input
stringlengths
5
25.1k
label
stringclasses
6 values
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage, amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanazingatia maadili na kuepuka dosari ambazo zinaweza kuathiri Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, huku akisema wapiga kura walio kwenye daftari ni milioni 29. Akifungua kikao kazi cha wasimamizi wa uchaguzi jijini Dodoma juzi, aliwataka kuzingatia sheria, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya tume na watakaokiuka watakuwa wametenda kosa la jina kwa mujibu wa kifungu 98 cha Sheria ya Uchaguzi. Pia alisema pamoja na wajibu wao wa kusimamia uchaguzi, wanatakiwa kujua jiografia, mazingia na maeneo wanayosimamia na wana wajibu wa kusimamia watendaji wa uchaguzi waliopo chini yao ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na umakini. “Wasimamizi wa uchaguzi hii ni nafasi ya kubadilishana na kupeana uzoefu wa utekelezaji shughuli za uchaguzi ili kuhakikisha tunaepusha dosari ambazo zinaweza kujitokeza na kuathiri shughuli za uchaguzi,” alisema Kaijage. Kaijage alisema tume ilianza kujiandaa kwa uchaguzi huo siku nyingi kwa kufanya shughuli nyingi zikiwemo za kukamilisha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ambao umefanyika mara mbili. Awamu ya kwanza ilifanyika Julai 18, 2019 hadi Februari 23, 2020 na awamu ya pili Aprili 17 hadi Mei 04, 2020. “Awamu ya pili ya uboreshaji ilifanyika pamoja na uwekezaji wazi wa daftari la awamu ya kwanza katika vituo 37,814 vilivyotumika katika uboreshaji awamu ya kwanza,” alisema. Kaijage alisema uwekaji wazi wa daftari awamu ya pili ulifanyika Juni 17-20, mwaka huu ambapo daftari la wapigakura lilibandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uandikishaji awamu ya kwanza. Kaijage alisema katika uboreshaji wa daftari hilo awamu zote mbili, waliandikisha wapigakura wapya 7,326,552 sawa na asilimia 31.63 ya wapigakura 23,161,440 walioandikishwa mwaka 2015. Aidha, wapiga kura 3,548,846 walioboreshewa taarifa zao na wapigakura 30,487 waliondolewa kwenye daftari kwa kukosa sifa na hivyo daftari lina wapigakura takaribani milioni 29. Kaijange aliwataka wasimamizi hao kuwa makini na matumizi ya fedha zinazotumwa kwao kwa kuzingatia sheria za fedha za umma, ya manunuzi ya umma, ya uchaguzi na maelekezo yanayotolewa na tume wakati wa matumizi ya fedha hizo ambazo awamu ya kwanza zimeshatumwa. Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, hakuna marekebisho ya sheria za uchaguzi, lakini tume imefanya marekebisho kanuni za uchaguzi wa rais na wabunge na kanuni za uchaguzi wa serikali za mtaa zote za mwaka huu na maboresho ya maelekezo kwa ajili ya wadau na watendaji yamekamilika. Kaijage alisema tume kwa kushirikiana na Serikali na vyama vya siasa iliandaa maadili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ambayo yalisainiwa Mei 27, 2020 yameainisha mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na tume, vyama na serikali. Hivyo wasimamizi wa uchaguzi ambao watakuwa wenyeviti wa kamati za maadili katika majimbo wanayosimamia, wayasome na kuyaelewa vizuri ili kuyasimamia vizuri. Kaijage alisema kanuni zilizorekebishwa zinaelekeza uteuzi wa wagombea, upigaji kura na mchakato mzima wa uchaguzi na hivyo watendaji wa tume wanatakiwa wakato wote kuwepo katika maeneo ya kazi, kwani uzoefu unaonesha  wamekuwa wakikiuka maadili kwa kutokaa vitutoni na hivyo kusababisha malalamiko. Tume imeshanunua baadhi ya vifaa vya uchaguzi pamoja na kuchapisha fomu, sheria za uchaguzi, kanuni na maelekezo na baadhi vimeshaanza kupokelewa bohari kuu ya tume, hivyo vikisambazwa kwao wasimamizi mnatakiwa kuvipokea, kuvihifadhi katika hali ya usalama. Tayari tume imeshatoa vibali 97 kwa ajili ya watazamajini wa uchaguzi mkuu wa ndani na tayari imewasilisha mwaliko kwa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki kuruhusu watazamaji wa kimataifa kuja nchini kuangalia uchaguzi huo. Pia Tume imetoa vibali kwa asali 245 Tanzania Bara na asasi saba za kiraia Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu kwa wapigakura wakati wa uchaguzi, hivyo wasimamizi wanatakiwa kuhakikisha elimu inayotolewa katika maeneo yao inazingatia mwongozo wa utoaji elimu uliotolewa na tume. Pia aliwataka wasimamizi hao kuhakikisha mawakala wa vyama wanaruhusiwa kuwepo vituoni, kwani kitendo hicho kioongeza uwazi lakini watakuwa na vitambulisho vinavyotambulisha. Alisema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo vituoni jambo ambalo linasahdia kudhihirisha uwazi katika uchaguzi huo, ni wajibu wao kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho na wakati wakiangalia utekelezwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi. Katika kufanikisha uchaguzi huo tume imeteua watendaji wake wakiwemo waratibu 28,  wasimamizi wa uchaguzi 194, wasimamizi wasaidizi wa majimbo 742 na wasimamizi wasaizidi katika kata 7,912.
KITAIFA
Anna Potinus Rais Dk. John Magufuli amewataka wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kigaidi hapa nchini kuacha mara moja kwani wamekuwa wakipoteza amani ya nchi na kuwafanya Watanzania kuishi kwa wasiwasi. Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 10, alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mpanda hadi Tabora na kuzindua kituo kipya cha mabasi kilichopewa jina la Waziri Mkuu msataafu, Mizengo Pinda. “Katika mkoa huu kuna wenzetu kutoka Burundi na maeneo mbalimbali ambao tuliwakaribisha katika nchi yetu kama Tanzania ilivyo na ukarimu kwa watu kutoka nje lakini pamejitokeza baadhi ya changamoto watu wako kambini baadhi yao wakawa wanashiriki katika masuala ya ujambazi kulifanya eneo hili lisiwe salama kwasababu ya ukarimu wetu,” “Hauwezi ukakaribishwa kwasababu ya shida ulizozitengeneza huko kwenu uje uzilete hapa hivyo nitoe wito kwa ndugu zetu ambao walikuja hapa tukawapokea kwa upole wasije wakalifanya eneo hili likawa la hatari,” “Hamuwezi mkakaribishwa halafu baadhi yenu wanashiriki kuwaonea raia wema na saa nyingine kupitisha silaha kupitia Ziwa Tanganyika ninawaomba waache na kutokana na mienendo hiyo ambayo haifurahishi tumeona tulichunguze hili suala la kuwapatia uraia watoto wao kwasababu wanaweza wakaleta watu wakasema ni watoto wao kumbe ni majambazi kwani wamekuwa na tabia ya kukaribisha wenzao wiki hii yuko hapa wiki inyokuja yuko Burundi na kadhalika,” Aidha amewataka Watanzania kuacha kuishi na raia hao wa kigeni kwa misingi kwamba wanawasaidia katika kazi kwasababu wao wanakuwa wanawasoma halafu usiku wanakuja, Tanzania ni nchi ya amani na palipo na amani kunakuwa na kila kitu,” amesema Rais Magufuli.
KITAIFA
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mussa Azzan Zungu amewataka wataalamu wa mazingira kufanya tathmini ya mazingira katika maeneo ya bahari kupata dawa ya madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi. Zungu alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipofanya ziara katika eneo la bahari lenye mgogoro kati ya Motison wanaomiliki hoteli ya Whitesand na wamiliki wa Hoteli ya Wellworth Kunduchi. Motison wanatuhumiwa na wamiliki wa Wellworth kwa kujenga ukuta baharini hatua iliyosababisha maji kujaa hotelini kwao. Akizungumza katika eneo hilo akiwa ameambatana na watendaji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Zungu aliwataka kuwa wavumilivu kusubiria wataalamu wa sayansi ya bahari wafanyie kazi na kutoa majibu wiki hii. Hata hivyo, Zungu aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwani ndio sababu kubwa ya maji ya bahari kujaa isivyo kawaida na kuingia katika maeneo yao. “Leo tunatazama mgogoro wa watu wawili, kesho tutakuwa na wa watu watano au sita. Tupeni muda, nimekuja hapa na mkurugenzi wa NEMC na wataalamu wake kutazama na dawa ya changamoto tunayo, kwa hiyo wiki ijayo tutawaita na tutawaambia tulichofanya kuhakikisha kila mtu ana amani, ndiyo kazi ya Serikali,” alisema Zungu. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka aliwataka wawekezaji wote kufanya tathmini ya athari za mazingira (EIA) ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima. Alisema kuwa binadamu wanaishi kwa kutegemeana kwenye mazingira na ndiyo maana NEMC haitoi cheti hadi ifanyike tathmnini hiyo kubaini madhara yanayoweza kutokea kwa wananchi kupitia uwekezaji unaofanyika. “Natoa rai kwa wawekezaji wote wawe wa viwanda ama hoteli katika fukwe zetu kufanya tathmni na kupitia tathmini hiyo tutapata maoni kutoka kwa watu wanaokuzunguka kujua je, uwekezaji wako unawaathiri vipi na kama kuna athari ndogo tunajua namna ya kuzitatua ili kuepusha migogoro,” alisisitiza Dk. Gwamaka. Akitoa maoni yake kuhusu changamoto hizo, mtaalamu wa sayansi ya bahari, Rose Mtui alisema kuwa suluhisho ni kuotesha mikoko ambayo inalinda fukwe zisibomoke kutokana na mmomonyoko wa udongo. Aliongeza kuwa uchimbaji mchanga holela katika kingo za mito na uvuvi haramu unachangaia changamoto za kimazingira katika fukwe za bahari kwani unaharibu matumbawe ambayo yakiharibika mawimbi ya bahari hugonga moja kwa moja na kwa kasi fukwe na hivyo maji kujaa kupita kiasi.
KITAIFA
Na EVANS MAGEGE JESHI la Polisi limewataka wananchi kuwa makini na biashara zinazofanywa kwa njia ya mitandao kwa sababu kuna ongezeko kubwa la watu wanaoibiwa au kutapeliwa. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP Advera Bulimba, alisema taarifa za matukio ya uhalifu wa biashara za mtandao zimeongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni. Kutokana na ongezeko la matukio hayo, alisema uchunguzi uliofanywa na polisi umebaini kuwa watu wengi waliojikuta katika kadhia ya kutapeliwa au kuibiwa kupitia aina hiyo ya biashara wanatokana na kuwa na tamaa za mafanikio ya haraka au kutokuwa na uelewa wa biashara hiyo. “Jeshi la Polisi linawakumbusha wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha kabla ya kutuma fedha. “Wengi wanajikuta wakitumbukia katika kadhia hiyo ya kutapeliwa kutokana na kuwa na tamaa za mafanikio ya haraka na wengine kutokuwa na uelewa wa biashara za kimtandao,” alisema Advera. Mbali na uhalifu huo, pia alisema matukio ya wananchi kuvamiwa na majambazi na kuporwa fedha nyingi wakati wanapozisafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine yametokana na wahusika kutokuwa na usiri. Advera alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini kuwa matukio hayo yamekuwa yakisababishwa na wafanyabiashara wenyewe au watendaji wa ofisi za uhasibu ambao wamekuwa na tabia ya kutoa taarifa kwa watu wanaowazunguka kwamba wanapeleka fedha benki. “Katika siku za hivi karibuni kumetokea matukio mbalimbali ya wananchi hususani wafanyabiashara kuvamiwa na majambazi na kuibiwa kiasi kikubwa cha fedha wakati wanaposafirisha fedha hizo kutoka eneo moja kwenda jingine. “Unakuta mfanyabiashara au mhasibu anamtaarifu mwenzake au ofisi nzima inajua kwamba siku fulani fedha zinapelekwa benki na inakuwa hivyo. Kwa msingi huo taarifa lazima ziwafikie wahalifu ambao hujipanga mapema na kufanya uhalifu,” alisema. Pia aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanaomba ulinzi wa polisi au kampuni binafsi za ulinzi zinazoshughulikia usafirishaji wa fedha. “Tunawataka wasafirishaji wa fedha kuwa na usiri katika michakato yote inayohusiana na usafirishaji wa fedha ili kuweza kupunguza matukio hayo, wafanyabiashara nao wanatakiwa kuepuka kubeba kiasi kikubwa cha fedha na badala yake watumie miamala ya kibenki ili kupunguza matukio hayo,” alisema.
KITAIFA
Zaidi ya asilimia 40 ya mazao yanayozalishwa nchini, hupotea kutokana na ukosefu wa masoko na maghala.Hayo yamesemwa na Rais John Magufuli leo Jumatatu, alipokuwa akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa serikali katika uzinduzi wa kiwanda cha kusindika mahindi cha Mlale JKT, mkoani Ruvuma.Rais Magufuli ameeleza kuwa kiwanda hicho kitasaidia kupunguza tatizo hilo kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali wa kufikia uchumi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda.Ameeleza kuwa kiwanda hicho chenye thamani ya milioni 414.7/- kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 440 za mahindi na kuzalisha tani 308 za unga wa sembe pamoja na tani 132 za pumba.Hatahivyo Rais Magufuli amesifia Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi Kulinda Taifa (JKT) kwa kazi nzuri wanayofanya kulinda taifa na kusaidia kudumisha amani.“Jeshi letu la Wananchi linafanya kazi nzuri sana katika sekta mbalimbali za ujenzi na hata viwanda, nawapongeza sanaa,” aliongeza.
KITAIFA
AGIZO la serikali katika kukifufua Kiwanda cha Chai cha Mponde kilichopo katika Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga, limeanza kutekelezwa kwa mafundi kuanza kufanya ukarabati wa kiwanda hicho.Mwandishi wa gazeti hili alitembelea kiwandani hapo na kukuta mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati wa miundombinu ya kiwanda na vifaa. Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika ameliambia gazeti hili kuwa mafundi wanaofanya kazi ni kutoka Mamlaka ya Chai Tanzania (TTA).“Kama ulivyoona mafundi wanaendelea na ukarabati wa kuziba paa la kiwanda lililokuwa linavuja, kichemshio cha maji (boiler), ukarabati wa nyumba za watumishi pamoja na magari ambayo yalikuwa yameharibika ambayo ni malori na matrekta,” alisema Lugangika.Aliongeza: “Tunatarajia ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari tunatarajia kiwanda kuanza uzalishaji.” Kuhusu wakulima wa chai, alisema wametolewa katika Ushirika wa Wakulima wa Chai wa Usambara(UTEGA) kutokana na ushirika huo kuwa na kesi badala yake wamejiunga katika vyama vya msingi vya wakulima (Amcos) 14 vilivyo chini ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Usambara. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ziarani mkoani Tanga mwezi uliopita, alitembelea kiwanda hicho na kuamuru kifunguliwe baada ya kufungwa kwa takribani miaka mitano kutokana na mgogoro kati ya mwekezaji na wakulima wa chai. Mkulima wa chai wa Kijiji cha Mponde, Juma Shemkande alisema kufunguliwa kwa kiwanda hicho kutaamsha matumaini kwa wakulima kutokana na kukaa muda mrefu huku chai ikiharibika shambani.“Kwa kweli tunaishukuru serikali kwa kufungua kiwanda hiki, hili ni tumaini jipya kwa wakulima kwa muda mrefu chai ilikuwa inaharibika shamba,”
KITAIFA
LEO wananchi wa Zanzibar sambamba na wenzao wa Bara wanaungana kuadhimisha miaka 55 ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu Zanzibar ya mwaka 1964.Sherehe za Mapinduzi huadhimishwa Januari 12 kila mwaka, kwa lengo la kutunza historia hii adhimu na pia kukifahamisha kizazi cha sasa Zanzibar ilipotoka, ilipo sasa na inakokwenda.Sherehe za leo pia zimekuwa zikitumika mara kwa mara kwa ajili ya ufunguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Kabla ya Mapinduzi hayo, Wazanzibari walitawaliwa na mataifa mbalimbali wakiwamo Waarabu, Wajerumani na Waingereza. Watu weusi waliwekwa katika daraja la chini ambapo walidharauliwa, kunyanyaswa na kukandamizwa wakiwa ndani ya nchi yao wenyewe.Baada ya kupigania uhuru kwa muda mrefu bila kupewa, Waingereza waliamua kutoa uhuru kwa Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar. Kitendo hicho kilisababisha Wazanzibari wengi kuendelea kukosa uhuru kamili kwa kuwa uongozi wa Kisultani uliendelea kuwaweka waafrika katika daraja la chini. Mpango wa Mapinduzi ulifanikiwa siku kama ya leo mwaka 1964 na hivyo kuung’oa utawala wa Kisultani na kisha wananchi walio wengi, wakashika hatamu ya kuongoza dola, chini ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume.Mapinduzi ya Zanzibar ni tukio muhimu ambalo wananchi wanapaswa kulikumbuka na kujivunia kwani kuanzia mwaka 1964 Wazanzibari wamekuwa huru katika nchi yao, wakijipangia mambo yao wenyewe kwa ajili ya maendeleo yao. Haki zote ambazo wananchi wazalendo walistahiki kuzipata ikiwemo elimu, matibabu na matumizi ya ardhi kwa kilimo na makazi ambavyo walinyimwa na utawala dhalimu wa Kisultani sasa wanazipata kutokana na mapinduzi hayo.Kwa lugha rahisi, ni mapinduzi hayo ndiyo yaliyomrejeshea haki mwafrika, haki ambayo aliyo nayo hadi leo ikiwemo kuunda chama cha siasa na kujiendeleza kadri anavyoweza. Ni mapinduzi yaliyokuwa pia chanzo cha Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuzaliwa Tanzania. Ni vigumu mtu kupata picha hali ingelikuwaje kuhusu muungano kama Sultani angeendelea kutawala visiwa vya Zanzibar.Pamoja na umuhimu wa mapinduzi haya yaliyomrejeshea Mzanzibari uhuru wake alionao leo pamoja na haki yake kama mkazi halali wa visiwa hivi kuna Wazanzibari walio katika kambi ya upinzani wamekua wakisusa kushiiki katika maadhimisho haya. Huko nyuma pia, kabla ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, Wapinzani walikuwa na kawaida ya kukisusa pia sherehe za kuadhimisha mapinduzi haya matukufu. Lakini kitu ambacho kimekuwa kikiwashangaza wengi ni Wapinzani kuchukia hata kutamka neno “Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” au kwa kufupi “SMZ”.Hatua hiyo kwa kweli ni sawa na kusema wapinzani wanachukizwa na mapinduzi! Hii imekuwa ikileta wasiwasi pia kwamba siku upinzani ukichukua uongozi wa dola, upo uwezekano wa kufuta sherehe za mapinduzi moja kwa moja. Lakini kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha Wakulima (AFP_, Said Soud amekuwa akisema kwamba sherehe za mapinduzi ni za kitaifa na hazipaswi kuhusishwa na itikadi ya vyama vya siasa. Soud ambaye kwa sasa ni Waziri asiye na Wizara Maalumu aliwahi kukaririwa akisema kwamba sherehe hizo ni utambulisho wa wananchi wa Zanzibar walivyojikomboa kutoka kwenye utawala wa Kisultani kwa hivyo zinatakiwa kuenziwa na kutunzwa na sio kubezwa au kususwa kama wanavyofanya wanasiasa wengine.
KITAIFA
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesamehe jumla ya Sh bilioni 328.4 za riba na adhabu kutoka kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni, baada ya kuwapatia fursa ya kulipa kodi ya msingi ndani ya mwaka wa fedha 2018/19.Pamoja na msamaha huo, mamlaka hiyo pia imeendelea kukusanya Sh bilioni 458.58 za kodi ya msingi kutokana na walipakodi 8,687 waliokidhi vigezo kati ya 9.406 waliomba msamaha kutokana na malimbikizo yao ya madeni.Hatua hiyo, imekuja baada ya TRA Julai, mwaka jana kutangaza msamaha kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19. Hayo yalielezwa na Naibu Kamishna wa mamlaka hiyo, Msafiri Mbibo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu mafanikio ya mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.Alisema mpaka sasa, mamlaka hiyo imeshakusanya Sh bilioni 120.01 kutokana na kodi ya msingi inayotakiwa kulipwa na walipakodi waliosamehewa riba na adhabu. Hata hivyo, alieleza kuwa serikali iliongeza muda wa kulipa kutoka muda uliowekwa awali wa Juni 30, mwaka huu hadi Desemba 31, mwaka huu. Pamoja na hayo, Kamishna huyo alieleza juu ya changamoto inayoikabili mamlaka hiyo ya ukwepaji kodi wa makusudi na biashara za magendo kutokana na kuwepo kwa ukanda mrefu wa Pwani, mipaka mingi na rushwa.Aidha, alitaja sababu nyingine za changamoto hizo kuwa ni utunzaji dhaifu wa kumbukumbu na baadhi ya wafanyabiashara wenye nia mbaya kutotumia mashine za kielektroniki(EFDs) ipasavyo, ikiwa ni pamoja wananchi wengi kutokuwa na utamaduni wa kutoa na kudai risiti. Alisema katika kudhibiti biashara za magendo, TRA imeimarisha kikosi chake maalumu ili kukabiliana na biashara za magendo kinachoitwa FAST (Flexible Anti-Smuggling Team). Alisema kikosi hicho kimepatiwa vitendea kazi bora na kuongezewa wafanyakazi wenye weledi ili kuhakikisha magendo yanakoma.“Endapo mzigo wowote utakamatwa, utataifishwa, ikiwemo chombo kilichotumika kuusafirisha, iwe ni gari, boti au nyumba iliyotumika kuuhifadhi,” alisisitiza. Awali, alibainisha hatua ambazo TRA imepiga katika ukusanyaji kodi ambapo imefanikiwa kuongeza mapato ya serikali kwa miaka minne mfululizo.Alifafanua kuwa mwaka 2015/16 mapato yalikuwa ni Sh trilioni 12.5, mwaka 2016/17 Sh trilioni 14.4, mwaka 2017/18 Sh trilioni 15.5 na mwaka 2018/19 makusanyo yaliongezeka zaidi kufikia Sh trilioni15.9 . Jumla ya makusanyo yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka hiyo minne ni Sh trilioni 58.3 ikilinganishwa na Sh trilioni 34.97 kwa kipindi cha miaka minne iliyopita kabla ya hapo.Alieleza kuwa mwaka 2011/12 TRA ilikusanya Sh trilioni 6.76, mwaka 2012/13 Sh trilioni 7.88 , mwaka 2013/14 Sh trilioni 9.52 na mwaka 2014/15 TRA ilikusanya Sh trilioni 10.81.
KITAIFA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanajiosayansi nchini kuongeza juhudi katika utafutaji wa madini, ikiwa ni pamoja na kufungua migodi mingine mikubwa, ili kuzalisha ajira kwa watanzania na kuiongezea nchi kipato kutokana na mapato ya kodi na gawio. Majaliwa alisema hayo hivi karibuni wakati akifun gua warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania jijini Dodoma.Majaliwa alisema ni vema wakatambua kuwa utaalamu wao unategemewa na serikali inatambua umuhimu wao. “Nitoe mwito kwenu kutumia ipasavyo utaalamu na uzalendo mlionao kwa nchi hii ili tuone idadi ya migodi midogo kwa mikubwa inaongezeka na kuleta tija ya maendeleo kwa taifa letu,”alisema. Alisema serikali kwa upande wake inaendelea kuhakikisha vijana wa kitanzania wanasomeshwa taaluma hiyo ya jiosayansi ili nchi iweze kunufaika nayo. “Kwa upande wenu ninyi wanajiosayansi mna kila sababu ya kuendelea kufanya tafiti kuhusu rasilimali za madini, mafuta, gesi asilia, joto ardhi na maji ya ardhini kwani bado sehemu kubwa ya nchi hii haijafikiwa na tafiti za namna hiyo na hivyo kuwanyima watanzania fursa ya kunufaika na uwepo wa rasilimali hizo,” alisema.Alishauri wawe na Bodi ya Usajili wa Wanajiosay ansi ambayo itasimamia maendeleo yao kitaaluma na kiutendaji ili wanapotimiza majukumu yao wazingatie maadili na misingi ya taaluma yao. Naye, Waziri wa Madini Angellah Kairuki alisema ili kuleta ufanisi zaidi katika ukuaji wa sekta ya madini nchini, serikali iliifuta iliyokuwa Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA), kuanzisha Tume ya Madini ambayo majukumu yake makubwa ni pamoja na kutoa vibali vya utafiti, uchimbaji, vilipuzi na ulipu aji, uchenjuaji, usafirishaji pamoja na kuishauri serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu madini. Kairuki alisema serikali kupitia wizara ya madini inategemea wanajiosayansi kuwa wazalendo kwa taifa kwa kutoa taarifa za kitaalamu zinazoendana na uhalisia, ili kuondoa malalamiko ya baadhi ya watu yanayotokana na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu hasa wale wanaojifanya wataalamu ilihali wakijua wazi hawana utaalamu wa fani hiyo.
KITAIFA
PATRICIA KIMELEMETA Na MAMII MSHANA (TURDAco) -DAR ES SALAAM KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amekuja na mikakati kadhaa ya kuweza kukabiliana na uhalifu jijini humo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Mambosasa alisema suala la uwepo wa vitendo vya utekaji vinavyofanywa na watu wasiojulikana halitafumbiwa macho tena, hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe haraka. Alisema kwa sasa atalifuatiliwa kwa kina suala hilo ili aweze kujua vyanzo vya baadhi ya watu wakiwamo wasanii kutekwa ili aweze kuwachukulia hatua wahusika. Alisema katika kipindi chake cha uongozi akiwa mkoani humo, atashirikiana na watendaji mbalimbali wakiwamo wanasiasa, viongozi wa dini, polisi jamii na wananchi wa kawaida ili kuhakikisha wanaendesha msako wa kuwakamata wahalifu hao. Alisema anatambua kuwa kuna kamati za ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya mkoa hadi kata, hivyo basi atashirikiana nao ili kuhakikisha anapata taarifa za wahalifu hao pamoja na kuwachukulia hatua. Alisema lakini pia kuna makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi ambayo na yenyewe anapaswa kuwa nayo karibu ili waweze kuhakikisha ulinzi unaimarika katika mkoa huo. Akizungumzia kuhusu baadhi ya askari polisi wanaotumia nafasi zao kwa ajili ya kunyanyasa wananchi, alisema wananchi watakaokumbwa na kadhia hiyo watoe taarifa ili watakaobainika wachukuliwe hatua. Alisema anatambua haki za binadamu na utawala bora, hivyo basi hawezi kuona baadhi ya askari wanatumia nafasi zao kwa ajili ya kuwanyanyasa wananchi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua. “Tuna taarifa za kuwepo kwa baadhi ya askari ambao wanatumia madaraka yao vibaya kwa ajili ya kunyanyasa wananchi, huku wakitambua kuwa, kitendo hicho ni kinyume na kifungu namba 5 cha sheria ya makosa ya jinai, siwezi kuvumilia suala hilo,” alisema.
KITAIFA
Badi Mchomolo Na Mitandao KABLA ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya uhamisho ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa ni nyota wa PSG, Neymar Jr kurudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona au kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid. Klabu hizo mbili zipo vitani kupambana kuinasa saini ya mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba wa kuitumikia PSG hadi 2022, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kufikia muda wa kumaliza mkataba wake baada ya uongozi wa timu hiyo kuchoshwa na tabia zake. Neymar Jr ni mchezaji ambaye hadi sasa ameweka rekodi ya usajili akitokea Barcelona mwaka 2017 na kujiunga na PSG kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 198, lakini kwa kipindi cha muda mchache aliokaa sasa anataka kuondoka. Kuondoka kwa Neymar ndani ya PSG kuna mambo mengi nyuma yake, miongoni mwake ni kushindwa kuelewana na baadhi ya wachezaji wenzake, viongozi na majeruhi yanayomsumbua. Majeruhi makubwa ambayo ameyapata akiwa na PSG ni kuanzia Februari 2018, Junari 2019 na Juni 2019. Kuumia kwa vipindi hivyo kumemfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu. Timu nyingi haziwezi kusajili mchezaji ambaye ni majeruhi, tena majeruhi hayo hayajulikana yatadumu kwa muda gani, wakati mwingine hawawezi kumsajili mchezaji ambaye mara kwa mara amekuwa akiumia. Neymar sasa ni mchezaji ambaye anaonekana hawezi kukaa muda mrefu bila ya kuumia tofauti na ilivyo wakati anakipiga Barcelona, kitendo hicho kinawafanya viongozi wa PSG kuona haina haja ya kuendelea kuwa na mchezaji wa aina hiyo ikiwa pamoja na sababu nyingi. Kwa sasa Neymar anasumbuliwa na mifupa ya vidole ambapo aliumia Juni mwaka huu ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Copa America ambayo imefanyika nchini Brazil. Tangu kuumia huko hadi sasa bado hayupo sawa japokuwa ameanza mazoezi wakati huo akisubiri kundoka wakati huu wa kiangazi. Kwa mujibu wa daktari mkuu wa zamani wa timu ya PSG, Eric Rolland, ameweka wazi kuwa, Neymar ataendelea kusumbuliwa na tatizo hilo la kuumia mifupa ya vidole kutokana na miguu yake kuwa miembamba. Kitaalamu inasemekana mchezaji mwenye miguu miembamba ana nafasi kubwa ya kuumia mara kwa mara mifupa inayounga vidole kwa kuwa inakuwa karibu na ngozi, hivyo ikiguswa kwa nguvu inakuwa na tabia ya kutawanyika kwenye sehemu zake za kawaida. “Miguu ya Neymar ndio tatizo, amekuwa na miguu miembamba hicho ni chanzo cha mchezaji huyo kupata tatizo kama hilo la kuumia mifupa ya vidole mara kwa mara. “Kama miguu ni miembamba mifupa hiyo ikigongwa kwa nguvu inaumia kwa haraka kwa kuwa inakosa nyama za kuweza kuizuia, hivyo inajitawanya, wapo wachezaji wenye miguu kama ya Neymar lakini hawajakutana na tatizo kama hilo, wakikutana litawasumbua,” alisema Rolland. Hata hivyo, daktari huyo aliongeza kwa kusema, mchezaji wa aina hiyo anatakiwa kukaa nje kwa muda mrefu ili aweze kupona kabisa, lakini akirudi viwanjani mapema ni rahisi kupata tatizo kama hilo mara kwa mara. “Kwa sasa Neymar ameanza mazoezi lakini bado hajacheza michezo ya ushindani, kutokana na aina ya miguu yake ni rahisi kuumia tena mifupa ya vidole kama hajapona vizuri. “Anatakiwa kutumia muda mrefu kufanyiwa matibabu ili mguu uweze kuwa sawa, lakini kama atarudi uwanjani mapema kuna uwezekano wa kuendelea kuumia mara kwa mara,” alisema. Neymar ni mmoja kati ya wachezaji wa kizazi cha sasa ambaye alipewa nafasi kubwa ya kuwa mfalme wa soka nchini Brazil baada ya mastaa mbalimbali kutikisa kama vile Ronaldo de Lima, Ronaldinho Gaucho, Kaka na wengine. Kutokana na majeraha anayokumbana nayo, wengi wanaamini ndoto za mchezaji huyo kuwa mfalme nchini Brazil haitokamilika kwa kuwa umri wake unazidi kuwa mkubwa akiwa na miaka 27 sasa, lakini anakumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Alitakiwa kuwa na mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo, lakini majeruhi yanaweza kupunguza thamani yake. Mbali na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, Real Madrid na Barcelona zinatoana jasho kuwania saini ya mchezaji huyo raia wa nchini Brazil. PSG wanadai thamani ya mchezaji huyo ni pauni milioni 206, ila wamewataka Barcelona kuweka mezani kiasi cha pauni milioni 93 pamoja na wachezaji watatu akiwa Philippe Coutinho, Ivan Rakitic na Nelson Semedo, lakini Barcelona wamedai hawezi kutoa wachezaji wote hao. Madrid wao wamedai wapo tayari kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 110 pamoja na kuwapa PSG wachezaji wawili. Kazi kubwa ya PSG ni kuangalia ukubwa wa ofa lakini kwa upande wa Neymar mwenyewe ameonesha dalili za kutaka kurudi Barcelona.
MICHEZO
RAIS John Magufuli ametoa Sh milioni 20 ili kuunga mkono juhudi na uzalendo wa wananchi wa mtaa wa Nyamazobe, Kata ya Mkolani katika Wilaya ya Nyamagana waliojitolea kujenga barabara ya mawe yenye urefu wa kilomita moja.Rais Magufuli ametoa fedha hizo baada ya kuridhishwa na umoja na mshikamano uliooneshwa na wananchi hao ambao walianza kujitolea kuijenga barabara hiyo ambayo ikikamilika itawezesha kaya 900, watu 3,005, kujiimarisha kiuchumi.Akikabidhi fedha hizo mwishoni mwa wiki kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo alisema Rais amefurahishwa na uamuzi wa kizalendo uliochukuliwa na wananchi wa kujitolea nguvu zao kuanza kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha mawe. “Rais amesema ninyi ni wananchi wa kupigiwa mfano, na alivyofurahi amenikabidhi kiasi cha shilingi milioni 20 niwaletee ili ziwaongezee nguvu kwenye ujenzi huu wa barabara mlioanza,” alisema Waziri Jafo huku akishangiliwa na wananchi hao.Jafo alisema Rais ameelekeza fedha hizo zitumike vizuri kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo na kwamba yeye binafsi atafuatilia kwa karibu kila matumizi ya kila senti itakayotumika ili ziweze kusaidia kukamilisha kwa wakati ujenzi wa barabara hiyo muhimu.“Rais amesisitiza kuwa fedha hizi si za kufanyia starehe bali ni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya wananchi wa Nyamazobe ambao anawapenda sana,” aliongeza.Katika hatua nyingine, Jafo alitoa unafuu kwa wananchi wa Kata ya Mkolani kwa kusema kwamba miundombinu yote ya barabara katika kata hiyo ijengwe na alimuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarula) katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mohamedi Muanda kuhakikisha anafanya uchambuzi wa barabara zote katika kata hiyo ili zijengwe mara moja.“Yote haya yanafanyika kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imeweka nidhamu katika matumizi ya fedha za umma,” alisema.
KITAIFA
Na KYALAA SEHEYE MWANAMITINDO wa kimataifa, Miriam Odemba, amesema warembo wanaoingia kwenye fani ya urembo hawajui misingi ya fani hiyo ndiyo maana wanafanya mambo ya ajabu yanayoaibisha fani hiyo. “Wakati sisi tunaanza tulifuata nyayo za wanamitindo na warembo waliowika dunia akiwemo Naomi Campbell na tuliangalia mema yake ambayo yanatusaidia hadi leo kuendelea kujitunza na kuendeleza fani hii kwa mafanikio tofauti na mabinti wa sasa ambao wengi wao huingia kwa mkumbo bila kujifunza misingi ya fani hiyo,” alieleza Odemba huku akidai kama misingi hiyo haitafuatwa hakutakuwa na warembo bora kwa miaka mingi.
BURUDANI
WANACHAMA wa Yanga bado wanajipa matumaini ya kurejea kwa Mwenyekiti wao wa zamani, Yusuf Manji baada ya kupokewa kwa barua yao.Kupitia mkutano mkuu wa wanachama hivi karibuni waliamua kwa kuandika barua ya kumuomba Manji kurejea na kuendelea na nafasi hiyo, wakiamini ndiye mkombozi wao baada ya kufanya vizuri kabla ya kuachia ngazi mwaka jana hali iliyofanya klabu hiyo kuwa katika mazingira magumu.Tangu kujiuzulu kwa Mwenyekiti huyo aliyekuwa msaada miaka iliyopita ni mwaka mmoja umepita. Hata hivyo, licha ya kupokelewa kwa barua hawajajibiwa.Mwenyekiti wa matawi wa klabu hiyo Bakili Makele amesema waliahidiwa baada ya mfungo wa Ramadhan mambo yatakuwa mazuri hivyo kuwaasa wanachama kuendelea kuwa watulivu.“Tunatarajia atatoa tamko kama atarudi au hatarudi, bado tuna imani kwa sababu ameshapokea barua na dalili za kurejea kwake zipo, tunaendelea kupata ushirikiano wake,” alisema.Makele alisema jambo linaloashiria huenda akarejea ni ushirikiano anaotoa kwenye usajili unaoendelea hivi sasa ambapo kupitia Kamati ya usajili wamekuwa wakiendelea na usajili kimya.Kiongozi huyo wa matawi alifafanua kuwa sasa hivi kuna mambo mengi mazuri yanafanywa na viongozi wa klabu na kuwatoa hofu mashabiki na wanachama wake kuwa silaha za hatari zilizosajiliwa zitatangazwa muda si mrefu.“Mambo ya klabu yanashughulikiwa na viongozi kimya kimya, watu waendelee kuwa watulivu. Manji tuna imani naye atarejea, tunajua ana shughuli zake nyingi akikamilisha atakuja,”alisema.Klabu hiyo imedhamiria kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji lakini tegemeo lake kubwa imeweka kwa Manji wakiamini ni mtu sahihi kwao.
MICHEZO
SERIKALI kupitia Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSCL) kwa kushirikiana na Shirika la Reli Uganda wameweka utaratibu wa kuwa na kituo kimoja cha malipo ya mizigo inayosafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Bandari ya Mwanza hadi Port Bell nchini Uganda, ili kuboresha huduma za usafirishaji wa mizigo na abiria kwa nchi hizo mbili.Hiyo ni katika kurahisisha biashara ya usafirishaji wa mizigo, ikiwamo kupunguza gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara na wawekezaji wanaotumia huduma za usafirishaji kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC). Hayo yamesemwa jana jijini hapa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alipozungumza katika hafla maalumu ya tukio la kihistoria ya uzinduzi wa huduma ya usafirishaji wa mizigo na abiria katika ushoroba wa kati kwa njia maji kupitia Ziwa Victoria kwenda bandari ya Port Bell, Uganda.Kamwelwe alisema mizigo itakuwa inasafirishwa kwa reli kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Mwanza na baadaye itasafirishwa kwa kutumia meli ya mizigo ya Mv Umoja kwenda Uganda na nchi jirani za Maziwa Makuu, kwa lengo la kuhudumia wananchi na nchi hizo zinazotumia bandari nchini kusafirisha mizigo na abiria. Waziri alifanya uzinduzi huo katika Bandari ya Mwanza Kusini katika hafla maalumu ya tukio la kihistoria ya kuanza kwa safari ya meli ya mizigo ya Mv Umoja itakayosafirisha mizigo kutoka Mwanza kwenda Uganda.Kamwelwe alisema treni ya mizigo itakapokuwa inawasili katika Bandari ya Mwanza itaingia moja kwa moja kwenye meli ya mizigo bila kushusha mzigo na kwenda nchini Uganda. “Ni jambo la kujivunia kwani ni nchi chache katika Afrika zenye miundombinu iliyounganishwa kwa utaratibu huu,” alisema na kuongeza kuwa utaratibu huo wa muunganiko wa njia za reli na maji katika usafirishaji wa mizigo na abiria, utawezesha mzigo unaposhuka kwenye meli katika Bandari ya Dar es Salaam kupakiwa kwenye treni ya TRC na kusafirishwa moja kwa moja kwenda jijini Mwanza.“Mfumo huu wa usafirishaji upo pia upande wa nchi jirani ya Uganda ambapo huwezeshwa mzigo kufika Kampala bila kushushwa kwenye treni,” alisema. Alibainisha kuwa taarifa zilizopo zinaonesha kuwa tangu kufunguliwa kwa njia hiyo ya usafirishaji Juni 6, 2018, jumla ya mabehewa 1,165 sawa na tani 45,720 zimekwishasafirishwa kupitia ushoroba huo kwa njia ya reli na maji. Alisema kati ya mzigo huo, mabehewa 864 sawa na tani 34,960 yalikuwa yamesafirisha mzigo wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) ambalo lilichangia takribani asilimia 75 ya mzigo wote uliosafirishwa katika kipindi hicho. Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa alisema kukamilika kwa huduma hiyo ya usafiri katika ushoroba wa kati ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi ambao utatoa fursa kwa nchi kutengeneza uchumi wa viwanda utakaoangalia masoko ya nje.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema usafirishaji huo wa njia ya reli na majini kwenda nchini Uganda utaboresha shughuli za kiuchumi kwa Jiji na Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa WFP, Michael Dunford aliishukuru serikali kwa jinsi ambavyo katika kipindi cha mwaka mmoja meli ya Mv Umoja ilisafirisha kontena 18 za mizigo zenye chakula cha msaada uliotolewa na WFP kwenda nchini Uganda.
KITAIFA
Na Upendo Mosha- Hai WAKUU wa wilaya wawili, wako hatarini kufikishwa mahakamani baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya kazi zao. Mmoja ni Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa Kilimanjaro, Gelasius Byakanwa, anayedaiwa kumwamuru Mwalimu wa Shule ya Sekondari Lerai, iliyopo Kata ya Bondeni, wilayani humo, kupiga ‘pushapu’ mbele ya wanafunzi wake. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, anayedaiwa kumpiga na kumjeruhi mkazi wa Kijiji cha Kambiyanyasa, Chindika Pingwa (57), ambaye ni mzazi wa mtoto anayedaiwa kuvunja kioo cha gari la kiongozi huyo, wakati wakicheza na wenzake. Tukio la wilayani Hai lilitokea Agosti 11 mwaka huu shuleni hapo baada ya mwalimu huyo, Erasto Mhagama, kushindwa kujibu maswali aliyoulizwa na mkuu huyo wa wilaya. Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwalimu Mhagama, alisema wakati analazimishwa kufanya hivyo, walikuwapo pia walimu wenzake baada ya mkuu huyo wa wilaya kufika shuleni hapo wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi. “Baada ya mkuu huyo wa wilaya kufika shuleni kwetu na kupokewa na makamu mkuu wa shule yetu, aliomba kufanya kikao kifupi na walimu. “Wakati wa kikao hicho, alituuliza maswali mbalimbali yakiwamo nini kirefu cha IGP, CDF, CUF na CAF na maswali mengine mengi. “Alipofika kwangu, aliniuliza Wilaya ya Hai ina shule ngapi nami nikamjibu sijui kwa sababu sina takwimu. “Niliposema sijui, alinikaripia kwa maneno makali ya kejeli na kunitaka nisishiriki tena katika mjadala wa kikao hicho alichokuwa akikiongoza yeye. “Baadaye, aliniita pembeni, nje ya kikao na kunitaka nichague adhabu mbili ambazo ni kukaa mahabusu kwa saa sita au kupiga pushapu 20 hadharani. “Nilimwambia siwezi kupiga pushapu kwa sababu nina matatizo ya kiafya, lakini alionekana kukasirika kwa sababu aliniambia hayo hayamhusu. “Kwa hiyo, alipiga simu polisi na baada ya muda mfupi, gari la polisi wa Kituo cha Bomang’ombe, lilifika na kunibeba na kunipeleka mahabausu ya kituo hicho, majira ya saa nane mchana hadi saa mbili usiku nilipotolewa. “Nilipotolewa mahabusu nilikuwa nimechanganyikiwa kidogo, lakini nilijikaza kiume na kurudi nyumbani kwangu. “Kwa kuwa nilidhalilishwa mbele ya walimu na wanafunzi wangu, naomba mamlaka husika zichukue hatua dhidi ya mkuu huyo wa wilaya ili kulinda haki na masilahi ya walimu,” alisema mwalimu huyo. Katibu wa Chama cha Walimu, Mkoa wa Kilimanjaro (CWT), Digna Nyaki,  alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema halileti taswira nzuri katika jamii. Kutokana na hali hiyo, alisema CWT imemtaka mkuu huyo wa wilaya aombe radhi dhidi ya tukio hilo ndani ya siku 30 kuanzia jana kabla hajafikishwa katika vyombo vya sheria. “Ni kweli tukio hilo lipo na lilifanywa na DC Ijumaa ya wiki iliyopita katika Shule ya Sekondari Lerai. Tumejiridhisha kwa hilo baada ya kupata taarifa na kutembelea shule hiyo na kuzungumza na walimu ambapo walikiri mkuu huyo wa wilaya kufanya tendo hilo. “Kwa hiyo, tunampa siku 30 aombe radhi na kama hatafanya hivyo, tutampeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria,” alisema Nyaki. “Tutamfikisha mahakamani kwa sababu hii siyo mara yake ya kwanza kufanya vitendo vya udhalilishaji kwani awali alifanya hivyo kwa walimu wa Shule ya Sekondari Boma. “Kwa kifupi, tumeshapata malalamiko mengi kutoka kwa walimu wa Hai wakimlalamikia, kwamba amezoea kufanya hivyo kwani hata mwaka jana, alimsweka ndani mwalimu mwingine kwa sababu zisizokuwa na msingi. “Kibaya zaidi, amekuwa akitoa vitisho mbalimbali, kwamba hakuna mtu anayeweza kumfanya chochote na kuna taarifa zinasema amesababisha walimu wetu wawili waache kazi na hadi sasa tunafuatilia mambo hayo. “Mpaka sasa tumepata taarifa za ndani kwamba kuna walimu wawili wameacha kazi kutokana na uzalilishaji unaofanywa na DC kwa sasa tupo katika ufuatiliaji zaidi tutatoa taarifa rasmi, lakini hatua inayofuata sasa tutapeleka malalamiko yetu kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira,” alisema. Alisema vitendo vya uzalilishaji vinavyofanywa na DC huyo vimekuwa vikififisha juhudi na jitihada za walimu katika kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kwamba havipaswi kufumbiwa macho bali hatua stahiki za kinidhamu zitachukuliwa ili kukomesha tabia hiyo. Akizungumza na MTANZANIA juu ya tukio hilo, mkuu huyo wa wilaya, alikana kumpigisha pushapu mwalimu huyo ingawa alikiri kufika shuleni hapo akiwa katika ziara ya kikazi. “Sikumpigisha pushapu wala kichura ila kilichotokea ni kwamba wakati namuuliza maswali huyo mwalimu alinijibu kwa ujeuri. “Kinachoonekana hapa ni kwamba kuna watu wanapinga jitihada zangu za kuleta maendeleo ndiyo maana wameanza kugeuzageuza maneno,” alisema mkuu huyo wa wilaya. Wakati kiongozi huyo wa wilaya akikanusha tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issa, alithibitisha mkuu huyo wa wilaya kumweka ndani mwalimu huyo kwa saa sita. “Hilo tukio lipo na nimeambiwa mkuu wa wilaya alimweka ndani mwalimu kwa saa sita baada ya kushindwa kujibu swali alilomuuliza. “Kwa hiyo, nadhani itabidi nitoe maelekezo kwa viongozi wetu ili wajue ni makosa gani ya kuwaweka watu ndani kwa sababu kiongozi anaruhusiwa kumweka mtu ndani pindi anapohatarisha amani na si vinginevyo,” alisema Kamanda Issa. Katika tukio jingine, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma, Simon Odunga, ametakiwa kumwomba radhi, Chindika Pingwa (57), baada ya kudaiwa kumpiga na kumuumiza. Hivi karibuni, Odunga alimcharaza  viboko mkazi huyo wa Kijiji cha Kambiyanyasa, wilayani Chemba kwa madai kuwa mtoto wake alivunja kioo cha gari lake lenye namba za usajili STL 669. Katika tukio hilo lililotokea wiki iliyopita, watoto hao walitajwa kuwa ni Baraka Chindika, Majala Chindika, Jacskon Stephano na Paschal Daud. Akizungumza na MTANZANIA juzi katika Kitongoji cha Mlongia, Kijiji cha Kambiyanyasa, Pingwa alisema amelazimika kulifikisha suala hilo katika vyombo vya sheria kwa sababu mkuu huyo wa wilaya alimdhalilisha. “Alinidhalilisha kupita kiasi kwa sababu siku ya tukio alinipiga na kuni kichwani nikiwa nimelazwa kwenye gari la polisi, huku nikiwa nimefungwa pingu. “Kwa kuwa naamini hakunitendea haki, namtaka aniombe radhi haraka, vinginevyo nitalazimika kumfikisha mahakamani. “Kosa la kuvunja kioo lilifanywa na mtoto, iweje mimi nipigwe kwa kosa ambalo sikulifanya?, namtaka aniombe radhi. “Pia, naiomba Serikali iwaangalie viongozi wake wanafanyaje kazi kwani wanaweza kusababisha madhara kwa wananchi wasiokuwa na hatia,” alisema Pingwa. Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mlongia, Marius Roman, alisikitishwa na kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya na kusema kiongozi huyo amekuwa na matukio mengi ambayo yanasababisha baadhi ya wananchi wakose imani naye,” alisema Roman. Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alipoulizwa siku ya tukio, alikiri kufanya kitendo hicho na kusema kuwa baadhi ya watu wa kijiji hicho wamekuwa na tabia ya kuweka mawe barabarani pamoja na kupiga magari mawe. Alisema watahakikisha tabia hiyo inakomeshwa, kwani vitendo hivyo ni hatari kwa wasafiri na jamii kwa ujumla. Mwisho
KITAIFA
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Yanga wamesema hawatafanya makosa katika mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda zaidi ya kuongeza umakini na kupata ushindi.Kikosi cha wachezaji 20 kilitarajiwa kuwasili jana Mtwara tayari kwa mchezo huo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Akizungumza na gazeti hili, Kocha Mwinyi Zahera alisema mchezo unaweza kuwa mgumu kwa sababu wachezaji wake hawajapata muda wa kupumzika ila ni lazima wakapambane kupata ushindi utakaowawezesha kutimiza lengo lao la ubingwa.“Hatutaki kurudia makosa yaliyotugharimu katika mchezo uliopita dhidi ya Lipuli tulipoteza bao 1-0 ugenini. Bado tuko kwenye mbio za ubingwa, muhimu ni kujitahidi ili tushinde mchezo wa Ndanda,” alisema. Alisema anajua wazi Ndanda wanaweza kuja na kasi ya kutaka matokeo kwenye uwanja wao wa nyumbani, hilo halimsumbui kwani hata wao wanajipanga kupata pointi tatu.Timu hizo kila zinapokutana ushindani unakuwa mkubwa kwani mara ya mwisho zilikutana Dar es Salaam na kutoka sare ya bao 1-1. Yanga huenda ikaendeleza morali baada ya kutoka kushinda mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Alliance na kushinda kwa mikwaju 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.
MICHEZO
Kamati Kuu ya chama cha ACT Wazalendo imetoa maazimio juu ya hali ya nchi baada ya kukaa kwa siku mbili katika kikao chake cha Kawaida ambapo ilipitia hali ya Kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na Bara la Afrika kwa ujumla. Akiwasilisha maazimio hayo leo Juni 11 mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe amesema moja ya maazimio waliyofikia ni kasi ya ukuaji wa uchumi kuporomoka kutokana na Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini rais John Magufuli kukata nishati ya kuendesha uchumi. “Takwimu za benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha kuwa kwa mwaka unaoishia Machi 2018 urari wa biashara kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani ulikuwa hasi kwa dola bilioni 2, Kwa mwezi unaoishia Machi 2019 urari wa biashara umetanuka kufikia hasi ya dola bilioni 2.5 sawa na ongezeko la dola milioni 500,” amesema. “Hata taasisi kama benki ya dunia wamezuia fedha kuja nchini, fedha ambazo zimezuiliwa ni pamoja na ambazo zinapaswa kufadhili miradi ya kuboresha elimu ya sekondari SEQIP dola milioni 400 sawa na shilingi bilioni 920, TASAF III dola za kimarekani milioni 300 sawa na shilingi bilioni 660 na mradi wa Maji Vijijini wenye thamani ya dola milioni 300, “Fedha hizi zimezuiwa Kwa sababu ya Serikali kutunga sheria kandamizi ya takwimu kwa lengo la kuwadhibiti wakosoaji wa Serikali wanaotumia ushahidi wa takwimu lakini madhara yake kwa nchi ni makubwa mno,” amesema “Sababu nyingine ni uminywaji wa demokrasia nchini, msingi wake mkuu ukiwa ni kuporwa kwa ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad Katika Uchaguzi mkuu wa Zanzibar 2015, kuzuia Bunge Live, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani  wakati ya CCM ikiruhusiwa na kuwabambikia kesi mbalimbali wanasiasa wa upinzani, kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu akiwa kwenye eneo la Bunge, na Kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa inayoua kabisa siasa za vyama vingi nchi,” amesema. Ameongeza kuwa Kupungua kwa Uwekezaji nchini (FDI) kunapekelea shughuli za Uchumi kutoongezeka, kutozalisha ajira rasmi za kutosha na kutoongeza mapato ya Serikali.
KITAIFA
Na Mwandishi Wetu MKOA wa Mara ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa  kupiga hatua kubwa kwenye matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango. Imeelezwa kati ya mwaka 2010 na 2015, mkoa huo umefanikiwa kuongeza matumizi ya njia hizo kutoka asilimia 11 hadi asilimia 29 katika kipindi hicho. Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Nila Jackson alisema hatua hiyo imetokana na uongozi kujitolea na kuungwa mkono na wananchi ambao wametambua umuhimu wa uzazi wa mpango katika mipango ya maendeleo. Dk. Jackson, alitoa kauli hiyo baada ya kushiriki  mkutano wa kubadilishana mawazo na wadau wa uzazi wa mpango. Alisema mafanikio ya mkoa huo, pia yametokana na kuendesha mikutano ya kila mwezi ya wadau husika kuangalia takwimu za matumizi ya huduma za uzazi wa mpango, kuzungumzia changamoto zilizopo na kuweka mikakati ili kuongeza kasi ya utekelezaji ya huduma hasa kwa kutoa taarifa na elimu juu ya njia sahihi. Alisema kwa kushirikiana na wadau wa afya, kwa mfano, Serikali ya mkoa ilianzisha kampeni maalumu ya kutoa elimu ili kuhamasisha watu kutumia uzazi wa mpango na kuinua kiwango kidogo kilichoiweka nyuma Mara miaka kadhaa iliyopita. Alisema wamekuwa wakiwashirikisha kikamilifu wazee wa mila  kuzungumzia na kutilia mkazo uzazi wa mpango. “Mila na desturi katika mkoa huu, zimekuwa sehemu ya changamoto zilizokuwa zikikwamisha harakati hizi, hivi sasa viongozi wa kimila wamekuwa chachu ya mafanikio yetu,”alisema Jackson. Alisema japo kwa kasi ndogo, Tanzania imefanikiwa kuongeza matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango kutoka asilimia 27 mwaka 2010 hadi asilimia 32 mwaka 2015. Alisema imejiweka lengo la kufikia asilimia 45 katika matumizi ya uzazi wa mpango, ifikapo mwaka 2020 katika jitihada za upunguza vifo vya akina mama ambavyo vimepanda hadi 556 katika kila vizazi hai 100,000 kutoka vifo 454/100,000 mwaka 2010. Kwa upande wake, James Mlali wa Kituo cha Mawasiliano na Maendeleo ya Jamii (TCDC),  mshirika mmoja wapo wa mradi wa Advance Family Planning, alisema uwekezaji zaidi kwenye uzazi wa mpango kutoka Serikali kuu unahitajika ili kuongeza kasi ya matumizi na kufikia lengo la Taifa.
KITAIFA
Na JUDITH NYANGE-MWANZA KUTOZINGATIWA kwa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kumetajwa kama chanzo cha kuendelea kuwapo mmomonyoko wa maadili kwa watendaji wenye dhamana kutofuata au kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utawala bora. Hayo yamebainishwa jana na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Fabian Pokela, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuriwa na viongozi kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali. Pokela alisema kutokuzingatiwa kwa ushauri uliomo katika taarifa hizo za CAG, kumechangia kuendelea kuwapo kwa upungufu na kasoro zinazoendelea kubainishwa kila mwaka katika halmashauri mbalimbali. “Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hazifanyiwi kazi ipasavyo na maofisa masuuli ili kuleta tija katika kuboresha na kuimarisha  uwajibikaji, hali hii inasababisha kutozingatia na kutekeleza ipasavyo mapendekezo na ushauri unaotolewa katika taarifa hiyo,” alisema Pokela. Alisema pamoja na kwamba majukumu ya CAG ni kutoa mapendekezo na ushauri kwa kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa, lakini kumeendelea kuwapo kwa mmomonyoko wa maadili kwa watendaji wenye dhamana kwa kutofuata au kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utawala bora. Pokela aliwataka wananchi kushiriki katika kuhimiza maadili katika ngazi zote kuanzia familia katika malezi ya watoto na vijana, hususani shuleni na hatimaye kuhimiza uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa katika ngazi zote za utumishi wa umma na uongozi. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema Serikali ya awamu ya tano imeweka nguvu nyingi katika kuhakikisha  maadili ya viongozi wa umma yanazingatiwa ili kupambana na rushwa na vitendo vya ufisadi ambavyo vilikuwa vimekithiri katika jamii, hivyo ni vyema kila mtumishi akazingatia sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika utendaji wake.
KITAIFA
Na SAADA SALIM -DAR ES SALAAM, MSHAMBULIAJI wa timu ya Azam FC, Kipre Tchetche, amedhamiria kuachana rasmi na klabu hiyo kwa kuendelea kuushinikiza uongozi umruhusu kuondoka ili akatafute maisha sehemu nyingine. Tchetche ambaye ni raia wa Ivory Coast, hadi sasa hajajiunga na wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao na Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani. Akizungumza na MTANZANIA jana, Tchetche alisema anasubiri ruhusa ya kuondoka Azam kwani amepata dili katika klabu moja kubwa nchini Misri. Tchetche alisema amefanya mawasiliano ya barua pepe na viongozi wa klabu hiyo akiomba kuondoka lakini hajajibiwa chochote, huku akidai kuwa anahitaji baraka zao kabla ya kucheza timu nyingine. Straika huyo ambaye ni kinara wa kupachika mabao Azam, alisema anahitaji kubadili maisha ya soka kwa kuwa amecheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa muda mrefu hivyo amechoka. “Juhudi zangu za kufanya mawasiliano na viongozi na pia wakala wangu kuwatumia ujumbe wa barua pepe ili kufikia makubaliano nikacheze Misri baada ya kupata ofa, zimegonga mwamba kwani hawajibu lolote. “Nimebakiza mkataba wa mwaka mmoja, lakini  nimepata ofa nzuri Misri ila viongozi wangu wamekata mawasiliano na mimi, kwa sasa sina furaha ya kucheza soka nchini Tanzania,” alisema Tchetche. Naye Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alikiri kwamba ni kweli Tchetche hajaripoti mazoezini na pia hajatoa sababu za msingi za kuchelewa, hali inayowapa wasiwasi  kutokana na kulazimisha kutaka kuondoka. Kawemba alisema kama amepata timu  nyingine inatakiwa kufuata taratibu za usajili  kwani thamani ya mchezaji huyo ni dola 150,000  za Marekani sawa na Sh milioni 322.
MICHEZO
Na MASANJA MBAULA- PEMBA   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindunzi, Dk. Ally Mohamed Shein  amesisitiza kuwa huduma za vipimo vya CT Scan na X-ray  pamoja na huduma za mama na mtoto zitaendelea kutolewa bure katika Hospitali za Mnazi Mmoja  na  Abdalla Mzee mkoani pemba. Alisema kutolewa bure kwa vipimo hivyo ni utekelezaji wa ilani ya  uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015  – 2020. Dk. Shein ameyaeeleza hayo   mkoani pemba wakati akifungua Hospitali ya Abdalla Mzee ambayo imejengwa upya kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China. Alisema kwamba ili kufanikisha azma hiyo serikali imejipanga kupeleka madaktari bingwa na wataalamu wa kutosha katika hospitali hiyo ambao watashirikiana kutoa huduma kwa wananchi. “Nasisitiza kwamba huduma za mama na mtoto zitaendelea kutolewa bila ya malipo katika hospitali zote za Unguja na Pemba,” alisema. Alisema lengo la kuipatia vifaa Hospitali ya Abdalla Mzee na kuifanya kutoa huduma bora, sawa na hospitali ya Mnazi mmoja na hivyo kuwapunguzia gharama  wananchi kwa kufuata huduma  hizo hospitali za Unguja.Aliwataka madakatari na wahudumu wa  afya kuwa waadilifu na kufuata maadili ya taaluma yao na kutumia lugha vizuri na hekima wakati wa kuwahudumia wagonjwa. “Nawasisitiza sana madaktari na wahudumu katika hospitali hii tumeifungua ikiwa na vifaa vya kisasa ni budi kufuata maadili na kutumia lugha za hekima na busara kwa wananchi wakati wanapokuja kufuata huduma,” alisema. Alisema Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mohamedd Thabit Kombo amesema kukamilika hospitali hiyo  na kuwepo wafanyakazi katika hospitali hiyo ni kuongeza huduma za afya kwa wananchi kama ilivyo ilani ya uchaguzi ya zanzibar. Waziri ameipongeza Serikali ya China kwa misaada yake  kwa zanzibar na kuahidi kuendelea kuithamini kudumisha undugu na uhusiano uliopo baina ya watu wa China na Zanzibar. balozi wa China   nchin, i Dk. LU Youqing alisema wataendeleza  kuisaidia Zanzibar katika nyanja mbalimbali ikiwamo elimu,afya na michezo. Pia ameahidi kuendelea kuleta madaktari bingwa ambao watafanya kazi katika hospitali hiyo na kuwapa mafunzo madaktari wazalendo waweze kuvitumia vifaa vya kisasa ambavyo vimewekwa katika hospitali hiyo.
KITAIFA
NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM JINA la mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Samatta, limegeuka gumzo na kivutio nchini Algeria na kuwapaisha Watanzania wanaoishi huko. Samatta, ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi cha Stars kitakachoshuka dimbani leo kuikabili Algeria ‘The Desert Foxes’ katika mchezo wa marudiano wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, ameendelea kujikusanyia sifa kutokana na kiwango chake. Katika mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Taifa juzi, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, huku Samatta akifunga bao la pili katika dakika ya 44 na Elias Maguli akipiga la kwanza huku Islam Slimani, akiipatia Algeria mabao mawili ya kusawazisha. Straika huyo alikuwa miongoni mwa wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu akilingana na Bakri Al-Madina wa El Merreikh, wote wakiwa na mabao saba, pia aliiwezesha klabu yake kutwaa ubingwa wa michuano hiyo dhidi ya USM Alger ya Algeria. Kituo cha redio cha Clouds FM jana asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast, kiliripoti taarifa ya mwanafunzi wa Tanzania anayesoma nchini Algeria pamoja na Watanzania wote wanaoishi nchini humo kuwa wamepachikwa jina la nyota huyo. “Yaani huku kila mtu anaitwa Samatta, nchi yetu ya Tanzania imekuwa kivutio sasa kila mahali wanatuzungumzia sisi tu. Mitaani kote ukipita na ukiwa mtu mweusi au unatokea Tanzania basi wanakuita Samatta, amekuwa maarufu sana hapa. “Ukionekana umevaa jezi ya Tanzania tu utasikia Samatta Samatta huyo anapita, yaani nchi yetu imekuwa gumzo, ni vyema mchezaji huyu akalilinda jina lake kwa kuongeza juhudi zaidi,” alisema mwanafunzi huyo. Aliongeza kuwa: “Tunaamini timu yetu itafanya vizuri na wachezaji wetu wengine kama Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu wataweza kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu kufanikisha ushindi wetu.” Makali ya Samatta yamemfanya awekwe kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Wachezaji wa Ndani itakayotolewa mwakani, huku akipewa nafasi kubwa kuibeba.  
MICHEZO
Na JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imekabidhi magari 12 kwa wakurugenzi wakuu na viongozi wa taasisi na vitengo wa mradi wa kitaifa wa unaohusisha shughuli za maendeleo ya uvuvi,  Southwest Indian Ocean Fisheries Covernance and Shared Growth (SWIOFish). Magari hayo ambayo yamefadhiliwa na Benki ya Dunia, yamegharimu Sh bilioni 1.4 na yalikabidhiwa na Katibu Mkuu wa Uvuvi, Dk Yohana Budeba, kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba. Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Budeba alisema mradi huo unahusisha nchi zilizoko Magharibi mwa ukanda wa Bahari ya Hindi, ambapo kwa Tanzania ulianza Juni 22, 2015, ikiwa na lengo la kuzijengea uwezo wa nchi katika kusimamia rasilimali za bahari. “Pamoja na mchango wa uvuvi kuwa mkubwa katika taifa, sekta hii imekuwa na changamoto nyingi, zikiwamo uvunaji usio endelevu kwa rasilimali  za uvuvi, hivyo kuhatarisha ajira za Watanzania. “Changamoto nyingine ni kuwapo kwa uhaba wa taarifa za kitafiti na takwimu sahihi za uvuvi kuhusu vitendo haramu, upungufu wa elimu na uelewa kwa sehemu kubwa ya jamii kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi,” alisema Dk. Budeba.
KITAIFA
NEW YORK, MAREKANI MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, amesema kwa hatua aliyofikia anapata maumivu ya tumbo wakati wa kulala kiasi cha kukosa usingizi. Mrembo huyo anatarajia kupata mtoto wa pili, baadaye Desemba, mwaka huu na mume wake Kanye West, lakini kutokana na hatua ambayo ujauzito wake umefikia, anadai inampa usumbufu mkubwa. “Natarajia kupata mtoto wa pili hivi karibuni, lakini kwakweli kwa sasa napata maumivu ya tumbo wakati wa kulala, hii ni dalili ya kuwa siku yoyote naweza kupata mtoto. “Hadi kufikia Desemba 26, tayari nitakuwa na mtoto wa pili, nitakuwa na furaha kubwa kuongeza familia yangu,” alisema Kim.
BURUDANI
BAO pekee lililofungwa na mshambuliaji David Molinga, lilitosha kuipandisha Yanga hadi nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaa, jana na kumalizika kwa 1-0 Molinga alifunga bao hilo dakika ya 51, akipokea pasi iliyopigwa na Ditram Nchimbi na kufikisha idadi ya mabao sita katika orodha ya wafungaji ambapo anayeongoza ni Meddie Kagere wa Simba kwa mabao 12. Matokeo hayo yameifanya Yanga kutoka kwenye nafasi ya sita na kupanda hadi ya nne ikiwa na pointi 31, katika michezo 16 waliyocheza sawa na Namungo FC ambayo inashika nafasi ya tatu zikitofautina kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa na idadi ya michezo. Yanga inazizidi pointi moja moja, Kagera Sugar, Coastal Union na Polisi Tanzania ambazo zote zimecheza mechi 18 na wanazidiwa pointi 16 na vinara, Simba ambao pia ndio mabingwa watetezi. Yanga walilipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu msimu uliopita uliochezwa Aprili mwaka jana Morogoro na msimu huu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 4-2. Ukosefu wa umakini kwenye safu ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar kumewafanya washindwe kusawazisha bao hilo kwani walitengeneza nafasi ambazo hakuweza kuzitumia. Pia washambuliaji wa Yanga wangeweza kupata mabao zaidi endapo wangetulia kwani walikosa nafasi za wazi za kuwapa mabao na sifa zimuendee kiungo mkongwe, Abduhalim Humud ‘Gaucho’ aliyemdhibiti kiungo Bernard Morrison.Kikosi cha Yanga: Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Patrick Sibomana/Ditram Nchimbi dakika ya 46, Haruna Niyonzima, David Molinga/ Yikpe Gislain dakika ya 68, Mapinduzi Balama na Bernard Morrison/Abdulaziz Makame dakika ya 85. Mtibwa Sugar: Shaaban Kado, Kibwana Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Henry Shindika, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’, Ismail Mhesa/Juma Luizio dakika ya 56, Ally Makarani, Riphat Msuya/ Haroun Chanongo dakika ya 81, Awadh Juma na Salum Kihimbwa/Omary Hassan dakika ya 73. Michezo mingine iliyochezwa jana, Azam FC ikiwa Uwanja wa Samora, Iringa ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, na kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 37, Simba ikiwa kileleni kwa pointi 47 na Mbeya City bado ipo kwenye hali mbaya kwani ipo katika nafasi ya 18 ikiwa na pointi 14.Katika mchezo wa JKT Tanzania na Polisi Tanzania ambao ulisitishwa juzi dakika ya 53 kufuatia Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujaa maji na kuahirishwa wakiwa hawajafungana umemaliziwa jana na Polisi Tanzania kushinda bao 1-0. Tanzania Prisons ikicheza katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC ambapo kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons imefikisha pointi 21 katika nafasi ya 12 na KMC imefikisha pointi 17 katika nafasi ya 17.
MICHEZO
Beatrice Mosses, Manyara Wazee wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Babati, Usharika wa Babati wamezuia ruzuku ya sadaka zinazopelekwa kwenye dayosisi na majimbo kwa madai kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk Solomon Masangwa kukataa kumhamisha Mkuu wa Jimbo la Babati, Niiteel Panga. Sakata hilo lilianza Jumapili iliyopita na jana baada ya Francis Lazaro ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Matengenezo ya Kanisa, kuingilia katikati ya ibada bila ruhusa ya Mchungaji Godlsten Mkenda wa Usharika wa Babati, na kudai wamechoshwa na mienendo ya mkuu huyo wa jimbo. “Tulikubaliana mama ahamishwe lakini Novemba 2, mama akarudi Jimboni tukasema sawa tumuache akae kae ofisini, Novemba 6 tulikaa tukafanya kikao chetu cha tathmini kuwa mama amesharudi sasa tunafanyaje, tukakubaliana kwamba kwa kuwa amerudi na sisi hatuna haja ya kupigana nae cha msingi hapa ni kuanza kuzuia sadaka. “Mmemsikia mzee wa Kanisa alivyosema kwenye matangazo kuwa taarifa nyingine mtasikia baadae ni kwamba hakuna uwiano ulioenda usharikani, jimboni wala Dayosisi, sadaka zote za Jumapili iliyopita zipo kwenye akaunti ya mtaa kwa hiyo niwaombe sana leo tutoe sadaka kwa wingi maana zinaingia kwenye akaunti ya mtaa iliyopo Benki ya Posta na fedha zenu ziko salama kabisa,” amesema. Pamoja na mambo mengine amesema Novemba 13 walikaa kikao wakakubaliana lazima kuwe na maazimio na azimio la kwanza ni lazima mkuu wa jimbo ahamishwe, azimio jingine ni kuendelea kuchukua sadaka zote na kupeleka kwenye akaunti ya mtaa. “Azimio kama Dayosisi haitamuhamisha mkuu wa jimbo tutapeleka kesi mahakamani na tutamfungulia kesi ya udhalilishaji na tunazo ‘clip’ nne zilizosimama,” amesema Lazaro.
KITAIFA
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kuangalia upya gharama za umeme zinazotozwa na wazalishaji binafsi wa umeme kwa wananchi ili kuwa na muongozo wa pamoja badala ya kila mzalishaji kutoza gharama yake.Aliyasema hayo Dodoma wakati wa kikao chake na waendelezaji wa miradi midogo ya umeme wanaonufaika na ruzuku ya Mfuko wa Nishati Vijijini ulio chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).“Suala la gharama za matumizi ya umeme wanazotozwa wananchi lazima Ewura mpitie upya na kuweka mwongozo, mfano kuna wananchi waliopo vijijini wanatozwa Sh 750 kwa uniti moja badala ya Sh 100 na unaweza kuta gharama anazotoza mzalishaji wa umeme jua wa eneo moja zinatofautiana na mzalishaji wa umeme jua wa eneo jingine,” alisema Dk Kalemani.Alisema kazi ya kujadili bei za umeme ishirikishe pia watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na REA na kueleza kuwa kama kuna sababu za msingi zinazosababisha wazalishaji hao wa umeme kutofautiana katika utozaji wa bei za umeme, ziwekwe wazi kwa serikali.Aidha, aliwaeleza wazalishaji hao wa umeme kuhusu msimamo wa serikali wa kuunganisha umeme vijijini kwa gharama ya Sh 27,000 tu kwani kuna wananchi wamekuwa wakilalamika kutozwa gharama kubwa.Dk Kalemani amewakumbusha kuzingatia gharama hiyo ya serikali baada ya wazalishaji hao kutaja gharama za uunganishaji umeme wanazotoza katika maeneo tofauti, ambako sehemu nyingine wananchi wanatozwa Sh 40,000 au Sh 150,000 au Sh 50,000 na sehemu nyingine wanaunganishwa kwa kukatwa katika bili za umeme.Katika kikao hicho, wazalishaji hao wameeleza kuhusu utekelezaji wa kazi ya kuunganishia umeme wananchi, ambako waziri aliwapongeza kwa kazi hiyo ambayo imewezesha wateja zaidi ya 10,000 kuunganishwa na umeme na vijiji zaidi ya 40 kusambaziwa umeme.Hata hivyo, Dk Kalemani amewataka kukamilisha kazi ya usambazaji umeme kwa maeneo waliyopangiwa ifikapo Juni 2019, na kuwataka mameneja wa Tanesco kuhakikisha wanasimamia pia miradi hiyo badala ya kusimamia miradi ya serikali pekee ili kuhakikisha inafanyika kwa ufanisi.Kikao hicho kimehudhuriwa na watendaji wa Wizara ya Nishati, REA na Tanesco wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimaliwatu, Raphael Nombo ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.
KITAIFA
Jengo kongwe la Kanisa Katoliki la Notre Dame, jijini Paris, Ufaransa, limeungua kwa moto usiku wa kuamkia leo, Jumanne.Chanzo cha moto bado hakijajulikana japo paa la jengo hilo pamoja na mnara wa msalaba, vimeteketea kabisa na kuanguka chini.Hata hivyo muundo wa kanisa hilo lenye umri wa miaka 850, haujaharibika ikiwa ni pamoja na minara miwili ya kengele.Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron ameliita tukio hilo ‘janga la kutisha’.Askari wa zimamoto wameeleza kuwa wanadhani moto huo unatokana na ukarabati uliokuwa ukiendelea kwenye kanisa hilo baada ya kujitokeza nyufa kwenye kuta zake.
KITAIFA
NA OSCAR ASSENGA, TANGA ULIPUAJI wa milio kwenye pikipiki (Exose) maarufu kama jango moshi, umetajwa kuwa miongoni mwa ugaidi mpya unaoitesa jamii ya Watanzania wengi ambao wameshindwa kuishi kwa amani. Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi limetakiwa kuona namna ya kudhibiti hali hiyo. Hayo yamesemwa jana na Sheikh wa Msikiti wa Bilal Muslim wa mjini Tanga, Mohamed Mbaraka, wakati wa kikao cha pamoja baina ya viongozi wa dini na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba. Alisema jambo hilo halina tofauti na ugaidi kutokana na kuwa milio hiyo imekuwa ikilipuliwa hadi saa nane usiku watu wakiwa wamelala majumbani mwao. “Ukiangalia ndugu yetu Kamanda wa Polisi, watu wamekuwa wakifikiria ugaidi ni vitendo vibaya, viovu tu, hata suala la ulipuaji wa milipuko kwenye pikipiki maarufu kama jango moshi, nao ni hatari,” alisema. Naye Mchungaji wa Kanisa la Moravian Chumbageni, Ibrahim Nzowa, aliunga mkono hoja hiyo na kusema jambo hilo ni hatari. Naye Kamanda Wakulyamba aliwataka viongozi wa dini kuacha kuwakumbatia watu wachache wanaotumia mianya ya dini kufanya vitendo viovu.  “Viongozi wa dini wana nguvu za Mwenyezi Mungu na kiroho ambazo wanaweza kuzitumia kwa ajili ya kuibadilisha jamii… umoja wenu huu ni muhimu katika masuala ya usalama,” alisema.
KITAIFA
Suala la mahusiano ni safari ndefu ambayo huwahusisha waliomo na wasiomo kwa njia moja ama nyingine Yapo baadhi ya mambo ambayo kwa kawaida demu hatokubali kufichua hadi pale unapomuoa ama kwa wakati mwingine hadi kifo Hizi ni baadhi yazo: 1.Aliavya ujauzito Si jambo rahisi kwa mwanadada kufungua roho na kukueleza kuhusu jinsi alivyopata uja uzito bila kutarajia na hatimaye kuavya mimba. Mara nyingi wanafahamu kuwa suala hilo huweza kutumika na mume kama njia ya kusambaratisha uhusiano ama hata kumfedhehesha. Ingawa wengi huweka siri hii hadi kifo, wapo baadhi ya wanadada ambao hukubali kufichua siri hii baada ya kueolewa wakishathibiti ndoa na kumfahamu kiundani zaidi mpenzi. 2. Anakojoa kitandani Kwa kawaida tunajua kwamba watu hukojoa kitandani wakiwa watoto lakini kwa wengine, tendo hilo huwapita hadi pale wanapokomaa. Ni wazi kuwa kujoa kitandani ni aibu na hakuna mwanadada yeyote ambaye huweza kuwa na ujasiri kumueleza mpenziwe kuwa anakojoa kitandani anapolala. Ikiwa utapata kujua,  ni pale tu mambo yanapomuendea mrama akakurashia mnapolala 3. Anaota ndoto za kutisha usiku. Kila mtu huota, nam, ndoto nzuri na hata zile mbaya. Wapo baadh ya watu ambao kuweza kutoa vita usiku wanapoota ama hata kuanza kuimba. Kunao wale wanoota hadi kufika kiwango cha kuwapiga waliolala nao bila ya kujua ama hata kuenda hadi jikoni na kujipakulia chakula na kula pasi kujua kuwa wapo ndotoni. Si rahisi kwa mwanadada yeyote ambaye ana ulemavu kama huo kuwa na ujasiri wa kumueleza mpenziwe hali halisi. 4. Wazazi ni waganga Ni kweli kuwa hakuna yeyote ambaye ana uwezo wa kuwachagua wanaokuwa wazazi wake. Baada ya kuzaliwa, ni wazi kuwa wale waliokuzaa ndio wazazi hata ikiwa wana taba mbaya kiasi kipi. Si rahisi kwa mwanadada ambaye wazazi wake ni waganga kuwa na uwezo wa kumuelezea mpenziwe wazi kuwa wazazi wake wana hila kama ya uganga, ama ushirikina.
BURUDANI
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Zainab Vullu amewaomba wanawake wa wilaya ya Kibiti kucheza upatu wa kununulia bima za afya na sio vyombo. Zainab alisema hayo alipozungumza na wanawake wa wilaya hiyo kwenye ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM Kibiti.“Mimi nawaomba wanawake wenzangu tuache kutunza vyombo, badala yake tutunzane kadi za CHF(Bima ya Afya ya Jamii) iliyoboreshwa ili tuweze kupunguza gharama za matibabu pindi tunapougua au kuuguliwa ndani ya familia,”alisema.Aliwaeleza kuwa kila mmoja akiuza kuku wawili na kujipatia bima kwa gharama ya Sh 30,000 ambayo itaweza kutibia watu sita ndani ya familia moja ambao ni baba, mama na wategemezi wanne. Alisema matumizi ya bima yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini usiokuwa wa lazima kwa kuokoa gharama za matibabu.Aidha alitaja kuwa matumizi ya bima yanapun guza presha pindi mama anapokuwa mjamzito hasa unapofika wakati wa kujifungua kwa kusaidia kupata huduma kwa uhakika.Pia aliwaomba wanawake hao kufikisha ujumbe huo kwa akinababa na waume zao kwani suala la afya ya familia ni jukumu la kila mmoja.
KITAIFA
Na WAANDISHI WETU – DAR ES SALAAM   WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, amewasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa na ukomo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/19, huku akiainisha maeneo ya vipaumbele. Dk. Mpango aliwasilisha mpango huo mjini Dodoma jana mbele ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika maelezo yake, Dk. Mpango alieleza vipaumbele katika mwaka huo wa fedha, kwamba ni pamoja na     miradi ya kielelezo itakayopewa msukumo wa kipekee. “Miradi hiyo itakayotekelezwa ni pamoja na kituo cha kuzalisha umeme wa maji katika Mto Rufiji, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge, kuboresha Shirika la Ndege Tanzania na ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga. “Miradi mingine ni uzalishaji wa makaa ya mawe na umeme wa Mchuchuma na chuma cha Liganga, uendelezaji wa shamba la miwa na ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, ujenzi wa Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini. “Uendelezaji wa kanda maalumu za kiuchumi hususani, Bagamoyo na Kigamboni, uanzishwaji wa kiwanda cha kusindika gesi asilia kuwa kimiminika mkoani Lindi, kuongeza idadi ya wataalamu katika fani mbalimbali na kuimarisha shughuli za Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO). “Mingine ni kiwanda cha ngozi na bidhaa za ngozi, Karanga, mradi wa magadi soda ulioko Bonde la Engaruka, Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CARMATEC) na viwanda vya Nyumbu na Mzinga. “Miradi ya kufungamanisha maendeleo ya viwanda na maendeleo ya watu pamoja kuimarisha sekta ya elimu, afya, barabara, reli, barabara, viwanja vya ndege na usafiri wa majini,” alisema Dk. Mpango. Akizungumzia sekta ya kilimo, Dk. Mpango alisema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, itaongeza upatikanaji wa zana na pembejeo za kilimo, itaongeza huduma za ugani, itaboresha upatikanaji wa miundombinu ya hifadhi ya mazao na masoko. “Pia itatatua vikwazo mbalimbali vinavyosababisha viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi zitokanazo na kilimo kushindwa kushindana na bidhaa husika kutoka nje,” alisema. DENI LA TAIFA Kuhusu deni la taifa, Dk. Mpango alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, lilikuwa limefikia Sh trilioni 47.756 na kwamba tathimini zinaonyesha bado ni himilivu. Kwa mujibu wa Dk. Mpango, deni la nje lilikuwa Sh trilioni 34.148, sawa na asilimia 71.5 na deni la ndani ni Sh trilioni 13.607, sawa na asilimia 28.5. “Lakini, ongezeko la deni hilo kwa kipindi cha Juni 2016 hadi Desemba 2017 limetokana na mikopo mipya na mabadiliko ya kiwango cha ubadilishaji fedha. “Uwiano wa deni la ndani na nje kwa pato la taifa kwa mwaka 2017/18 ni asilimia 34.4 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 56, hivyo deni bado lipo chini ya kiwango cha hatari,” alisema. HALI YA UCHUMI Kuhusu mwenendo wa uchumi, Dk. Mpango alisema umeendelea kukua katika viashiria vingi. Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba 2017, uchumi ulikua kwa kiwango cha wastani wa asilimia 6.8. “Kiwango hicho ni cha juu zaidi ikilinganishwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya (asilimia 6.1), Rwanda (asilimia 6.0), Uganda (asilimia 5.5), Burundi (asilimia 0.0) na Sudani Kusini (asilimia hasi 6.3). “Kwa upande wa nchi zote za Bara la Afrika, kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania ilikuwa ya tatu baada ya Ethiopia yenye asilimia 8.2 na Ivory Coast yenye asilimia 7.6. “Ukuaji huo wa uchumi, umechangiwa na ongezeko la shughuli za uchimbaji madini na mawe, habari na mawasiliano, usafirishaji na hifadhi ya mizigo, uzalishaji viwandani na ujenzi. “Kwa upande wa kilimo, katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2017, sekta hiyo ilikua kwa asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 2.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2016. “Kutokana na hali hiyo, Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa pembejeo za kilimo, huduma za ugani na maghala ya kuhifadhi mazao na upatikanaji wa masoko,” alisema. Pamoja na hayo, alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017, mfumuko wa bei ulikuwa wastani wa asilimia 5.3 na umeendelea kupungua na kufikia asilimia 4.1, Februari mwaka huu. Kuhusu akiba ya fedha za kigeni katika kipindi kinachoishia Desemba 2017, alisema imefikia Dola za Marekani milioni 5.9 ikilinganishwa na Dola za Marekani, milioni 4.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2016. Pamoja na hayo, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuongeza ukwasi katika uchumi na ukuaji wa mikopo yenye gharama nafuu kwa sekta binafsi. “Kutokana na hali hiyo, mwenendo wa mikopo kwa sekta binafsi umeanza kuongezeka kutoka kiwango cha ukuaji hasi wa asilimia 1.5 Oktoba 2017 hadi ukuaji chanya wa asilimia 2.0 Januari 2018. “Aidha mikopo chechefu imeanza kupungua kutoka asilimia 12.5 ya mikopo kwa sekta binafsi mwezi Septemba 2017 hadi kuwa asilimia 11.2 Desemba 2017,” alisema. Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
KITAIFA
    Na JUSTIN DAMIAN, SEHEMU nyingi duniani, watu wanapenda kunywa kahawa ingawa kwa hapa Tanzania wanywaji ni wachache. Kahawa husaidia kumfanya mnywaji kujisikia vizuri baada ya muda mwingi wa kufanya kazi. Hata hivyo, wapo baadhi ya watu ambao hufikiri kuwa kahawa ni mbaya kwa afya. Lakini utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Edinburg na Southmpton nchini Uingereza umeonyesha kuwa unywaji kahawa unamlinda mnywaji kupata ugonjwa wa saratani ya ini ambao ni hatari na hauna tiba. Watu ambao wanaiponda kahawa wanasema, kinywaji hicho kina caffeine ambayo inasababisha ugonjwa wa moyo na kuwafanya wanaougua magonjwa ya moyo kufariki mapema zaidi. Tofauti na mtizamo huo, sasa wanasayansi wanasema utumiaji mzuri wa kahawa unaweza kumwepusha mtumiaji na hepatocellular carcinoma ambayo ni aina ya saratani ya ini. Timu kubwa ya watafiti walichunguza data kutoka kwenye tafiti 26 zilizohusisha zaidi ya washiriki milioni mbili. Watafiti hao waliobobea kwenye masuala ya afya ya umma, waligundua kuwa saratani ya ini aina ya hepatocellular carcinoma ilikuwa ikiwaathiri takribani watu 50 katika kila watu 1000 waliwachunguza katika utafiti huo. Hata hivyo, waligundua kuwa katika kundi la wanywaji wa kahawa, watu 33 walionekana kuwa wameathirika kati ya watu 1000 ikiwa ni upungufu wa asilimia 40 ukilinganisha na kundi la wasiokunywa kahawa. Watafiti hao pia waligundua kadiri unavyokunywa kahawa zaidi, ndivyo ambavyo unapunguza uwezekano wa kupata aina hii ya saratani. Timu hiyo ilisisitiza kuwa unywaji wa kikombe kimoja cha kahawa yenye caffeine inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa huo usio na tiba kwa asilimia 20 huku unywaji wa vikombe viwili vya kahawa ukiwa unapunguza uwezekano kwa asilimia 35. Hepatocellular carcinoma inashika nafasi ya pili kati ya magonjwa wa saratani yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani. Kujilinda dhidi ya ugonjwa huu ni jambo jema kwa kuwa hauna tiba lakini pia wanasayansi hao wanasisitiza unywaji kahawa uliopindukia si salama kwa afya ya mtumiaji na hivyo kuwataka watumiaji watumie kwa kiasi. Wanasayansi wanawezaje kujua ni kiasi cha kahawa mnywaji akitumia hakiwezi kumletea madhara ya kiafya? Dk. Oliver Kennedy wa Chuo Kikuu cha Southampton anasema; “hatua inayofuata ni kwa watafiti kuchunguza ufanisi kupitia utafiti usiochagua sampuli maalum kwa kuzingatia wanywaji wa kahawa ambao wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu, watu wengi walichangia katika mafanikio ya utafiti huu.” Pamoja na faida hiyo, unywaji kahawa una faida nyingi ikiwamo kupunguza maumivu ya misuli baada ya kazi. Unywaji kahawa wa kiasi pia unapunguza uwezekano wa kupata ungonjwa kisukari namba mbili – Diabetes Type 2. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani unaonyesha kuwa unywaji wa kikombe kimoja cha kahawa kwa siku unapunguza uwezekano wa kupata aina hiyo ya kisukari kwa asilimia tisa. Unywaji kahawa pia unapunguza uwezekano wa kujiua pamoja na mfadhaiko (depression). Utafiti uliofanyika kwa kipindi cha maika 10 uliohusisha wauguzi wanawake 86,000 ulionyesha kupungua kwa uwezekano wa kujiua kwa wale waliokuwa wakitumia kahawa. Utafiti mwingine ulifanyika na Shule ya Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani  ulionyesha kuwa wanawake wanaokunywa vikombe vine au zaidi vya kahawa wanapunguza uwezekana wa kupata mfadhaiko kwa asilimia 20.
AFYA
Na MWANDISHI WETU -DODOMA BAADHI ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji, wamehofia gharama za nyumba zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kusema ni kubwa na haziwalengi wananchi wa kawaida. Wamesema kwamba pamoja na NHC kueleza mara kwa mara, kwamba nyumba hizo zinauzwa kwa gharama nafuu, kauli zao haziwezi kukubaliwa kwa kuwa zinauzwa kwa bei kubwa ambazo mwananchi wa kawaida hawezi kuzimudu. Wabunge hao walitoa kauli hizo jana, walipokuwa wakizungumza wakati wa ziara yao ya kutembelea ujenzi wa nyumba 300 unaoendelea katika eneo la Iyumbu, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Akizungumza katika ziara hiyo, Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), alisema kama NHC wanawalenga wananchi wa kawaida, wanatakiwa kuangalia uuzaji wa nyumba hizo ili wengi waweze kuzinunua. “Mmekuwa mkisema mnauza nyumba kwa gharama nafuu, lakini ukweli ni kwamba nyumba zenu mnazouza kwa gharama ya shilingi milioni 50, 60 na nyingine milioni 99, haziwezi kununuliwa na wananchi wa kawaida. “Kwa hiyo, nawaomba muangalie upya bei zenu na kama tatizo ni VAT mnayotozwa kupitia vifaa vya ujenzi, ielezeni Serikali ili iangalie namna ya kuondoa VAT hiyo,” alisema Mwakajoka. Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM), alilalamikia bei za nyumba hizo na kusema zinauzwa kwa gharama kubwa tofauti na nyumba zinazojengwa na Taasisi ya Viguta inayojenga nyumba kama za NHC na kuziuza kwa bei nafuu. Kwa upande wake, Mbunge wa Chambani, Yusuph Salim Hussein (CUF), alisema kama NHC wanajenga nyumba ili kuwauzia wananchi wa kawaida, lazima washushe bei na kuuza kama inavyouza Taasisi ya Viguta. Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Mali za NHC, Haikamen Mlekio, alisema katika eneo hilo la Iyumbu, wanatarajia kujenga nyumba 300 ingawa kwa sasa wameshajenga 151. Kwa mujibu wa Mlekio, mradi huo ulianza Desemba mwaka jana na unatarajia kukamilika Desemba 4, mwaka huu.
KITAIFA
MKUU wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo amewataka wananchi waliovamia eneo la Pangani wilayani Kibaha lenye ukubwa wa ekari 500 na kujigawia viwanja kuondoka mara moja.Amesema hatua hiyo inalenga katika kuiacha Halmashauri ya Kibaha kufanya taratibu ya kulirudisha eneo hilo serikalini baada ya mmiliki wake kushindwa kuliendeleza na kulifanya kuwa sehemu ambayo watu wanauawa na kutupwa humo.Amelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mtu yoyote atakayekutwa kwenye eneo hilo na wale waliouziwa kwenda polisi ili wahusika ambao ni matapeli waweze kukamatwa kwa kuwauzia watu kinyume cha sheria kwani eneo hilo linamilikiwa kihalali.Ndikilo aliyasema hayo alipotembelea eneo hilo ambalo linamilikiwa na mtu anayefahamika kwa jina la Seamens na maeneo mengine yenye ukubwa wa ekari 500 yanayomilikiwa na watu wengine wawili ambao hawajaendeleza kwa muda mrefu hivyo wananchi kujigawia viwanja wakidai kuwa eneo hilo limekuwa sehemu ya wahalifu kufanya mauaji au kutupa maiti kutoka maeneo mbalimbali.Alisema kuwa kuna watu 18 ambao wanajifanya ndiyo viongozi na wamewagawia watu hatua 30 kwa 30 kwa kila mtu na eneo hilo wahalifu wameligeuza la kupumzikia baada ya kufanya uhalifu au wanapowateka watu au kuwaua."Kuanzia sasa sitaki kuona mtu na Jeshi la Polisi likamate mtu yoyote watakayemkuta humu kama achukuliwe hatua kwani ardhi haipatikani kwa njia hizo kwa sasa acheni serikali iendelee na taratibu zake ," amesema Ndikilo.Aidha alisema kuwa kwa wale waliouziwa watoe taarifa polisi ili wahusika wa kuuza wakamatwe na Mkuu wa Wilaya awasake ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao kwani hawawezi kuuza eneo la mtu ambaye anamiliki kisheria hata kama hajaendeleza kwani kuna taratibu zake za kumiliki ardhi lakini si kwa njia hiyo.Aliitaka kamati iliyoundwa kinyemela ili kuwauzia watu maeneo hayo iwarudishie fedha wale wote waliowauzia kwani wamewatapeli na serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hilo .Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumter Mshama amesema, wananchi hao kutoka maeneo mbalimbali ya Kibaha na Dar es Salaam waligawana maeneo hayo ambayo yanamilikiwa na watu watatu.Mshama alisema kuwa mtu wa kwanza eneo lake lina ukubwa wa ekari 300 mwingine 200 na mwingine 500 ambapo wananchi waliamua kugawana viwanja kinyume cha sheria wakidai kuwa eneo hilo limekuwa likitumika kwa vitendo vya kihalifu.Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amesema eneo hilo lina wamiliki hivyo ni vema kukaa nao na kuona watawekaje mipango miji ya serikali katika kuupanga mji wa Kibaha.
KITAIFA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa. Alisema serikali kupitia Bodi ya Mazao Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.Waziri Mkuu aliyasema jana alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma. Alisema bodi hiyo inaendelea kufanya tathmini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora na baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika. Waziri Mkuu alisema serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.“Lengo la serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ndipo Rais John Magufuli alisitisha ununuzi baada ya kuona wakulima wanataka kudhulumiwa,” alisema. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu hadi sasa tayari tani 181,000 zimeshakusanywa, hivyo aliwataka wakulima wa zao hilo nchini waendelee kuiamini serikali yao.Kadhalika, Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono jitihada za serikali kukuza uchumi kwa kupitia sekta ya viwanda. Awali Meneja Utawala wa kiwanda cha Terra, Peter Ngwale alisema uwezo wao ni kubangua tani 6,000 kwa mwaka, ambapo tayari wamebangua tani 3,000 na kuiomba serikali iwasaidie katika suala la ubora wa korosho kwa kuwa kiwango cha ubora kinachoandikwa kinakuwa tofauti na uhalisia wa korosho yenyewe.
KITAIFA
Christian Bwaya KILA mwaka mpya unapoanza, watu wengi hujiwekea malengo mapya. Kichocheo kikubwa cha malengo haya ni ule msisimko wa kuingia mwaka mpya lazima kuambatane na mabadiliko ya maisha yetu. Bahati mbaya, wengi wanaojiwekea malengo haya ya mwaka mpya huyasahau muda mfupi baada ya kuuzoea mwaka. Kwanini watu husahau malengo yao? Sababu ni pamoja na tabia ya watu kuweka maazimio kwa msisimko tu wa kuingia mwaka mpya usioenda sambamba na tafakari ya kina; kuweka malengo makubwa yasiyopimika; na pale malengo yanapohusisha mabadiliko ya tabia, kutokujua uliko mzizi wa mabadiliko hayo. Hapa ninakupa dondoo zinazoweza kukusaidia kufikia malengo uliyojiwekea kwa mwaka huu. Weka malengo yanayopimika Usiweke malengo makubwa yasiyolenga jambo mahususi. Vunja vunja wazo kuu ulilonalo liwe malengo madogo madogo yanayolenga jambo moja utakaloiishi kila siku. Kwa mfano badala ya kuazimia kujenga tabia ya jumla kusoma vitabu, vunja vunja lengo hilo liwe kusoma kitabu kimoja kwa juma moja. Ukisema unalenga kujenga tabia ya kusoma, haieleweki unalenga kusoma vitabu vingapi kwa mwezi, miezi sita na hata miezi 12. Lengo la kusoma kitabu kimoja kila juma ni mahususi na utaweza kulitathimini. Kama unataka kuwa na uhusiano imara na familia yako mwakani, fafanua kwa namna gani. Je, unataka kujenga mazoea ya kuwahi nyumbani kila siku baada ya kazi? Je, unataka kutoka na wanao kila mwisho wa juma? Fanya malengo yako yawe madogo madogo na yapimike kwa muda maalumu. Lengo lisilopimika ni matamanio yatakayoendelea kuwa njozi tu. Jiwekee mfumo wa kujipima Utekelezaji wa malengo mengi, kwa kawaida, huhusisha mabadiliko ya tabia. Huwezi kubadili tabia usiyoweza kuipima. Hakikisha malengo yako yanapimika kadri unavyoendelea kuyatekeleza. Ili uweze kupima, weka muda maalumu wa kuyatekeleza. Andika malengo yako mahali ikusaidie kukumbuka. Malengo yasiyoandikwa yanabaki kuwa ndoto tu. Na kwa kawaida, ndoto huwa hazitekelezeki kirahisi. Kama unalenga kupanua biashara yako kwa mwaka huu, fikiria utakavyoweza kupima upanuzi huo. Je, utatazama kiasi cha mtaji unaoongezeka? Je, ni kiasi cha bidhaa unachoouza, idadi ya wateja unaowapata? Lazima uwe na utaratibu utakaokusaidia kupima unavyotekeleza malengo yako kadri muda unavyokwenda. Jiwajibishe Wakati mwingine ni rahisi kuachana na mipango uliyojiwekea kadri muda unavyokwenda kwa sababu huna mfumo wa kukuwajibisha pale unapoteleza. Ni muhimu kuwa na watu watakaokufanya ujisikie vibaya kuachana na mpango wako. Baada ya kuhakiki malengo yako, fikiria watu wako wa karibu unaoweza kuwaambia kile ulichokipanga. Kama maazimio yako yanamhusu mkeo/mumeo, mshirikishe malengo yako mapema. Kama malengo yanawahusu wanao, waambie. Kwa kufanya hivyo, unatengeneza mfumo wa kukuwajibisha pale unapoanza kususua sua.  Itakusaidia kuwa na hamasa ya kufanyia kazi malengo yao kuliko yanapokuwa siri yako mwenyewe. Kadhalika, unapolenga kubadili tabia fulani usizozipenda waambie watu. Ikiwa unataka kuacha sigara, pombe au tabia fulani wanazozijua rafiki zako, tangaza wazi wazi. Waambie unataka kuacha sigara, pombe au uzinzi. Wanapojua mpango wako unajiweka katika mazingira ya kulazimika kutekeleza ili usionekane mtu wa maneno yasiyo na vitendo. Muhimu kuzingatia kuwa watu wanaweza kuwa kikwazo cha malengo yako. Huwezi kuambatana na watu wanaoshabikia sigara, pombe na uzinzi na ukategemea ufanikiwe kuachana na tabia hizo. Amua kukaa mbali na watu wenye tabia unazolenga kuachana nazo. Ambatana na watu wenye tabia unazotaka kuzijenga. Kama unataka kuanza kusoma, jenga urafiki na watu wanaopenda kusoma. Kama unataka kuwa na familia imara, jenga urafiki na watu wenye familia imara. Kama unataka kuwa na mafanikio kitaaluma, ambatana na watu wenye ari ya kusoma. Watu wenye tabia unazotaka kuzijenga, watakusaidia kuwa na motisha ya kwenda unakotaka kwenda. Usisubiri kuanza kesho Mara nyingi watu husahau malengo yao kwa sababu wanasubiri kuanza kesho. Wanaahirisha kwa sababu wanajifariji kuwa bado wanajipanga. Lakini kadri muda unavyokwenda, wanajikuta wakikosa hamasa. Usisubiri kesho kuanza kufanya kitu sahihi. Anza mara moja. Kama lengo ni kuanza kusoma, kanunue kitabu leo anza kukisoma hata kama unafikiri huna muda. Muda haukusubiri, utengeneze. Azimia kutengeneza muda wa kusoma. Utaweza. Kama unalenga kuongeza akiba kila mwezi, usisubiri mwezi ujao. Anza mwezi huu. Weka akiba kabla ya kufanya matumizi. Ukisubiri mwezi ujao, hutaanza. Ni rahisi kuahirisha kile usichoona sababu ya kukifanya leo. Jambo la kuzingatia ni kwamba huwezi kutekeleza lengo kubwa bila hatua ndogo. Jifunze kufurahia hatua ndogo unayopiga ilmuradi inakusaidia kuelekea kwenye lengo kubwa. Usisubiri utekelezaji mkubwa ili ufurahie. Hata unapokwama, usikate tama na kughairi maazimio yako. Songa mbele. Christian Bwaya ni mhadhiri wa Saikolojia Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Mawasiliano 0754870815, Twitter: @bwaya
AFYA
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Ikulu jijini Dar es Salaam.Akizungumza baada kukutana, Rostam ameeleza kuwa amekwenda ikulu kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtakia kila la kheri kwenye utendaji wake."Kama mfanyabiashara naona kinachofanyika hivi sasa na Rais Magufuli ni kutengeneza misingi ya uchumi ambao utakua kwa uhakika zaidi," alisemaAliongeza kuwa Rais anatengeneza uwanja sawa ili watu waweze kufanya biashara zao kwa uhuru na haki, jambo ambalo litapelekea uchumi kukua zaidi, ikilingalishwa na kipindi cha nyuma.
KITAIFA
“BABA naomba unisamehe… ni ujinga wangu na upumbavu wangu wa kukutaka uje kwenye ‘gradu’ (graduation- mahafali),” ni maneno ya kuchoma moyo ya mtoto Anna Zambi baada ya kufi ka kwenye makaburi ya wazazi na wadogo zake.Mtoto huyo alifika nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam jana saa 10 alfajiri, baada ya kumaliza mitihani ya kidato cha nne na kuanza safari kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mother Theresa of Calcutta ya Same mkoani Kilimanjaro bila kufahamu juu ya vifo vya ndugu zake.Baba yake, Lingston Zambi, mama yake, Winfrida Lyimo pamoja na wadogo zake, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda kwenye mahafali yake kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwezi uliopita wilayani Handeni mkoani Tanga.Alivyosafirishwa hadi Dar Baada ya kumaliza mtihani, bibi mzaa mama na nduguze wanaoishi mkoani Kilimanjaro, walitumia mbinu ya kwenda na keki hadi shuleni kwa Anna, wakampongeza kwa kumaliza mitihani kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam.Binti huyo akiwa na furaha ya kurudi nyumbani, ilikatishwa na taarifa alizopokea hiyo alfajiri ya jana umbali mdogo kabla ya kufika nyumbani. Baada ya kukaribia nyumbani, watu wanne ambao ni waumini wenzake na marehemu wazazi wake, ndiyo walikwenda kumpa taarifa ndani ya gari. Mtoto huyo alilipuka kwa kilio, ikabidi asaidiwe kufikishwa nyumbani akiwa amebebwa.Akiomboleza, mtoto huyo alisema licha ya kufichwa taarifa za msiba, alipata ishara kwani alikuwa hajisikii vizuri kiafya wakati wa kipindi chote cha mtihani.Kilio ibadani, makaburini Wakati ibada ikiendelea, mtoto alikuwa akilia na kuomboleza kwa sauti hali iliyosababisha watu wengi kushindwa kujizuia kulia.Mtoto huyo alisikika akisema: “umeniachia msiba… familia yetu sita nimebaki mmoja!” Vilio viliendelea kutawala miongoni mwa waombolezaji baada ya mtoto kupelekwa makaburini, umbali mdogo kutoka nyumbani na kushuhudia makaburi matano ya wazazi na wadogo zake.Akiwa amekaa pembeni mwa kaburi la baba yake, Anna alilia akimuomba baba yake amsamehe kwa kile alichosema ni ‘ujinga’ wake wa kumshawishi aende kwenye mahafali yake.“Baba naomba unisamehe…ni ujinga wangu na upumbavu wangu wa kukutaka uje kwenye ‘gradu’ ( graduationmahafali),” alisema.Akiwa kwenye kaburi la mama yake, Anna alisema, “mama bora ungebaki tasa… tumekulipa zawadi ya makaburi”. Vile vile akiwa kwenye kaburi la mdogo wake Lulu, alilia akimshukuru kwa zawadi ya matokeo mazuri ya darasa la Nne. “Matokeo yako niliyaona lakini ya kwangu hukuyaona” alisema.Anna aliendelea kuliza umati wa watu makaburini, kwa kusema, “ona makaburi haya yote ni yangu...mimi ni mdogo sana. Mliona wapi mtoto wa miaka 16 akibeba majeneza matano?...naomba mniombee (wazazi na wadogo zake) nami nife na mimi ni mwenzenu.”Katika maombolezo, Anna alieleza wasiwasi wake wa kuendelea na masomo na kukidhi ndoto zake.Aliwashukuru wazazi wake akisema walijitahidi kuwasomesha na wao hawakuwaangusha, kwani yeye na wadogo zake walikuwa wakifaulu vizuri.Akilia mbele ya baba yake mdogo, Ibrahim Zambi, mara baada ya mtoto huyo kuwasili nyumbani alfajiri,Anna alisema, “nina kuwa mzigo wenu…sijui kama nitasoma na kutimiza malengo yangu…Baba na Mama Anna (Ibrahim na mkewe) nipokeeni mnione kama mtoto wenu kama mnavyowaona Anna na John.”Baba mdogo, Ibrahim alimhakikishia mtoto huyo kuwa atafanya kila liwezekanalo, kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kielimu. Kwa mujibu wa baba mdogo, ndoto ya Anna ni kuwa Mwanasheria.Daktari ashauriDaktari Fredric Doya alisema anapaswa apumzike kwanza na aachwe apitie hatua zote za kupokea habari mbaya, kabla ya kuanza kupata ushauri wa kisaikolojia. Dk Doya ambaye yuko karibu na familia na wakati huo huo binti yake alikuwa akisoma shule moja na Anna, alitaja hatua hizo ni kukataa, hasira, kujiuliza maswali (kama taarifa husika ni za kweli) na kisha kukubaliana na hali halisi.Alisema wakati akipitia hatua hizo, ni vizuri akaendelea kupata nasaha za kiroho na kuongeza kuwa hayo yakifanyika ipasavyo atarejea katika hali ya kawaida.Shule ilivyozuia taarifaAkizungumza kama mwakilishi wa wazazi wa watoto katika shule hiyo ya Mother Theresa of Calcutta , Doya alisema baada ya msiba, uongozi wa shule uliwathibitishia kwamba utahakikisha unazuia mianya yote, inayoweza kuruhusu taarifa hizo kuenea shuleni na kumfikia mtoto huyo, jambo lililotekelezwa.Miongoni mwa mianya ya taarifa iliyozibwa kuhakikisha Anna hafahamu kuhusu msiba wa nduguze, ni pamoja na televisheni kutowashwa na pia kuhakikisha hakuna mawasiliano ya simu yanayowafikia wanafunzi.Taarifa kutoka shuleni hapo, zinasema jana ndipo wanafunzi walipata taarifa hizo, baada ya wazazi kufika kuwachukua na baadhi yao kusikika wakitoa pole kwa uongozi wa shule, hali iliyosababisha vilio miongoni mwao.Nasaha za MchungajiAkihubiri katika ibada ya shukurani iliyofanyika nyumbani hapo Goba, Mchungaji Hance Mwakisoja wa Kanisa la Moravian alisisitiza juu ya ukuu wa Mungu na kutaka Anna apewe zawadi ya kufarijiwa, badala ya machozi.Amesema laiti jamii ingefahamu Anna ajaye atakuwa nani, kusingekuwa na majonzi.Kwa upande wake, Mchungaji Gentleman Mwansile alihimiza kanisa lifuatilie maisha ya mtoto huyo ikiwa ni pamoja na kufahamu kama anasoma au hasomi.Anna na baadhi ya wanafamilia wanatarajiwa kusafiri kwenda Mbozi mkoani Mbeya kwa ajili ya kupeleka msiba.
KITAIFA
WAZIRI Mkuu, Kassimu Majaliwa amewataka viongozi wa serikali mikoani kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja. Pia amewataka mawaziri kuacha mtindo wa kufanya ziara katika mikoa, bila kuwapa taarifa wakuu wa mikoa.Waziri Mkuu alitoa onyo hilo, wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya wakuu wa mikoa (RCs) na makatibu tawala wa mikoa (RAS), yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uongozi (UI) na Ofisi ya Rais (Tamisemi) jijini hapa jana.Alisema viongozi hao wanatakiwa kuheshimiana. Alisema hata kama wote ni wateule wa Rais, siyo utaratibu mzuri kwa viongozi hao, kutoheshimiana na kudharauliana, kwani kila mmoja amekabidhiwa maeneo ya kushughulikia.Alisema wakuu wa mikoa, nao wanapofanya ziara katika mikoa ya wakuu wa mikoa mingine, wanatakiwa kutoa taarifa, kutokana na utaratibu kwamba huo siyo mkoa wao. Waziri Mkuu alisema pia wakuu wa mikoa, wanapofanya ziara katika wilaya mbalimbali, wanatakiwa kutoa taarifa kwa wakuu wa wilaya, kabla ya kufanya shughuli zozote katika wilaya hizo.Akizungumzia suala la ziara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika alisema waziri kufanya ziara katika eneo fulani, bila kutoa taarifa ya dhati hilo ni kosa, ni wajibu kutoa taarifa. Alisema kitendo cha viongozi kufika katika eneo fulani kulala hotelini, pamoja na kuwa walinzi wao na kuondoka bila kumweleza au kueleza ratiba yake kwa mkuu wa mkoa, ni kosa.Pia, aliwataka viongozi hao kwenda kutatua migogoro mbalimbali katika maeneo yao, mfano migogoro ya ardhi. Kwamba haipendekezi kuona waziri wa ardhi, anakwenda kutatua migogoro midogo ya ardhi, ambayo wanaweza kuitatua. Waziri Mkuu aliwataka viongozi wazingatie mafunzo hayo ili wakirudi mikoani kwao, wakasimamie kikamilifu shughuli zao, kwa kuwaheshimu watendaji wa chini yao.Akizungumzia uhusiano baina ya viongozi, Majaliwa alimwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, kwenda mkoani Kilimanjaro, ambako hali si shwari kutokana Mkuu wa Mkoa, kutoelewana na baadhi ya wakuu wa wilaya. Mkuu wa Mkoa huo wa Kilimanjaro ni Anna Mghwira na wilaya za mkoa huo ni Hai, Siha, Moshi, Rombo, Same na Mwanga.Pia, alimtaka katika ziara hiyo, aandamane na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, naye kwenda huko kwa lengo la kutoa semina kwa viongozi hao ili kuacha tofauti zao, ambazo zinakwamisha maendeleo. Aliwataka viongozi hao, kufuata itifaki katika kuandika barua. Alisema ni kosa kwa mkuu wa wilaya, kuandika barua kwa Rais, bali anatakiwa kumwandikia mkuu wa mkoa.Vile vile, alisema Naibu Waziri anatakiwa kumwandikia waziri, badala ya kuandika moja kwa moja kwa Rais. Akizungumza, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mussa Iyombe alisema viongozi hao, wanatakiwa kuzingatia mafunzo, kwani uzoefu unaonesha kwamba viongozi waliopitia mafunzo hayo, matunda yake hayaonekani sana. Alisema serikali inatumia fedha nyingi, lakini matunda yake hayaonekani sana.Wengi wanapata mafunzo lakini hawazingatii mafunzo kwani wanafanya kazi nyingi za ofisi kwa kupitia simu. Alisema kumekuwa na migogoro na kutoheshimiana mipaka baina yao. Alisema kuna migogoro kati ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa, makatibu tawala na makatibu tawala wasaidizi, makatibu na mawaziri. Alisema kutoelewana huko, kunakwamisha maendeleo na kunaichafua serikali. Akizungumza, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mkuchika aliwataka viongozi hao kuendesha serikali kwa sheria, kanuni na taratibu.Aliwataka waachane na vitendo vya kuwaweka watu ndani saa 24 kama hawatishii usalama wa wengine na wao wenyewe. Pia aliwataka kuacha kuchelewa kwenye mikutano. Aliwataka wakuu wa mikoa, kupanga ratiba ya kufanya mikutano na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) katika mikoa yao. Alisema anashangaa kigugumizi kinatoka wapi na aliahidi kwamba wasishangae taasisi hiyo, inafika hapo na kuomba mikutano.Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof Joseph Semboja alisema viongozi hao katika mafunzo hayo hadi Desemba 7, wanatakiwa kuvishinda vishawishi vya kufanya mambo mawili wakiwa katika mafunzo.Mafunzo hayo yanashirikisha wakuu wa mikoa 26 na makatibu tawala 26 pamoja na watendaji wa Tamisemi, lengo ni kuwajengea uwezo wao, kuongoza rasilimali watu na nyingine na kuongeza sifa zao binafsi. Alisema taasisi ya uongozi ilianza kutoka mafunzo hayo Mei mwaka jana hadi Oktoba mwaka huu, ambapo wakuu wa wilaya 139 na wakurugenzi 185 walipata mafunzo hayo. Hivyo, mafunzo ya wakuu wa mikoa na katibu tawala ni mwendelezo
KITAIFA
NAIROBI, KENYA MIVUTANO katika Chama tawala cha Jubilee umezidi kutokota huku Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria, akitangaza mipango ya kuunda chama kipya kitakachotetea maslahi ya jamii za Mlima Kenya. Kuria alieleza wazi kwamba uamuzi uliochangia kuvunjwa kwa chama cha zamani cha The National Alliance (TNA), ambacho Rais Uhuru Kenyatta alikitumia kuwania urais mwaka wa 2013, uliacha Mlima Kenya bila namna ya kujitetea vilivyo kisiasa. TNA kilivunjwa pamoja na vyama vingine vya muungano uliokuwepo wa Jubilee, kikiwemo Chama cha United Republican Party (URP) kilichoongozwa na Naibu Rais William Ruto, kuunda Chama cha Jubilee ambacho kilishinda urais mwaka 2017. Kauli ya Kuria imetokea wakati ambapo joto la kisiasa linazidi kuiandama Jubilee baina ya upande unaounga mkono azimio la Dk. Ruto kuwania urais mwaka 2022, maarufu ‘Team Tangatanga’, na kundi jingine linalopinga kampeni za mapema maarufu kama ‘Team Kieleweke’. Wandani wa Dk. Ruto wamekuwa wakidai kuna njama zinazoendelezwa kumzuia Ruto kufanikiwa katika azma ya kuwa rais mwaka 2022 ikiwa ni pamoja na kuivuruga Jubilee. “Tulikosea wakati tulipovunja chama chetu cha The National Alliance kwa sababu Jubilee ni chama kisicho na mwelekeo ambacho hatuwezi kukitumia kufanya mipango yetu ya Mlima Kenya. “Nitasajili chama kipya cha siasa ambacho kitawapa viongozi wa Mlima Kenya nafasi ya kufanya mipango kuhusu masilahi yetu ya siku za usoni serikalini,” alisema Kuria. Alikuwa akizungumza katika Kanisa Katoliki la Sabasaba, Kaunti ya Murang’a ambapo aliandamana na viongozi wengine wa Jubilee. Viongozi hao ni pamoja na Mbunge wa Kandara,  Alice Wahome na mwenzake wa Maragua, Mary Waithira pamoja na Seneta wa Murang’a, Irungu Kang’ata. Kang’ata alikiri siasa zinazoendelezwa zimesababisha mgawanyiko wa viongozi na sasa chama kinaelekea mahali pabaya. “Chama chetu kinaelekea pabaya kwa sababu pande mbili za Tangatanga na Kieleweke zinasababisha chuki miongoni mwa wale wanaochukuliwa kuwa wapinzani wao,” alisema. Suala la iwapo Dk.  Ruto atatumia Chama cha Jubilee kuwania urais 2022 limekuwa kwenye ndimi za baadhi ya wafuasi wake na wachanganuzi wa siasa kwa muda mrefu hasa tangu mwafaka wa Rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga upatikane. Wakati mmoja, ilifichuka kwamba viongozi wanaoegemea upande wa Naibu Rais walisajili vyama vipya na kushukiwa kuwa hayo yalikuwa maandalizi ya kujitafutia makao salama endapo Dk. Ruto ‘atasalitiwa’ na viongozi wa Jubilee wanaotoka Mlima Kenya.  Wahome alitoa wito kwa Rais Kenyatta kuingilia kati ili kutuliza hali chamani na kuepusha mashua ya Jubilee kuzama katika dhoruba kali inayoshuhudiwa. “Tulipiga kura kwa wingi kuwachagua Uhuru Kenyatta na Dk. Ruto na tunamtegemea kiongozi wa chama kudhibiti hali iliyopo chamani kwa sasa,” akasema
KIMATAIFA
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema Ndanda FC ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo wameiandikia barua bodi ya ligi kuomba mchezo wao na Yanga kuchezwa Dar es Salaam badala ya Mtwara.“Ndanda FC na Yanga wameiandikia Bodi ya Ligi kuomba mchezo wao uchezwe Uwanja wa Taifa, kwa sababu timu zimekubaliana zenyewe na kanuni zinaruhusu, basi bodi imeridhia ombi lao,” alisema Lucas.Pia Lucas alisema Bodi ya Ligi imesogeza mbele ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, badala ya kumalizika Mei 21 sasa itamalizika Mei 22 ili kuipa fursa Yanga ambayo itakuwa imetoka kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika, siku tatu za kupumzika na kusafiri kwenda Songea kucheza na Majimaji.“Yanga watasafiri kwenda kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola mchezo utakaochezwa kati ya Mei 17 au 18 na Mei 19 watarudi, ili wapate nafasi ya wachezaji kupumzika, ndio maana bodi imeamua kusogeza mbele ratiba ya kufunga pazia la ligi kuu, kwani Yanga itasafiri kwenda Songea,” alisema Lucas.Wakati huo huo, Lucas amesema TFF imepokea rufaa ya Azam FC, ikipinga kupokwa pointi tatu kwa kumchezesha Erasto Nyoni kwenye mchezo wao na Mbeya City kwa madai alikuwa na kadi tatu za njano.Lucas alisema kwa sababu Azam FC wamefuata taratibu zote za kukata rufaa imepokelewa na itawasilishwa kwenye kamati husika kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
MICHEZO
RAIS John Magufuli anatarajia kuongoza maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza leo, kupokea ndege aina ya Bombadier Q 400 kutoka Canada. Ndege hiyo ni ya pili kukamatwa na mzungu mkulima wa Afrika Kusini, Hermanus Stern kwa muda wa wiki tatu sasa.Nyingine iliwahi kukamatwa Afrika Kusini hivi karibuni. Hayo yamesemwa jana jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa ndege hiyo hapa nchini kupitia Mwanza. Pia, alizungumzia ujio wa Rais katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya kuipokea ndege hiyo.“Niwaombe wananchi wa mkoa wetu na mikoa jirani, wajitokeze kwa wingi kuipokea ndege yao baada ya wanasheria wazalendo kuipigania ndege hiyo katika mahakama za nchini Canada hivi karibuni na kufanikiwa,” alisema.Rais Magufuli alitangaza ujio wa ndege hiyo, alipokuwa akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi jijini Mwanza wiki hii. Alisema ndege hiyo imeachiwa kutoka Canada na mapokezi yake yangefanyika jijini Mwanza. Moja ya mambo makubwa ambayo Serikali ya Rais Dk Magufuli imeyafanya baada ya kuingia madarakani mwaka 2015 ni kuifufua Kampuni ya Ndege nchini (ATCL), ambayo hali yake ilikuwa mbaya.Ilichokifanya serikali ni kununua ndege mpya na za kisasa ambazo imeikodisha ATCL. Kutokana na juhudi hizo za serikali, kwa sasa ATCL ina jumla ya ndege mpya nane, ambazo ni Boeing 787-8 Dreamliner mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 262 kila moja na Airbus A220-300 mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja.Ndege zingine ambazo zimeshawasili nchini na zinaendelea kutoa huduma ni Bombardier Dash 8 Q400 tatu, zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, na ndege nyingine mpya ni Bombardier Dash 8 Q400 ndiyo itakayowasili leo.
KITAIFA
NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM UONGOZI wa klabu ya KMC umefikia uamuzi wa kusitisha kibarua cha kocha Mganda Jackson Mayanja, kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi chao tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mayanja ambaye aliwahi kuinoa Simba, aliingia mkataba wa mwaka mmoja kuinoa KMC, akichukua mikoba iliyoachwa na mtangulizi wake, Etienne Ndayiragije aliyetua Azam FC kabla ya kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars. Alianza kuiongoza timu hiyo katika michuano ya Kombe la Kagame ilyofanyika nchini Rwanda, huku timu hiyo ikiishia hatua ya makundi. Mayanja alishindwa kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kutolewa na AS Kigali ya Rwanda kwa kuchapwa mabao 2-1 nyumbani. Kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar ,anakuwa wanne kuachishwa kazi tangu Ligi Kuu Bara ilipoanza  kutimua vumbi Agosti mwaka huu. Wengine ni Athumani Bilal aliyekuwa akiinioa Alliance, Fred Minziro  aliyekuwa akiifundisha Singida United na Mwinyi Zahera aliyetupiwa virago na Yanga. Hata hivyo, majina ya makocha Masoud Djuma raia wa Rwanda na Mcameroon, Joseph Omogo yanahusishwa na kikosi hicho kilichokuwa moto wa kuotea mbali msimu uliopita. Akizungumza jana Dar es Salaam,Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde alisema kuwa wamekubaliana na Mayanja kuvunja mkataba huo kutokana na masharti yaliyowekwa. “Tumekubaliana kuachana na Mayanja kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi chetu, pande zote mbili zimeridhiana kuachana kwa amani, hivyo tunamtakia kila la kheri huo aendapo,”alisema Binde.
MICHEZO
RAIS John Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kuwasaidia wawekezaji wazawa ili waweze kujenga viwanda. Pia amewataka wakazi wa Ukerewe mkoani Mwanza, kushirikiana na serikali ili kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi imara. Aliyasema hayo katika mikutano aliyoifanya katika maeneo ya Magu na Ukerewe mkoani Mwanza akiwa katika ziara ya kutembelea mikoa ya Kanda ya Ziwa.Akizindua kiwanda cha Lakairo Industries Group Limited kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza, Rais Magufuli aliziagiza wizara hizo mbili kuwasaidia wawekezaji wazawa ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa viwanda. Alitoa mfano kuwa Mbunge wa Rorya mkoani Mara, Lameck Airo ni mfano wa kuigwa kwa wawekezaji wazalendo katika kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na aliwataka wabunge wengine kuiga mfano wake.Akiwa Ukerewe, Rais Magufuli aliwataka wakazi wa kisiwa hicho, kushirikiana na serikali ili kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi imara. Alisema katika kutekeleza sera ya maendeleo serikali yake imeanza kuiandaa Tanzania ya neema kwa kuwabana wezi, mafisadi na wala rushwa, ambao wamekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi kwa muda mrefu. Alitolea mfano wa fedha zilizokuwa zikipotea kuwalipa wafanyakazi hewa, lakini kwa sasa zimeokolewa na zinatumika kwenye ununuzi wa ndege, kujenga miundombinu za usafiri wa gari, treni na shughuli nyingine za maendeleo.Alisema: ”Miradi mikubwa ya umeme kama vile Stiegler’s Gorge, mradi wa usafiri wa kisasa wa treni ya Standard Gauge itakayoanzia Dar es Salaam kuja Mwanza kupitia Dodoma itatekelezwa tena kwa fedha za kodi zenu. Kwa sasa tumejipanga kuifanya Tanzania kuwa mpya na yenye neema, ni jukumu lenu na nyie kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo wenu kuendeleza Ukerewe na serikali itawasaidia. Hivi iweje viwanda vya nguo na uwekezaji mwingine unapotea tu, sasa basi ni lazima tujipange kurekebisha hali hii,” alisema.Alisema, katika kuwafikishia neema mkoani humo, serikali imenunua meli ya kisasa itakayobeba abiria na mizigo kwa bei ya kawaida ili kuwapatia fursa wakazi wa Mkoa huo wakiwamo hao wa Ukerewe kufanya biashara. Aliongeza, miradi ya umeme ya Kinyerezi 1,2,3 na 4 inazalisha megawati za umeme 2,263 zitakazokuja kuongezewa nguvu na Stiegler’s Gorge ambao ukikamilika utazalisha megawati 2, 265 na hivyo nchi kuwa na umeme wa megawati 4,263, ambazo zinatosha kuendesha viwanda. Pia aliwataka viongozi wa serikali, kuacha kufanya kazi kwa kutaka sifa, badala yake wawe na mikakati endelevu itakayowawezesha viongozi hao kuwahudumia wananchi. Leo Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoa wa Mara, ambapo atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.
KITAIFA
Na PENDO FUNDISHA, MBEYA MFANYABIASHARA maarufu jijini Mbeya, Steven Samweli maarufu kwa jina la Maranatha, ametiwa nguvuni akituhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Kutiwa nguvuni kwa mfanyabiashara huyo ni mwendelezo wa nia ya Serikali ya kupambana na biashara ya dawa hizo nchini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi juzi kwamba, Maranatha alikamatwa juzi usiku akiwa katika moja ya maduka yake ya dawa baridi. “Baada ya polisi kupata taarifa za mfanyabiashara huyo kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, tuliweka mtego na hatimaye kufanikiwa kumtia nguvuni. “Kwa sasa tunamshikilia kwa mahojiano na baada ya uchunguzi kukamilika, atafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Kidavashari. Pamoja na hayo, kamanda huyo wa polisi alisema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kunafikisha idadi ya watu wanane waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya mkoani Mbeya. “Miongoni mwa hawa tunaowashikilia, baadhi yao walikutwa na vielelezo, hivyo watafikishwa mahakamani wakati wowote wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. “Kwa hiyo, nawaomba wananchi mkoani hapa, waachane kabisa na biashara ya dawa hizo kwa sababu wakikutwa nazo, watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola,” alisema Kamanda Kidavashari.
KITAIFA
Anna Potinus Rais Dk. John Magufuli amewataka viongozi wastaafu nchini kujenga utaratibu wa kuandika vitabu vinavyohusu maisha yao ili viwe chachu kwa vijana wanaotamani kuingia katika masuala ya uongozi. Ametoakauli hiyo leo Jumanne Novemba 12, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha historia ya maisha ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kilichopewa jina la ‘My life my purpose’ iliyofanyika Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein. “Ninawahimiza viongozi wastaafu wengine kuiga mfano wa mzee Mkapa kwa kuandika vitabu ili uzoefu wao katika uongozi uwe chachu kwa vijana wetu wanaoinukia kwenye uongozi, nimefurahi kusikia kuwa mchato wa kukamilisha kitabu cha Mzee Mwinyi uko mbioni kukamilika na Mzee Kikwete pia anaendelea na uandishi wa kitabu chake. “Uandishi wa vitabu usiishie kwa viongozi wastaafu wa nafasi za urais tu tunataka na viongozi wengine nitafurahi kusoma kitabu cha Mzee Warioba, Maalim Seif, Job Ndugai na wengine wengi kwani haya ni masuala muhimu katika historia na maendeleo yetu,” amesema Rais Magufuli. Aidha amewahimiza Watanzania kukuza na kujenga utamaduni wa kujisome akisema vitabu havitakuwa na manufaa yoyote kama havitasomwa.
KITAIFA
      Na CLARA MATIMO PAROKIA ya Kung’ara Bwana wetu Yesu Kristo Mabatini  Kanisa Katoliki  Jimbo kuu la Mwanza, inakabiliwa na changamoto ya waumini wake kuendelea kuamini ushirikina. Hayo yalielezwa na Katibu wa Halmashauri  ya Walei wa Parokia  ya Mabatini, Lawrence  Mayunga, wakati akisoma risala  katika sherehe ya kutimiza miaka 13 ya parokia hiyo   kanisani hapo. Alisema baadhi ya  waumini  wa parokia hiyo ambao wanatenda matendo ya ushirikina bado wameghubikwa na imani kwamba wakitenda hivyo watapata utajiri wa haraka na kuishi maisha bora. “Mheshimiwa mgeni rasmi wapo baadhi ya waumini ambao walikabidhiwa mikoba ya ushirikina kutoka kwa wazazi, bibi au babu zao na wakati wanakabidhiwa  walitishwa kwamba endapo wakiacha na kumtumikia Yesu watapata majanga makubwa. “Hivyo wanaamua kuwatumikia mabwana wawili wakati  Yesu Kristo alisema ukitaka kumfuata lazima ujikane,” alisema Mayunga. Alisema kanisa linatatua changamoto hiyo kwa kuwapa semina, mfungo na maombezi ya mara kwa mara  waachane na imani za  zamani waweze kumpokea Yesu katika roho   ikiwa ni pamoja na kutenda matendo mema ambayo aliyafundisha. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Sala Ibanda Ziwani Parokia ya Mabatini  Jimbo kuu la Mwanza, Padri, Jeme Ebo, aliwataka watu wote kujenga moyo wa upendo. Alisema upendo wa moyoni unajenga uhusiano mzuri kati ya Mungu na mwanadamu. Aliwasisitiza wakristo wote waliompokea Yesu kuachana na imani za ushirikina kwa sababu kumchanganya na shetani ni sawa na kuweka mafuta na maji  ambavyo havichanganyiki. “Achaneni na dhambi ndugu zangu maana ni mbaya  ng’areni kama ambavyo jina la parokia yenu lilivyo. “Pia tatueni changamoto zinazowakabili bila kutegemea wafadhili naamini mkiungana mnao uwezo wa kufanya maboresho makubwa katika parokia yenu. “Mlikotoka ni mbali na mmepiga hatua katika maendeleo,  wekezeni fedha zenu kwa Mungu ukimtolea naye atakuzidishia,”alisema Padri Ebo.
KITAIFA
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) haichapishi kiholela fedha kwa ajili ya kukidhi matumizi ya serikali, bali huchapishwa kulingana na taratibu za kisheria, imesema taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya benki hiyo. Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amewapongeza Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga na wataalamu wake kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha hakuna fedha za ziada kwenye uchumi. Dk Kijaji alikuwa akijibu swali la msingi la nyongeza la Mbunge wa aliyehoji kama uchumi umekua mbona wananchi ni masikini na hawana fedha.Dk Kijaji alimpongeza gavana huyo kwa kudhibiti uingiaji wa fedha za ziada kwenye uchumi. Alisema kupatikana kwa fedha kwenye mzunguko si kigezo cha kukua kwa uchumi na kuna madhara makubwa na kuwa upatikanaji mkubwa wa fedha kwenye mzunguko ni ishara ya Taifa kushindwa kudhibiti uchumi. “Money supply (upatikanaji fedha) kwenye uchumi si kigezo cha kukua kwa uchumi wa Taifa. Money supply kwenye uchumi inaonesha kwamba Taifa hilo limeshindwa kucontrol (kudhibiti) ukuaji wa uchumi wake.“ In short run (kwa muda mfupi) unaweza ukajidanganya kwamba ukuaji wa uchumi upo in long run (kwa muda mrefu) matatizo yake na madhara yake ni makubwa sana. Hivyo nampongeza sana G avana na wataalamu wake kwa kuthibiti uingiaji wa fedha za ziada kwenye uchumi.” Taarifa ya BoT Taarifa ya BoT imekuja baada ya benki hiyo kudaiwa kuwa imechapisha noti zenye thamani ya Sh trilioni 1.5 kwa ajili ya matumizi ya serikali. Katika taarifa hiyo iliyotolewa jana, Benki Kuu iliuarifu umma kuwa, taarifa ya uchapishaji noti haina ukweli na kwamba inalenga kuathiri imani ya wananchi na wadau wa kimataifa kuhusu uthabiti wa fedha ya Tanzania.“Benki Kuu haijachapisha noti mpya katika kipindi hiki, hata hivyo noti mpya, hazichapishwi kiholela ili kutoa pesa kwa serikali, bali huchapishwa kulingana na taratibu za kisheria,”ilieleza taarifa hiyo. Aidha, Benki Kuu iliwaasa wananchi kuwa utoaji wa taarifa potofu kuhusu sekta ya fedha unaweza kuleta athari kubwa kwa mwenendo wa uchumi. Kuhusu jinsi fedha mpya zinavyochapishwa, taarifa hiyo ilieleza kuwa katika hali ya kawaida utengenezaji wa noti na sarafu huanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa usanifu wa michoro, aina ya karatasi itakayotumika, alama za utambulisho wa nchi pamoja na alama za usalama.“Na mara baada ya kukamilika kwa mchakato huo, Benki Kuu huandaa kiasi gani kitakachoweza kutosheleza mahitaji ya nchi kwa kipindi maalum kwa kuzingatia ukuaji wa pato la Taifa, mfumuko wa bei na pia kufidia fedha zilizochakaa ambazo hazipaswi kurudi katika mzunguko na kiasi kilichobaki (buffer stock) ili kutosheleza kipindi chote cha mchakato wa uchapishaji,” ilifanunua taarifa hiyo. Serikali inavyokopa BoT Katika ufafanuzi juu ya utoaji wa fedha kwa matumizi ya Serikali, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilisema kuwa mapato ya serikali huwa hayawiani moja kwa moja na matumizi yake mwezi hadi mwezi na kwamba kuna wakati mapato yanakuwa makubwa.Hivyo taarifa hiyo inasema kuwa kutokana na kupishana kwa mapato na matumizi ya serikali, sheria imeruhusu serikali kuchukua mkopo wa muda mfupi kutoka Benki Kuu ili kuziba pengo pale linapotokea na kurejesha baadaye. “Utaratibu wa serikali kukopa unatumika duniani pote na hapa Tanzania sheria inairuhusu Serikali kukopa kutoka Benki Kuu kwa vipindi vifupi hadi ukomo wa asilimia 12.5 ya mapato ya ndani ya serikali ya mwaka uliotangulia,” ilieleza taarifa hiyo.Katika taarifa ya kila mwezi ya uchumi ya Benki Kuu toleo la mwezi Julai, mwaka huu inaonesha kwamba mkopo wa muda mfupi (overdraft) wa Benki Kuu kwa serikali uliongezeka kutoka Sh bilioni 610.0 kwa mwezi Mei, mwaka huu hadi Sh bilioni 1,937.4 kwa mwezi Juni, sawa na ongezeko la Sh bilioni 1,327.4. BoT inasema kuwa ongezeko hilo halipaswi kuangaliwa kama tukio la mwezi Juni, mwaka huu pekee kwani taarifa hiyo hiyo inaonesha kuwa kati ya mwezi Juni, 2017 na mwezi Mei mwaka huu, mkopo huo wa muda mfupi wa BoT kwa serikali ulipungua kwa Sh bilioni 936.6, kutoka Sh bilioni 1,546.6 hadi Sh bilioni 610.0. Inatajwa kuwa kupungua huko kulichangiwa na mapato ya kawaida ya serikali pamoja na mikopo kutoka nje ya nchi.
KITAIFA
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Ramadhan Haji alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na mikakati yao kuelekea msimu mpya wa ligi.Alisema kuwa mabadiliko hayo yalilenga katika maeneo matatu makuu ambayo ni kuanzia kwenye uongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji.Alisema kuwa katika uongozi kama wanavyojua kuwa mwenyekiti wao amejiuzulu lakini nafasi hiyo itabakia wazi kama ilivyo isipokuwa sasa timu hiyo itakuwa na kurugenzi ya ufundi.“Tumefanya mabadiliko ndani ya timu yetu katika maeneo matatu, lengo tukiwa tunataka maboresho katika kuelekea msimu mpya wa ligi ili timu yetu iweze kufanya vizuri”, alisema.Alifahamisha kwamba katika kurugenzi ya ufundi kutakuwa na watu watatu ambao hao ndio watakaokuwa na dhamana nzima katika ufundi wa timu nzima, ikiwemo katika masuala ya fedha na ufundi.Kati ya watatu hao wawili aliwataja ingawa hakuwataja kwa majina lakini alisema kuwa mmoja ni raia wa Marekani na mmoja wa Uingereza ambao wamepata zawadi kutoka kwa wenzao ambao wanamitandao ya kijamii nje ya nchi.Katika benchi la ufundi mwenyewe kocha ameomba aongezewe washauri wengine ambao wamempa dhamana ya kutafuta mwenyewe watu hao, pamoja na kupatiwa daktari wa timu yao ambaye ni raia wa Quba.Timu ya Kilimani City inashiriki ligi daraja la pili wilaya ya Mjini ambapo msimu uliopita ilionekana kufanya vibaya jambo ambalo lilipelekea aliyekuwa Mwenyekiti wao Khamis Shaali kujiuzulu.
MICHEZO
  Na Gurian Adolf-Sumbawanga CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Rukwa, kimeiomba Idara ya Uhamiaji mkoani humo kufanya kazi zake kwa weledi bila kuburuzwa na wanasiasa tofauti ili kuepuka mvutano usiokuwa na sababu. Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa, Sadrick Malila, alisema chama hicho kinaiomba idara hiyo kubadilika kutokana na kitendo cha kuwakamata madiwani wa Kata ya Korongwe, Venance Bamilitwaye na Ruben Mkisi wa Kata ya Mkinga Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, wakiwatuhumu kuwa si raia wa Tanzania. Akizungumza na gazeti hili, Diwani Bamilitwaye, alisema mwaka 2005, aligombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu kupitia Chadema hakushinda na hakukuwa na shida yoyote na uraia wake haukutiliwa mashaka. Alisema mwaka 2010, aliingia tena katika kinyang’anyiro na akafuata taratibu zote na hakuwekewa pingamizi na alishinda katika kata hiyo ndipo tabu ilipoanza kwani alikamatwa nakufikishwa mahakamani kuwa si raia wa Tanzania. Naye Diwani Mkisi, alisema baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, iliibuka hoja kuwa si raia wa Tanzania ambapo alikamatwa na kufikishwa mahakamani, lakini alishinda kesi. Alisema anashangazwa na Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Carlos Haule, kuwapelekea wito wa kufika ofisini kwake. Naye Katibu wa Madiwani wa Chadema wa kanda hiyo, Joseph Nzala, alisema vitendo vinavyofanywa na idara hiyo ni vya unyanyasaji. Kwa upande wake, Haule alipozungumza na gazeti hili alikiri kuwaita madiwani hao na kuwataka wafike ofisini kwake leo.
KITAIFA
ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM KOCHA msaidizi wa Azam, Idd Nassoro ‘Cheche’, amesema hawajakata tamaa katika harakati ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na BINGWA jana, Cheche alisema licha ya Simba kuonekana kutangulia mguu mmoja katika mbio za kutetea ubingwa wao wanaendelea na mapambano ya kuwania taji hilo. Cheche alisema pamoja na  kuzidiwa alama nyingi na Simba walio juu yao katika msimamo lakini wanaamini wana nafasi ya kutwaa ubingwa.  “Simba wmaetuzidi alama 14 ambazo ni sawa kama na michezo mitano, hatujakata tama tunanafasi ya kutwaa ubingwa wa msimu huu kwa sababu  waliojuu yetu wanaweza kupoteza mechi. “Ligi ni ngumu kila mtu anapambana  sitaki kuamini kuwa mechi walizobaki nazo Simba watashinda zote, kwa sababu timu nyingi wanazokutana nazo zipo katika hatari ya kushuka daraja najua haziwezi kukubali kupoteza kirahisi na hiyo ndio nafasi yetu ya kuchukua kombe.” Azam ambayo ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 45, baada ya kucheza mechi 23 sawa na Simba,  lakini wakizidiwa kwa alama 14 baada ya Wekundu wa Msimbazi kujikusanyia 62.
KITAIFA
NAIROBI, KENYA WAZIRI wa Elimu wa Kenya, Amina Mohamed ameivuja Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Moi, baada ya mwanafunzi kubakwa katika bweni Hatua hiyo imekuja huku mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyopo mjini hapa, Jael Mureithi akichukua hatua ya kustaafu kama ilivyotaafiwa na Tume ya Huduma za Walimu (TSC). Aidha, chama cha walimu na wazazi wa shule hiyo kimevunjwa huku wazazi wakipanga kukutana na mameneja wa shule waliobakia, Jumapili ijayo. Hayo yote yametokea jana wakati Serikali ikiwachukulia hatua maofisa wa shule hiyo ambayo vyombo vya habari vya Kenya vimekuwa vikiripoti tukio la lililotokea shule hapo kwa uzito mkubwa. Mohamed ameamuru kuvunjwa kwa timu ya ulinzi katika shule hiyo iliyopo Kaunti ya Kibra mapaka ja[p mabadiliko ya usalama yatakapokamilika. Alisema wanafunzi, walimu, wafanyakazi na wageni wote wanaoingia shuleni lazima wakaguliwe. Uamuzi wa mkuu wa shule kustafu mapema umekuja siku moja tu baada ya wapelelezi kutoka Kitengo cha Upelelezi wa Makosa Makubwa ya Jinai na Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua sampuli za vinasaba kutoka kwa wafanyakazi wanane wa kiume, wakiwamo walimu sita kwa ajili ya uchambuzi wa alama za vidole. Kwa mujibu wa uchunguzi wanaume hao wanaishi ndani ya shule au wanaaminika walikuwa shuleni wakati wa kitendo cha ubakaji kilipofanyika, alfajiri ya Jumamosi. Wakati huo huo, vurumai, milio ya risasi na mabomu ya machozi yalitawala eneo la Kibra jana wakati maafisa wa polisi walipokabiliana na wakazi wanaopinga kubomolewa kwa vibanda vya biashara vilivyopo karibu na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Moi. Polisi wameweka kambi shuleni hapo kuendelea na uchunguzi na kuondoa mazingira yoyote yanayohatarisha au kuwa maficho ya uhalifu katika shule hiyo ambayo mwaka jana pia ilikuwa vochwa vya habari katika vyombo vya habari baada ya wanafunzi wanane kufa kwa moto ulioteketeza moja ya
KIMATAIFA
Celine arudi kwenye muziki LAS VEGAS, MAREKANI BAADA ya Celine Dion kukaa kwa muda mrefu bila ya kufanya muziki kutokana na kumuuguza mume wake, Rene Angelil, sasa ameanza kazi ya muziki upya. Celine alipanda jukwaani juzi huku mume wake akiwa pembeni na kabla ya kuimba aliwaambia mashabiki: ‘Nadhani kila mmoja anajua nini ninataka kukufanyia leo siku yangu rasmi.’ Hata hivyo, msanii huyo alijikuta akidondosha chozi kutokana na mapokezi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki wake. Baada ya kumaliza kuimba msanii huyo aliwashukuru mashabiki hao na kuwaahidi kuwapa burudani mbalimbali siku zijazo. “Nashukuru kwa uwepo wenu hapa, lakini kikubwa kilichonifanya niwe hapa ni watoto wangu watatu na mume wangu ndio waliniambia nifanye hivi, nawapenda sana watoto wangu pamoja na mume wangu na nipo tayari afie mikononi mwangu,” alisema Celine.
BURUDANI
AMINA OMARI-HANDENI HOSPITALI ya Wilaya ya Handeni   inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chumba maalum cha uangalizi wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) na kusababisha baadhi yao kufariki dunia. Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Faisal Said alipozungumza MTANZANIA  jana. Alisema hali hiyo imesababisha kuongezeka vifo vya watoto wachanga. Alisema   huduma hiyo kwa sasa inapatikana katika Hospitali ya Rufaa   Bombo pekee ambayo ni umbali wa zaidi ya kilometa 150  kutoka wilaya hiyo.   Mganga huyo aliwaomba wadau wa maendeleo kujitokeza kuchangia ujenzi wa chumba hicho  kusaidia kusogeza huduma hiyo karibu na kunusuru maisha ya watoto wachanga. “Umbali wa huduma hiyo nao unachangia kwa kiasi kikubwa   mnapopata mtoto ambaye amezaliwa njiti, hivyo wakati mwingine anafia njia kabla ya kufikishwa Bombo,” alisema Dk. Faisal. Muuguzi wa Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo, Mwajuma Mvungi alisema kitengo cha huduma ya mama na mtoto licha ya kufanya vizuri kinakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba. Alisema hali hiyo inazorotesha utoaji wa huduma kwa sababu hospitali hiyo wakati mwingine hulazimika kupokea wajawazito kutoka   wilaya ya jirani ya Kilindi. Baadhi ya wajawazito waliozungumza na MTANZANIA, Tahiya Ali alisema licha ya huduma nzuri zinazotolewa kuna ukosefu wa kipimo cha mapigo ya moyo ya mtoto kwa wajawazito.  “Nilipoteza mimba ya mtoto wa tatu kwa ukosefu wa kifaa hicho kumbe mtoto alikufa mapema mpaka kujua ilikuwa imeshapita miezi miwili,” alibainisha.
AFYA
WANANCHI wenye makazi na wanaofanya shughuli zao kwenye hifadhi za wanyama wilayani Songwe, wametakiwa kuhama kutoka maeneo hayo kwa kuwa si salama na yanahatarisha maisha yao kutokana na uwapo wa wanyama wakali. Kwa mujibu wa ofisa maliasili kata ya Kapalala, wilayani Songwe, Benard Nenje, kumekuwapo na matukio mengi ya wakazi wa maeneo yaliyo jirani na hifadhi kushambuliwa na wanyama sambamba na kuharibiwa mali zao ikiwamo mazao shambani.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Nenje alisema kwa mwaka jana pekee, wananchi 24 walipata madhara ya kuvamiwa na wanyama, ambapo kati yao 22 wanatokea kata ya Gua na wawili kata ya Ngwala ambao serikali ililazimika kuwalipa fidia kutokana na mazao yao kuliwa na tembo. Alisema kwa mwaka huu wananchi 30 wanatakiwa kulipwa fidia kutokana na tembo kula mazao yao na wengine kujeruhiwa na simba na fisi.Ofisa huyo alisema asilimia kubwa ya wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi wanakuwa hawaelewi madhara yake hivyo kujikuta wakijenga makazi na kujishughulisha na kilimo bila kuujulisha uongozi wa kijiji pamoja na kata ili kupata utaratibu. “Watu hao wamekuwa wakijeruhiwa na wanyama wakali wakiwamo simba pamoja na mazao yao kuliwa na tembo jambo linaloigharimu serikali kuwalipa fidia kutokana na kosa walilofanya wenyewe,” alisema.
KITAIFA
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM TIMU ya Azam imepeleka barua rasmi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikiomba wamfungie beki wa Mbeya City, Juma Nyosso, kwa kitendo cha udhalilishaji dhidi ya nahodha wao, John Bocco. Nyosso alifanya kosa hilo wakati timu yake ilipokubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Jumapili iliyopita, tukio lililokemewa vikali kwa watu mbalimbali wakitaka beki huyo aadhibiwe vikali. Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inatarajia kukutana muda wowote kuanzia sasa kupitia suala la beki huyo pamoja na mambo mengine. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Azam, Jaffary Idd, alisema uongozi wa timu hiyo umelaani vikali sana tukio la beki huyo, huku ukidai hawawezi kuingilia uhuru wa TFF katika kutoa adhabu stahiki kwa Nyosso. “Tunawashukuru Watanzania wote, vyombo vya habari vilivyochukizwa na kitendo hicho na kuanza kukilaani. Lakini sisi kama Azam FC hatuwezi kuingilia uhuru wa TFF. “TFF kupitia kamati yake ya nidhamu, ndio inaweza kukaa na kutoa uamuzi kwamba ni adhabu gani impe huyo mchezaji kutokana na sheria zilizopo zinazotokana na kosa lake,” alisema. Azam imeomba itolewe adhabu inayoendana na Kanuni za Ligi za shirikisho hilo, 37(24) za udhibiti wa wachezaji inayoeleza kuwa: “Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi, au ya kidhalilishaji, au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinadamu, atatozwa faini ya kati ya Sh milioni moja mpaka milioni tatu au/ kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka 10 ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.” Hiyo ni mara ya pili ndani ya mwaka huu Nyosso kufanya tukio hilo, mara ya kwanza ilikuwa Machi, alipomdhalilisha aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Elias Maguli, katika mechi yao msimu uliopita na kupelekea kufungiwa mechi nane. Wahanga wengine wa tukio hilo ni beki Amir Maftah, wakati akiichezea Yanga kwenye mchezo na Simba, ambapo baada ya kufanyiwa hivyo alimpiga kichwa na kutolewa kwa kadi nyekundu kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji Joseph Kaniki.  
MICHEZO
KOCHA Msaidizi wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Simba, Masoud Djuma amesema anatamani kukutana na Gor Mahia kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Juni 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Simba ilipoteza kwa magoli 2-0 dhidi ya Gor Mahia, katika mchezo wa fainali wa michuano ya SportPesa Super Cup, iliyoshirikisha timu nane iliyofanyika hivi karibuni mjini Nakuru, Kenya. Akizungumza na gazeti hili jana, Djuma alisema kitu cha msingi anachokifanya kwa sasa ni kurekebisha mapungufu aliyoyaona kupitia kwenye michuano hiyo ili wacheze fainali za Kagame kama walivyokusudia.“Lengo langu kubwa ni kucheza fainali na Gor Mahia ili kulipa kisasi kwa sababu walitufunga kwenye fainali ya SportPesa kule kwao Kenya, tulikuwa na mapungufu lakini tupo kwenye maandalizi kabambe ya kuhakikisha tunabakiza taji Tanzania,” alisema Djuma. Kocha huyo alisema amewaita wachezaji wake wote kuingia kambini ili kuanza maandalizi ya michuano hiyo ambayo pia alisema ataitumia kama kipimo cha kuwajaribu wachezaji wake waliosajiliwa kwa msimu ujao.Alisema anatambua kuwa msimu ujao wa ligi watakuwa na changamoto kubwa ya kutetea taji lao kutokana na mafanikio waliyopata msimu uliopita hivyo wanalazimika kujenga kikosi imara kitakachopambana kupata matokeo bila kuhofia timu yoyote ndani na nje ya nchi. Simba ndiyo bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ya Kombe la Kagame, ikilitwaa mara sita na kuzipiku timu nyingine kubwa zikiwemo watani zao wa jadi Yanga ambao wamelibeba mara tano. Yanga haitashiriki michuano ya mwaka huu baada ya kujitoa kwa madai ya kujiandaa na michuano ya kimataifa.
MICHEZO
LEONARD MAG’OHA – DAR ES SALAAM WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe, ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) kukutana na madereva teksi, wahudumu wa hoteli na waongoza utalii ili kuongeza ufanisi wa sekta ya usafiri wa anga nchini. Akizungumza katika kongamano la pili la wadau wa sekta ya usafiri wa anga Dar es Salaam juzi, Kamwelwe alisema watoa huduma hao ni watu muhimu katika shughuli za utalii na usafiri wa anga, kwa sababu wana mawasiliano ya watalii wengi ambao wamewahi kutembelea nchini.  “Hamza (Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari) nendeni Arusha, Kilimanjaro na Mbeya mkutane na ‘taxi drivers’, ‘tour guiders’ na wahudumu wa hoteli, mtapata mambo ya ajabu, mnaweza kukuta kijana ana namba 200 za watalii. “Watalii ni watu wasiopenda kutumia muda mwingi safarini na sisi hivi karibuni tunakuwa na ndege za moja kwa moja,” alisema Kamwelwe. Alisema wizara yake iko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ili ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa fani za urubani na uhandisi wa ndege kuwezesha kuandaa wataalamu wa ndani. Aidha alilitaka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuongeza safari moja ya ndege kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam itakayokuwa ikitoa huduma mchana tofauti na sasa ambapo kuna safari tatu wakati wa asubuhi na jioni. Aliongeza kuwa huenda kuanzia Julai shirika hilo likaanzisha safari ya kutoka Mwanza kwenda barani Ulaya na kufungua fursa kwa wafanyabiashara kutumia soko la samaki lililopo nchini humo. Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, alisema kongamano hilo litawawezesha wadau kuendelea kujitafsiri na kuielewa sekta ya usafirishaji wa anga na kujua kama inaendana na dira ya taifa ya maendeleo ya viwanda. “Litatuwezesha kuangalia nafasi ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji katika kuziba pengo la wataalamu katika sekta hii, kuangalia mchango na umuhimu wa mashirika madogo ya ndege katika dira ya taifa na kuangalia namna ya kukabili athari za mazingira zinazotokana na moshi wa ndege,” alisema Johari. Aliongeza kuwa kutokana na wadau kuanza kuchangia katika mfuko wa mafunzo, kumesaidia kukusanya fedha ambazo zitatumika kusomeaha marubani na wahandisi wa ndege 10 kuanzia Septemba ili kuwawezesha kuingia katika soko la ndani ambalo linakua kwa kasi.
KITAIFA
NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM BAADA ya kuanza kwa kishindo katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema uimara wa kikosi ndio umechangia wachezaji kujiamini na kuendelea kuwa fiti uwanjani. Yanga ambao wametetea taji la ubingwa wa ligi hiyo kwa misimu miwili mfululizo, ilianza msimu mpya kwa kasi baada ya Jumapili iliyopita kuichapa African Lyon mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kocha huyo raia wa Uholanzi, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wachezaji wanajiamini uwanjani kutokana na mambo mengi hasa kama miili yao iko fiti na imeimarishwa kwenye mazoezi kwani hata akili zao zinakuwa zimetulia ili kufikia malengo. Alisema pamoja na wachezaji kujikita kwenye mambo hayo muhimu katika kusaka ushindi, bado haamini kama uwezo wa timu uwanjani unaweza kubaki kwenye kiwango bora muda wote bila kufanyiwa maboresho kila wakati ili kuendana na ushindani uliopo. Alieleza kuwa ushindi unatokana na motisha kwa wachezaji, jambo ambalo analifanyia kazi na kulipa kipaumbele kila mara wakati akitoa maelekezo kwenye mazoezi. “Kama akili za wachezaji zimetulia lazima watafanya mambo mazuri uwanjani kutokana na kujiamini kwao, pia ninaamini ushindi unatokana na motisha wanayopata wachezaji katika kufikia malengo yaliyokusudiwa,” alisema Pluijm. Aidha, Mholanzi huyo alisema jambo la msingi kwake ni kuhakikisha timu inajiandaa vizuri kwa kuitilia mkazo mechi inayofuata Ligi Kuu ili kuendeleza wimbi la ushindi huku akidai kwa sasa hawana muda wa kupoteza. Kikosi cha Yanga kimerejesha makali yake Ligi Kuu baada ya kushindwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza kushiriki mechi za kimataifa kwenye Klabu Bingwa Afrika lakini ikaondolewa hatua ya 16 bora na kuingia Kombe la Shirikisho ambapo ilifanikiwa kuingia hatua ya makundi.
MICHEZO
WIKI hii, Julai 1, Benki ya Dunia iliingiza Tanzania katika kundi la nchi zenye kipato cha kati. Hizi ni habari njema hata pamoja na kwamba wapo wanaoona kuna mapungufu fulani fulani katika utendaji. Hatua ya kutoka katika umaskini na kupanda kwenda katika hatua nyingine ya juu huusisha suala zima la uchumi au maendeleo ya kiuchumi. Lakini pamoja na hayo maendeleo ya kiuchumi huguswa na vitu au mambo mengi mfano kutenda haki, amani, usalama, utulivu nakadhalika. Mtu yeyote anapokuwa katika mazingira yenye kutenda haki, amani, utulivu humwezesha kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuwa mzalendo kwa nchi yake ikiwa ni pamoja na kulipa kodi. Sasa mazingira yanapokuwa tofauti na hayo, ndiyo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi . Kwa sababu hiyo sisi tunaweza kusema tumekuwa mabalozi wazuri wa kusisitiza suala la haki kila wakati, kwa sababu tumekuwa tukiamini haki ni msingi wa mambo yote mazuri. Na ndio maana tumekuwa tukikosa na wakati mwingine kukumbusha kutenda haki hasa katika vyombo vile vya kimaamuzi na kiutendaji. Tumekuwa tukisisitiza kwamba vyombo hivyo vinapaswa kutambua wajibu wao kuwa ni kutafuta namna ya kutatua matatizo na si kuyaongeza. Yapo baadhi ya matukio si yote ambayo yamefanywa na vyombo hivyo na hivyo kutoa taswira ya kukomoa au kuumiza baadhi ya watu kwa makusudi. Tumekuwa tukisisitiza  hayo kutokana na kuwapo kwa ripoti ambazo zinaonyesha kuwa barani Afrika kwa muda mrefu sasa watu wameumizwa na vitendo vya kudhulumiwa haki zao msingi. Kwa mujibu wa ripoti hizo hata kutopea katika umaskini wa kimawazo, na hivyo wengi kuhadaika na kauli za wanasiasa, viongozi na watu wenye nafasi katika jamii, msingi wake ni dhuluma ya haki zao za msingi.  Kwa misingi kama hiyo sisi kama  chombo cha habari  tunao wajibu wa kukumbusha kwamba vyombo hivyo kila inachofanya kabla ya kutoa uamuzi wowote basi vitambue vinao wajibu wa kuchunguza, kusikiliza, kubadilisha na kuboresha. Zipo nyakati tumeshuhudia vyombo hivi vikichukua uamuzi wa ghafla hata katika masuala nyeti sana katika mifumo ya sheria, utumishi nk.  Vyombo hivi vinapaswa kutambua kwamba chochote kitakachofanyika bila kufuata misingi hiyo tuliyoitaja hapo juu kitakwenda kuathiri mustakabali mwema wa Taifa letu. Wakati fulani aliyepata kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedikto wa XVI, alitoa changamoto kubwa kwa watawala wa dunia.  Kwa maneno yake mwenyewe alisema; “jamii yenye haki hujengwa na wanajamii wenye haki”.  Maana yake tukitaka kujenga jamii yenye haki hatuna budi sisi wenyewe kuwa wenye haki. Kiongozi huyo alikwenda mbali na kusema; wao kama kanisa hawana mbinu za kiufundi wala nafasi ya kuingilia mambo ya siasa moja kwa moja lakini alibainisha wazi utume ambao alisema kama kanisa haliwezi kuuacha hata kidogo ni ule wa kuutangaza ukweli. Ukweli si jambo ambalo linapaswa kubebwa na taasisi zetu za kidini tu bali hata katika serikali zetu na taasisi zake, mahakama zetu, vyombo vya ulinzi na uslama kama Jeshi la Polisi,  Bunge nk. Kuna msemo mmoja kwamba; ukweli ndio utakaowaweka watu wote huru: iwe katika siasa au katika nyanja yoyote ya kijamii.  Kwa sababu hiyo tunaamini ujenzi wa jamii yenye misingi ya haki ni wajibu wetu sote lakini serikali, mahakama na Bunge linawajibika kujenga dhamira hiyo.  Mahakama itambue kama ni taasisi ya kupigania haki, serikali ni wakala wa haki vivyo hivyo hata Bunge.  viongozi  wakiwamo wale wa kisiasa, na wananchi watambue kuwa wao ni wawajibikaji katika shughuli za kijamii na iwapo wote hawa watauzingatia ukweli ndani ya dhamiri zao zilizojengwa juu ya ukweli na ukweli tupu, basi jamii ina uhakika wa kujenga haki na amani na matokeo ya hayo ni kupaa kimaendeleo.
UCHUMI
Msaani wa bongo fleva maarufu Afrika Diamond Platinumz amesema yupo katika mpango wa kuanzisha Akademi ya soka hapa nchini. Platinumz ambaye jina lake halisi ni Nasibu Abdul amesema tayari yupo katika mazungumzo na mchezaji wa zamani wa soka la kulipwa wa nchini Cameroon Samwel Eto’o. Diamond anasema ana amini Afrika mashariki kuna vipaji vingi vya soka ambavyo ni hazina kwa baadaye. “Hapo awali nilidhani kujihusisha na michezo si jambo la faida lakini sasa naamini tofauti. Huko mbeleni nitamiliki timu yangu mwenyewe inayoshiriki ligi kuu na sitataka kuanza mwanzo,” amesema Diamond.
MICHEZO
Na MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM ASILIMIA 96 ya wanawake wanapitia ukatili wa kijinsia katika masoko ya Manispaa ya Ilala na Temeke, Dar es Salaam. Aidha, kikundi cha wahuni kinachofahamika kwa jina la Mashabanga, kimetajwa kuhusika na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake wanaofanya biashara katika soko la Mchikichini wilayani Ilala. Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye masoko, Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa, alisema kikundi hicho kinaongoza kwa kufanya vitendo hivyo, na matumizi ya dawa za kulevya. “Hili suala limekuwa tatizo kubwa si soko hili tu na mengine, kuna vijana hawana uadilifu, walevi wa dawa za kulevya na bangi, waliofikia hatua hata kuwadhalilisha wanawake kwa kuwafanyia ngono huku kwenye vibanda vya kuuzia nguo. “Tulishawafuatilia na kuwakamata vijana hao ambao uhamisha tabia hizo kwenye masoko mengine, lakini cha kusikitisha wafanyabiashara wanawatetea na kuwadhamini polisi, wakidai ni vijana wao wa kufanyia biashara zao,” alisema Ngowa.
KITAIFA
Tanasha Donna kwa kawaida aliipakia picha yake moja mtandaoni, chini ya picha hiyo aliashiria kuwa alikuwa nchini Kenya. Hii ilikuwa muda mfupi tu baada ya kubainika kuwa alizing’oa picha zote walizopiga na Mondi katika mtandao wake wa Instagram. Hatua ambayo inaonekana kuibua hisia mseto kati ya mashabiki wa msanii huyo. Baadhi ya wapinzani wake walijimwaya mtandaoni na kumshauuri amkome kabisa Mondi na ajishughulishe na kazi ya kumlea mwanawe pasi kumhusisha msanii huyo. Wapo walioshangazwa wakidai kuwa Donna alionekana kujawa huzuni katika picha hiyo. Home! 💓💓 #Nairobi Kenya 💥🚀🚀🚀 #TANASHADONNA A post shared by Tanasha Donna Oketch (@tanashadona._) on Mar 1, 2020 at 10:40pm PST Si hayo tu, wapo waliopiga hatua zaidi na kumpa kwaheri na kumkumbusha kutomuacha mwanawe Tanza Ni dhahiri kuwa wengi wa mashabiki walijua wazi kuwa uhusiano wake na Mondi ulikuwa umefikia ukingoni, hii ni kulingana ma jumbe hizo walizommiminia. Licha ya kurushiwa tope kiasi hicho, wapo mashabiki waliojitokeza kumliwaza na kumwambia asiogope japo magumu yanamuandama. Yupo mmoja aliyempa ujumbe spesheli, alimwambie Donna kuwapa salamu Wakenya na kuwaambia kuwa Tanzania ni mziki tu na wala si uhusiano. Uhusiano kati ya Diamond na Tanasha Donna umekuwa na misukosuko hivi karibuni licha ya Donna mwenyewe kujitokeza hivi majuzi na kufutilia uvumi huo akieleza kuwa uhusiano wao ungali imara na kamwe hautasambaratika. Iweje sasa?  
BURUDANI
KIPANDE cha barabara za magari ya kawaida kutoka eneo la Ubungo hadi Shekilango jijini Dar es Sal aam, kitafungwa kwa takriban miezi miwili kuanzia sasa ili kupisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaofanywa Ubungo katika makutano ya barabara za Mandela na Morogoro.Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kampuni ya Ujenzi ya CCE CC inayojenga barabara hizo, barabara hiyo itafungwa kuanzia O ktoba 6, mwaka huu hadi Novemba mwishoni ili kupisha ujenzi eneo hilo. Ilisema wakati utekelezaji utakapoanza, barabara mbadala itakayotumika ni ile ya Mabasi  Yaendayo Haraka (DART), ambazo mbili zitatumiwa na magari ya kawaida kuanzia kituo cha mabasi hayo cha Ubungo hadi eneo la Benki ya NB C eneo la Ubungo Stendi ya Mabasi ya mikoani.Aidha, barabara hizo mbili zitatumika pia kipindi cha msongamano mkubwa nyakati za asubuhi na jioni na mabasi ya DART yatatumia barabara yake moja kwa eneo hilo. H ata hivyo, katika kutekeleza matumizi ya barabara hizo, ipo michoro inayoongoza magari yenye rangi kijani, nyekundu na nyeupe huku madereva wakitakiwa kuwa waangalifu wakati wa kutumia barabara hizo. Ujenzi wa barabara hizo za juu ulizinduliwa Machi 20 mwaka jana na Rais John Magufuli na mradi huo utagharimu Sh bilioni 247 na utajengwa kwa muda wa miaka mitatu.Wakati ujenzi huo ukisubiriwa kukamilika kwa hamu na kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo na barabara nyingine zinazoingiliana nayo, Septemba 27 mwaka huu, Rais Magufuli alizindua Daraja la Juu la Mfugale eneo la Taraza lililojengwa kwa gharama ya Sh bilioni 106.9. Daraja hilo lilijengwa na mkandarasi Kampuni ya Japan ya Sumitomi Mitsui kwa muda wa miezi 29, hivyo kukamilika kabla ya muda uliopangwa ambapo lilikuwa likamilike O ktoba 31, mwaka huu.
KITAIFA
LONDON, ENGLAND MSHAMBULIAJI wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez, ataikosa michezo miwili ya awali ya Ligi Kuu nchini England kutokana na kusumbuliwa na tumbo mazoezini. Mchezaji huyo ambaye anashinikiza kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho katika kipindi hiki cha majira ya joto, ataukosa mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Leicester City kesho Ijamaa na Jumamosi ya wiki ijayo dhidi ya Stoke City. Hata hivyo, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amewaondoa wasiwasi mashabiki wao kwamba mchezaji huyo atajiunga na wenzake baada ya hali yake kuwa sawa na kukitumikia kikosi chake. Wenger aliongeza kwa kusema tayari wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo juu ya kumwongezea mkataba mpya, hivyo wamefikia pazuri na kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza mkataba mpya. “Katika michezo yetu miwili ya mwanzo katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, tutamkosa mshambuliaji wetu, Sanchez. “Mchezaji huyo amepatwa na tatizo kidogo la tumbo wakati wa mazoezi ya mwisho, hivyo anatakiwa kufanyiwa vipimo ili kuangalia tatizo alilonalo, kuna uwezekano mkubwa wa kuikosa huduma ya mchezaji huyo kwa wiki mbili,” alisema Wenger. Katika suala la kumwongezea mkataba, Wenger alisema kila kitu kupo wazi na kuna uwezekano wa kumalizana na mchezaji huyo hivi karibuni. “Kuna uwezekano mkubwa wa kumwongezea mkataba mpya, siku zote mchezaji akiwa anafikia mwisho wa mkataba wake tunakuwa na mazungumzo naye juu ya kumwongezea, hatuna sababu ya kumuacha Sanchez akiondoka, tupo kwenye hatua za mwisho sasa,” aliongeza Wenger. Hata hivyo, kocha huyo ameweka wazi kuwa hadi sasa hajapokea ofa yoyote kutoka kwa klabu ya PSG na nyingine ambazo zinadaiwa kuonesha nia ya kuitaka saini ya mchezaji huyo. “Hadi sasa sijafanya mazungumzo yoyote na mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, juu ya kutaka kumsajili Sanchez, alikuwa anapambana kuhakikisha anaipata saini ya mshambuliaji wa Barcelona, Neymar, nadhani kwa sasa wanaifuatilia saini ya Kylian Mbappe na wala si Sanchez. “Kwa sasa siangalii juu ya kupokea ofa kwa kuwa nilishasema tangu awali kuwa mchezaji huyo hauzwi, bado Arsenal inahitaji huduma yake hadi pale mwisho wa mkataba wake.
KIMATAIFA
Kufuatia kutangazwa kusaini makaba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Simba, Habari za uhakika ni kwamba mshambulizi wa Mabingwa hao Ligi Kuu Tanzania Bara John Bocco inaelezwa amesaini mkataba pia na timu ya Polokwane inashiriki Ligi Kuu Afrika Kusini. Akifanya mahojiano na kupitia kipindi cha Sports Headquarters kinachorushwa na kituo cha redio cha Efm moja ya watu wa karibu wa klabu ya Polokwane City amesema  John Bocco alisaini mkataba na klabu hiyo mapema mwezi April mwaka huu kutokana na mkataba na klabu yake kuelekea ukingoni. “Nimeshangazwa na taarifa za John Bocco kusaini mkataba na klabu ya Simba wakati tayari ni mchezaji wa Polokwane, ninachoweza kusema ni kwamba, pengine John Bocco hakuwa tayari kufanya kazi Afrika Kusini. Ninachoweza kusema labda ni vilabu vyote viwili kukaa kwa pamoja na kufikia makubaliano kuangalia namna gani ya kutatua tatizo,” amesema. Lakini kwa sasa ninachoweza kusema na kuhitimisha ni kwamba Bocco ni mchezaji wa Polokwane City. Simba ndiyo wanapaswa kuwasiliana na Polokwane ili kujua namna ya kutatua suala hili.”  
MICHEZO
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeisifu serikali kwa kuendelea kulipa fedha zinazohitajika na kwa wakati kadiri ya mkataba wa ujenzi, kwa mkandarasi ujenzi wa mradi mkubwa wa kimkakati wa kitaifa wa bwawa la kufua umeme wa megawati 2,115 ( JNHPP).Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco, Dk Alexander Kyaruzi aliipongeza serikali kulipa fedha kwa mkandarasi.Ametoa pongezi hizo Morogoro wakati akifunga mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa shirika hilo.“Ninayo furaha kuwataarifu mradi wa kimkakati wa kitaifa wa kuzalisha umeme wa maji wa megawati 2115 wa Julius Nyerere unaendelea vizuri. Napongeza juhudi kubwa zinazofanywa kusimamia mradi huu ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,” amesema Mwenyekiti huyo wa Bodi.Mradi huo unatekelezwa na wakandarasi, Arab Contractors na Elsewedy Electric za Misri. Ujenzi wake ni wa miezi 42 ikijumuishwa miezi sita ya matayarisho na unapaswa kukamilika ifikapo Juni 14, 2022.Serikali kulingana na mkataba imelipa Sh trilioni 1.07 sawa na asilimia 15 ya gharama, Sh trilioni 6.5. Mbali na hayo, Dk Kyaruzi aliitaka menejimeti ya shirika kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 wa Singida – Arusha – Namanga na ule mpango wa ujenzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 400 Iringa – Mbeya – Tunduma.Alisema kuharakishwa kwa ujenzi wa miradi hiyo kunaunganisha mifumo miwili ya gridi ya taifa ya nchi za Kusini mwa Afrika (SAPP) na wa nchi za Afrika Mashariki (EAPP) ( Eastern Africa Power Pool)“Nchi iko katika nafasi nzuri ya kijiografia kufaidika na mpango huu utakaowezesha kufanya biashara ya nishati ya umeme mara mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere utakapokamilika,” amesema.Pamoja na hayo alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyakazi wa shirika na menejimenti kwa kuwezesha shirika kutoa mchango wa huduma kwa serikali wa Sh bilioni 1. 436 na kusema huo ni mwanzo mzuri kwa shirika katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta maendeleo katika nchi yetu.Aliutaka uongozi wa shirika hilo kusimamia vizuri masuala ya usalama kazini ili kuhakikisha rasilimali watu ambayo imeandaliwa kwa muda mrefu inaendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema walijadili mafanikio, changamoto na mustakabali wa shirika hilo kwa maendeleo ya sekta ndogo ya nishati ya umeme hapa nchini.Alisema mambo yaliyowekewa mkakati ni uboreshaji upatikanaji wa umeme, usalama kazini, kudhibiti upotevu wa umeme na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya shirika ili liweze kujiendesha vyema.Awali Mratibu wa Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP), Stephen Manda aliyewasilisha mada ya mradi huo alisema kazi kubwa inayoendelea ni kujenga njia ya kuchepusha maji ambayo imefikia asilimia 19 kabla ya kuanza ujenzi wa bwawa lenyewe ambayo ndiyo sehemu muhimu ya mradi huo.Manda, msimamizi wa mradi huo kutoka Tanesco alisema madaraja yamekamilika na la mwisho limefikia asilimia 75 na litamalizika mwezi huu kupitisha magari upande wa pili wa mto kwa ujenzi huo mkubwa.
KITAIFA
NA JOSEPH HIZA NA MASHIRIKA YA HABARI, ANAITWA Liu Lingchao, raia wa China, ambaye alitembea kwa mguu kwa miaka mitano akiwa na nyumba mgongoni mwake. Miaka zaidi ya 20 iliyopita, Liu Lingchao aliondoka mji wake mdogo wa nyumbani uliopo katika Jimbo la Guangxi kuelekea majiji makubwa ya ndoto yake Guangzhou na Shenzhenof kutafuta maisha. Naam, alifanikiwa kupata ajira. Lakini miaka zaidi ya mitano iliyopita mambo yalimwendea vibaya baada ya kufukuzwa kazi na kisha kutimuliwa kutoka nyumba alimokuwa akiishi kutokana na ukosefu wa fedha za kulipia pango. Hilo lilimfanya achukue uamuzi mgumu kinyume na ule alioufanya zaidi ya miaka 20 iliyopita;- kurudi nyumbani kuliko kuishia kutaabika katika miji ya watu, ambako hakuwa na msaada. Katika safari hiyo ya kurudi nyumbani, badala ya kuchukua usafiri wa kueleweka, ambao ungemchukua saa zisizozidi 12 iwapo angetumia njia ya barabara kama hapa Tanzania, pengine kutokana na kutokuwa na kitu mfukoni alichagua kutembea maili 450 nzima kurudi nyumbani kwa mguu. Kichekesho zaidi ni kwamba ili kukabiliana na hali ya hewa kama vile mvua, ilibidi atengeneze nyumba ambayo ataibeba mgongoni kwa safari yake yote hiyo ya mwendo wa konokono. Utembeaji huo kutoka Shenzhen hadi jimbo la nyumbani la Guangxi ni sawa wa kutembea kutoka New York hadi North Carolina nchini Marekani au karibu sawa na umbali kutoka Dar es Salaam hadi Njombe nchini Tanzania. Umbali huo si mchezo! Lakini pia mbona kuna simulizi za watu wakitembea maili 3,000 kutoka pwani moja hadi nyingine ya Marekani ndani ya mwaka tu? Sasa kwanini ilimchukua Liu miaka mitano kutembea moja ya sita (1/6) ya umbali huo? Pengine ni nyumba hiyo yenye uzito wa kilo 60. Urefu na upana wa futi 5 x 7 iliyong’ang’ania mgongoni mwake ilimchelewesha? Maswali hayo yanaweza kujibiwa na hili, Liu alikuwa akijitegemea kwa asilimia 100 kwa mahitaji yake ya msingi ya kimwili ikiwamo maji, chakula na kadhalika wakati wa safari hiyo. Fedha za kujitegemea angezipata wapi ilihali hana ajira wala kipato? Lingchao alikuwa akiokota barabarani makopo na chupa zilizotumika na kuziuza katika miji aliyopitia katika safari yake hiyo ya kurudi nyumbani na hilo lilimwezesha kupata mahitaji yake. Hivyo, hakuwa katika haraka ya kufika nyumbani mara moja, kwamba ilimbidi ahangaike nyumbani. Hayo kwa pamoja ni kiini kilichomchelewesha, yaani kilichomfanya achukue miaka mitano kuwasili nyumbani. Muuzaji huyo (38), alijiwa na wazo la kuwa na nyumba hiyo aliyoitengeneza kutokana na mianzi na plastiki ili kukabiliana na changamoto ya hali ya hewa wakati wa safari yake hiyo ya miaka mitano. Anasema nyumba yake hiyo inamfanya kuwa huru na anaibeba kila aendako kusini mwa China wakati akiuza chupa za vinywaji anazoziokota barabarani. “Nilichoshwa na matukio ya mara kwa mara ya kujikuta nikinyeshewa na mvua mithili ya kuku nisiye na makao maalumu. “Hata nilipoona mahali pakavu kama vile chini ya daraja, au katika jengo lililotelekezwa nilikuta tayari kuna mtu ameniwahi kujihifadhi na ilinibidi niombe ruhusa ya kuchangia kujihifadhi. “Ikaja siku nilipochoshwa na hali hii nikaamua kujenga nyumba yangu kutokana na mianzi katika shamba moja nilililopata kibarua cha wiki kadhaa. “Wakati kazi ilipoisha na hivyo vibarua kutawanyika, wakati wa kuhama niliona vyema nihame na nyumba hiyo na hivyo nikairekebisha ili iniwie rahisi kuibeba na tangu hapo sikurudi nyuma,” anaeleza. Akipewa jina la ‘Konokono Mkubwa wa Kibinadamu,’ nchini humo, Lingchao alitembea maili 20 kwa siku 20 na alitumia nyumba tatu alizozitengeneza na kuzibeba mgongoni baada ya mbili za awali kubomoka.
KIMATAIFA
MWALIMU wa Shule ya Msingi Forest katika Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro, Pendo Manyama (29) na wanawe wawili wamekufa baada ya mtungi wa gesi iliyokuwa imevuja, kujaa ndani ya chumba na kulipuka.Moto huo ulilipuka mama huyo alipoingia ndani na jiko la mkaa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Wilbroad Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea Desemba 26, mwaka jana saa 8:30 mchana maeneo ya Mtaa wa Kola B katika Manispaa ya Morogoro nyumbani kwa Baltazar Kineneko (37). Kwa mujibu wa Kamanda inaonekana mtungi wa gesi ulifunguliwa na kusababisha gesi kujaa ndani.Alisema mke wa Baltazar, Pendo Manyama ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Forest, bila kujua aliingia na jiko la mkaa na kusababisha moto kulipuka na kuwaunguza mama na watoto wawili, Angela na Adrian Baltazar (2) na kusababisha vifo vyao watatu hao. Kutokana na tukio hilo, Kamanda Mutafungwa alitoa mwito kwa wananchi kuwa waangalifu wakati wote wanapokuwa wakitumia vyombo hivyo vya nyumbani ili kujiepusha na madhara yoyote yale.Katika tukio jingine, mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye pia jina lake halikutajwa, ameuawa kwa kupigwa risasi sehemu ya kichwani na mlinzi wa Kampuni ya New Bantu ambaye ni mlinzi wa Hoteli ya Green Leaf iliyopo maeneo ya Mtaa wa Mji, Kata ya Tungi katika Manispaa ya Morogoro.Kamanda Mutafungwa alisema mauaji hayo yametokea saa 9.15 usiku wa kuamkia Desemba 31, 2018 wakati mtu huyo akiwa na wenzake wawili wakiruka ukuta wa uzio wa jengo hilo kisha kuvunja na kuingia ndani ya stoo kupitia dirishani kujaribu kuiba jenereta aina ya Boss iliyohifadhiwa stoo. Kutokana na kitendo hicho, ndipo mlinzi huyo ambaye jina lake halikutajwa alifyatua risasi iliyompata kichwani huku wenzake wawili wakikimbia.Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na mlinzi anaendelea kuhojiwa. Wakati huo huo, basi lenye namba za usajili T 190 DGK aina ya Yutong mali ya Kampuni ya OTTA likiendeshwa na Jackson Kanza likitokea Dar es Salaam kwenda Bukoba limemgonga mwanamke mtembea kwa miguu asiyefahamika kwa jina anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50-55 na kusababisha kifo chake papo hapo. Kamanda Mutafungwa alisema ajali hiyo imetokea Desemba 30, 2018 saa 5.30 asubuhi Sokoine Shuleni katika Barabara Kuu ya Morogoro – Dodoma.
KITAIFA
MUFTI na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally ametangaza kuwa Sikukuu ya Idd El-Adh’haa itakuwa Agosti 12, mwaka huu. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu, Nuhu Mruma ilisema kuwa Shehe Zubeir ameutangazia umma kuwa Sikukuu ya Idd El-Adh’haa itafanyika Jumatatu Agosti 12, mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maadhimisho ya Sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika jijini Dar es Salaam na kuwa swala ya Idd kitaifa itaswaliwa katika Viwanja vya Masjid Kibadeni, eneo la Chanika Zogowali, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam na Baraza la Idd litafanyika hapo hapo mara baada ya Swala hiyo. Taarifa hiyo ilisema “kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania, Mufti na Shehe Mkuu Zubeir anawatakia Waislamu na wananchi wote sikukuu njema na anawaomba kusheherekea kwa salama na amani”.
KITAIFA
BIASHARA mipakani imezidi kushika kasi, baada ya Wizara ya Viwanda na Biashara kujenga vituo tisa vya biashara mipakani kati ya Tanzania na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) .Aidha, vikundi tisa vya wafanyabiashara wanawake wadogo na wa kati viliundwa; na wafanyabiashara wanawake 292 mpakani, wamerasimisha biashara zao katika halmashauri nane nchini. Hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda mjini Dodoma imeeleza kuwa Tanzania ina njia 48 za kupitisha bidhaa katika mipaka na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC), Zambia, Malawi na Msumbiji.Alisema vituo tisa mipakani ni Holili/Taveta, Sirari/Isebania (Tanzania na Kenya), Namanga (Tanzania na Kenya ), Kabanga/ Kobero (Tanzania na Burundi), Rusumo (Tanzania na Rwanda, Mtukula (Tanzania na Uganda), Horohoro/ Lungalunga (Tanzania na Kenya), Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia) na Kasumulu/ Songwe (Tanzania na Malawi).“Hali ya biashara mipakani inaendelea vizuri na serikali imeendelea kutumia itifaki za umoja wa forodha na itifaki ya soko la pamoja kurahisisha biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya huku nchi za Zambia, Malawi na Msumbiji biashara inasimamiwa kupitia itifaki ya biashara ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika,” alisema.Alisema katika kuchochea biashara rasmi, serikali inahamasisha na kuanzisha biashara rasmi kwa kuanzisha ujenzi wa masoko mipakani ili kukuza biashara na kusaidia kuboresha hali za maisha ya wakazi wa maeneo hayo. Kakunda alisema mikoa iliyotenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa masoko ni Kagera Mtukula, Murongo, Kabanga na Rusumo), Mara (Sirasi na Shirati), Mtwara (Kilambo na Mtambaswala), Ruvuma (Mbamba Bay na Mkenda), Kigoma (Kibirizi na Manyovu), Rukwa (Kirando, Kipuli, Kisanga na Kasesya).Maeneo mengine ni mkoa wa Mbeya (Tunduma na Kasumulu) na mikoa mingine ni Tanga (Horohoro), Kilimanjaro (Tarakea) na Arusha (Namanga) kuwezesha wafanyabiashara, magari na bidhaa kukaguliwa mara moja wakati wa kuingia na kutoka katika mpaka wa gharama na muda mfupi. Alisema wizara hiyo kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na shirika la biashara la kimataifa, iliratibu mradi wa kujenga na kuimarisha uwezo wa wanawake wanaofanya biashara isiyo rasmi katika wilaya zilizopo kwenye mipaka ya Tanzania na nchi jirani.Kakunda alisema biashara hizo zilirasimishwa katika wilaya nane za Buhigwe, Kasulu, Ngara, Misenyi, Tarime, Longido, Rombo na Mkinga na kuunganishwa na fursa za masoko katika jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zimekidhi matakwa ya hati ya uasili wa bidhaa.Alisema wizara inaendelea kusimamia utekelezaji wa utaratibu wa kurasimisha ufanyaji biashara mipakani kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo, ambapo mfanyabiashara mdogo mwenye bidhaa zisizozidi thamani ya dola za Marekani 2,000 hazihitajiki, kutumia cheti za uasili wa bidhaa na badala yake anatumia utaratibu rasmi wa Simplified Trade Regime.
KITAIFA
WAZIRI Mkuu, Kasssim Majaliwa ameagiza nyumba 1,500 zilizopo katika miradi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Shirika la Nyumba (NHC) pamoja na Watumishi Housing zilizopo Toangoma na Mtoni Kijichi zitolewe kwa vyuo vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam ili kuwawezesha wanafunzi kupata makazi ya gharama nafuu.Aidha, amewataka wakuu wa vyuo hivyo na wakurugenzi wa mashirika hayo kukutana pamoja ili kuona namna ya utekelezaji wa suala hilo linalolenga kuyafanya majengo hayo kutumika.Waziri Mkuu ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 45 ya Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambako pamoja na mambo mengine, amesema ofisi yake itatoa majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wizara mbali mbali kwa vyuo hivyo ili kutatua uhaba wa majengo unaovikabili.“Nimeshatoa maelekezo kwa wakuu wa mashirika hayo kuona namna bora ya matumizi ya majengo hayo ambayo mengi yamekamilika lakini hayatumiki, hatua hii naomba utekelezaji wake ufanyike haraka ili kuwapa fursa hiyo wanafunzi,” alisema Majaliwa na kuibua shangwe kutoka kwa wanafunzi.Pia alisema ili kuhakikisha wanafunzi watakaoishi katika nyumba hizo wanaondokana na adha ya usafiri, ameagiza wa wakuu wa wilaya zote za Dar es Salaam, kukutana na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) ili kupanga vizuri njia za usafiri kutoka Kigamboni, Tuangoma, Mtoni Kijichi hadi Feri ili kurahisisha usafiri kwa wanafunzi hao.Aidha, aliwataka wahitimu kwenda kuwa mfano bora katika jamii na kufanya kazi kwa bidii pindi watakapopata ajira, huku akitoa wito kwa vyuo kuhakikisha vinawafundisha wanafunzi mbinu bora za kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.Alisema Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani inakabiliwa na changamoto ya ajira ambayo katika kukabiliana na hali hiyo, serikali katika kipindi cha miaka minne imeongeza wigo wa utoaji ajira kutoka milioni 20 mwaka 2014 hadi milioni 22 mwaka jana.Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema uwepo wa IFM umekuwa msaada mkubwa kwa serikali kutokana na kuzalisha wataalamu mbali mbali wanaofanya kazi katika usimamizi wa kodi, bima na uhifadhi wa jamii na kuiomba serikali kuendelea kukisaidia chuo hicho ili kizidi kutimiza malengo yake.Aidha, alisema katika kuhakikisha chuo hicho kinatimiza malengo yake, serikali imekuwa ikikiachia fedha zote chuo hicho zinazotokana na ada ili kukiwezesha kijiendeshe katika maendeleo na kwamba ili kuonesha kuwa kina uwezo huo, hivi karibuni kilitoa gawio serikalini kiasi cha Sh bilioni mbili.Awali Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Profesa Thadeo Satta alisema tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972 kikiwa na wanafunzi 72, kimeendelea kupitia hatua mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi uliokiwezesha kufikisha wanafunzi 10,820 katika mwaka wa masomo 2019/2020.Alisema juhudi mbalimbali kutoka kwa wahadhiri wa chuo hicho umekuwa ukitoa matunda mazuri kwa wahitimu chuoni hapo huku akimueleza Waziri Mkuu mipango ya upanuzi wa chuo hicho katika Jiji la Dodoma na Simiyu.Jumla ya wahitimu 2,275 wametunukiwa tuzo zao katika kozi mbalimbali zikiwamo za usimamizi wa kodi, bima na majanga, benki na fedha, teknolojia na habari na zinginezo
KITAIFA
Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM MADAKTARI wa Hospitali ya Mercy, Sioux City nchini Marekani, juzi walifanikiwa kumaliza kumfanyia upasuaji mkubwa wa mti wa mgongo Doreen Mshana, ambaye ni majeruhi wa ajali iliyohusisha wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent, iliyopo Arusha. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye ni mmoja wa waasisi wa Taasisi ya Elimu na Afya (STEM), (Sioxland Tanzania Educational Medical Ministries), alisema Doreen, ambaye ni miongoni mwa majeruhi watatu, alifanyiwa upasuaji huo kwa muda wa saa nne badala ya tano zilizokuwa zimepangwa na madaktari. “Mtoto Doreen amemaliza kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo kwa ufanisi mkubwa kupita matarajio waliyojiwekea,” alisema Nyalandu. Alisema zoezi hilo, ambalo lilikuwa chini ya usimamizi wa madaktari sita, wakiwamo Dk. Meyer na Dk. Durward, ambao ni madaktari bingwa, lilipaswa kufanyika kwa muda wa saa 5:30, badala yake lilikamilika ndani ya saa nne. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kwa sasa Doreen ameshatolewa chumba cha upasuaji na kupelekwa katika chumba cha watu mahututi (ICU), huku madaktari wakieleza kuridhishwa na hali ya mtoto huyo. “Kwakuwa hali yake imeridhisha sana, baadaye leo (jana) watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya upasuaji na kumrudisha wodi ya watoto  ambako ataendelea na mapumziko,” alisema Nyalandu. Doreen na wenzake wawili, Saidia Ismail na Wilson Tarimo, wapo nchini Marekani kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali mbaya ya gari kwa msaada wa Shirika la STEMM.
AFYA
NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Tyga, amefunguka na kusema kwamba alikuwa tayari kufanya lolote kwa aliyekuwa mpenzi wake mwanamitindo, Kylie Jenner. Msanii huyo amedai ataendelea kumpenda kwa kuwa alimzoea, lakini kwa sasa atakuwa kama rafiki yake wa kawaida na anaweza kumsaidia kama atahitaji msaada wake. Akihojiwa na Big Boy TV, Tyga alisema Kylie alianza kubadilika tabia na alijaribu kumweka sawa lakini hali iliendelea kuwa hivyo japokuwa walikuwa wanaonekana wanapendana sana. “Uhusiano unaonekana kuwa bora nje ya nyumba lakini ndani kuna mambo mengi yanatokea ila ni siri kati ya wahusika wenyewe. Ni kweli nilikuwa naishi vizuri na Kylie lakini kuna baadhi ya mambo tulikuwa tunapishana, lakini nilikuwa tayari kumfanyia lolote katika maisha yake ila ndio hivyo tena kwa sasa hakuna la ziada kilichobaki ni kuwa marafiki wa kawaida,” alisema Tyga.
BURUDANI
Meneja bidhaa wa Vodacom, Fred Onesmo alisema hayo wakati akitambulisha maboresho yaliyofanywa na kampuni yake kwenye bidhaa za Vodacom pamoja na kutaja huduma mpya ya namba ya utambulisho (Code number) kwa wateja wa mtandao huo.Alisema, katika maboresho hayo wanawasogeza wateja karibu ili waendelee kutumia mtandao huo na kurahisisha shughuli zao kupitia Intaneti ya Vodacom na huduma ya M-Pesa.
UCHUMI
NA GEORGE KAYALA TAMASHA kubwa la kuibua waimbaji wa nyimbo za injili limepangwa kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, alisema tamasha hilo pia litatumika kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tamasha hilo litaanza Mwanza, kisha mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, lengo likiwa ni kupinga mauaji ya albino, lakini pia kuibua na kukuza vipaji vipya vya waimbaji wa nyimbo za injili,” alisema Fanuel. Katika tamasha hilo, waimbaji maarufu wa muziki wa injili wataongozwa na Flora Mbasha.
BURUDANI
SHULE ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salam imeongoza kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa wanafunzi wengi katika 10 bora kwa wasichana na wavulana na kupeleka wanafunzi wengi shule za vipaji maalumu.Hayo yalibainika jana wakati wa mchakato wa kuwapangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba ambao matokeo yake yalitangazwa Novemba mwaka huu na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kwenye matokeo hayo, shule hiyo imetoa wanafunzi saba kwenye 10 bora kwa upande wa wasichana Mkoa wa Dar es Salaam na wanafunzi watano katika 10 bora kwa upande wa wavulana.“Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa kwanza kitaifa na Tusiime kwenye wanafunzi 20 bora kwa upande wa wasichana na wavulana jumla ya inawanafunzi 12 hivyo ni dhahiri kwamba imesaidia sana kufanikisha ushindi huo wa Mkoa wa Dar es Salaam kitaifa na Wilaya ya Ilala,” alisema Mwalimu wa Taaluma, Makson Binomtonzi. Alisema shule ya Tusiime ilikuwa na watahiniwa 240 ambayo ni idadi kubwa kuliko shule zote na wote walipata alama A kwenye matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni na Necta.“Vile vile shule hii imeongoza Mkoa wa Dar kwa kutoa wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalumu nchini si jambo la bahati hili limewezekana kutokana na maandalizi ambayo huwa tunawapa wanafunzi wetu kwa kuwapa programu maalum ya masomo ya ziada,” alisema Binomtonzi. Alisema katika nafasi 28 zilizotengwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa wanafunzi na kwenda kwenye shule za vipaji maalumu, Tusiime imepeleka wanafunzi 16 kwenye shule hizo za vipaji maalumu na kati ya hao, watano ni wasichana na 11 ni wavulana.
KITAIFA
Nora Damian Na Aveline Kitomary -Dar es salaam WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewataka wahudumu wa afya kutokuwakimbia wagonjwa kwa hofu ya kuambukizwa magonjwa na badala yake wafuate kanuni na miongozo iliyopo katika kujikinga. Ummy alitoa rai hiyo jana wakati akipokea msaada wa vifaa vya kunawia mikono 100 vyenye ujazo wa lita 500 kutoka kwa Shirika lisilo la kiserikali la Water Mission Tanzania. Alisema kama mtaalamu wa afya atafuata mwongozo wa kuzuia maambukizi wa mwaka 2018  na mwongozo wa uzuiaji wa maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19), hataweza kupata maambukizi kutoka kwa mgonjwa.  “Wakati tunaendelea kukabiliana na janga la ugonjwa wa Covid-19, tukumbuke kuwa kuna magonjwa mengine kama ya moyo, kisukari, malaria, figo na ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na kifua kikuu.   “Hivyo basi mgonjwa wa aina hii akifika katika kituo cha kutolea huduma za afya anatakiwa kutibiwa na siyo kukimbiwa. “Baadhi ya wahudumu wakimpokea mgonjwa mwenye joto kali wanamkimbia kwa kudhani kuwa ana ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona.  “Mwongozo wa utoaji wa huduma za afya hauwataki kuwakimbia wagonjwa, jambo la muhimu ni kufuata miongozo iliyopo hii ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kuvaa barakoa na glovu wakati unamuhudumia mgonjwa,” alisema Ummy. Alishukuru msaada uliotolewa na Water Mission Tanzania na kuwataka wananchi kuzingatia maagizo wanayopewa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuvaa barakoa katika kukabiliana na ugonjwa wa corona. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov, alisema taasisi yake imetoa msaada huo wa vifaa ambavyo vitatumika katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Abubakar Khunenge, alisema watahakikisha vifaa hivyo vinatumika kama ilivyokusudiwa katika kupambana na maambukizi ya Covid-19. “Tutahakikisha vifaa hivi vinapelekwa katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyokusudiwa na vitawekwa katika mlango wa mbele wa kuingilia katika kituo husika,” alisema Khunenge. TAHARUKI AMANA Katika hatua nyingine, taharuki imezuka katika Hospitali ya Rufaa Amana iliyopo Manispaa ya Ilala baada ya baadhi ya wagonjwa wa corona waliokuwa wamelazwa kutaka kuondoka kwa madai wanajisikia vizuri.
AFYA
Uhusiano kati ya msanii Diamond Platnamz na Tanasha Donna ilisambaratika ghafla bila kutarajiwa, hii ni baada ya Tanasha mwenyewe kujitokeza wazi na kueleza kuwa uhusiano wao ulikuwa imara na kuwa hakuna lolote ambalo lingeweza kuusaambaratisha. Mwezi mmoja baadaye, wawili hao walipeana visigo na visigino. Huku wengi wakisalia na uvumu tu kuhusu kilichowakosanisha wawili hao, Diamond sasa amejitokeza wazi kutegua kitendawili. Akihojiwa katika Wasafi fm Jumatatu, Aprili 27, Mondi alieleza kuwa alikuwa na mpango wa kumfungisha pingu za maisha Donna kabla mambo yote kuenda mrama na kila mmoja kuenda zake. #GoodMorning "Misukumo ya kusaidia watu , imetokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia , napata Moyo wa kusaidia Wengine " – @diamondplatnumz . . Endelea kusikiliza 88.9 @wasafifm MUDA HUU mpaka saa 2:30 asubuhi na Kutazama @wasafitv, pia unaweza kufuatilia matangazo haya moja kwa moja kupitia Channel yetu ya YouTube #WasafiMedia #GoodMorning na @zembwela @rwenyagira salmadacotha @charles_william2 #HabariZaAsubuhi A post shared by DIAMOND PLATNUMZ 🦁 (@diamondplatnumzfamily) on Apr 26, 2020 at 10:23pm PDT Kulingana na msanii huyo, walitofautiana kuhusu baadhi ya masuala muhimu na ndiyo ikabidi watengane. ‘’ Siwezi kusema kiundani maana hata Tanasha hajajitokeza wazi kwa umma kueleza kuhusu chanzo cha kutegana kwetu. Kilichofanyika kilituzidi na ndiyo maana tukaamua kujipa nafasi. Hatukuachana maana nilikuwa na mpenzi wa kando. Nilikuwa mtiifu kabisa nilipokuwa katika uhusiano na Tanasha na nilikuwa tayari kumuoa. Ni ile tu hatukukubaliana kuhusu masuala mengine muhumi kama vile familia na maisha ya baadaye. Tulikuwa tukihitaji vitu tofauti na hakuna aliyekuwa tayari kulegeza msimamo. Tuliachana na Mungu akipenda tunaweza kurudiana,’’ Alisema Mondi. By @diamondplatnumz Nisikile Live kupitia GOOD MORNING ya 88.9 @wasafifm Muda Huu… waweza sikiliza na kutazama pia kupitia Channel yao ya youtube WASAFI MEDIA A post shared by DIAMOND PLATNUMZ 🦁 (@diamondplatnumzfamily) on Apr 26, 2020 at 10:19pm PDT Baba huyo wa wanne alikiri kuwa alikuwa na nia kubwa ya kumuoa Tanasha. ”Ukweli nilitaka kumuoa Tanasha 100% lakini hatukuwa katika ukurasa mmoja kwa baadhi ya vitu,’’ aliongezea. Tofauti na jinsi wengi walivyotarajia kuwa msanii huyu tayari amekwachua kipenzi mwengine baada ya kutengana na Donna, alikiri kuwa  hayuko katika uhusiano wowote wa kimapenzi. Mondi alieleza kuwa anaipa kazi kipaumbele  nakuamua kupigisha breki kidogo masuala ya mahusiano.
BURUDANI
Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR ZAIDI ya nyumba 70 zimeezuliwa mapaa kisiwani Unguja, Zanzibar baada ya kimbunga cha dakika 45 kutikisa. Kimbunga hicho ambacho kimeathiri zaidi wakazi wa maeneo ya Kinuni na Nyarugusu, Wilaya ya Magharibi Unguja, kiliwafanya wananchi hao kushindwa kufanya lolote kutokana na hali hiyo. Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa wakazi wa eneo la Nyarugusu, Mohamed Khamis Issa, alisema kuwa hatua ya nyumba zao kuezuliwa na kimbunga hicho imewaacha wasijue la kufanya. “Sijui tutaishi vipi leo, maana kwetu ni mtihani mkubwa, nyumba yangu pamoja na jirani zangu zote zimeezuliwa mapaa. Sijui kuna nini maana binafsi sijawahi kuona upepo mkali kama huu ambao sasa umesababisha athari kubwa kwetu. “Tunaomba mamlaka za Serikali zitusaidie kwa haraka maana sasa tupo kwenye hatari hata ya kuibiwa. Ewe Mwenyezi Mungu tupe heri na ustahamilivu waja wako,” alisema Issa. Kutokana na athari hiyo, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari. “Sisi Serikali tupo pamoja nao wananchi wote walioathiriwa na kimbunga hiki. Tutatoa kila aina ya msaada uliopo ndani ya Serikali. “Pia ninawapongeza wananchi waliopatwa na athari hizi kwa ushirikiano wa aina zote walioutoa kama ilivyotokea Pemba, ambapo pamoja na kusuguana katika siasa, lakini kwa tukio lililotokea la mafuriko wote walikuwa wamoja. Hakuna CCM wala CUF, wote walikuwa wamoja. “Naamini sote tukiendelea na mshikamano huu wa kuwa wamoja, ikiwemo kuwasaidia wenzetu waliopatwa na maafa, hakika nchi yetu itasonga mbele,” alisema.  Balozi Seif aliwapa pole viongozi wa Serikali wa eneo hilo kutokana na maafa hayo.
KITAIFA
Kufuatia sakata la usajili wa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu kuzidi kushika kasi kubwa katika klabu ya Yanga imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera amewashangaa viongozi ya klabu hiyo kwa kuanza majadiliano ya kumpa mkataba mpya mchezaji huyo. Ka mujibu wa vyanzo vya karibu na kocha Zahera, tangu wakati wa mchakato wake wa usajili kwenda TP Mazembe yeye alishamuondoa Ajibu kwenye mipango yake ya msimu ujao. Zahera ambaye kwa sasa yuko Hispania katika majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na fainali za AFCON 2019, ameshangaa sana kuona uongozi wa Yanga umeanza kumbembeleza nyota huyo asaini mkataba mpya. Zahera ameenda mbali na kusema ripoti yake aliyokabidhi kwa uongozi haina jina la Ajibu na anashangaa viongozi wanamtaka Ajibu yupi wakati ameshamuondoa kwenye mipango yake. Wakati huo huo Mshambuliaji wa klabu ya Zesco United ya Zambia, Lazarous Kambole amekubaliana maslahi binafsi na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika kusini ambayo atajiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao, imeelezwa. Taarifa zinadai kwamba Kaizer Chiefs italazimika kulipa dau la dola 200,000 ambazo ni zaidi ya milioni 459 za kitanzania kwa klabu ya Zesco kama ada ya usajili kwa mshambuliaji huyo. Ikumbweke Kambole aliwahi kutajwa kusajiliwa na mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Yanga ili kuboresha kikosi chao lakini dili hilo likafeli. Yanga waliingia kwenye rada za kumsajili mchezaji huyo lakini baadaye kukawa na ukimya ambao viongozi wenyewe walishindwa kuutolea ufafanuzi.
MICHEZO
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Oktoba mwaka jana, bao la Atupele Green lilitosha kuizima Simba nyumbani kwake.Lakini jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Ramadhani Singano na Ibrahim Ajib na kuiwezesha kufikisha pointi 35 baada ya mechi 21, ikiwa ni pointi moja nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC katika nafasi ya pili na pointi tano nyuma ya vinara, watani wao wa jadi, Yanga.Kwa Kagera Sugar, kipigo hicho kimewarudisha nyuma katika kuwania kushika nafasi mbili za juu kwani sasa inabaki na pointi zake 28 katika nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 21.Wekundu wa Msimbazi walipata bao la kwanza katika dakika ya 49 lililofungwa na Singano kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Kagera Sugar, Agaton Anthony, baada ya kipa kutema mpira wa Dan Sserunkuma.Iliwachukua dakika nane, Kagera Sugar ambayo inatumia Uwanja wa Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani baada ya ule wa Kaitaba mjini Bukoba kuwa katika matengenezo, kusawazisha bao hilo.Mshambuliaji wao hatari, Rashid Mandawa alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi ya Paulo Ngwai. Kwa bao hilo, Mandawa amefikisha mabao 10 akifungana na Didier Kavumbagu wa Azam FC. Simon Msuva anaongeza orodha ya wafungaji akiwa amefunga mabao 11 hadi sasa.Simba iliandika bao la pili katika dakika ya 68 lililofungwa kwa penalti na Ajib baada ya beki wa Kagera Sugar, Eric Kyaruzi kuunawa mpira katika eneo la hatari na mwamuzi Erick Anoka wa Arusha kuamuru adhabu kubwa.Katika kipindi cha kwanza, timu zote zilishambuliana kwa zamu na katika dakika ya 29, Dan Sserunkuma aliikosesha Simba bao baada ya shuti lake kugonga mwamba na kuokolewa na wachezaji wa Kagera Sugar.Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa pambano hilo, wachezaji wa Kagera Sugar walimzonga mwamuzi Anoka wakilalamikia maamuzi yake ikiwamo madai ya kunyimwa penalti katika dakika ya 85, baada ya beki na nahodha wa Simba, Isihaka Hassan kuunawa mpira katika eneo la hatari.Mwamuzi huyo alitolewa nje ya uwanja kwa kusindikizwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) zaidi ya 10 huku akiwa amefuatana na wasaidizi wake, lakini pia kipa wa Kagera, Anthony akiwa anaongea naye.Pambano hilo la jana awali lilipangwa kufanyika Jumamosi, lakini liliahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Shinyanga na kusababisha uwanja kujaa maji, wakati juzi pambano kati ya Stand United dhidi ya Mtibwa Sugar lilivunjwa katika dakika ya 37 baada ya mvua kubwa kunyesha wakati likiendelea kuchezwa.Hali hiyo ilisababisha mechi hiyo kurudiwa jana saa mbili asubuhi kwenye uwanja huo na Stand United iliendelea kutamba baada ya bao lake la juzi la dakika ya 14 lililofungwa na Haruna Chanongo, kushindwa kusawazishwa au kuongezwa jingine na wakata miwa hao wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.Kwa matokeo hayo, Stand United imefikisha pointi 24 na kuishusha Mtibwa Sugar hadi nafasi ya 12, kwa pointi zake 23. Timu sita za Coastal Union, Mbeya City, Ndanda FC, JKT Ruvu, Mgambo JKT na Stand United zina pointi 24 kila mmoja katika msimamo wa ligi hiyo iliyo na ushindani.Kagera Sugar iliwakilishwa na: Agathon Anthony, Salum Kanoni, Erick Murilo, Erick Kyaruzi, George Kavila, Maregesi Mwangwa, Juma Mkopi/Paul Ngwai, Babu Ally, Mandawa, Atupele Green na Benjamin Asukile/Adam Kingwande.Simba: Manyika Peter, Nassoro Masoud, Mohammed Hussein, Hassan Isihaha, Joseph Owino, Awadh Juma, Singano, Said Ndemla, Dan Sserunkuma/Issa Rashid, Emmanuel Okwi na Ajib/ Ibrahim Twaha.
MICHEZO
Chanzo cha picha, Getty Images Hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023, inayofanyika nchini Ivory Coast, imeibuka na matokeo yasiyotarajiwa na kushtukiza, na kurekebisha historia ya michuano hiyo. Vigogo wa soka barani kote wamejikuta wakipata kushindwa kwa kushtukiza, huku wapinzani wasiotarajiwa wakichukua nafasi hiyo katika tamasha kubwa sana. Mojawapo ya matukio ya kustaajabisha sana ilitokea wakati wenyeji, mbele ya mshambuliaji mashuhuri wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, walipopata kichapo cha 4-0 kutoka kwa Equatorial Guinea katika mchezo mzuri kwenye Uwanja wa Stade Olympique Alassane Ouatara mjini Abidjan. Visa kama hivyo vya matokeo yasiyotarajiwa vilijitokeza kwa nguli mwingine wa soka barani Afrika, Samuel Eto'o , ambaye timu yake ya Cameroon ilikabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa mabingwa watetezi, Senegal, kabla ya kushindwa kwa mabao 3-1. Mfungaji wa bao la rekodi ya Afcon, ambaye ni Rais wa shirikisho la Soka la Cameroon, FECAFOOT, alitazama timu yake ikipambana na nguvu ya kikosi cha Senegal katika onyesho kuu kwa mabingwa hao. Vinara wa kitamaduni wa soka kama vile Misri, wanaojivunia kuwa na rekodi ya kutwaa mataji saba ya Afcon, Ghana, Tunisia na Algeria tayari wamekumbwa na misukosuko kwenye michuano hii huku wanyonge wakionyesha umahiri wao na kuvuruga timu zenye nguvu katika soka la Afrika. Kutotabirika kwa mechi hizo kunaweza kuonekana huku timu kama Equatorial Guinea, Cape Verde na Angola zikiibuka kileleni mwa makundi yao bila kutarajiwa, na kukaidi matokeo na kuwaacha mashabiki na wadadisi wakishangaa. Hatua ya makundi ya Afcon 2023, iliyo na mshangao na misukosuko, imeweka mazingira mazuri ya awamu ya muondoano ya kusisimua, ambayo inaahidi nyakati zisizotabirika na vita vikali katika kutafuta bingwa wa bara hilo. Chanzo cha picha, Getty Images Emilio Nsue Lopez (Guinea ya Ikweta) Nahodha wa National Thunders ya Equatorial Guinea, ameibuka kinara katika hatua ya makundi, akifunga mabao matano katika mechi tatu tayari. Licha ya kuwa mlinzi wa klabu yake, mchezaji huyo wa zamani wa Middlesbrough na Birmingham City anaongoza safu ya ushambuliaji katika timu yake ya taifa. Akiwa na mabao matatu ya ajabu dhidi ya Guinea Bissau na mabao mawili dhidi ya wenyeji Ivory Coast, Nsue ni mshindani mkubwa wa tuzo ya Golden Boot Georges-Kevin N'koudou (Cameroon) Akiwa na msaada wa kufunga mabao mara tatu kwenye michuano hiyo, winga wa Cameroon, Nkoudou ni mmoja wa waliobadilisha mchezo kwenye Afcon 2023. Huenda Indomitable Lions walitatizika kupita hatua ya makundi, lakini kiungo huyo anayeishi Saudia hajashindwa kufanya vizuri wakati muhimu zaidi. Misaada yake mara mbili katika mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Gambia, uliokoa ushindi wa mabao 3-2 kwa Simba, ambao sasa wanatarajiwa kumenyana na wapinzani wanaowafahamu, Nigeria katika hatua ya 16 bora. Sadio Mane (Senegal) Wengi walidhani kwamba uhamisho wa pesa nyingi wa Sadio Mane kwenda klabu ya Saudia, Al-Nassr ungeweza kuashiria mdororo wa mchezo kwa winga huyo wa Senegal, lakini mwanasoka huyo bora wa mwaka wa Afrika mara mbili anadhihirisha wenye shaka kuwa sio sahihi nchini Ivory Coast. Akija kwenye dimba hilo, siku chache baada ya harusi yake, Mane amekuwa na ushawishi mkubwa katika utendaji bora wa mabingwa hao watetezi kwenye hatua ya makundi, akiwa na bao moja na asisti mbili. Achraf Hakimi (Morocco) Hakimi has been at the heart of the Atlas Lion's campaign at the Afcon so far. With one goal and an assist to his name, Hakimi has been involved in most of the goals scored by the pre-tournament favourites, creating attacking threats from the flanks and stepping up to set piece duties. Gelson Dala (Angola) Gelson Dala alifunga mabao mawili wakati Angola ilipoilaza Mauritania 3-2 katika moja ya mchezo wa kuburudisha sana Afcon 2023. Mchezaji huyo wa Angola amekuwa mzuri kwa kuiongoza nchi yake katika michuano hiyo kwa kasi yake ya kulipuka na ustadi wa kucheza chenga na kusababisha matatizo kwa wapinzani. Mshambulizi huyo wa Qatar anatarajiwa kuimarika katika kiwango chake kizuri kwa Palancas Negras katika hatua za mwisho za shindano hilo. Stanley Nwabali (Nigeria) Kuingia kwa Afcon mwaka huu, wasiwasi mkubwa wa Nigeria ulikuwa kuhusiana na nafasi ya golikipa huku mashabiki wakihoji uwezo wa makipa, Francis Uzoho na Maduka Okoye. Mchezaji wa Chippa United Stanley Nwabali aliingia pichani kwa ajili ya Nigeria usiku wa kuamkia mchuano huo na alicheza mechi yake ya kwanza tu katika kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa awali dhidi ya Guinea. Onyesho lake la hadi sasa kwenye dimba, hata hivyo imekuwa msaada mkubwa kwa safu ya ulinzi ya Super Eagles, kwa kutofungwa mara mbili katika mechi tatu. Kwa kutumia mtandao wetu, chagua timu yako unayoipenda ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutoka kwenye orodha yetu na uishirikishe marafiki zako. Chagua mbinu Michuano hiyo itajumuisha makundi sita ya timu nne (A-F) huku timu mbili za juu zikifuzu moja kwa moja hatua ya 16 ya mwondoano. Timu hizo 12 zitaunganishwa na timu nne zilizoshika nafasi ya tatu bora kutoka makundi sita, zikiwa na vigezo vinavyozingatia matokeo sambamba baina ya timu na pili tofauti ya mabao. Utafiti na Damilola Ojetunde, uliyofanyiwa kazi na Olaniyi Adebimpe na Umeandaliwa na Boaz Ochieng Chanzo cha picha, Getty Images Lamine Camara (Senegal) | 20 | Kiungo wa kati | Klabu ya sasa – Metz (France) Mwanasoka huyo bora chipukizi wa Afrika amejitangaza kwenye onyesho kubwa zaidi la soka barani Afrika kwa kufunga mabao mawili na kufanya vyema kwa mabingwa hao watetezi katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Gambia. Baada ya kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (Chan), Camara anaweza kuwakito cha thamani kwa dimba hilo huku vilabu vya juu vya Ligi ya Premia vikimtaka kinda huyo mwenye umri wa miaka 20. Jesus Owono (Equatorial Guinea) | 22 | Mlinda lango | Klabu ya sasa– Alaves (Spain) Golikipa huyo wa Equatorial Guinea amekuwa kipa bora zaidi kwenye michuano hiyo akiwa amecheza vyema dhidi ya Nigeria na Ivory Coast, jambo ambalo lilimwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi. Akiwa na umri wa miaka 22, anaweza kuwa kipa bora zaidi barani Afrika, akifuata njia ya magwiji kama Carlos Kameni, Vincent Enyeama na Thomas Nkomo, kama wafungaji bora kutoka bara. Mohammed Kudus (Ghana) | 23 | Kiungo wa kati | Klabu ya sasa – West Ham Huenda ikawa kampeni ya kutamausha kwa Black Stars ya Ghana kwenye Afcon 2023 lakini Mohammed Kudus wa West Ham, aliridhisha matarajio ya wengi licha ya kusumbuliwa na majeraha. Alikosa ushindi wa 1-2 dhidi ya Cape Verde katika mechi ya kwanza ya kundi la Ghana lakini akarejea kwa kufunga bao moja katika mchezo bora dhidi ya timu ya Mo Salah ya Misri. Alipata tena tuzo ya mchezaji bora wa mechi katika sare ya 2-2 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wao wa mwisho wa kundi, ambao ulihitimisha matumaini ya Ghana kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Emam Ashour (Egypt) | 25 | Kiungo wa kati | Klabu ya sasa - Al Ahly (Egypt) Kiungo wa Al Ahly, Emam Ashour amekuwa bora mpaka sasa -Misri, licha ya Farao kutinga hatua ya 16 bora Afcon 2023. Washindi hao ambao walimpoteza nahodha Mohammed Salah kutokana na majeraha katika mchezo wao wa pili wa kundi, wamefanikiwa kutinga hatua hiyo ya mtoano, baada ya Msumbiji kuharibu nafasi za Ghana. Ashour, ambaye anafananishwa na wengi na mchezaji wa zamani wa Misri, Ahmed Hassan, amekuwa mtu mzuri wa kati kwa Mafarao, akitoa msaada wa ulinzi na kulipuka kwa nguvu kwenye mashambulizi ya timu hiyo. Anahusishwa na uhamisho wa kwenda Uhispania, Barcelona msimu ujao wa joto Aboubakary Koita (Mauritania) | 25 | Mshambuliaji | Klabu ya sasa - Sint Truidense (Belgium) Bila shaka Mauritania ni moja ya timu za kushtukiza kwenye Afcon 2023 na mtu mmoja, anayeendesha ndoto ya timu kwenye mashindano hayo ni Aboubakary Koita. Miondoko yake ya kasi, uchezaji wa winga na jicho la kulenga lango kumeisaidia Al-Murabitun kutinga hatua ya 16 bora, waliyoipata kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa wa Afcon 2019, Algeria. Bila shaka Koita ndiye wa kuangaliwa katika hatua inayofuata ya shindano hilo. Aguibou Camara (Guinea) | 22 | Mshambuliaji wa pembeni |Klabu ya sasa - Atromitos (Greece) Camara alivutia wengi kwenye michuano ya Afcon inayoendelea baada ya kuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Gambia. Bao lake la dakika ya 69 lilitosha kuwapatia Waafrika Magharibi ushindi wa kwanza kwenye dimba hilo na Camara anaweza kuweka historia zaidi huku Syli Nationale wakijikatia tiketi ya kutinga hatua ya mtoano kama moja ya timu zilizo nafasi ya tatu bora. Imetafsiriwa na Yusuf Jumah
MICHEZO
Na Jacquiline Mrisho– MAELEZO. WASICHANA 3,738 wa mikoa ya Mara na Geita wanategemea kunufaika na mradi wa kuzuia ndoa za utotoni na ukeketaji unaofadhiliwa na Umoja wa   Ulaya (EU) na kuratibiwa na Shirika la Plan International kwa kushirikiana na mashirika ya CDF, NELICO  na Molly”s Network. Takwimu hizo zilitolewa  jana  na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Plan – Tanzania, Gwynneth Wong wakati wa uzinduzi wa mradi huo   katika ukumbi wa ofisi za Umoja wa Ulaya,  Dar es Salaam. Gwynneth alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikisaidiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha haki za wasichana zinalindwa na hakuna msichana atakayeachwa nyuma kwenye nyanja za maendeleo hali itakayopeleka wasichana kuwa na haki sawa na wavulana. “Tumeona kuna haja ya kuweka mradi mwingine utakaodumu kwa miaka mitatu, wa uzuiaji wa mimba za utotoni na ukeketaji kwa mikoa ya Mara na Geita. “Mikoa hiyo imeonekana kuongoza kwa matatizo hayo hivyo tunaushukuru Umoja wa Ulaya kwa kutoa Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya kuendeshea mradi huu,” alisema. Gwynneth. Alisema takwimu za mwaka 2016 za Utafiti wa Demographia na Afya zinaonyesha kuwa ndoa za utotoni mkoani Mara ni asilimia 55 na kwa Geita ni asilimia 37 na ukeketaji kwa Mkoa wa Mara ni asilimia 32 kwa asilimia za  taifa, hivyo ni lazima kuanza na maeneo yaliyoathirika zaidi. Balozi wa Umoja wa Ulaya, Roeland Van de Geer alisema umoja huo unatambua nafasi ya msichana katika jamii na nafasi ya baadhi ya mashirika yanayoshirikiana na Serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kuhakikisha haki sawa kwa wote. “Sisi tunatoa fedha lakini nyie ndiyo watendaji hivyo tunawashukuru sana, lakini pia tunatakiwa tutambue kuwa maendeleo ya kudumu hayawezi kupatikana kwa kuwaacha wanawake nyuma kwa maana hiyo tunatakiwa tufanye juhudi za kuhakikisha tunaenda pamoja,” alisema Balozi  Roeland Van de Geer.
KITAIFA
Matatizo hayo ni ya bei, mbegu kutoota vizuri na baadhi ya wanunuzi wa zao hilo, kujitoa mapema baada ya bei ya Soko la Dunia kuwa chini, tofauti na walivyokuwa wametarajia, hivyo kuona wataingia hasara.Hayo yalisemwa na Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), Joseph Mihangwa jana.Alisema malalamiko ya utumiaji mbegu ya pamba iliyotangazwa kwa wakulima wa zao hilo katika maeneo tofauti, yamekuwa ni kero.Hali hiyo imeonesha Wizara ya Kilimo kutofanya majaribio kwanza ya mbegu hizo, kabla hawajazitangaza kwa wakulima kuzitumia.“Huenda zao la pamba kwa mwakani likapungua na kuwa adimu,” alisema Mihangwa na kuongeza kuwa sababu nyingine ni mbegu kutokuota mara wazipandapo mashambani wakulima, bei ya ununuzi wa pamba pamoja na baadhi ya wanunuzi wa zao hilo kujitoa mapema baada ya kuona bei ya soko la dunia kuwa baya.“Sisi Chama Kikuu cha Ushirika ni wanunuzi wa zao hilo na tayari kwa mwaka huu tumenunua kilo milioni nane za zao la pamba, ambapo kitu kilichojitokeza baadhi ya wanunuzi wamejiondoa mapema kwa kutokubaliana na bei iliyopo kwenye Soko la Dunia kuwa wanapata hasara.“Halafu kuna suala la mbegu kutoota vizuri baada ya wakulima kutumia pesa nyingi kununulia mbegu na kuona fedha zinapotea bure na pia wanapoteza nguvu, huenda ikawa sababu ya kupungua kwa zao hilo mwakani,” alisema Mihangwa.Mihangwa alisema maeneo kama Wilaya za Itilima, Kishapu, Meatu na Bariadi na mkoa wa Geita, wakulima wameonekana kulalamikia mbegu hizo kutoota, hivyo hakuna budi kuilalamikia sekta ya kilimo kwa kutofanya majaribio na utafiti wa mbegu, ambapo kwa wakulima tayari wameingia hasara ya kupoteza fedha, nguvu na muda.Wengi wa wakulima katika kata za Mbita, Mwamapalala, Kinamweli, Lagangabilili na Nkoma Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wamelezea kuwa kwa sasa wameingia hasara kubwa baada ya kupanda mbegu hiyo takribani mwezi mmoja mpaka sasa mbegu hiyo imeshindwa kuota.Luhende Jisena na Ngassa Malimo, kwa niaba ya wakulima wenzao, walitoa malalamiko mbele ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo katika mikutano ya hadhara iliyokuwa ikifanyika kila kata wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi hao.
UCHUMI
KINSHASA, DR CONGO MWANAMUZIKI mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide, amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa nchini humo kutokana na tukio la kumpiga teke mwanamuziki wake walipowasili nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliopita. Olomide alifukuzwa nchini Kenya kutokana na kuenea kwa video ambayo ilimuonesha msanii huyo akiwa anampiga msanii wake wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Alipanga kutumbuiza mashabiki wake kwenye ukumbi wa Bomas nchini Kenya Jumamosi, lakini tamasha hilo liliahirishwa na msanii huyo kurudishwa nchini kwake ambapo jana alikamatwa na polisi. Hata hivyo, msanii huyo alitakiwa kwenda kutumbuiza mashabiki wake nchini Zambia, lakini kutokana na tukio hilo Shirika la Kilimo na Biashara la nchini Zambia, limefutilia mbali tamasha hilo ambalo lilitakiwa kufanyika Agosti mosi mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa facebook, Jumapili ya wiki iliopita, msanii huyo aliomba radhi mashabiki wake na hasa ‘wanawake na watoto’. “Najutia sana yaliyotokea, ilikuwa ni kipindi kifupi cha wendawazimu wangu, lakini ninaomba radhi kutokana na tukio hilo,” aliandika Koffi.
BURUDANI
Kwa maana hiyo timu hiyo sasa inarudi Mbande na itakuwa ikifanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kwa vile wenyewe (Azam) watakuwa Zanzibar.Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alisema mwanzoni mwa wiki iliyopita kwamba Twiga itaweka kambi Zanzibar ili kubadili mazingira.Hakuna kiongozi yeyote aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo la kukosekana kwa kambi, lakini habari za uhakika kutoka ndani ya TFF zinasema kuwa chanzo cha kambi hiyo kukwama ni kukosekana kwa uwanja wa kufanyia mazoezi.Aidha kocha wa timu hiyo Rogasian Kaijage alisema kukosa mechi za kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya All African Game kunawanyong’onyesha.Twiga Stars ina wiki tatu za kujiandaa dhidi ya michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Congo Brazzaville ambapo Kocha huyo alihitaji mechi za kimataifa kwa ajili ya kujipima kabla ya kuelekea huko.Akizungumza jana baada ya mazoezi yao ya Karume, Kaijage alisema walitamani kucheza mechi za kujipima ili kujua nafasi zao lakini ni gharama na timu haiwezi kumudu.“Hatuna jinsi, tutaendelea na mazoezi yetu na kucheza na timu za wanaume. Tulitaka mechi za kimataifa lakini hakuna pesa za kuwaleta,” alisema.Pia, alizungumzia ukata katika timu hiyo imesababisha timu kushindwa kupata baadhi ya vitu muhimu katika maandalizi yao.Kaijage ameomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo katika maandalizi yake ili kwenda kufanya vizuri katika michuano hiyo ya kimataifa.Kwa mujibu wa Kaijage, leo watahamishia kambi yao Mbande na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, kutokana na kuwa na mazingira tulivu kwa maandalizi yao.Alisema licha ya hali ngumu wanayokutana nayo, lengo lao ni kuhakikisha wanakwenda kushiriki na kushinda.
MICHEZO
NCHI za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeonesha ukuaji mzuri wa kiuchumi, uliojengwa kwa misingi ya uchumi wa viwanda. Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.2.Hayo yameainishwa katika Ripoti ya Uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki mwaka 2018, iliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), ikiangazia maendeleo ya uchumi mwaka 2017.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rwanda ni ya pili kwa ukuaji mzuri wa uchumi ikiwa na wastani wa asilimia 6.2. Ripoti hiyo imeonesha kuwa Kenya na Uganda zimefungana zote zikiwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.1 huku Burundi ikiwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia 2.0.Ukuaji wa uchumi katika nchi hizo umeenda sambamba na ukuaji wa viwanda kutokana na nia ya nchi hizo kujenga uchumi wa viwanda. Ripoti hiyo imeonesha kuwa Tanzania imefanya vizuri katika juhudi za kujenga viwanda.Mpaka kufikia mwishoni mwa 2017 Tanzania ilikuwa na maendeleo ya viwanda asilimia 8.9 huku Rwanda ikiongoza kwa asilimia 9 ya maendeleo ya viwanda nchini humo. Uganda imefuatia ikiwa na asilimia 5.5, Kenya 4.8 huku Burundi ikiwa na asilimia 1.5.Je, viwanda hivyo vimechangia kwa kiwango gani katika ukuaji wa Pato la Taifa (GDP)? Ripoti hiyo imeonesha kuwa Tanzania imefaidika zaidi na ukuaji huo wa viwanda vyake kwa kuwa vimechangia kwa asilimia 2.1 katika ukuaji wa pato la taifa. Ingawa Rwanda imeongoza kwa kuwa na maendeleo mazuri katika sekta ya viwanda, lakini imeshika nafasi ya pili katika kuvifanya viwanda hivyo kuwa na faida katika uchumi wa nchi na pato la taifa kwa ujumla.Ripoti hiyo imeonesha kuwa Rwanda imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na asilimia 1.6 ya mchango wa sekta ya viwanda katika ukuaji wa pato la taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla. Uganda imeshika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 1.5 huku Kenya ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na mchango wa asilimia 1.1 wa viwanda katika ukuaji wa pato la taifa na Burundi ikiwa na asilimia 0.3. Ripoti hiyo imeonesha kuwa sekta ya kilimo na viwanda ndio mihimili mikubwa ya ukuaji wa uchumi katika nchi hizo.Kilimo kimekua kwa asilimia 5 na kuwa na athari chanya katika ukuaji wa uchumi katika mataifa yote ya Afrika Mashariki. Kwa upande wa viwanda Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshuhudia ukuaji wa viwanda kwa asilimia 10.5 katika kanda nzima. Ukuaji huu umesababisha sekta hiyo kuwa namba mbili katika kuchangia ukuaji wa uchumi ikiiacha sekta ya madini katika nafasi ya tatu.Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas alipozungumza na vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni alisema Tanzania imekuwa na ukuaji wa uchumi wa kasi inayokubalika duniani na kuongeza kuwa kilichochangia ukuaji huo ni ujenzi wa uchumi wa viwanda.Dk Abbas alikuwa akizungumzia mambo makubwa 10 ambayo yametekelezwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani.Mbali na ukuaji mzuri wa kiuchumi ambao Tanzania inajivunia, taifa hilo kubwa kuliko yote Afrika Mashariki pia limekuwa la kwanza katika kipengele cha uchumi shirikishi katika nchi za Kusini mwa Afrika.Uchumi shirikishi ni ukuaji wa uchumi unaoshirikisha wananchi. Aidha, Dk Abbas alisema Tanzania imefanya vizuri kiuchumi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kati ya nchi zote za kanda hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya nne katika ukuaji mzuri wa uchumi.
KITAIFA
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM TIMU ya Yanga inatarajia kucheza na JKT Ruvu kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Jumatano ikitarajiwa kuwafuata wapinzani wao timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius, kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm, amesema maandalizi yao yapo vizuri na yanatosha kuiwezesha kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao hao Jumamosi katika Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe. Yanga ambao wapo kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 40, watakuwa wanahitaji ushindi dhidi ya JKT Ruvu ili iweze kujiweka vizuri katika msimamo wa ligi hiyo kabla ya kuelekea Mauritius. Mbali na Yanga, michezo mingine ya ligi hiyo itakayoendelea kesho ni Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya wakati Ndanda FC watawakaribisha Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Leo kutakuwa na mchezo mmoja katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kati ya wenyeji African Sports dhidi ya Stand United ya Shinyanga. Katika mwendelezo wa ligi hiyo kesho, Kagera Sugar watacheza dhidi ya Simba SC katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Azam FC watawakaribisha Mwadui FC katika Uwanja wa Chamazi, Majimaji dhidi ya Mgambo Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Toto Africans watawakaribisha Coastal Union katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
MICHEZO
WANAWAKE wanane wa Kitanzania na wengine 16 kutoka nje ya nchi, wameokolewa kufanya biashara ya ukahaba, baada ya kudanganywa kuwa wanapelekwa nje ya nchi kwa lengo la kupatiwa kazi nzuri.Aidha, kati ya wanawake hao wanane wa Kitanzania, wawili wanawasili leo saa saba mchana wakitokea Thailand, ambako walikuwa wakifanyishwa kazi hiyo ya ukahaba. Kamishna Msaidizi Magereza aliyeko katika Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji wa Haramu wa Binadamu, Ahmed Mwendadi alisema hayo jana kwenye mafunzo ya majaji kuhusu masuala ya kupambana na usafirishaji huo haramu wa binadamu jijini Dar es Salaam.Mwendadi alisema wanawake hao wanane wa Kitanzania kati ya hao wanne walitolewa nchini India na wanne nchini Thailand, ambapo kati ya hao wanne, wawili wanafika leo mchana saa saba. “Wanaotoka nje kuja Tanzania tumewahi kuokoa wanawake 12 kutoka nchini Burundi waliokuwa wanapita kwenda Uarabuni pamoja na Wanyarwanda wanne ambao walikutwa mkoani Singida wakifanyishwa kazi za nyumbani,” alisema Mwen-dadi.Alisisitiza kuwa Sekretarieti hiyo ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, imebaini kuwa wanawake wengi wamekuwa wakisafirishwa nje ya nchi ya Tanzania kwa ajili ya kufanyishwa kazi ya ukahaba katika nchi za India, Thailand, Malasia pamoja na Indonesia. Aliitaja mikoa inayoongoza kwa usafirishaji wa biashara hiyo ya binadamu kuwapeleka nje ya nchi kuwa ni Dar es Salaam, Tanga, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma hususan katika wilaya ya Kondoa.“Hatua tunazochukua ni kufanya utafiti ili kubaini hayo, ikiwa ni pamoja na kutoa uelewa kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria pamoja na mbinu za kuwagundua wahanga. Pili kutoa elimu kwa umma,” alisema. Alisema wanatarajia kuanza kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kutoa elimu, ikiwamo jitihada kubwa ya serikali kuzuia pasipoti za makundi, lengo likiwa ni kuzuia watu wasiingie katika biashara haramu.Alisema serikali pia imechukua hatua ya kunyang’anya leseni kampuni zote zilizosajiliwa kutafutia kazi Watanzania nje ya nchi. Alisema nchini mpaka sasa kesi 23 za biashara hiyo haramu, zinaendelea mahakamani na kesi saba zimeshatolewa hukumu. Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Adatus Magere alisema takwimu halisi za matukio hayo mpaka sasa hawana japo tatizo hilo lipo.“Hili ni tatizo kubwa hapa nchini kwa sababu uhalisia unapoajiri binti kutoka kule Iringa kuja Dar es Salaam kwa tafsini ni usafirishaji wa binadamu kwani ujira unaomlipa wa kazi na pesa unayolipa hailingani na kazi anazozifanya,” alisema Magere. Alisema biashara hiyo ipo katika maeneo mawili nchini; watoto wadogo wanatolewa mikoani kuletwa katika miji mikubwa kwa ajili ya kutumikishwa katika kazi, wengi wao hawaelezwi ukweli wanakwenda kufanya nini matokeo yake wanaishia kwenye ukahaba.“Wale ambao wanasafirishwa ni waathirika wanapochukuliwa wanapewa hadhi ambayo si kweli. Wakishachukuliwa na kwenda Uarabuni, Pakistan, India, China matokeo yake wanaishia kutumika katika Danguro,” alisema. Alisema wadau wakubwa wa jambo hilo ni polisi, magereza, ustawi wa jamii, uhamiaji na majaji kwani wana mpango kazi unaoshirikisha wadau wengi katika kupambana na biashara hiyo.Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya Temeke, Karim Mushi alisema mafunzo wanayoyapata yana mchango mkubwa yatawasaidia, kwani biashara haramu inahitaji uelewa mkubwa kwa wahusika wote.Akimwakilisha Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, Jaji wa Kanda ya Mashariki Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, Beatrice Mutungi alipongeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Kitengo cha Usafirishaji Haramu wa Biashara ya Binadamu kwa kutoa elimu kwa wasimamizi wa sheria ili kuwaongezea elimu na maarifa zaidi wa kufanya kazi kwa ufanisi.
KITAIFA
“Nilianza maandalizi dhidi ya mechi ya Stand United siku ya Jumapili na kesho nategemea tutasafiri kuelekea Shinyanga kwaajili ya mechi,” alisema Glawogger.Kocha huyo raia wa Austria mpaka sasa amekinoa kikosi cha Toto African kwa mechi moja dhidi ya Tanzania Prison siku ya Jumamosi na aliweza baada ya timu yake kuchapwa 1-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba.Kwa upande wake wa kocha wa Stand United, Mfaransa Patrick Liewig alisema kuwa, ushindi alioupata dhidi ya Kagera Sugar umeweza kuamsha ari ya wachezaji wake.Liewig ameahidi kupambana kwa hali na mali na kuhakikisha kuwa mwisho wa msimu timu yake inamaliza ndani ya sita bora.Stand United ipo katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 25 huku Toto Africans ipo nafasi ya nane baada ya kujikusanyia pointi 17.Katika mechi zingine; Ndanda FC itacheza na Mbeya City katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.JKT Ruvu itacheza na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Mgambo Shooting na Azam FC, African Sports itacheza na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani na Yanga itacheza na Maji Maji ya Songea.
MICHEZO
JUMLA ya watoto 2,345 wenye umri chini ya miaka mitano wamepatiwa chanjo ya Surua Rubella katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida kati ya Januari na Machi, mwaka huu.Mratibu wa chanjo katika halmashauri hiyo, Emmanuel Mawa alieleza kuwa idadi hiyo ya watoto waliochanjwa ni sawa na asilimia 89 ya malengo ya kuwapatia huduma hiyo watoto 2,648. Aidha, alieleza kuwa katika kipindi hicho halmashauri ililenga kufikia jumla ya watoto 2,648 kwenye chanjo ya Penta, lakini walifanikiwa kuwachanja watoto 2,571 ambayo ni sawa na asilimia 97.Alifafanua kuwa licha ya mafanikio hayo, bado kuna baadhi ya wazazi na walezi kutojitokeza kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo za aina mbalimbali, hali inayosababisha malengo yanayowekwa na halmashauri kwenye utoaji wa huduma hiyo, kutofikiwa kwa asilimia 100. “Kwa mfano, chanjo ya Surua Rubella tumefikia asilimia 97.Mtu anaweza kudhani kuwa idadi ya asilimia tatu iliyosalia ni ndogo lakini kwa malengo tuliyojiwekea ya kufikia watoto 2,648 na kuchanja 2,345 tu, hapo ni kuzungumzia watoto zaidi ya 300 ambao hawakupata huduma hiyo,” alisema.Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kuhusu kutofikiwa malengo ya chanjo katika halmashari hiyo, umebaini kuwa moja ya sababu ni imani potofu juu ya chanjo zitolewazo na serikali; dhana ambayo imeenea maeneo mengi ya mkoa huo. Imebainika kuwa baadhi ya wazazi na walezi wanaamini kuwa chanjo kwa watoto huathiri mfumo wa uzazi kwa kundi hilo na kwamba mara baada ya kupatiwa huduma hiyo mtoto huwa tasa au mgumba kwa maisha yake yote.Uchunguzi huo unaonesha kuwa licha ya serikali kuhakikisha inatimiza wajibu wake katika kutoa huduma ya afya kwa watoto wote kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 na kutumia gharama kubwa ili kundi hilo lipate huduma hiyo bila malipo, baadhi ya wazazi hasa wa maeneo ya vijijini bado wanakwamisha juhudi hizo kutokana na imani potofu.Akizindua kampeni ya chanjo katika kituo cha afya Sokoine Manispaa ya Singida, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskasi Muragili alikemea imani hizo potofu, akisema chanjo zinazotolewa zimefanyiwa utafiti wa kitaalamu na kuonekana kuwa hazina madhara yoyote kwa mtoto. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa watoto wachanga milioni 22 hawapati chanjo inayostahili, ambapo zaidi ya milioni 1.5 walio na umri chini ya miaka tano hufariki dunia kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiwa kupitia chanjo, huku wataalamu wakisema chanjo ina tiba ya kuaminika na kwamba inaweza kuzuia vifo kati ya milioni mbili na milioni tatu kila mwaka.
KITAIFA
Na PATRICIA KIMELEMETA – Dar es Salaam BAADA ya kuwapo kwa mjadala wa muda mrefu wa Tanzania kuibiwa dhahabu kutokana na mchanga wake kusafirishwa nje ya nchi, leo ukweli unatarajiwa kujulikana wakati kamati iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli itakapokabidhi ripoti yake. Machi 29, mwaka huu, Rais Magufuli aliunda kamati yenye watu wanane, ambayo ilipewa jukumu la kuchunguza na kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali nchini. Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Profesa Abdulkarim Mruma na wajumbe wake ni Profesa Justianian Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk. Yusuf Ngenya, Dk. Joseph Philip, Dk. Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery Gombela. Kamati hiyo iliundwa ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu Rais Magufuli kutangaza kuzuia usafirishaji wa mchanga wa dhahabu kuanzia Machi 2, mwaka huu, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kukuta makontena 20 ya mchanga huo yakitaka kusafirishwa nje ya nchi. “Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu,” alisema Rais Magufuli. Jana Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, alitoa taarifa kwa umma ikisema kamati iliyoundwa kuchunguza mchanga huo, itamkabidhi Rais Magufuli ripoti yake leo kuanzia saa 3:30 asubuhi.  “Kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga yaliyokamatwa bandarini, itawasilisha ripoti yake leo kwa Rais,” alisema Msigwa. Awali mara baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku mchanga kusafirishwa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitembelea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi mjini Kahama, na kuchukua sampuli ya mchanga wa dhahabu kuupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili aupime na kuona kuna aina ngapi na kiasi gani cha madini kinachopatikana. Pia Machi 28, Rais Magufuli alimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini mianya yote inayosababisha nchi kukosa mapato makubwa, hususani katika misamaha ya kodi, mikataba na ulipaji wa kodi. “Haiwezekani Watanzania wanakosa dawa hospitali wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa maji wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa umeme wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa barabara wakati dhahabu zao zinaondoka, nataka ukakague kwa kina hii sekta ya madini ili Watanzania wajue chao nini na kama kinapatikana sawasawa?” alisema Rais Magufuli. Itakumbukwa kuwa mara baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga huo nje ya nchi, baadhi ya watu walitoa mawazo kinzani juu ya hatua hiyo, huku wengine wakiunga mkono. Mmoja wa watu waliotoa maoni ni Mbunge wa Igunga na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Viwanda na Biashara, Dk. Dalali Kafumu, ambaye alisema suala la kuhakikisha Tanzania inachenjua madini yote nchini ni sahihi kwani ni la kisera. “Sera ya madini ya mwaka 2009 niliyosimamia utengenezaji wake, kifungu 5.11; policy statement no. 3 inasema hivi: (iii) The Government will collaborate with the private sector, regional and international organizations to strategically invest in smelting and refining.  “Kwahiyo mchakato wa kuchenjua mchanga hapa nchini ni matakwa ya kisera, lakini shida inakuja tu pale ambapo shughuli hii inaanzishwa kwa haraka na dharura kubwa. Hali hiyo inaweza kuleta uhusiano usio sawa na makampuni ya kimataifa na hata nchi makampuni yanakotoka,” alisema.
KITAIFA
MADRID, HISPANIA  WABABE wa soka nchini Hispania Barcelona na Real Madrid, wanaendelea kupigana vikumbo kwa ajili ya kuwania saini ya mshambuliaji wa PSG, Neymar kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu nchini Hispania wiki ijayo. Ligi ya Hispania inatarajia kuanza kutimua vumbi Ijumaa ya wiki ijayo, huku uhamisho wa Neymar ukisubiliwa kwa hamu kubwa nchini humo. Nyota huyo raia wa nchini Brazil, amethibitisha anataka kuondoka katika klabu hiyo ya PSG katika kipindi hiki cha majira ya joto ambapo dirisha la usajili nchin Hispania bado lipo wazi hadi Septamba 2 mwaka huu. Neymar ambaye aliwahi kuitumikia Barcelona kwa mafanikio makubwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2017, aliweka rekodi ya uhamisho wake kwa kitita cha pauni milioni 198, lakini sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameonesha dalili za kutaka kurudi katika klabu hiyo ya zamani, lakini Madrid na wao wanataka kuonesha jeuri ya fedha kumsajili mchezaji huyo. Madrid wamedai wapo tayari kuvunja benki yao kumsajili mchezaji huyo baada ya kushindwa kuipata saini ya kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba ambapo dirisha la usajili la Uingereza likifungwa juzi. Sababu za Manchester United kugoma kumuuza Pogba kwa Real Madrid ni kutokana na kukosa mbadala wake katika kipindi hiki cha kiangazi. Matajiri wa soka nchini Ufaransa, PSG wameripotiwa kuwa tayari kumuacha Neymar akiondoka kwenye kikosi chao kwa uhamisho wa pauni milioni 110 pamoja na wapewe mchezaji mmoja. Kwa upande wa Barcelona waliwataja miongoni mwa wachezaji wao sita ili waweze kumchagua mmoja pamoja na kupewa fedha ili waweze kumrudisha Neymar kikosini, lakini PSG wanaonekana kuhitaji fedha zaidi kuliko mchezaji. Uongozi wa PSG, unadaiwa kuchoshwa na tabia za mchezaji huyo alizozionesha katika msimu uliopita.
MICHEZO
NAIROBI, KENYA WIZARA ya Nishati nchini Kenya, imepiga marufuku uingizaji gesi ya kupikia kutoka Tanzania. Uamuzi unatarajiwa kuibua uhaba wa nishati hiyo na kusababisha bei kupanda. Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Andrew Kamau, mwanzoni mwa wiki hii, alisema wafanyabiashara hawataruhusiwa kuingiza gesi kupitia mipaka ya ardhini ndani ya wiki moja kuanzia siku hiyo. Alisema kuwa hatua hiyo imelenga kuondoa mitambo haramu ya gesi za kupikia, ambayo imesambaa sehemu mbalimbali nchini humo na kuhatarisha usalama. “Waziri ameandika barua kwenda Tume ya Usimamizi wa Nishati, Forodha na Shirika la Viwango Kenya, ikizitaarifu kuwa Mombasa ni kituo pekee cha kuingiza gesi ya kupikia. “Iwapo unataka kushiriki biashara hii, njoo uwekeze Kenya, ingiza kupitia Mombasa, kisha hilo litatuwezesha kuwabaini wale wanaowasambazia wafanyabiashara wasio na vibali. “Lakini sasa suala zima kuhusu Tanzania, ni suala lisilo na nafasi tena,” Kamau aliuambia mkutano wa Kampuni za Masoko ya Mafuta (OMCs), ulioandaliwa na Kampuni ya Mabomba ya Kenya. Waziri Kamau, baadaye alithibitisha kwamba utekelezaji wa suala hilo utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu. OMCs, zimekuwa zikilalamika kukwamishwa biashara zao na wafanyabiashara haramu wa gesi, ambao huchukua mitungi yao, kuijaza kisha kuirudisha sokoni. Marufuku hiyo, inatarajia kuwaacha njia panda wafanyabiashara wa gesi inayotokea Tanzania, maana wengi wao wamekana kufahamu uwapo wa mpango huo. Chama cha Wafanyabiashara wa Nishati, kilisema bado hakijapokea taarifa ya marufuku hiyo.
KIMATAIFA
Mwandishi Wetu -Dodoma MRADI wa kuendeleza zao la mtama nchini wa kampuni ya Bia ya TBL Plc, unaendelea kunufaisha wakulima wa zao hilo mkoani Dodoma, ambapo wanapatiwa mbegu za kisasa, mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kinachofanikisha kuongezeka kwa mavuno pia wanakuwa na uhakika wa kuuza mavuno yao kwa kampuni hiyo. Akizungumza n kwa niaba ya wakulima wenzake katika mahojiano yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, Issa Dinya,  alisema kutokana na mradi huo wameanza kulima zao la mtama kibiashara kwa kuwa wana uhakika wa soko tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walilima zao jilo kwa ajili ya matumizi ya chakula. Kupitia mradi huo wa majaribio unaoendeshwa kwa ushirikiano wa TBL Plc, WFP na FtMAumenufaisha zaidi ya wakulima wadogo 2,000 ambao mavuno yao yaameongezeka kwa asilimia 77 na maisha yao kuwa bora, mkakati wa kampuni ni kuinua wakulima wadogo kupitia kununua mazao yao kwa bei nzuri kwa ajili ya malighafi za kuzalisha biadhaa zake. Mradi huo wa ushirikiano ulianza mwezi Januari Mwaka 2020 ambapo TBL Plc, Ilikubaliana na wakulima kununua zao lao la mtama mkoani Dodoma na Manyara, ambapo taasisi za WFP na FtMA zimewezesha wakulima kupata mbegu za mtama, bima, ushauri wa kilimo cha kitaalamu na uhakika wa masoko. Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman, alisema anafurahia kuona mafanikio ya mradi huo wa mtama kwa kuwa umeenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuboresha kilimo cha mtama nchini Tanzania na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuendelea kuwa na kipato cha uhakika kuanzia sasa na katika siku za mbele.  “Mkakati wetu wa kununua malighafi ni mkakati wetu mojawapo wa kuchangia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi,” alisema Redman. Akiongea katika moja ya mikutano ya uhamasishaji wa kilimo cha mtama mkoani Dodoma karibuni, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa, Mustapha Yusuf, aliipongeza TBL kwa mkakati wake wa kununua malighafi kutoka kwa wakulima nchini. “Mkakati huu kwa kiasi kikubwa umeleta hamasa kwa wakulima kuzalisha zao la mtama kibiashara nchini na utawanufaisha kwa kuboresha maisha yao sambamba na kupata mbegu bora ambazo zinafanikisha kuzalisha mtama wenye kiwango kizuri na mavuno yao kuongezeka,” alisema
UCHUMI
 MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema chama hicho hakijamfukuza uanachama Diwani wa Ubungo ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob na wala hakijawahi kujadili suala lolote kuhusu yeye.  Mnyika alitoa kauli hiyo jana, siku moja baada ya kusambaa barua iliyodaiwa kuandikwa na mtu aliyejitambulisha kama Katibu Kata ya Ubungo, Asheri Mlagwa ambaye hata hivyo amekanusha kuhusuia na barua hiyo.  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mnyika alisema alishamwandikia barua Mkurugenzi wa Maniapaa ya Ubungo, kumtaka afute barua yake aliyoandika na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, ambayo inaonesha uongozi wa Chadema pia umepewa nakala japokuwa bado hawajakabidhiwa nakala hiyo.  “Chama kinamtambua Jacob kama mwanachama, diwani na Meya wa Manispaa ya Ubungo. Pamoja na barua hii tumemtaka afute barua yake kwani utaratibu wa hatua za kinidhamu upo wazi kwa mujibu wa Katiba.  “Mstahiki Meya pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na nimemweleza Mkurugenzi kwa mujibu wa Katiba ya chama chetu Ibara ya Sita kifungu cha Saba inaeleza wazi hatua za kinidhamu kwa mwanachama mwenye nafasi.  “Kiongozi wa kitaifa isipokuwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti , mamlaka yao ya nidhamu itakuwa ni Kamati Kuu ya chama Mstahiki Meya kwa kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama na mmoja wa madiwani ni mjumbe wa Kamati Kuu ya chama.   “ Lakini kwa barua hii tumemweleza vilevile Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kwamba taratibu hata kama mstahiki Meya asingekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa nafasi yake tu ya umeya, utaratibu wa kinidhamu unaongozwa na muongozo wa chama ambapo chama kina muongozo wa kusimamia wabunge, halmashauri wakiwamo madiwani na viongozi wa vijiji na mitaa na katika mwongozo huu sehemu E inahusu hatua za kinidhamu kwa wabunge na mameya.  “Ambapo kwa hatua za kinidhamu za mameya ni tofauti na hatua za kinidhamu za madiwani wa kawaida, mameya hatua zao za kinidhamu zimeelezwa katika kipengele cha pili I: Kinasema kama kwa mfano maana hadi sasa hatujapokea malalamiko yoyote juu ya mstahiki Meya Jacob na hata kama kungekuwa na malalamiko juu ya utovu wa nidhamu au tatizo lolote inapaswa yafikishwe kwa Katibu Mkuu kwa maandishi ili yafikishwe kwenye kamati ya maadili ya taifa,” alisema Mnyika .  Alisema kwa hiyo kwa mwongozo huo hata kama asingekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema kwa nafasi yake tu ya umeya masuala yake hayawezi kushughulikiwa na ngazi ya kata wala wilaya au ngazi ya kanda, bali yanapaswa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu.  “Mimi kama Katibu Mkuu wa chama sijapokea malalamiko yoyote kuhusiana na mstahiki meya wa manispaa ya Ubungo. Baada ya kupata hizi taarifa kwenye mitandao ya kijamii pia tulifanya ufuatiliaji ili kuona pamoja na kuwa je kuna kitu chochote kimetokea kwenye ngazi za chini za chama?  “Na nimebaini kwamba kinachotajwa   kwenye barua ya mkurugenzi kuwa eti kuna kikao kimekaa cha kamati ya utendaji ni jambo ambalo si la kweli na hakuna kikao chochote cha kamati kilichokaa cha Kamati ya Utendaji ya Kata kuhusu kujadili hatua za kinidhamu za mstahiki meya na tumethibitisha kwamba ambaye anaelezwa kuwa amesaini barua, Asheri Mlagwa si Katibu wa Chadema wa Kata ya Ubunge ila Katibu wa Chadema wa Kata anaitwa Ezekiel Miraji,” alisema.  KAULI YA JACOB  Akizungumza muda mfupi baada ya kusambaa kwa barua hiyo ya kufukuzwa kwake uanachama ambayo hata hivyo ilidaiwa baadaye kuwa ni ya kughushi, diwani huyo wa Ubungo, Boniface Jacob alikanusha taarifa na barua hiyo akiwa na Asheri Mlagwa akieleza kuwa hakuhusika kwa kuwa tayari alishaondoka katika uongozi wa kata hiyo.  Jacob alisema ameshtushwa na barua hiyo ambayo bado chanzo chake hakijajulikana na kwamba yeye bado ni mwana Chadema na hakuna kikao chochote cha chama kilichokaa hata kumjadili tu.  Alisema kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Meya anafukuzwa na Kamati Kuu na Diwani anafukuzwa na uongozi wa Kanda lakini kwa kuthibitishwa na Kamati Kuu. Alisema kwa mujibu wa Katiba hatua za kumfukuza Diwani au Mbunge hazihusiani moja kwa moja na uongozi wa kata, japokuwa unaweza kutoa mapendekezo ambayo yanapelekwa kwenye Kanda na kwenye Kamati Kuu.  “Tunaendelea kuwasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ambaye alipokea barua hiyo ili atoe mwanga kuhusu wahusika waliopeleka barua hiyo ofisini kwake ili hatua za kisheria zichukuliwe, kwa kuwa wameghushi na pia wamefanya hivy kujaribu kunichafulia jina langu,” alisema.  Kwa upande wake, Asheri Mlagwa ambaye jina lake lilitumika kuonyesha kuwa yeye ndiye Katibu wa Chadema Kata ya Ubungo, alikanusha kuhusu barua hiyo ya kumfukuza uanachama Jacob, akieleza kuwa hajawahi kuandikana kwamba hata sahihi iliyowekwa kwenye barua hiyo si ya kwake.  Alisema anashangaa kuona jina lake likitumika katika barua hiyo kwa kuwa yeye   tayari alishaachia uongozi wa kata hiyo na katibu alishabadilishwa muda mrefu.  Alisema taarifa hizo zipuuzwe kwa kuwa si za kweli na kwamba yeye hakuhusika kwa namna yoyote kwa kuwa si kiongozi wa chama kwa sasa na aliachia nafasi hiyo ili aweze kutekeleza maukumu yake mengine kikamilifu.  BARUA YA MKURUGENZI  Katika barua iliyoonesha kuandikwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Aprili 2, 2020 yenye kumbukumbu KUMB:NA. CAB./74/216/01/07 kwenda kwa Mstahiki Meya, Boniface Jacob, ilimweleza kuhusu kupokea nakala ya barua hiyo ya kufukuzwa kwake uanachama.  “Kutokana na barua hiyo kunitaarifu kuwa “Umefukuzwa Uanachama” kuanzia  tarehe 28/04/2020, nachukua nafasi hii kukutaarifu rasmi kuwa umekoma kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mujibu wa kitungu cha  39(2)(f) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mtaa sura ya 292 toleo la Mwaka 2015 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 73(1)(e) na (f) ya kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo za Mwaka 2019. Sheria na kanuni hizo zinazofafanua kwamba “Mjumbe atapoteza sifa kuwa Mjumbe wa Halmashauri endapo atakoma kuwa mwanachama wa chama cha Siasa kilichompendekeza kuwa mgombea wa kiti cha udiwani.  “Kwa kuwa umekoma kuwa Mjumbe wa Halmashauri, pia umepoteza sifa ya kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuanzia tarehe ya barua hii, hivyo unatakiwa kukabidhi ofisi pamoja na vifaa au mali yoyote ya Manispaa ya Ubungo ikiwemo gari kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo.  Haya hivyo, alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuthibitisha kupokea barua hiyo inayodaiwakuwa ya kughushi na yeye kuandika baru hiyo ya kumtaka meya huyo kukabidhi vifaa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alisema hawezi kuzungumza suala hilo kwa muda huo na kutaka apigiwe baadaye kwa alikuwa kwenye kuratibu shughuli za uboreshaji wa daftari wa uandikishaji wapigakura vituoni.  Hata hivyo, alipotafutwa kwa mara nyingine kama alivyoagiza simu yake iliita bila kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni. 
KITAIFA
WAZIRI wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema nchi hiyo imeanza kuweka kituo cha kudumu cha kijeshi nchini Syria, hatua ambayo imeidhinishwa na Baraza la Juu la Bunge la Urusi. Hatua hiyo itajumuisha kukipanua kituo cha jeshi la majini cha Tartus ili kuweza kuwezesha meli 11 za kijeshi kutia nanga kwa wakati mmoja badala ya moja kama ilivyo sasa. Kama sehemu ya makubaliano na Serikali ya Syria, Urusi pia itapewa fursa ya kudumu kutumia kituo cha jeshi la anga cha Hmeimim. Urusi imekuwa muungaji mkono mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu nchini humo.
KIMATAIFA