text
stringlengths
0
4.5k
Rapa mahiri wa nyimbo za Injili kutoka kundi la Borne Kingz akifahamika kwa jina la Elly Joh siku ya tarehe 8.10.2017 anatarajia kuachia albamu yake mpya inayobebwa na jina la ”PUMZI” ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo ambazo zitakwenda kugusa nafsi za watu na kuwabariki wengi.
Akiongea na gospomedia.com rapa Elly Joh amesema kuwa uzinduzi wa albamu hiyo ya “PUMZI” itafanyika katika kanisa la Wordalive Centre, Kimara baruti (Kanisa Jipya) Kuanzia saa tisa mchana na kuendelea hivyo amewasihi wadau na mashabiki wote wa muziki wake kutoka pande zote za jiji la Dar na mikoa ya jirani kuja kumpa sapoti na kumtia moyo katika kutangaza ufalme wa Mungu na kushusha Baraka kutoka kwa Mungu Baba kupitia Jina la Yesu Kristo.
Rappa Elly Joh kwasasa ameachia video yake mpya iitwayo ”Misri” ikiwa inaendelea kufanya vyema sana kupitia mtandao wa gospomedia na vyombo vingine vya habari nchini ukiwa ni wimbo wa pekee unaozungumzia ukiri wa mwana wa Mungu(Kijana) ambaye ameamua kuachana na vitendo vya dhambi na kuamua kumkabidhi Yesu Maisha yake. Kama bado hujawahi kutazama video hii, leo nakukaribisha kuitazama na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Usikose kufika siku ya uzinduzi huu na hakika utabarikiwa.
1. Kuzaliwa kwa Yesu —- Noeli tarehe 25/12
2. Pasaka —- Ufufuko wa Bwana Yesu
3. Kupaa Yesu —- Siku 40 baada ya Pasaka.
5. Sikukuu ya Watakatifu Wote 1/11
⏪Swali lililopita: Katika Amri ya kwanza ya Kanisa tumeamriwa nini?
⏩Swali linalofuata: Katika Amri ya Kwanza ya kanisa tumekatazwa nini?
⏬⏬ Endelea kusoma maswali haya yafuatayo ili kuelewa zaidi swali hili kuhusu 👉Sikukuu zilizoamriwa ni zipi?👇
MMOJA KATI YA WATANO WALIOOKOLEWA MGODINI BAADA YA KUFUKIWA KWA SIKU 41 AFARIKI DUNIA
Meneja Uhusiano wa Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud
Mmoja wa majeruhi watano waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na kufukiwa na kifusi cha mchanga na kukaa siku 41 chini ya mgodi na kuokolewa, Onyiwa Kaiwao (55) amefariki dunia.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Joseph Ngowi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa chanzo cha mauti hayo ni kutokana na majeruhi huyo kutapika akiwa amelala hali ambayo ilifanya matapishi hayo kuingia katika njia ya hewa.
Dk Ngowi alisema Kaiwao alifariki jana saa sita mchana na kuongeza kuwa pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa nimonia unaosababishwa baridi kali hali iliyomfanya kutokuwa katika hali ya kawaida tofauti na wenzake.
Hata hivyo, Dk Ngowi alisema majeruhi huyo pia alikuwa na matatizo katika utumbo, na hivyo kila akienda haja kubwa alikuwa akitoa magome ya miti waliyokuwa wakiyatumia kama chakula wakati wakiwa chini ya ardhi.
Alisema hali za majeruhi wengine wanne zinaendelea vizuri, na wanaendelea na mazoezi huku wakila wenyewe hali ambayo wamepanga kesho kuangalia uwezekano wa kuwafanyia vipimo kwa mara nyingine tena.
Aidha, Dk Ngowi alisema endapo hali zao hazitakuwa nzuri na kubadilika, watawahamishia katika Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya uangalizi wa juu hali ambayo watapata mabadiliko zaidi ya afya zao.
Tazama matokeo ya kidato cha sita – MwanaHALISI Online
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) jana lilitangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita, kama ulikosa matokeo hayo basi MwanaHALISI Online imekusogezea.
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) jana lilitangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita, kama ulikosa matokeo hayo basi MwanaHALISI Online imekusogezea. BONYEZA HAPA KUTAZAMA  
DK MANDAI: ZIFAHAMU SABABU ZA MWANAUME KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA
ZIFAHAMU SABABU ZA MWANAUME KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA
Tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa kwa mwanamme huweza kusababishwa na vitu mbalimbali.
Miongoni mwa sababu hizo zinaweza kuwa ni zile sababu za kisaikolojia au kimaumbile.
Kama unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi mara unaporudi nyumbani. Hii ni kwa sababu mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.
Matumizi ya pombe na madawa
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Kuandamwa na matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Mfano magonjwa kama kisukari na hata hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango.
Mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke
Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi, hii huweza kuwa sababu endapo hakuta kuwa na mahusiano mazuri kati ya mwanaume na mwanamke katika mahusiano ya kimapenzi.
Kama wewe ni mwanaume na unasumbuliwa na tatizo hili au tatizo la nguvu za kiume jitahidi ufike Mandai Herbalist Clinc ili tukupatie tiba ya tatizo hilo na uweze kuwa vizuri kabisa katika masuala ya tendo la ndoa.
Hii video mpya ya G Nako ‘Lucky Me’ itazame hapa..
Itazame hapa video mpya ya G Nako ‘Lucky Me‘ Enjoy na Good Music kutoka kwa Weusiii…
• Soma hii, kama wewe ndio mzazi wa huyu msichana ungefanyaje?. 06 Oct 2015 16:59, (vichekesho: kichekesho vituko vunja mbavu sms meseji). Soma hii, kama wewe ndio mzazi wa huyu msichana ungefanyaje?
• KITUKO-NA-WAHENGA. 18 Aug 2017 23:24, (vichekesho-na-picha: kichekesho vituko vunja mbavu sms meseji). KITUKO-NA-WAHENGA
• Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo. 28 Oct 2016 04:38, (vichekesho: kichekesho vituko vunja mbavu sms meseji). Tofauti kati ya Binti wa Kizungu na Binti wa Kibongo
• Huyu jamaa ni shida, Chezea wimbo wa Taifa!. 06 Aug 2016 23:31, (vichekesho: kichekesho vituko vunja mbavu sms meseji). Huyu jamaa ni shida, Chezea wimbo wa Taifa!
Posted on: December 14th, 2018 Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi kijijini Ngombo</p> <p>Naibu waziri wa mifugo na uvuvi bwana Abdallah Hamis Kulega amefanya ziara ya siku &nbsp;moja wilayani Malinyi na kutembelea na kuzungumza na ...
Posted on: November 12th, 2018 Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa wilaya ya Malinyi &nbsp;Mhe.Ngollo Ng’waniduhu Malenya kwenye uzinduzi wa upimaji wa afya ,ambao umefanyika tarehe 05/11/2018 &nbsp;wilayani hapa katika viwanja v...
ZAMBARAU NAUWEZO WAKE DHIDI YA UGONJWA WA KISUKARI
Habari za leo msomaji wetu wa www.dkmandai.com napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha katika muendelezo wetu wa kufahamishana namna mimea na matunda yanavyoweza kuwa msaada mzuri katika afya zetu.
Leo napenda kuzungumzia namna zambarau inavyoweza kuwa msaada kwa mtu mwenye ugonjwa wa sukari.
Lakini kwanza ni vyema ifahamike kuwa kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili. Ukosefu au upungufu wa kemikali inayoitwa insulin husababisha ongezeko la kisukari inayojionesha kwa kiwango kikubwa katika mkojo wa mwathirika.
Pia ni vyema ikafahamika kuwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuuponyesha ugonjwa, ila kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kwaida.
Baada ya kufanya hivyo tumia nusu kijiko cha chai cha unga huo wa zambarau katika nusu glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chakula chochote.
Asante sana kwa kuendelea kuwa karibu nasi, kama unatatizo lolote la kiafya unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na pia unahaki ya kuwasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. Kisha utatuambia tatizo lako nasi tutakuwa tayari kuweza kukusaidia.
Kinadada wengi huangaika mara kwa mara kwa lengo la kuhitaji kuwa na nywele nzuri zenye muonekano mzuri kila siku, lakini kwa bahati mbaya sana si wote wanabahatika kufanikiwa kuwa na nywele hizo nzuri.
Kama wewe ni dada ambaye huenda unashida hiyo basi tambua kwamba moja ya sababu ya nywele kushindwa kukua vizuri ni pamoja na hii sababu ya kuwa na mba kichwani mwako.
Sasa leo napenda kukupatia hii mbinu ya kumaliza shida ya mba kwa kutumia mchanganyiko wa mafuta ya nazi na ndimu ili baadaye uweze kuwa na nywele zenye afya bora.
Weka mafuta ya nazi kwenye kibakuli kisha pima kijiko kimoja cha chakula chenye maji ya ndimu na ukoroge vyema. Kisha tumia mchanganyiko huo kwa kuweka kichwani na uhakikishe unafika hadi kwenye mizizi ya nywele kabisa fanya hivyo kwa dakika kadhaa. Kisha kaa na mchanganyiko huo bila kuosha kichwa kwa dakika kama 20 hivi.
Baada ya dakika hizo kupita osha kichwa chako vizuri, kisha ufanye zoezi hilo kwa mara mbili hadi tatu kwa wiki ili kupata matokeo mazuri zaidi.
Ikiwa unahitaji kuuliza zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisini kwetu tupo Ukonga, Mombasa maeneo ya Mongolandege jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)...
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi ...
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi amezindua Ujenzi wa Zahanati ya Shenda ambayo inatarajiwa kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na...
Najua wengi tunaifahamu sana kabichi kama mboga na baadhi yetu tunaitumia sana katika maisha yetu ya kila siku.
Moja ya faida za kabichi ni ule uwezo wake wa kuwasaida wale wenye nia au malengo ya kupunguza miili yao au wanene kupita kaisi. sifa hiyo inatokana na kalori ndogo zilizomo ndani ya kabichi pamoja na ufumwele mwingi.
Aidha, ulaji wa kabichi pia huweza kumsaidia mwili kujenga kinga madhubuti dhidi ya magonjwa hatari ikiwemo saratani. Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee wa kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za mada za 'Antioxidant', 'Anti-inflammatory' na 'Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.
Hizi ni aina za kabichi
Pamoja na kuwa mboga hii ya kabichi si mboga pendwa sana na watu wengi, lakini ni mboga yenye kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin hasa vitamini K, B1, B2, vitamin A na C. Pia kabichi ina kiasi kingi cha ufumwele au kamba lishe kwa maana ya fiber, ambapo vyote hivyo ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.
Hizi ni faida za kabichi nimeona ni vyema uzipate leo kutoka kwetu Mandai Herbalist Clinic, lakini kwa maoni na ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na Dk.Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe dkmandaitz@gmail.com Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu
Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakihitaji kufahamu kuhusu faida za muembe katika tiba.
Kwa ufupi naweza kusema kuwa majani yake yana nafasi kubwa katika kuzaidia kutibu ugonjwa wa kisukari hasa pale yanapokaushwa vizuri.
Ikiwa utapenda kufahamu zaidi kuhusu tiba hii ya majani ya muembe unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au tupiga simu kwa namba zifuatazo ili kupata maelekezo zaidi jinsi ya kufika kwa urahisi Mandai Herbalist Clinic 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.
HUU NI UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNAOFANYWA KANDO KANDO YA MITO NDANI YA MITA 60 WILAYA YA IRINGA ~ Mzee wa matukio daima
Home » » HUU NI UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNAOFANYWA KANDO KANDO YA MITO NDANI YA MITA 60 WILAYA YA IRINGA
HUU NI UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNAOFANYWA KANDO KANDO YA MITO NDANI YA MITA 60 WILAYA YA IRINGA
Vijana wakiendelea kufyatua tofali katika eneo la Muwimbi wilaya ya Iringa kando kando ya mto ,hivi sasa serikali imeagiza wote wanaoendesha shughuli hatarishi kwa mazingira ndani ya mita 60 kutoka katika kingo za mito kuondoka
Hivi ndivyo mazingira yanavyoharibiwa eneo hili ambalo lipo kando kando ya barabara kuu ya Iringa ,Mbeya
Eneo hili ni moja kati ya maeneo maarufu kwa ufyatuaji wa tofari katika wilaya ya Iringa
Home » » LOWASSA AHOJIWA KWA SAA NNE,AACHIWA KWA DHAMANA
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.
Akizungumza baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00 mchana.
"Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29," amesema.
Jeshi lazima uasi Madagascar _ Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili _ DW _ 22.11.2010
Jeshi ambalo ni tiifu kwa uongozi wa serikali ya Andry Rajoelina limefanikiwa kuzima uasi uliofanywa na maafisa wa ngazi za chini katika kisiwa hiki cha Bahari ya Hindi
Watu wa Madagascar kwa mara nyingine wameshtushwa na uasi wa wanajeshi!
Waziri Mkuu wa Madagascar, Camille Vital, amesema kuwa jaribio la kuiangusha serikali limezimwa bila ya damu kumwagika, baada ya maafisa 16 wa kijeshi waliohusika na uasi huo wamejisalimisha.
Hapo awali waasi walitangaza kuwa walikuwa wanatwaa mamlaka kutoka kwa kiongozi wa sasa, Andry Rajoelina, ambaye mwaka jana pia alitwaa uongozi kutokana na kuungwa mkono na wanajeshi. Mamia ya Wanajeshi watiifu walionekana wakikusanyika karibu na uwanja wa ndege ambapo waasi walikuwa wameweka kambi yao. Maafisa waasi walikuwa wametangaza kuvunjwa idara zote za uongozi za Madagascar na kusema kuwa wameunda baraza la uongozi la kijeshi.
Waziri Mkuu Vital amesema licha ya kusikika milio ya silaha, hakuna mtu hata mmoja aliyejeruhiwa, na kwamba sasa hali imerejea kuwa shwari katika nchi hiyo.
Watanzania wawili wametangazwa washindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017.