa pete ya uchumba. “Nina furaha kwa maamuzi ya Nick Jonas ya kuamua kunivisha pete ya uchumba, alifunga safari hadi jijini New York kwa ajili ya kwenda kuifuata na sasa kila kitu kipo wazi, sikuwa tayari kuweka wazi kwa mashabiki kabla ya mipango kukamilika, lakini sasa ninaweza kuongea, nampenda sana Nick,” aliandika mrembo huyo. Priyanka mwenye umri wa miaka 36, raia wa nchini India, amedai yupo tayari kufunga ndoa na mpenzi wake huyo mwenye umri wa miaka 25 bila ya kujali tofauti ya umri wao.
BURUDANI
['Tottenham iko kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cape Verde, Ze Luis, 28 kwa mkopo akitokea Porto.(Record - in Portuguese)', 'Inter Milan imekubaliana na kiungo Christian Eriksen, 27, kuhusu uhamisho wa kudumu mwezi huu, lakini Tottenham inataka timu hiyo ya ligi ya italia kutoa mara mbili ya dau la pauni 8.5 (Calciomercato - in Italian)', 'Mkataba wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, umeisha lakini Paris St-Germain imeiambia Atletico Madrid kuongeza dau mpaka pauni milioni 30. (Marca - in Spanish)', 'Liverpool inajiandaa kutenga pauni milioni 107 kumnasa kiungo wa Bayer Leverkusen Kai Havertz na kuipiku Manchester United,Barcelona na Bayern Munich katika mbio za kumnasa mchezaji huyo raia wa Ujerumani. (Mundo Deportivo, via Mirror)', 'Washika bunduki na mahasimu wao Tottenham ni miongoni mwa timu tano za primea zinazomuwinda beki wa kati wa Getafe Djene Dakonam,28. (Sun)', 'Spurs itakabiliana na upinzani kutoka Sevilla mwezi huu kumnasa mshambuliaji wa Poland na timu ya AC Milan Krzysztof Piatek, 24. (Mail)', 'Manchester United inataka kumshajili kiungo mchezeshaji na kwa mkopo na miongoni mwa wanaowindwa na Mhispaniola Marcos Llorente, 24 , Atletico Madrid. (Manchester Evening News)', 'Barcelona ipo mbioni kumsajili kiungo wa Brazil Matheus Fernandes, 21, kutoka Palmeiras kwa Euro milioni 7 na nyongeza ya Euro milioni 4 kutokana na mafanikio yake yatakavyokua. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Barca pia inafuatilia maendeleo ya kiungo wa Japan Jun Nishikawa,17, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Cerezo Osaka. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Mlinzi wa pembeni wa AC Milan na Uswizi Ricardo Rodriguez, 27, amechagua kwenda kwa mkopo Fenerbahce na sio PSV Eindhoven huku akitazamia kusajiliwa kabisa kwa Euro Milioni 6. (Calciomercato - in Italian)', 'Southampton haitamuuza Che Adams kwa kuwa meneja Ralph Hasenhuttl ameomba uongozi kumbakisha kikosini mshambuliaji huyo Muingereza mwenye miaka 23. (Express)', 'Mlinzi wa pembeni wa Uholanzi Mike van Beijnen, mtoto wa wakala wa kiungo Frenkie de Jong ameondoka Barcelona bila ya kucheza mchezo wowote miezi sita baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa Euro milioni 100. (Mail)', 'Meneja wa zamani wa Chelsea na Spurs Andre Villas-Boas amesema anaweza kuondoka Marseille baada ya mkurugenzi wa zamani wa West Ham na Sheffield Wednesday Paul Aldridge bila kupewa taarifa. . (Le Parisien - in French)', 'Kiungo wa Rangers Greg Docherty, 23, anataka kujiunga na Sunderland kwa mkopo katika kipindi kilichosalia cha msimu kukilo kwenda Charlton. (Northern Echo)', 'Uefa imebadili mfumo wa timu bora ya mwaka ya mashabiki ili kumuongeza mshambuliaji wa Juventus na Ureno mwenye miaka 34, Cristiano Ronaldo. (Mail)', 'Manchester United inataka kumshajili kiungo mchezeshaji na kwa mkopo na miongoni mwa wanaowindwa na Mhispaniola Marcos Llorente, 24 , Atletico Madrid. (Manchester Evening News)', 'Barcelona ipo mbioni kumsajili kiungo wa Brazil Matheus Fernandes, 21, kutoka Palmeiras kwa Euro milioni 7 na nyongeza ya Euro milioni 4 kutokana na mafanikio yake yatakavyokua. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Barca pia inafuatilia maendeleo ya kiungo wa Japan Jun Nishikawa,17, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Cerezo Osaka. (Mundo Deportivo - in Spanish)', 'Mlinzi wa pembeni wa AC Milan na Uswizi Ricardo Rodriguez, 27, amechagua kwenda kwa mkopo to Fenerbahce na sio PSV Eindhoven huku akitazamia kusajiliwa kabisa kwa Euro Milioni 6. (Calciomercato - in Italian)', 'Southampton haitamuuza Che Adams kwa kuwa meneja Ralph Hasenhuttl ameomba uongozi kumbakisha kikosini mshambuliaji huyo Muingereza mwenye miaka 23. (Express)', 'Mlinzi wa pembeni wa Uholanzi Mike van Beijnen, mtoto wa wakala wa kiungo Frenkie de Jong ameondoka Barcelona bila ya kucheza mchezo wowote miezi sita baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa Euro milioni 100. (Mail)', 'Meneja wa zamani wa Chelsea na Spurs Andre Villas-Boas amesema anaweza kuondoka Marseille baada ya mkurugenzi wa zamani wa West Ham na Sheffield Wednesday Paul Aldridge bila kupewa taarifa. . (Le Parisien - in French)', 'Kiungo wa Rangers Greg Docherty, 23, anataka kujiunga na Sunderland kwa mkopo katika kipindi kilichosalia cha msimu kukilo kwenda Charlton. (Northern Echo)', 'Uefa imebadili mfumo wa timu bora ya mwaka ya mashabiki ili kumuongeza mshambuliaji wa Juventus na Ureno mwenye miaka 34, Cristiano Ronaldo. (Mail)']
MICHEZO
TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys, jana iliyaaga kiume mashindano ya Kombe la Cecafa baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Pamoja na kipigo hicho, Serengeti Boys imefuzu kwa fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019 U-17) zitakazofanyika jijini Dar es Salaam mwakani. Mashindano hayo ya Cecafa kwa U-17 yanatumika pia kupata mwakilishi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati akayeungana na Serengeti Boys kucheza fainali hizo. Kwa ushindi wa jana, Uganda sasa itacheza na Ethiopia katika fainali itakayofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, baada ya timu hiyo kuifunga Rwanda kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya 2-2 katika dakika 90 za kawaida.
MICHEZO
Chanzo cha picha, Getty Images West Ham bado wana matumaini ya kumsajili mchezaji wa Ajax, Mohammed Kudus baada ya ombi lao la awali la kiungo huyo wa kati wa miaka 23 kukataliwa. (Sky Sports) The Hammers wamewasilisha ofa ya pili ya £35.8m (euro 42m) ya kumnunua Kudus lakini imekataliwa na Ajax. (Fabrizio Romano) Ofa ya Liverpool ya pauni milioni 25.6 (euro 30m) kwa ajili ya kiungo wa Brazil Andre, 22, imekataliwa na Fluminense ambao wanasitasita kumpoteza mchezaji huyo kabla ya kumalizika kwa msimu wao wa ligi mwezi Desemba. (ESPN) Chanzo cha picha, Getty Images Manchester City huenda wakafufua mkataba wa pauni milioni 80 na West Ham kwa kiungo wa kati wa Brazil Lucas Paqueta, 25, mwezi Januari, mara tu uchunguzi wa Chama cha Soka kuhusu madai ya ukiukaji wa sheria ya kamari ya mchezaji huyo kukamilika. (Sky Sports) Fiorentina wamempa kiungo wa Morocco Sofyan Amrabat, 27, hadi Ijumaa kuamua kama anataka kusalia katika klabu hiyo huku Liverpool huku Manchester United na Atletico Madrid zikimuwania. (Corriere dello Sport via Football Italia) Mustakabali wa kiungo wa kati wa Buyern Munich Mholanzi Ryan Gravenberch anayewaniwa na Liverpool uko mashakani huku klabu hiyo ya Bundesliga ikikaribia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (The Athletic - Usajili unahitajika) Chanzo cha picha, Getty Images Arsenal wamewafahamisha wawaniaji wa Saudi Arabia na Real Madrid kwamba mlinzi wao Mbrazil Gabriel, 25, hapatikani. (Mirror) Bernardo Silva, 29, ametia saini mkataba mpya katika klabu ya Manchester City, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno akijitoa kwa mabingwa hao wa Ligi ya Primia hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano). Meneja mkuu wa Roma Lina Souloukou amesafiri kwa ndege hadi London, na hivyo kuchochea uvumi wa mazungumzo na Chelsea kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano) Lukaku kwa sasa anafanya mazoezi na wachezaji wa chini ya miaka 21 wa Chelsea na hata hajazungumza na kocha mpya Mauricio Pochettino, huku klabu hiyo ikikataa kumruhusu kuondoka tena kwa mkopo. (Telegraph - usajili unahitajika) Chanzo cha picha, Getty Images Everton wamejiondoa katika mpango wa kumnunua winga wa Chelsea na Muingereza Callum Hudson-Odoi, 22, lakini The Toffees wanasalia kwenye mazungumzo na Southampton kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Scotland Che Adams, 27. (Liverpool Echo) Manchester United wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Fenerbahce na Uturuki Altay Bayindir, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akiwa na kipengele cha kumuachia cha £4.2m. (Mail) Bayindir amefanyiwa uchunguzi wa awali wa matibabu nchini Ugiriki kuhusu tatizo la mgongo lililopo, ambalo matokeo yake yataamua iwapo United itaendeleza mpango huo. (Star) Chanzo cha picha, Getty Images Klabu kadhaa za Ligi ya Premia zinafuatilia hali ya mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati katika klabu ya Barcelona huku klabu hiyo ikijiandaa kwa mazungumzo na wakala Jorge Mendes kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sport - kwa Kihispania) Mshambuliaji wa Leicester City Mnigeria Kelechi Iheanacho, 26, ameibuka kama mlengwa mkuu wa klabu ya Crystal Palace. (Leicestershire Live) Manchester United na Chelsea zimeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Croatia Dino Klapija mwenye umri wa miaka 16 kutoka Kustojia. (Mail)
MICHEZO
JOSEPH HIZA NA MTANDAO JUNI 12 ya kila mwaka ni siku ya kupinga ajira kwa watoto duniani, ikiangazia maswahibu yanayowakumba kwa namna mbalimbali tangu ilipoanzishwa mwaka 2002 na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Ajira za watoto ni jambo linalopigwa vita dunia nzima kutokana na ukweli kwamba ni kazi zinazohatarisha makuzi ya mtoto na kumweka katika hatari au hali tete na kumsababishia maisha mabovu mbeleni. Miongoni mwa namna inavyoangaziwa ni jinsi mizozo, vita na majanga inavyoathiri watoto hadi kulazimika kufanyishwa kazi kinyume na sheria za kimataifa. Mara nyingi watoto ndiyo huathirika zaidi kwa kukosa elimu na hata kupoteza familia zao. Hali hiyo huwalazimisha wengi kufanya kazi ili mradi mkono uende kinywani, lakini katika hali ya kinyonyaji mno kutokana na ukubwa wa kazi na malipo duni huku mara nyingi wakiathirika kiafya. Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Watoto (UNICEF), takriban watoto 40,000 wanafanya kazi katika migodi iliyo na madini ya Cobalt katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Aidha, Shirika la kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema baadhi ya watoto hao ni wa umri mdogo wengine wakiwa na miaka saba na huwa hawana vitenda kazi vinavyotakiwa kama mavazi ya kuwakinga dhidi ya madhara ya uchimbaji madini. Wanafanyakazi wakati mwingine hadi saa 24 ndani ya migodi, watoto hao hulipwa chini ya dola mbili kwa siku na wengi wao hupokea ujira mdogo kuliko huo. Madini hayo adimu ya Cobalt hutumika kutengezea betri za simu za kisasa za mkononi na hivyo, mashirika makubwa ya teknolojia kama vile Apple, Tesla, Microsoft, Samsung na Sony huyategemea madini hayo kutengezea bidhaa zao za kielektroniki. Madini hayo pia yanatumika katika magari ya kieletroniki yanayotengezewa na kampuni kama vile Daimler na Volkswagen. Hata hivyo, kampuni hizo hazikutaka kuhusishwa na biashara ya watoto kutumikishwa katika ajira. Hivi majuzi, Shirika la Habari Marekani CBS kupitia mwandishi wake Debora Patta, liliendesha uchunguzi ikiwa ni miaka miwili tangu ripoti ya kushtusha ya Amnesty ichapishwe. Katika safari hiyo ya karibuni maeneo ya kusini mwa nchi, CBS News ilishuhudia kile kinachoonekana kama Pori la Magharibi, ambako watoto huonekana wakichimba mitaro na kufanyishwa kazi ziwani – wakisaka hazina katika mazingira ya kutisha. Ni kazi ngumu kwa mtu mzima, lakini inayofanywa na watoto wadogo. Na bado makumi kwa maelfu ya watoto wa Kongo wanahusika katika kila hatua ya uchumbaji wa cobalt. Zaidi ya nusu ya usambazaji wa madini hayo duniani hutokea DRC na asilimia 20 huchimbwa kwa mikono, kwa mujibu wa Kampuni ya utafiti ya Darton Commodities Ltd yenye makao makuu London, Uingereza. Patta na timu yake waliosafiri katika barabara mbovu waliona watoto kila mahala, wakichimba cobalt katika mashimo yaliyotelekezwa. Inaonekana wazi maofisa wa usalama wanaosimamia hapo, wachache wakiwa wamevalia sare, wana kitu cha kuficha. Ni kwa sababu hiyo, timu ya CBS News ilizuiwa kila baada ya hatua chache, maofisa wakitaka barua na nyaraka za kuwaruhusu licha ya kwamba walikuwa tayari na kibali cha kufika hapo. Lakini mawakala wa Kichina wanaonunua cobalt, hawakukumbana na kikwazo chochote kuingia na kutoka eneo hilo hilo la mgodi. Katika migodi wanawake na watoto wanaowasaidia wanaoitwa wataalamu wa madini. Lakini watoto wa miaka hadi minne huonekana wakibeba vifusi vizito kutoka mashimoni huku vichanga vilivyopo migongoni mwa mama zao vikikumbana na uchafu au kucheza katika uchafu bila kujua wakivuta hewa ya sumu. Maofisa eneo hilo hukana ajira ya watoto, lakini wanakana kitu kinachoonekana dhahiri kuwaumbua na ili kukabili hilo, kila kamera au watu wa usalama au polisi wanapoonekana, watoto hufukuzwa haraka kutoka mgodini. Mmoja wa watoto, Ziki Swaze (11) baada ya kuulizwa na Patta kwanini hayuko shule, anajibu: “Wazazi wangu wamekufa, naishi na bibi. Kipato chetu na mahitaji ya shule yanatokana na madini ya cobalt. Faustin Adeye anayefanya kazi na shirika la Kikatoliki la Misereor ameliambia Shirika la Habari la Ujerumani (DW) kuwa mazingira ya kazi migodini nchini humo ni ya kusikitisha na kuongeza kuwa watoto wengi huathirika kimwili kutokana na kufanya kazi katika migodi hiyo. Adeye anasema hali katika migodi kadhaa kusini mwa Congo ni mbaya kiasi kwamba wakati mwingine watoto wao huzikwa wakiwa hai wakati migodi hiyo inapoporomoka. Desemba mwaka juzi, DW ilizitaka baadhi ya kampuni hizo kuzungumzia suala hilo la watoto kuajiriwa Congo kuchimba madini. Daimler, moja ya kampuni kubwa za kutengeneza magari Ujerumani ilijibu kwa maandishi kuwa inahitaji watu wanaowauzia bidhaa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo kimataifa. Daimler ilisema mwongozo wa kampuni hiyo kuhusu mazingira ya kazi, viwango vya kijamii na kimaadili pamoja na uhifadhi wa mazingira unakwenda mbali ya vigezo vya kisheria vya kuzingatia yote hayo. Iliongeza kuwa inatarajia wanaowauzia bidhaa za kutengeza magari yao kuheshimu na kuzingatia angalau vigezo vyote hivyo. BMW, kampuni nyingine ya Ujerumani ya kutengeza magari imekubali kuwa imetumia madini ya Cobalt kutoka Congo katika utengenezaji wa baadhi ya betri zao na kutangaza kuwa itaanzisha ukaguzi wa kuhakikisha wanaowauzia bidhaa hiyo hawakiuki sheria za haki za binadamu. Kampuni ya Marekani ya Apple ilitangaza Machi mwaka jana kuwa inanuia kuacha kununua cobalt inayochimbwa kwa kutumia mikono kutoka Congo.
AFYA
Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo zitaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.Alisema baba yake Mbwana, Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanawe katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakua nchini.“Baba yake Samatta alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya 1960 kama vile timu ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni, “ alisema Taalib.Alisema sherehe hizo pia zitapambwa na wasanii kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi kutoka, Dar es Salaam na mkoa wa Pwani.Alisema Shiwata ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyo baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo. Hivi sasa Samatta anachezea timu ya KRC Genk ya Ubelgiji na ameonesha uwezo wa hali ya juu katika timu hiyo iliyopo Ligi Kuu nchini humo. Samatta pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
MICHEZO
LONDON, ENGLAND KOCHA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Antonio Conte, amemmwagia sifa mshambuliaji wake, Alvaro Morata, huku akidai kuwa ana nidhamu ya hali ya juu na angeweza kumpa nafasi ya kumuoa mtoto wake. Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa yupo kwenye mipango ya kumfanya mchezaji huyo aendelee kuwa bora zaidi na nidhamu ya hali ya juu. Mchezaji huyo amejiunga na Chelsea katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea Real Madrid kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Diego Costa ambaye tayari yupo nchini Hispania kwa ajili ya kujiunga na klabu yake ya zamani, Atletico Madrid. “Nimekuwa nikimjua Morata kwa kipindi kirefu sana, ukweli ni kwamba mchezaji huyo ana nidhamu ya hali ya juu, nadhani Chelsea imefanya maamuzi sahihi ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. “Naweza kusema ninampenda mchezaji huyo kwa kuwa amekamilika kwa kiasi kikubwa na anaweza kubadilika kutokana na mazingira yaliyopo. “Tabia yake akiwa mazoezini inafaa kuigwa na kila mchezaji, mchezaji mwenye upole wa hali ya juu na nampenda kwa kuwa ni mmaliziaji mzuri, kutokana na hali hiyo, unaweza kumpa mtoto wako akamuoa, hata kwa upande wangu ningeweza kumpa mwanangu, lakini tayari ana mke wake,” alisema Conte. Conte amedai kuwa uwepo wa Morata ndani ya kikosi hicho utaweza kuziba nafasi ya Costa, hivyo hana wasiwasi na kuondoka kwake. “Napenda kumshukuru Costa kwa mchango wake katika kipindi chote ambacho tulikuwa pamoja, tuliweza kutwaa taji tukiwa wote, hivyo ninajivunia kuwa na mchezaji kama huyo kwenye kikosi kwa kuwa amekuwa miongoni mwa historia ya Chelsea. “Napenda kumtakia kila la heri huko aendako na ninaamini ataendelea kufanya vizuri zaidi ya hapa, sikuwa na tatizo na mchezaji huyo na tunaweza kushikana mikono popote nitakapokutana naye. “Hata hivyo, siwezi kuzungumzia sana mambo ya Costa kwa kuwa si tena mchezaji wa Chelsea, lakini naomba niweke wazi kuwa kila mchezaji msimu uliopita alikuwa muhimu kwenye kikosi na ndio maana tulichukua ubingwa na si kwa sababu ya fulani, hii ni timu,” aliongeza. Kwa upande wa Morata tangu ajiunge na kikosi hicho cha mabingwa watetezi amefanikiwa kufunga mabao matatu huku akitoa pasi mbili za mwisho katika michezo minne aliyoanza kabla ya mchezo wa jana.
MICHEZO
Chanzo cha picha, Getty Images Ajax wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson kutoka klabu ya Saudi Pro League Al-Ettifaq lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vya Premier League na Bundesliga kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 . (ESPN) Al-Ettifaq haitashinikizwa kumuuza Henderson mwezi Januari, au kumruhusu kuondoka kwa mkopo, huku nahodha huyo wa zamani wa Liverpool akiwa na mazungumzo na meneja Steven Gerrard na mkurugenzi wa michezo Mark Allen (Talksport) Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, anatazamiwa kujiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo lakini atarejea katika klabu yake ya Manchester United baada ya kuitumikia kwa sababu klabu hiyo ya Ujerumani haiwezi kumudu kufanya mkataba huo kuwa wa kudumu.(Mirror) Bayern Munich wamewasilisha ombi la kuchelewa kumnunua mchezaji anayelengwa na Tottenham Radu Dragusin na sasa utakuwa uamuzi wa beki huyo wa Genoa na Romania mwenye umri wa miaka 21 kuamua ni wapi anataka kuhamia (Sky Sports) Chanzo cha picha, EPA Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasema anataka mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 25, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu wa joto, kusalia na mabingwa hao wa Ufaransa kwa kuwa ndio klabu bora kwake. (RMC Sport - kwa Kifaransa) PSG wanashughulikia mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich mwenye umri wa miaka 28 kutoka Bayern Munich mwezi Januari. (Sky Germany - kwa Kijerumani) Newcastle United itakataa ofa zozote za Januari kutoka kwa PSG kwa kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akitua Tyneside. (The i) Mshambulizi wa kimataifa wa Uingereza Cole Palmer, 21, anasema alitaka kuhama kwa mkopo kutoka Manchester City msimu uliopita lakini akaambiwa anaweza "kusalia au uuzwe" kabla ya kujiunga na Chelsea. (Sky Sports) Fulham inamfuatilia mshambuliaji wa AZ Alkmaar na Ugiriki Vangelis Pavlidis , 25 , ambaye amekuwa akitazamwa na Chelsea, AC Milan na Barcelona wiki za hivi karibuni. (Evening Standard) Mkufunzi wa Leicester City Enzo Maresca anashinikiza kumnunua kiungo wa kati wa Italia Stefano Sensi mwenye umri wa miaka 28 kutoka Inter Milan. (Sky Sports Italia - kwa Kiitaliano) Chanzo cha picha, Getty Images Barcelona wamesitisha mazungumzo kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wa Atletico Madrid anayecheza kwa mkopo Joao Felix, huku klabu hiyo ya Uhispania ikiwa na mashaka kuhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 24 kwa sababu ya kushuka kiwango chake. cha mchezo(Sport - kwa Kihispania) Juventus wanapanga kukutana na winga Mwingereza Samuel Iling-Junior kujadili kuhusu kuongezwa kwa kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika 2025. (Tuttosport - in Italian). Tottenham wako tayari kujiunga na kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa Middlesbrough Hayden Hackney na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 pia akizivutia Manchester City, Manchester United na Liverpool. (Evening Standard) Imetafsiriwa na Yusuf Jumah
MICHEZO
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM WAKATI tukielekea katika msimu wa sikukuu, kasi ya upandaji bei za bidhaa za vyakula na nyingine, imeongezeka. Takwimu zinaonyesha mfumuko wa bei wa taifa, mwezi Novemba, mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 ilivyokuwa Oktoba, mwaka huu. Hii inamaanisha kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Novemba, mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa Oktoba, mwaka huu. Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Huduma za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari. Kwesigabo alisema fahirisi za bei nazo zimeongezeka hadi 104.32 Novemba, mwaka huu kutoka 99.54 Novemba, mwaka jana. Mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Novemba, mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 6.2 kutoka asilimia 6.0 ilivyokuwa Oktoba, mwaka huu. “Kuna vitu vingi vilivyochangia kupanda kwa mfumuko wa bei, ikiwamo bidhaa za vyakula, nyie ni mashahidi, mahindi yamepanda 15.6, samaki 23.7 nishati hasa mkaa umepanda hadi 22.1. “Kundi la vinywaji na vilevi tumbaku zimepanda na gharama za afya na ukarabati nyumbani hasa vifaa vyake vimepanda kidogo,” alisema. Alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 1.1. “Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 104.32 Novemba, mwaka huu kutoka 103.17 ilivyokuwa Oktoba, mwaka huu. Kuongezeka kwa fahirisi hizo kumechangiwa na ongezeko kwa bei ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula. “Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia ongezeko hilo ni mbogamboga kwa asilimia 7.4, unga wa ngano 2.4, unga wa muhogo asilimia 1.7, unga wa mahindi 1.5, mtama 1.5, dagaa wakavu 1.1 na mchele 1.0,” alisema. Kwesigabo alisema kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi, ni pamoja na mafuta ya petroli kwa asilimia 1.4, mkaa 1.4, kuni 1.0, viatu vya watoto 0.7, mafuta ya taa 0.6, mavazi ya kike 0.5, mavazi ya kiume 0.4, mavazi ya watoto 0.4, viatu vya kike 0.3 na mafuta ya dizeli 0.2. Alisema uwezo wa Sh 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa umefikia Sh 95.98 Novemba, mwaka huu ikilinganishwa na Sh 95.86 ilivyokuwa Oktoba, mwaka jana.
KITAIFA
LONDON, ENGLAND KOCHA wa Tottenham, Jose Mourinho ameendelea kusotea ushindi baada ya jana kulazimishwa suluhu na Watford katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa kwenye Uwanja wa Vicarage Road, Watford. Huo  ni mchezo wanne mfululizo kwa Tottenham kushindwa kuvuna pointi pointi tatu, mara mwisho kushinda ilikuwa Disemba 26 mwaka jana, ilipoichapa Brighton mabao 2-1. Baada ya mchezo huo, Tottenham ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Nowrich, ikachapwa bao 1-0 na Southampton, kabla ya kukubali kichapo kama hicho kutoka kwa Liverpool. Kabla ya mchezo huo, Mourinho alitoka kuiongoza Tottenham kuvuna ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Middlesbrough katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la FA. Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kushika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 31, baada ya kucheza michezo 23, pointi 30 nyuma ya Liverpool  inayoongoza katika msimamo, ikiwa imecheza michezo 21. Kikosi hicho kimekuwa na wakati mgumu wa kupata matokeo baada ya kuumia kwa mshambuliaji wao, Harry Kane. Hata hivyo, Watford watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia vema nafasi ya mkwaju wa penaltii, lakini nahodha wa kikosi hicho, Troy Deeney alipoteza  penaltii  hiyo iliyotokana na beki wa Tottenham, Jan Vertonghen kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari. Licha ya timu zote kufanya mabadiliko , ambapo Mourinho alimtoa Delle Alli na nafasi yake kuchukuliwa na Christian Eriksen,huku Gedson Fernandes akiingia kwa mara kwanza kuchukua nafasi ya Le Celso. Watford nayo ilimtoa Ismailia Sarr na nafasi yake kuchukuliwa na Ignacio Pussetto. Hadi dakika 90 za mtanange huo zinakamilika timu hizo zilitioka uwanjani zikigawana pointi moja kila mmoja baada ya kumaliza kwa sare ya 0-0.
MICHEZO
Akizungumzia katika warsha ya kitaifa ya wadau ya sekta ya kilimo inayofanyika Dar es Salaam yenye mada kuu ya “Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi, alisema ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya kilimo nchini.Samkyi alisema, ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo, Serikali iliamua kuanzisha TADB kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo.“Katika kutekeleza majukumu yetu, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Samkyi.Kwa mujibu wa Samkyi, benki hiyo inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani.Mikopo mingine ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamba hadi upatikanaji wa masoko, alisema. Aliongeza kuwa, wamejipanga kutoa mikopo ya ununuzi wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao, ikiwamo fedha za kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao.Akizungumzia mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo, Robert Pascal alisema, benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili, mikopo ya muda wa kati ya miaka miwili hadi mitano, na mikopo ya muda mrefu.Marejesho yanaeleweka kuwa ni kati ya miezi 60 hadi 180. Aliongeza kuwa, riba inayotozwa kwa upande wa mikopo ya muda mfupi ni asilimia saba mpaka nane kwa mwaka, ambayo mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani.
UCHUMI
Na Waandishi Wetu RAIS Dk. John Magufuli, amewakosoa baadhi ya watendaji wa Serikali waliombeza aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wakati wa sakata la kashfa ya Escrow. Rais Magufuli alisema Kafulila ameonesha uzalendo mkubwa ambao hauwezi kusahaulika katika historia ya Tanzania na kumpongeza kwa hatua yake ya kujitoa muhanga kutetea rasilimali za Watanzania. Akizungumza na wananchi wa Kata ya  Nguruka jana katika uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilaya ya Uvinza alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua ubadhirifu uliofanywa na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL. Alisema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwa sababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa. “Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea kumpongeza maisha yangu yote” alisema. Rais Magufuli alisema maendeleo hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea fedha za umma zilizo kuwa zikiibwa na mafisadi wachache na kujinufaisha wao wenyewe. “Ninajua Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu walikuita tumbili mimi najua  wewe sio tumbili, wao ndiyo matumbili. “Kafulila wewe hongera alisimamia wizi tuliokuwa tunafanyiziwa IPTL. Ni wizi wa ajabu na wengine wakamtisha kumpeleka mahakamani, wakamtukana weee! Na wengine wakamwita tumbili, sasa tumbili amefanya kazi kubwa kwa ajili ya Watanzania. “Tunahitaji wazalendo katika nchi hii, nchi hii ilikosa uzalendo ikawa na watu watafutaji, ukimchagua kiongozi anatafuta pesa yake badala ya kwenda kuongoza kwa ajili ya watu ambao ni masikini. “Tulikosa uzalendo wa utanzania, tukashindwa kumwogopa Mungu kwamba mali ni za muda tu baadae tutaziacha na kwenda kwenye shimo moja tu (kaburini) tutakapozikwa kule kaburini. Ninawaomba Watanzania tujenge uzalendo. “Kafulila wewe najua ni wa chama kingine, lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi ya nchi, kwa hiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza. Kitu ulichokifanya kwa taifa ni kikubwa naomba nikupongeze kwa hilo,” alisema. Alisema kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala siasa za uchochezi, hivyo atahakikisha kuwa wananchi hawateseki na wale ambao wameiba fedha za Serikali wanazirudisha bila kujali nyadhifa walizonazo ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo. Rais Magufuli aliwaahidi wananchi wa Nguruka kuwa atahakikisha anatatua kero ya maji na umeme katika kata yao, wakati katika suala la umeme atamtuma Waziri wa Nishati na Madini ili aweze kutatua tatizo hilo na kuwasaidia. Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Nguruka uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 2, ambao unatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu. Kafulila Akizungumza na MTANZANIA jana, Kafulila ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia (NCCR- Mageuzi), alimshukuru Rais Magufuli kwa kutambua kazi aliyokuwa akiifanya na sasa imeanza kuleta matokeo mazuri. “Kwa kweli nafarijika na inanipa moyo wa kizalendo zaidi ninapoona Rais anaunga mkono sakata la Escrow ambalo mimi ndo nililiibua wakati nikiwa mbunge japo nilipitia kwenye kipindi kigumu. “Nimefarijika sana mkuu wa nchi kuguswa na kutambua mchango wangu  katika vita hatari ya ufisadi wa IPTL / ESCROW, natambua kwenye vita hii hakuna chama. “Niliteseka sana ndani na nje ya jimbo kutokana na vita hii, zilifanyika kila hila na njama lakini Namshukuru Mungu kuwa upande wangu hata nimebaki hai,’’alieleza Kafulila. Aliendelea kueleza.  “Ukweli nimefarijika sana kuona mkuu wa nchi amelizungumzia jambo hili jimboni kwa wananchi walionipenda sana amezungumzia kwa hisia na uzito wa kutosha binafsi kwenye vita ya ufisadi nchini ninamuunga mkono Rais ,”alieleza Kafulila. Kafulila alimshauri Rais ajenge mfumo wa taasisi imara za uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka katika eneo hilo ili kuhakikisha vita hiyo inakuwa ya mafanikio makubwa. Msuguano   Kafulila alipoibua sakata hilo alipata upinzani mkubwa  ndani na nje ya Bunge, ambapo kulikuwa na mvutano mkali kati yake na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, wanasiasa na watendaji wengine wa Serikali waliohusishwa na sakata hilo.   Wakati Bunge likiwa linaendelea mwaka 2014 katika hali isiyokuwa ya kawaida  kuliibuka na mvutano mkali baada ya Kafulila kuomba mwongozo juu ya ESCROW na wizi uliofanyika. Werema wakati huo akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipotakiwa kutoa maelezo, kwanza alianza kushambulia vielelezo vya Kafulila kuwa ni vipeperushi visivyokuwa na maana hali hiyo ilipelekea Mbunge wa Ubungo wakati huo, John Mnyika (Chadema) kudai kuhusu utaratibu lakini mwenyekiti  wakati huo Mussa Zungu alipotezea. AG aliendelea  kumtaka Kafulila wakutane nje kama anamambo mengine ila bungeni kunautaratibu wake (walikuwa wakimwingilia wakati anazungumza wakionesha kutokubaliana naye). Majibishano yalipozidi Werema alipandwa na hasira alisema. “Kafulila wewe ni sawa na tumbili asiyeweza kuamua mambo ya msituni,” alisema na baadae Kafulila aliposimama naye alimwita Werema mwizi.   Kutokana na mvutano huo Werema alionesha dalili za kutaka kumfuata Kafulila akampige, lakini baadhi ya mawaziri walimzuia na kumsihi atulize hasira. Baada ya Bunge kuahirishwa wakiwa nje Jaji Werema alilalamika hadharani kuhusu Kafulila kumwita mwizi ndani ya Bunge na ndipo jaji huyo alipotaka kumvamia tena Kafulila. “Mimi nakwambia Kafulila nitakukata kichwa, we subiri tu labda ukiniomba msamaha” alisema Werema kwa sauti ya hasira. Kutokana na maneno hayo Kafulila naye alijibu. “Huwezi kunikata kichwa, huwezi, yaani uniue, hapana huwezi tena nakwambia huwezi,” alisema Kafulila. Ampongeza Sakaya Wakati huo huo akiwa mkoani Tabora, Rais Dk. Magufuli amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF), kwa kazi nzuri anayoifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo licha ya kuwa anatoka chama cha upinzani. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana wilayani Kaliua mkoani Tabora alipokua akizindua barabara ya Kaliua-Kazilabwa yenye urefu wa kilomita 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Chico ya China. Dk. Magufuli alisema kuwa ni heri kuwa na mbunge wa upinzani anayetekeleza mambo ya Chama Cha Mapinduzi  kuliko kuwa na mbunge wa CCM anayetekeleza ya upinzani kwani huo ni usaliti mkubwa kwa chama. “Nasema haya kwa sababu nafahamu hata wakati wa kampeni niliyashudia haya, ndiyo maana nasema ni bora kuwa na mbunge wa CUF, Chadema anayetekeleza mambo ya CCM kuliko wa CCM anayetekeleza mambo ya vyama vingine. “Najua mwili wake wote na akili yake yote ni CUF lakini damu yake ni CCM” alisema Dk. Magufuli. Akizunguzia ujenzi wa barabara hiyo Dk. Magufuli alisema imejengwa kwa fedha za Serikali bila mfadhili kuchangia, ambapo aliwataka wananchi kutozidisha uzito wa mizigo na kuchimba mchangan kado ya barabara ili idumu kwa muda mrefu. Aliutaka Wakala wa Barabara (Tanroads) kubomoa nyumba zote zitakazojengwa katika hifadhi ya barabara bila kutoa taarifa. “Kuna zoezi litaanza hivi karibuni la kubomoa nyumba ziliopo kando ya reli, hakikisheni zote zinaondoka, tunaaza kujenga reli ya kisasa lazima nyumba zote ziondoke kupisha ujenzi, najua wapo viongozi wengine wa CCM wanapitishapitisha maneno wa kubomoa anzeni na za hao wa CCM” alisema Dk, Magufuli. Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 56 umegharimu zaidi ya sh bilioni 61.9 ambazo ni pamoja na gharama za ujenzi, usimamizi na fidia kwa wananchi waliopisha utekelezaji wa mradi huo. Wakati huo huo Dk. Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Kaliua hadi Urambo yenye urefu wa kilomita 28 kwa kiwango cha lami ndani ya mwezi mmoja kutoka sasa. “Tafuteni mkandarasi kama hamjampata ndani ya mwezi mmoja apatikane msaini mkataba, pesa zipo hata mkitaka kesho njooni mchukue” alisema. Akizungumzia kero zinazowakabili wakulima wa tumbaku Dk. Magufuli alisema suala hilo amemwachia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alishughulikie na kisha kumpelekea taarifa. Alizitaka mamlaka husika kutotumia nguvu kubwa kuwaondoa waliovamia misitu badala yake wawaeleweshwe ili watafahamu madhara ya uharibifu wa mazingira. Kuhusu suala la mimba shuleni, Rais Magufuli aliwataka wanaume wanaowapatia wanafunzi ujauzito kujiandaa kwenda jela miaka 30 ili wakatumie nguvu zao kuzalisha wakiwa gerezani. Habari hii imeandaliwa na Editha Karlo, Kigoma, Leonard Mang’oha na Asha Bani, Dar Mwisho
KITAIFA
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (pichani), amesema alama anayotaka kuiacha katika wilaya hiyo siku akiondoka ni kupaisha kiwango cha elimu.Ndivyo pia anavyotaka akumbukwe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mussa Gama. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na timu ya waandishi wa habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), viongozi hao wawili wamekiri kwamba hali ya elimu katika wilaya hiyo haikuwa nzuri miaka michache iliyopita kwa maana ya watoto wengi kutofaulu vizuri.Jokate alisema kutokana na hali hiyo walichukua hatua ya kuanzisha kampeni ya ‘Tokomeza Zero Kisarawe’ aliyosema imezaa matunda kwa kuwa wanafunzi wameanza kufanya vizuri.“Wakati sisi tulijielekeza katika kutokomeza (daraja) sifuri, watoto wameipokea vizuri na sasa wamekuja na kauli mbiu ya kupata ‘A’ pekee,” alisema.Alisema, katika muktadha huo wa kupaisha elimu Kisarawe, wamefanikiwa kuongeza shule mbili mpya kwa ajili ya kidato cha tano na sita na hivyo kuwa shule tatu, moja ikiwa ni shule kongwe ya Minaki.Alisema mbali na ukarabati mkubwa wa miundombinu katika mashule ambao wamefanya na wanaendelea kufanya, wanatarajia pia kuongeza shule zingine mbili za kidato cha tano na sita.“Lakini lingine tunakwenda kuanzisha shule ya sekondari ya bweni kwa ajili ya wasichana pekee,” alisema na kuongeza kwamba anaamini shule hiyo itasaidia kuhamasisha wasichana wilayani humo kusoma.Alifafanua kwamba katika hii shule hiyo wanataka kuchukua wasichana wanaofanya vizuri na kuwawea shuleni huku wakiwaangalia vizuri.“Tunataka kutengeneza wasichana wa mfano kwa sababu nilivyokuja kuangalia jamii inakosa watu wa namna hiyo. Unaweza kumuuliza mtoto unatarajia kuwa nani ukiwa mkubwa, anakwambia ninataka kuwa mwali, au mtoto wa kiume anasema ninataka niwe dereva nikaishi mjini,” alisema.Katika kuhakikisha vijana wa Kisarawe pia wananufaika na ujio wa viwanda ambavyo vimeanza kubisha hodi wilayani humo,Jokate anasema wamekaribisha uongozi wa Chuo cha Cha Ufundi Stadi (VETA) kufungua tawi katika wilaya hiyo na kwamba tarehe 12/2/2019 waliwakabidhi eneo bure kwa ajili ya kujenga chuo hicho.
KITAIFA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwepo kwa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi wakuu, kunadhihirisha kwamba watendaji wa halmashauri, hawawatembelei wananchi katika maeneo yao na kutatua kero zinazowakabili.“Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekana wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao, sasa jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu hoja zote ni za ngazi ya halmashauri,” alisema Majaliwa.Aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora kwenye mkutano wa hadhara ,uliofanyika kwenye Viwanja vya Parking, ambako aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kutenga siku maalumu kwa ajili ya kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.Amesema serikali ya inayoongozwa na Rais John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia na kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.Amesema serikali inataka kuona wananchi wakihudumiwa, makatibu tawala wa wilaya wanatakiwa kujiridhisha kwenye halmashauri zao kama watumishi wa umma wanafanya kazi ipasavyo na iwapo hawaridhishwi wanatakiwa kutoa taarifa kwenye ngazi husika.“Serikali hii haimlindi mfanyakazi ambaye ni mbadhirifu, mwizi na ambaye hafanyi kazi kwa weledi au anayebagua wananchi eti kwa uwezo wake wa kifedha au rangi au dini yake au chama chake. Hivi vitu havipo katika serikali kila mwananchi aliyeko Nzega anatakiwa kuhudumiwa,” alisisitiza.Aliwaagiza pia wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya, wafuatilie na kujua kiasi cha fedha kinachopelekwa na serikali katika halmashauri zao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kujiridhisha kama zinatumika kama ilivyokusudiwa.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitoa siku 30 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega uwe umekamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari ya Magengati. Miaka minne iliyopita wananchi walijitolea kwa kujenga maboma na kuiachia halmashauri imalizie hatua zilizofuata.
KITAIFA
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM ALIYEKUWA Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya soka ya Yanga, Jerry Muro, ameliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuomba kupunguziwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja baada ya kutumikia nusu ya kifungo hicho. Kamati ya Maadili ya TFF, Julai mwaka jana ilimfungia Muro kutojihusisha na masuala ya soka pamoja na kumtoza faini ya shilingi milioni 3 baada ya kumkuta na hatia katika mashtaka mawili kati ya matatu, yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Wakili Wilson Ogunde. Makosa yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015, alipotakiwa kulipa faini ya Sh milioni 5 baada ya kufanya makosa. Shtaka lingine ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo timu yake ilifungwa bao 1-0. Kutokuwepo kwa Ofisa habari huyo mwenye maneno ya kinazi yaliyokua yanatia hamasa hasa pale alipojibizana na Ofisa mwenzake wa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, kumepoteza ladha na hamasa katika soka hali iliyomfanya swahiba wake huyo kuwa wa kwanza kuandika barua kwa TFF kumwombea msamaha na kumwondolea kifungo. Lakini pia kutokuwepo kwa Muro, kumeathiri kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa kutoka katika klabu ya Yanga, kwani licha ya mambo ya kibinadamu ya Muro alikuwa ni kati ya maofisa habari bora wanaokidhi haja za wapokeaji taarifa hizo. Akizungumza na MTANZANIA jana, Muro alisema barua hiyo aliwasilisha TFF Januari mbili mwaka huu, akieleza kuwa ni baada ya kushawishiwa na mashabiki na wadau wa soka baada ya kuona anahitajika kuongeza hamasa katika mchezo huo nchini. “Nimeandika barua kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa kuwa yeye ndiye mwenye dhamana kubwa na ambaye anaweza kutengua adhabu yangu kulingana na mamlaka aliyonayo katika shirikisho hilo. “Nimefanya hivyo baada ya mchezo wa soka kukosa hamasa kwa kipindi kirefu tangu nifungiwe na Kamati ya Maadili, mbali na swahiba wangu Haji Manara kuniombea msamaha, wadau, mashabiki na waandishi wa habari wameniomba pia kufanya hivyo ili niweze kutoka katika kifungo,” alisema Muro. Muro alisema kuwa ameandika barua hiyo pia ili arudi aweze kushirikiana na wadau wengine wa soka, katika kulisukuma gurudumu la mpira wa miguu nchini.
MICHEZO
KULWA MZEE -DAR ES SALAAM VIGOGO sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Halotel, Son Nguyen (46), wanaokabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara ya zaidi ya Sh bilioni 78, wanaendelea kusota rumande wakisubiri majibu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini. Washtakiwa hao ambao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Machi 27 mwaka huu, jana walisomewa kesi yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo upande wa Jamhuri ulidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba upelelezi haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi haujakamilika na akaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa utetezi, Benedict Ishabakaki akijibu alidai waliandika barua kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kumaliza kesi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) hivyo wanaendelea na mazungumzo na ofisi ya DPP. Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja hizo, alisema mazungumzo yakikamilika kabla ya tarehe ya kutajwa tena Julai 22 mwaka huu washtakiwa wataletwa kwa hati ya wito. Awali ilidaiwa kuwa washtakiwa hao  Aprili 21 mwaka huu waliandika barua kwa DPP kukiri makosa. Barua hiyo inadaiwa ilipokewa, majadiliano yalianza na yalikamilika kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuendelea na shauri hilo kutoka kwa DPP. Mbali na Nguyen washtakiwa wengine ni Nguyen Minh (40)  na Vu Tiep wote ni Mameneja wa Halotel, Ha Than (39) ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Halotel, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Nguyen Cong na Kampuni ya Viattel. Awali waliposomewa mashtaka Machi 27 mwaka huu mbele  ya Hakimu Simba, washtakiwa hao walidaiwa  kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia faida. Inadaiwa kati ya Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020  maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, kwa pamoja walitumia masafa ya redio bila kupata kibali kutoka TCRA. Pia inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu maeneo hayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Vietnam kwa pamoja walitengeneza mfumo ambao ulitumia huduma za mawasiliano zinazojulikana kama Virtual Private Network (VPN) kinyume na taratibu. Katika shtaka la nne, inadaiwa washtakiwa hao walikwepa kulipa kodi kwa TCRA kwa kutumia mitambo ya mawasiliano yaliyounganishwa Viettel Tanzania na Vietnam  kinyume na sheria. Inadaiwa Juni 8, 2017 na Machi 26, 2020 maeneo hayo kwa kutumia masafa ya redio bila kupata kibali cha TCRA walisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 75. Pia wanadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu kwa kutumia mitambo ya VPN waliisababishia TCRA hasara ya Sh bilioni 3.03. Katika shtaka la saba, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 3.03 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuongoza genge la uhalifu. Kampuni ya Viettel Tanzania inadaiwa kati ya Julai 7, 2016 na Machi 26, mwaka huu ilitakatisha Sh bilioni 3.03 na shtaka la tisa na 10, washtakiwa wote wanadaiwa kutakatisha Sh bilioni 75 wakati wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu.
UCHUMI
  Na Mwandishi Wetu-Serengeti WATU wa saba waliokuwa kwenye ndege moja aina ya Cessna Caravan yenye namba za usajili F 406  yenye uwezo wa kubeba abiria 12 mali ya Kampuni ya Air Excel. Ndege hiyo ilikuwa inatoka katika Uwanja wa Sasakwa Singita Grumeti, karibu na hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wamenusurika kifo, baada ya ndege hiyo kuanguka na kuteketea kwa moto. Tukio hilo lilitokea jana na kuthibitishwa na Meneja Uhusiano wa Singita Grumeti na Wadau wa Maendeleo Ami Hamidu Seki,  alisema ajalihiyo ilitokea juzi saa tano asubuhi, baada ya ndege hiyo kuruka na kuanguka nje kidogo mwa uwanja huo. Seki alisema wakati ndege hiyo ikiruka muda mfupi ilipata hitilafu na kuanguka katika eneo hilo, ambapo abria watano ambao wote ni watalii waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walinusurika kifo wakiwamo na marubani wawili wa ndege hiyo. “Tayari wataalamu wa anga wako hapa wanafanya utaratibu ili kujua chanzo cha ajali ya ndege hiyo ila siwezi kujua chanzo chake ni nini,” alisema Seki Alisema majeruhi wote wa ajali hiyo wamesafirishwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema siku ya ajali hiyo ndege ilikuwa na abiria watano ambao ni familia ya baba, mama na watoto watatu ambao wote ni raia wa Marekani. Aliwataja abiria waliokuwamo kuwa ni Greg Martin Perelman (60),  Susan Perelman (52), Sara Milessa Perelman (23), Danielle Jaffe Perelman (21) na Emma Stephanie Perelman (19) ambao wote wamenusurika kwenye ajali hiyo. Kwa upande wa marubani waliokuwa wakirusha ndege hiyo ni Mohammed Seleman akiwasaidiwa na Fahd Saleh ambao wote walikimbizwa Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya matibabu.
KITAIFA
  VATICAN CITY, VATICAN PAPA Francis amekosoa kiwango kidogo cha uzazi barani Ulaya na kutaka vijana wadogo wasaidiwe wajiandae kwa njia nzuri za wakati ujao katika jamii. “Ulaya ambayo inajibaini yenyewe kama jamii, ni chanzo cha maendeleo yake na dunia nzima,” Papa aliuambia mkutano wa ‘(Re) Thinking Europe’, mradi unaofadhiliwa na Baraza la Maaskofu wa Katoliki Ulaya (COMECE). “Ulaya, inaugua kwa kipindi kibaya cha ‘utasa’. Si tu kwa sababu Ulaya ina watoto wachache na wengi kunyimwa haki za kuzaliwa, bali pia kwa sababu kuna kushindwa kutengeneza utamaduni mzuri wanaohitaji vijana kukabiliana na wakati ujao.” Hii si mara ya kwanza Papa huyo raia wa Argentina kuonyesha kukerwa na kiwango kidogo cha uzazi barani humo kwani mwaka 2014, wakati akilihutubia Bunge la Ulaya aliueleza Umoja wa Ulaya kama ‘bibi mchovu’, ambaye hana uwezo tena wa kuzaa. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya, Frans Timmermans na Mtendaji Mkuu wa Bunge la Ulaya, Antonio Tajani. Walimsikia Papa Francis akisisitiza Ulaya si chombo cha takwimu au taasisi, bali kilichoundwa na watu, ambao hawapaswi kupukutishwa. Aidha alisisitiza kuwa viongozi wa Ulaya wana wajibu wa kuhamasisha Ulaya iliyo na jamii jumuishi, badala ya ile ya uwiano mbaya baina ya walio nacho na wasio nacho.
KIMATAIFA
Kwa mujibu wa ripoti ya Dunia ya mwaka 2015 kuhusu uwekezaji iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, ongezeko hilo linaifanya Tanzania iendelee kuwa kinara kwenye aina hiyo ya uwekezaji dhidi ya mataifa mengine yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.Hata hivyo, ripoti hiyo imebainisha kuwa dunia kwa ujumla imeporomoka kwenye aina hiyo ya uwekezaji kwa asilimia 16 hadi kufikia kiasi cha Sh trilioni 1.2 katika kipindi cha mwaka 2014 hali iliyosababishwa na mdororo wa uchumi wa dunia sambamba ukosefu wa sera rafiki katika uwekezaji miongoni mwa mataifa mengi duniani.Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika Dar es Salaam, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florens Turuka alisema kiasi cha uwekezaji huo hapa nchini kimekuwa zaidi kwa mwaka 2014.Alisema katika mwaka 2014 taifa lilifanikiwa kuvutia uwekezaji wenye thamani ya Sh milioni 2,142 ikilinganishwa na kiasi cha Sh milioni 2,131 mnamo mwaka 2013.“Kiasi hiki ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na kiwango cha chini zaidi cha Dola 640 kati ya mwaka 2005-2007 (kabla ya mgogoro wa uchumi). “Mafanikio haya yanatokana na uvumbuzi wa gesi hapa nchini na hivyo kuifanya nchi yetu kuendelea kuwa kinara kwenye aina hii ya uwekezaji ililinganishwa na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,’’ alisema.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Afrika Kusini ndio inayoongoza barani Afrika kwa aina hiyo ya uwekezaji kwa mwaka 2014 huku nafasi kama hiyo ikishikiliwa na China katika ngazi ya kidunia, ikifuatiwa na Hong Kong huku Marekani ikitajwa kushika nafasi ya tatu.Zaidi ripoti hiyo imebainisha kuwa katika mataifa kumi yanayofanya vizuri kwenye aina hiyo ya uwekezaji, nusu yanatoka kwenye kundi la mataifa yanayoendelea yakiwemo Brazil, Hong Kong, India na Singapore."Katika mazingira haya kuna haja ya kuimarisha sera za uwekezaji za kimataifa, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya uwekezaji ya kimataifa (IIA) huku pia suala la kodi za kimataifa likipewa kipaumbele,’’ alisema.Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji hapa nchini (TIC), Profesa Lucian Msambichaka pamoja na mambo mengine alikipongeza kituo hicho kwa jitihada zake katika kuvutia uwekezaji hapa nchini sambamba na kupunguza vikwazo katika uwekezaji huo.
UCHUMI
Na BADI MCHOMOLO NI siku tano sasa tangu nguli wa filamu na muziki nchini Marekani, Will Smith, apate majonzi kutokana na kumpoteza baba yake mzazi Willard Carroll Smith Sr. Imekuwa ni wiki ya majonzi kwa familia ya Smith, kutokana na marehemu kuacha maneno mazito wakati wa uhai wake kwenda kwa watoto wake pamoja na wajukuu. Smith Sr, alikuwa mpambanaji katika maisha yake japokuwa hakufanikiwa sana kama ilivyo kwa mtoto wake Will Smith ambaye ana jina kubwa katika tasnia ya filamu na muziki. Will Smith baada ya kifo cha baba yake ameweka wazi jinsi alivyolelewa na baba yake hadi anafanikiwa huku baba yake akiwa hana jina kubwa kama alivyo yeye. “Baba yangu hakuwa na jina kubwa sana duniani kama nilivyo mimi, lakini aliweza kupambana kwa ajili ya watoto wake waweze kuwa na majina makubwa na utajiri. “Kwa hatua hiyo alifanikiwa, lakini katika familia kuna maneno ambayo hatuwezi kuyasahau ambayo alikuwa anayaongea kwa ajili ya sisi kuweza kupigania maisha, aliwahi kusema, ‘Kama umekamilika kiakili, mwili, ni vizuri kupambana na maisha. ‘Maisha yapo vilevile, lakini kikubwa kinachotakiwa ili  ufanikiwe ni kupambana, kujiamini, kujitambua na kujituma, ipo siku nitaondoka duniani na muyaweke wazi maneno yangu hasa kwa familia yangu pamoja na wajukuu kwa ujumla. ‘Hakuna njia nyingine ya kuweza kufanikiwa kama utashindwa kuyafanya hayo, naamini kila mmoja akiweza kufanya hivyo ataishi kutokana na ndoto zake.’ “Ni maneno nisiyoyasahau kamwe kutoka kwa baba yangu,” anasema Will akimnukuu baba yake marehemu mzee Smith Sr. Will Smith ameweka wazi kuwa alikuwa anayatumia maneno hayo ambayo yalisemwa na baba yake na ndiyo maana amefanikiwa na anazidi kufanya vizuri katika mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kazi zake za muziki na filamu. “Kila siku baba yangu alikuwa ananiambia maneno hayo wakati nakua, niliweza kuyaweka kichwani na kuyafanyia kazi na ndiyo maana kwa sasa nipo hapa, nitaendelea kuyakumbuka maneno hayo kwa kuwa yamenifanya niwe hivi. “Maneno hayo yapo wazi hata kwa familia ya watoto wangu, nimewaambia vile ambavyo alikuwa ananiambia baba, hivyo na wao wanatakiwa kuwa na mafanikio makubwa ikiwezekana yawe zaidi yangu,” anasema Will Smith. Ni wazi kwamba watoto wa Smith, ambao ni Jaden na Willow, wameonekana kuwa na mafanikio makubwa  wakiwa na umri mdogo. Jaden kwa sasa anafanya muziki na filamu, aliweza kuwateka watu katika filamu ya baba yake inayojulikana kwa jina la The Pursuit of Happyness, huku Jaden akiwa na umri wa miaka 10, kabla ya kuachia filamu yake ambayo inajulikana kwa jina la Karate Kids aliyoiachia mwaka 2010. Kutokana na kujituma kwake, msanii huyo mwenye umri wa miaka 18, kwa sasa ana albamu mbili ambazo ni The Cool Cafe na This Is The Album. Kwa upande mwingine mtoto wa Smith ambaye ni wa kike mwenye umri wa miaka 16, Willow, amekuwa na mafanikio kutokana na kujitambua kwake, kupamba, kujituma na nidhamu, kwa sasa ni msanii wa muziki, filamu na mwanamitindo. Jaden na Willow, kupitia mitandao ya kijamii wamedai kuwa mafanikio waliyonayo ni kutokana na maneno ya babu yao ambayo aliyaacha kwa baba yao na sasa wanayafanyia kazi kama baba yao alivyofanya na kwamba  wataendelea kumkumbuka babu yao daima milele kwa kuwa huo ndiyo urithi walioachiwa.
BURUDANI
Hata hivyo, Mlandizi ndio yenye faida zaidi kutokana na kuwa na mchezo mmoja kibindoni, imecheza michezo mitatu na JKT imecheza minne.Mlandizi ina nafasi nzuri ya kuendelea kuongoza endapo leo itashinda mchezo wake dhidi ya Sisterz ya Kigoma iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi saba baada ya kucheza michezo mitatu.Mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Karume, Ilala inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kutokana na timu hizo kusheheni wachezaji nyota wa timu za taifa, Twiga Stars na ile ya vijana Tanzanite.Kwa upande wa timu ya Marsh Athlete ya Mwanza inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi nne baada ya kucheza michezo mitatu na Panama ya Iringa na Fair Play ya Tanga hazina pointi baada ya kucheza michezo mitatu. Katika mchezo uliochezwa juzi mchana, Sisterz iliifunga Panama mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.Mabao ya Sisterz yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa raia wa Kenya, Awour Owour dakika ya saba na mawili yakifungwa na Asha Juma dakika ya 79 na 82 na lile la Panama likiwekwa kimiani na Protosia Mbunda dakika 29.Kwenye mchezo wa jioni, JKT Queens iliifunga Marsh Athlete mabao 4-1 ambayo yalifungwa na Stumai Athuman dakika 12, Fatuma Swalehe dakika ya 20, Asha Rashid dakika 29 na Johari Shabani dakika ya 85 na lile la Marsh likifungwa na Veronika Matto dakika ya 45.Matokeo hayo yameifanya JKT kupanda nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi tisa huku ikiwa na mabao mengi ya kufunga kwani imefunga mabao 20 na kuruhusu mabao manne.Mchezo mwingine utakaochezwa leo ni kati ya Panama na Fair Play ambazo hazina pointi. Ligi hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza nchini.Ilianza kwa kushirikisha timu 12 zilizogawanywa makundi mawili yenye timu sita kila moja ambapo timu tatu za juu kutoka kila kundi ndizo zilizosonga mbele hatua ya sita bora na zinacheza kwa ligi ya mkondo mmoja, ambapo timu yenye poinbti nyingi ndio itakayotwaa ubingwa.
MICHEZO
* Kampuni za TTCL, DSTv zamwandalia zawadi Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi, atawaongoza Watanzania kumpokea mwanariadha, Alphonce Simbu, anayetarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo akitokea jijini Rio de Jeneiro, nchini Brazil alikoshiriki michezo ya Olimpiki. Mwanariadha huyo anarejea nchini akiwa amefanikiwa kuipa heshima kubwa Tanzania katika michezo ya Olimpiki upande wa mbio ndefu (marathon), zilizofanyika Jumapili iliyopita kwa kushika nafasi ya tano. Simbu alikimbia mbio za marathon akitumia muda wa saa 2:11:15, ikiwa ni sekunde 11 nyuma ya mshindi wa nne, Ghirmay Ghebreslassie na kushika nafasi hiyo ya juu ambayo haijawahi kushikwa na mwanariadha yeyote tangu mwaka 980, licha ya kukosa medali. Akizungumza na MTANZANIA jana Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka, alisema Simbu atawasili saa 7:00 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ndege shirika la Afrika Kusini na kupokelewa kishujaa. Aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kumpokea shujaa huyo aliyepeperusha vyema bendera ya taifa na kueleza kuwa wadau wanapaswa kutambua kwamba Simbu na wanariadha wengine wanahitaji kusaidiwa ili kupata  tunachotarajia. “Watu waamke sasa na kuiangalia riadha kwa namna ya kipekee, kwani RT tunaamini kuwa kama wanariadha wetu watapata maandalizi ya kutosha michezo ijayo tutapata medali,” alisema. Wakati mwanariadha huyo akisubiriwa kwa hamu kubwa, tayari Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na MultiChoice (DStv) zimetangaza kuwa zitampatia zawadi maalumu shujaa huyo kutokana na kuiwakilisha vyema nchi kwenye michezo ya Olimpiki. Mtaka pia aliliambia MTANZANIA kuwa, Simbu ameandaliwa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa ajili ya kumpongeza itakayofanyika Jumapili hii, jijini Dar es Salaam itakayoongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Rais huyo aliongeza kuwa RT inahitaji sapoti kubwa ya wadau katika maandalizi ya mashindano mengine ya kimataifa yakiwemo ya Nyika yatakayofanyika mwakani nchini Uganda na yale ya dunia yaliyopangwa kufanyika jijini London, Uingereza. Wakati huo huo, akizungumzia mafanikio ya mwanariadha huyo kwa upande wa Serikali, Nape alisema Simbu anastahili pongezi maalumu  kutokana na kuipeperusha vyema bendera ya taifa katika mbio za marathon Olimpiki. “Tukiendelea kuwa na utamaduni wa kutowapongeza wanamichezo wetu tutakuwa tunafanya vibaya, kwani Simbu amefanya vizuri kwa taifa lake. “Nawashauri wadau wa michezo nchini kwamba mbali na kutoa pongezi binafsi kutokana na juhudi za Simbu, pia tufanye jambo la kuwapongeza washiriki wote waliokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki kwa kuthamini mchango wa kila mmoja wao,” alisema Nape. Waziri huyo pia alitoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kumtumia Simbu kama balozi kwenye nembo ya biashara au taasisi zao, ili kumsaidia mwanariadha huyo kujiendeleza kimichezo na maisha yake kwa ujumla. Aidha, Nape alieleza kuwa kutokana na maisha duni ya wanamichezo, Serikali imepanga kuunda kamati ya kufanya tathmini ya maisha ya jumla ya wanamichezo na kubadili mfumo wa uendeshaji wa vyama vyao ili kuongeza tija katika kazi zao. Simbu atawasili nchini akiongozana na wanariadha wenzake, Saidi Makula na Fabiano Joseph, walioshiriki mbio ndefu.
MICHEZO
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Eliud Sanga ameahidi kwamba ndani ya miezi sita, mfuko huo utakuwa umelipa malimbikizo ya madai yote ya wastaafu. Madai hayo ni ya wafanyakazi waliokuwapo kwenye mifuko minne ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ambayo imeunganishwa na kuzaa PSSSF ndani ya kipindi chote cha mchakato wa takribani mwaka mmoja ya kuiunganisha mifuko hiyo.Sanga alitoa kauli hiyo jijini Dodoma jana wakati wa kuzindua Bodi ya Wakurungezi wa PSSSF, uliofanywa na Waziri wa Nchi, Ofi si ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama. Alisema baada ya kumaliza malimbikizo hayo, mfuko huo utakuwa ukilipa ambapo mdaiwa mafao atakuwa akienda kwenye ofi si za mfuko huo na kunywa chai wakati akisubiri mafao yake badala ya kusubiri kesho.Sanga alisema tayari mfuko huo, umeshaapisha watendaji wa ofi si za mikoa 26 Tanzania Bara na mmoja wa Visiwani. Alisema wiki ijayo wanaanza kazi ya mfuko huo, ikiwa ni pamoja na kuhakiki wanachama waliopo katika mikoa yao. Wastaafu sasa kucheka ndani ya miezi 6 INATOKA UK.1 Wanatakiwa kufahamu wastaafu wote tangu mwezi Julai mwaka huu na kuwaandalia mafunzo ya kustaafu kabla hawajastaafu ili kuhakikisha hawafi mapema au hawafi kabisa.Akizindua Bodi hiyo, Jenista aliwataka watendaji wa mfuko huo, kutofumbia macho mfanyakazi yoyote atakayeshindwa kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma nzuri kwa wadai wa mafao hayo mahali popote. Aliwataka watendaji hao waangalie miradi zaidi ya 16, iliyokuwa ikitekelezwa na mifuko minne iliyounganishwa na kuhakikisha kama inafaa na kama ina manufaa kwa taifa, basi waiendeleze au kuifufua. Pia aliwataka wafanye kazi kuongeza wanachama, kwani mifuko hiyo kwa umoja ilikuwa na wanachama asilimia 11 ya wafanyakazi wote, hivyo lazima wafi kie malengo ya kuwa na wanachama asilimia 40 ifi kapo 2025.Alimtaka Mkurugenzi Mkuu kuhakikisha anatekeleza ahadi yake ya kwamba ifi kapo F ebruari mwakani, wafanyakazi wastaafu watakuwa wanafi ka ofi si za mfuko na kupewa chai wanywe wakati wanasubiri mafao yao badala ya njoo kesho njoo kesho. Akizungumza Mwenyekiti wa Bodi, Mussa Iyombe alisema bodi ni nzuri na wamejipanga kuhakikisha kero zilizokuwa zikiwakumba wastaafu, zimalizika ndani ya kipindi cha miezi sita, kama Mkurugenzi Mkuu, Sanga alivyoahidi.Iyombe ambaye ni Katibu Mkuu Tamisemi, alisema wanataka kuondoa kero ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikililalamikiwa na wastaafu, ambao wamekuwa wakifuata mafao yao. Alisisitiza kwamba ndani ya kipindi kifupi, kero hizo zitakuwa historia. Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Tumaini Nyamhokya alisema wao ndio walikuwa wapiganiaji wa mifuko hiyo kuunganishwa. Lakini, alisema halikuwa jambo rahisi kuunganisha mifuko na hatimaye jana kuzinduliwa bodi hiyo.Nyamhokya aliwataka watendaji wa mfuko huo, kuweka kipaumbele kwa wanaostaafu kulipwa mafao yao kwa lengo la kuanzisha shughuli mbalimbali katika maisha yao. Akitoa neno la shukrani, Rais wa Chama Cha Walimu (CWT), Leah Ulaya alisema wapo tayari kufanya kazi kwa weledi. Aliahidi kuwa hawatamuangusha waziri, wizara na wanachama wa mfuko huo. Leah ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo, alisema wamejipanga kumshauri waziri na watahakikisha wanamshauri vizuri. Kwa sasa kutakuwa na mifuko minne, ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa ajili ya sekta binafsi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa F idia Kwa Wafanyakazi (WCF) na PSSSF.
KITAIFA
Meneja wa nyota wa Bongo fleva Sallam Sk amesema hatonyoa wakati huu ambao atakuwa Karantini. Salla ambaye leo hii anafikisha siku 5 akiwa Karantini baada ya kukutwa na Ugonjwa wa Virusi vya Corona baada ya kurejea kutoka ulaya. Kutipia ukurasa wake wa instagram leo Machi 24 Sallam pamoja na kusema kuwa hatonyoa ameongeza kuwa anaendelea vizuri na zimebakia siku chache kuchukua vipimo vingine vya kujua mwenendo wake. Katika picha aliyoposti akiwa na mtoto wake wa kiume amesema anawashukuru watu wote kwa dua zao na madaktari ambao wako bega kwa bega naye wakati huu. Alhamdullilah naendelea vizuri zimebakia siku chache kuweza kuchukua vipimo tena kuona kama nipo negative au positive. Nashukuru kwa dua zenu wote asanteni sana. Na pia niwashukru madaktari wote waliopo bega kwa bega na sisi tuliopo kwenye kituo. 🙏🏽🙏🏽🙏🏽 A post shared by Sallam SK (@sallam_sk) on Mar 24, 2020 at 4:55am PDT
BURUDANI
Kufuatia kuenea kwa hofu kubwa juu ya kuendelea kuhudumu kama Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Simba baada ya nafasi yake kutangazwa miongozi mwa nafasi za kazi katika tangazo lililotolewa jana, Haji Manara amewaondoa hofu mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba kuwa bado ataendelea kuwepo sana klabuni hapo hata kama ni kwenye nafasi nyingine Manara ambaye amekuwa maarfu sana kutokana na mbwembwe zake nyingi katika kuisemea Simba katika muktadha mbalimbali, amesema kutangazwa kwa nafasi hiyo si jambo la ajabu kwani kwa sasa kila nafasi ya kuajiriwa klabuni hapo ni lazima itangazwe kutokana klabu hiyo kujiendesha kisasa. Amesema kwamba wale wote wanaopenda kuona akiondoka Simba, basi wasitarajie hilo kwani bado yupo sana huku akiainisha kwamba muda sio mrefu atataja nafasi mpya ambayo atakuwa akihudumu. “Huu ni utaratibu sahihi na ndio hufuatwa na taasisi nyingi zilizobadisha muundo, yes Simba kwa sasa ni Simba SC Limited, so kutangaza upya nafasi za ajira kwa wafanyakazi ni jambo correct kabisa!!Mnaohoji uwepo wangu klabuni, yes nipo sana inshaallah, ondoeni hofu na wale wanaodhani kutakuwa na relief labda wakidhani sipo, big NO nipo na mtaambiwa kwa nafasi gani !! This is Simba,” ameandika Haji Manara kupitia Instagram yake. Simba wametangaza nafasi mbalimbali za kazi jana ikiwemo ya Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O), ambapo dhamira yao ni kuona klabu hiyo inapiga hatua ya mbali zaidi Afrika na duniani hasa baada ya kubadili rasmi mfumo wao wa uendeshaji.     Huu ni utaratibu sahihi na ndio hufuatwa na taasisi nyingi zilizobadisha muundo, Yes Simba kwa sasa ni Simba SC Limited,so kutangaza upya nafasi za ajira kwa wafanyakazi ni jambo correct kabisa!! Mnaohoji uwepo wangu klabuni,Yes nipo sana inshaallah,ondoeni hofu na wale wanaodhani kutakuwa na relief labda wakidhani sipo,Big NO nipo na mtaambiwa kwa nafasi gani !! This is Simba 💪 A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on Jun 28, 2019 at 8:28am PDT
MICHEZO
ILI kila mmiliki wa eneo aweze kulipa kodi na serikali kuingiza mapato pamoja na kurahisisha mipango miji, serikali imeanzisha usajili wa viwanja nchini. Kutokana na hatua hiyo, viwanja milioni 1.5 viko hatarini kuchukuliwa na serikali iwapo wamiliki wake hawatavisajili katika miezi mitatu ijayo.Mkuu wa kitengo cha ardhi katika Mamlaka ya Usimamizi wa Ardhi Rwanda, Grace Nishimwe, ameliambia gazeti la The New Times kuwa, baadhi ya maeneo hayo yanamilikiwa na watu waliodanganya umiliki wake.Kwa sasa mikakati ya usajili wa ardhi ulioanzishwa miaka 10 iliyopita umekuwa ukipunguza migogoro ya ardhi, hususan katika maeneo ya vijijini na sasa sheria mpya imewapa haki sawa wanawake na wanaume kumiliki ardhi nchini humo.Alisema ingawa serikali itachukua viwanja ambavyo havijasajiliwa ndani ya miezi mitatu, lakini wamiliki halali wanaweza kuthibitisha umiliki baada ya kuwasilisha nakala zinazoonesha umiliki wao baada ya kipindi hicho.“Sheria inaruhusu serikali kuchukua umiliki wa ardhi isiyosajiliwa hivyo wamiliki wa vipande hivyo vya ardhi wanatakiwa kwenda kwa serikali za mitaa kutafuta ufumbuzi wa suala hilo mapema,” alisema.Alisema zaidi ya viwanja 18,000 vilivyosajiliwa vina migogoro na wanaogombea umiliki wake wanatakiwa kuwasilisha nakala ndani ya mwezi mmoja ili kupeleka kesi mahakamani.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Matumizi ya Ardhi, Esperance Mukamana, alisema usajili wa ardhi umeongeza makusanyo ya kodi. Mamlaka ya Mapato Rwanda (RRA) nayo imesema kodi imepanda kwa zaidi ya faranga bilioni 67 katika mwaka huu wa fedha kutoka faranga bilioni 61.5 katika mwaka wa fedha 2017/18.
KITAIFA
Hivi karibu Mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji almaarufu ‘Mo’ alikubwa na sintofahamu kutokana na inavyosemakana kukosekana kwa maelewanao miongoni mwa viongozi wa klabu hiyo hali iliyosababisha kuposti maneno yasiyoashiria furaha kwa upande wake. Lakini leo, mmiliki huyo wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited ameonekana kuwa na aina fulani ya amani kutokana na aina ya ujumbe alioandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Mohemmed Dewji ameandika hivi: “Hate no one no matter how much they have wronged you. Live humbly no matter how wealthy you have become, think positively no matter how hard life is. Give much even if you have been given a little, and forgive who has wronged you”- “Usimchukie yoyote bila kujali wamekukosea kwa kiasi gani. Ishi kwa upendo bila kujali utajiri ulionao, kuwa na fikra chanya bila kujali ugumu wa maisha ulivyo. Toa zaidi hata kama ulipewa kidogo na wasamehe waliokukosea”, ameandika Mohammed Dewji kupitia ukurasa wake wa Instagram.” “Hate no one no matter how much they have wronged you. Live humbly no matter how wealthy you have become, think positively no matter how hard life is. Give much even if you have been given a little, and forgive who has wronged you”- Imam Ali (A.S) A post shared by Mohammed Dewji (@moodewji) on Jul 14, 2019 at 12:52am PDT
MICHEZO
Na MWANDISHI WETU-DODOMA WAZIRI Mkuu na Makamu wa Rais wa zamani, John Malecela, amefanya ibada ya shukrani na kueleza machungu aliyopitia, ikiwemo kufanyiwa upasuaji mara kadhaa wa mwili wake. Kutokana na hali hiyo, alisema haamini ni kwa namna gani Mungu alivyomtendea miujiza ikiwemo ya kuendelea kuwa hai hadi sasa. Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa baada ya ibada ya shukrani kwa Mungu, huku akiongozana na familia yake, wabunge, wazee wa Dodoma na watu maarufu kwa ajili ya kushukuru kanisani kutokana na afya yake kuimarika. Alisema alipitia katika shida kubwa ambayo awali hakuwa anaijua, lakini ghafla alijikuta akipasuliwa mwili wake na kufumuliwa zaidi ili kuurudisha katika hali yake ya awali. “Kwanza naamini hakuna binadamu ambaye aliwahi kufumuliwa mwili wake kama ilivyotokea kwangu mimi kati ya wote waliojaa ndani ya kanisa hili, nasema ni Mungu pekee tu na wala si kitu kingine,” alisema Malecela. Alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kila hali kwani ndiye anayewezesha kila jambo na bila mkono wake hali ingekuwa ni ngumu zaidi kwake. Akizungumza wakati wa kutoa neno ya shukrani kanisani, mtoto mkubwa wa Malecela, Dk. Mwele Malecela, alisema mwanasiasa huyo mkongwe alipitia katika vipindi vigumu zaidi katika afya yake. Alisema baba yake alifanyiwa upasuaji mkubwa mara tatu; tatizo la moyo alifanyiwa upasuaji mara mbili na kisha akapasuliwa tena kwa tatizo la mgongo. “Yote hayo yalifanyika katika kipindi cha miaka michache, leo (jana) hii tunapomuona mzee anaimarika na kuwa na afya njema, kwetu sisi ni jambo la kushukuru sana kwa Mungu na ndiyo maana tumeona tuje tuseme asante Mungu,” alisema Dk. Mwele. Awali Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk. Dickson Chilongani, alisema hakuna mtu aliye mkubwa mbele za Mungu na wala hakuna mwenye cheo cha kumshinda Mungu. Alisema jambo kubwa ni kwa kila mmoja kuendelea kujishusha na kunyenyekea mbele za Mungu wakati wote ili Mungu awe zaidi ya wote maana ndiye mgawaji mwema. Kutokana na hali hiyo, Askofu huyo aliwataka Watanzania kuendelea kuilinda amani ya Taifa ili iweze kudumu na kuliepusha kuingia katika machafuko kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani. Kuhusu Malecela, alimshukuru kwa uamuzi wake pamoja na michango mikubwa aliyotoa ikiwemo kusaidia ujenzi wa Kanisa katika Kijiji cha Chinangali II, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya shukrani zake mbele za Mungu. Pamoja na hali hiyo, jana aliongoza utoaji wa sadaka kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya utumishi katika kanisa hilo lililoko kijijini hapo.
KITAIFA
Baada ya msafara wa timu hiyo uliokuwa ukiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ahmed Mgoyi kufika uwanjani hapo saa sita usiku, ulipigwa na mshangao baada ya kukuta gari moja aina ya Coaster huku kukiwa na watu zaidi ya 20.“Mbona wametupa gari hili hawa? Sisi kwetu tuliwapa mabasi matatu nyie kwa nini mmetupa basi moja, halitutoshi hili, kaleteni jingine,” alisema Haroub akiwaambia baadhi ya maofisa wa Fufa waliofika kuipokea timu. “Kama hawaleti gari lingine sisi hatuondoki hapa, tupo wengi hatutoshi humu,” alisema.Hata hivyo baada ya majadiliano kati ya Mgoyi na maofisa hao wa Fufa lililetwa gari jingine na safari ya kwenda Kampala ikaanza, ambapo msafara huo ulifika saa saba usiku.Stars ipo mjini hapa kucheza na timu ya taifa ya Uganda mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) itakayochezwa leo kwenye uwanja wa Nakivubo.Katika mechi hiyo, Stars inahitaji ushindi wa zaidi ya mabao matatu ili kusonga mbele baada ya kufungwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Zanzibar wiki mbili zilizopita.Wachezaji walio kwenye msafara wa timu hiyo ni Ally Mustafa, Mudathir Khamis, Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla, Saimon Msuva, Deus Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid Mandawa, John Bocco na Ame Ally.
MICHEZO
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM KLABU ya soka ya Simba imeingia rasmi kwenye mfumo wa uendeshaji wa kutumia hisa na kuachana na ule wa awali wa uanachama uliodumu kwa miaka mingi. Mabadiliko hayo ambayo mchakato wake ulianza mwaka jana, yalipitishwa jana na wanachama wa klabu hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kuanza kutumika kwa mfumo huo kunatoa fursa kwa mfanyabiashara maarufu na mwanachama wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kuwa mmiliki wa klabu hiyo baada ya kuweka wazi nia yake ya kununua hisa zenye thamani ya Sh bilioni 20. Katika mkutano huo, wanachama 1,216 kati ya 1,217 walipiga kura ya kuunga mkono mabadiliko hayo ambayo yanafungua historia mpya ya klabu hiyo yenye makao yake makuu Mtaa wa  Msimbazi, jijini Dar es Salaam. Muundo huo umegawanywa katika sehemu kuu tatu, wapenzi, wanachama na wawekezaji ambao kwa pamoja watatengeneza kampuni inayofahamika kama Simba Sport Club Limited. Wawekezaji kwenye muundo huo watakuwa na fursa ya kumiliki asilimia 50 ya hisa za umiliki wa klabu hiyo, huku asimilia 50 nyingine ikimilikiwa na wanachama na wapenzi. Katika muundo huo mpya, wawekezaji watatakiwa kununua hisa zenye thamani ya Sh bilioni 20. Muundo wa kiutawala ndani ya mfumo huo utakuwa na bodi ya wakurugenzi itakayoongozwa na mwenyekiti pamoja na wajumbe saba ambao ni wanachama wa Simba na wawekezaji. Ndani ya muundo huo pia kutakuwa na bodi ya ushauri ambayo itaongozwa na wazee wa klabu hiyo na nyingine itakayoongozwa na wachezaji wa zamani wa Simba. Bodi nyingine ya ushauri ni ile ya kibiashara itakayohusisha wanachama wa klabu hiyo wenye taaluma hiyo ili kuunda utawala wa uendeshaji. Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alisema mabadiliko hayo yanatokana na nia ya dhati ya klabu hiyo kutaka kuwa klabu bora Afrika na yenye uwezo mkubwa kiuchumi. “Simba inahitaji kuwa klabu bora Afrika, lakini kwa mfumo tuliokuwa nao awali ilikuwa vigumu kufikia malengo. “Lengo la Simba ni kuwa na uwekezaji ambao klabu itakuwa na uwezo wa kibajeti, miundombinu ya kisasa, shule za mpira na kumiliki uwanja wake,” alisema. Aliongeza: “Kwa wanachama, kwa kuwa wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha, wao wanatakiwa kuchangia Sh bilioni 4 tu ambazo ni sawa na asilimia 10, huku asilimia 40 ambazo ni sawa na Sh bilioni 16 zitawekwa kando kwa kuangalia uwezo wao hapo baadaye. “Suala la nani atakuwa mwekezaji itaundwa kamati ya wataalamu ili kuandaa tenda na baada ya watu kujitokeza, kamati ya utendaji itaandaa mkutano kama huu na kuwaita wanachama ili kuwaeleza waliojitokeza ni akina nani. “Wawekezaji kwenye muundo huo wanaweza kuwa wawili, watatu au vinginevyo na mgawanyo wa hisa kwa maana ya thamani na asilimia ndiyo utakaohusika.” Naye mgeni rasmi katika mkutano huo, Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hamisi Kigangwalla, alisema Serikali inaunga mkono mabadiliko hayo kwa kuwa yana tija katika maendeleo ya soka nchini. “Serikali itafaidika kadiri klabu zinavyorasimishwa na kuongeza kipato ambacho kitasaidia kulipa kodi. “Serikali inaelewa changamoto zote na tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinachomiliki kwa asilimia kubwa viwanja nchini, kimeanza kufanya maboresho na kuimarisha viwanja hivyo,” alisema Kigwangalla.
MICHEZO
LOS ANGELES, Marekani HABARI mbaya kwa mashabiki wa mrembo wa vipindi vya trelevisheni anayetokea familia ya Kardashian, Kylie Jenner, ni kwamba juzi mtoto wa binti huyo alikimbizwa hospitali. Hata hivyo, Kylie mwenye umri wa miaka 21 amedai kuwa Stormi mwenye umri wa miezi 15 alifikishwa kwa madaktari akisumbuliwa na wa mzio (allergy) na amesharejea nyumbani. Kuwataarifu mashabiki wake, Kylie aliposti picha katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha dogo huyo akiwa amelala. “Nilitumia siku nzima nikiwa hospitali na mtoto wangu. Alikuwa na tatizo la mzio lakini yuko sawa kwa asilimia 100 na sasa tuko nyumbani,” alisema bibiye huyo.
BURUDANI
Mwandishi wetu, Tanga MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itawasaidia wafanyabiashara wanaokwepa kodi kuacha vitendo hivyo vya kuikosesha Serikali mapato. Shigela ameyasema hayo ofisini kwake alipotembelewa na maafisa wa TRAwanaofanya kampeni hiyo mkoani humo ambayo imelenga kuwaelimishawafanyabiashara kuhusu masuala ya kodi ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.  Amesema kuwa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikwepa kulipa kodi pengine kwa kujua au kutokua, jambo ambalo linahitaji elimu ya uelewa ili kila mwananchi afahamu wajibu wake kwenye ulipaji wa kodi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Akiizungumzia kampeni hiyo, Shigela ameipongeza TRA kwa kuendesha zoezi hilo katika mikoa mbalimbali na kusema litaongeza ukusanyaji wa mapato baada ya wafanyabiashara kuelimishwa na kufahamu kuwa maendeleo ya nchi yanasababishwa na ulipaji wa kodi kwa ajili ya kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, barabara, umeme na maji. Shigela amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari bila kusubiri kubugudhiwa na serikali, huku akieleza kuwa serikali itaendelea kupambana na wakwepa kodi wanaoingiza bidhaa za magendo nchini kwa kupitia bandari bubu zilizopo kandokando ya Bahari ya Hindi. “Nchi yoyote haiwezi kupiga hatua ya maendeleo bila wananchi wake kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa sababu kodi ndio kila kitu huwezi kujenga barabara kama wafanyabiashara hawataki kulipa kodi, huwezi kuimarisha huduma za afya kama hakuna kodi na pia huwezi kuimarisha mifumo ya elimu bila kodi,” alisema Shigela. Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Tanga, Specioza Owure amesema kuwa, maafisa hao wa TRA wanaofanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi, watafika maeneo mbalimbali yenye wafanyabiashara katika mkoa wa Tanga na watawaelimisha kuhusu umuhimu wa kodi na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati. “Maafisa hawa wanatumia jitihada zote kuwaelimisha wafanyabiashara, tunafanya hivi ili kila mmoja afahamu wajibu wake wa kulipa kodi sambamba na kusogeza huduma za TRA karibu na wateja,” alisema Owure.Kampeni ya elimu kwa mlipakodi mkoani Tanga inatarajia kumalizika Juni 30, 2020 ambapo lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, kusikiliza maoni na changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati.
UCHUMI