text
stringlengths
0
4.5k
Wawili hao watazawadiwa $5,000 kila mmoja katika sherehe ambayo itafanyika jijini Nairobi mwezi ujao.
Waziri wa habari, utamaduni na Sanaa Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amewapongeza wawili hao kwa ushindi huo na kusema ushindi wao "unachagiza juhudi za serikali kuibidhaisha lugha ya Kiswahili."
"Ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa taifa kwa ujumla," amesema Dkt Mwakyembe kupitia taarifa.
Tuzo hiyo ilianzishwa mwaka 2014 na Dkt Lizzy Attree (Mkurugenzi wa Tuzo ya Caine) na Dkt Mukoma wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani), kwa lengo la kuthamini uandishi kwa lugha za Kiafrika.
Aidha, tuzo hiyo inakusudiwa kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe, na pia kutafsiri maandishi ya lugha nyengine kwa lugha za Kiafrika.
Majaji walikuwa Ken Walibora Waliaula (Mwenyekiti wa Majaji), mwanataaluma na mwandishi; Daulat Abdalla Said, mwanataaluma na mwandishi, anayesomesha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar; na Ali Attas, mwandishi na mwalimu wa Kiswahili na Kiingereza, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Japan.
"Licha ya kwamba matukio ya riwaya hii yanatokea katika kisiwa cha kubuni, maswala yanayojadiliwa humu ni miongoni mwa yale maswala sugu yanayoendelea kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii na kiuchumi."
Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika, yenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani 15,000, hutolewa kila mwaka kwa miswada bora, au kwa vitabu vilivyochapishwa miaka miwili kabla ya mwaka wa kutolewa zawadi, katika fani za riwaya, ushairi, wasifu na riwaya za picha.
Tuzo hii inadhaminiwa na kampuni ya Mabati Rolling Mills, Kenya, na kampuni ya ALAF Limited, Tanzania na pia Ofisi ya Makamu wa Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Cornell, na Idara ya Taaluma za Afrika ya Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani.
Swahili na Waswahili: HUYU NA YULE: Mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.‏
Kuna usemi usemao "Makundi ya WhatsApp ni kama mchezo wa mpira wa miguu ambao huwajumuisha uwanjani wachezaji 22 na jukwaani kukawepo watu elfu sitini au zaidi ambao ni watazamaji." Lakini hebu tujiulize, ni raha zipi na vile vile ni karaha zipi za makundi haya?
Wenyeji wakiwa kwenye maongezi ya hapa na pale
Kona ya Afya: Kula zabibu usipatwe na ugonjwa wa moyo
MATUKIO NA JAMII BLOG: Somo kwa wote wenye wapenzi huko vyuoni... hii muhimu kwenu
Somo kwa wote wenye wapenzi huko vyuoni... hii muhimu kwenu
KARIBU KATIKA TOVUTI YA MKOA WA MANYARA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara , inayo furaha kukukaribisha katika tovuti hii. Tunatumaini utapata taarifa za kuaminika unazozihitaji kwa ukamilifu kuhusu wigo, upeo wa taasisi, dira, dhamira, malengo, mikakati, shughuli kuu, ahadi na utekelezaji wa shughuli za Serikali.
Ujio wa tovuti hii ni tukio la kihistoria katika kufikia dira na matarajio yetu hasa kutangaza shughuli za Serikali lakini pia na huduma zetu kwa umma.
Kupitia tovuti hii tunaamini kwamba itakuwa rahisi kwa wananchi kupata taarifa mbalimbali. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayetembelea tovuti hii atapata jambo la kumfurahisha, kumfundisha au kumuelimisha.
Ni nia yetu kuendelea kuboresha tovuti hii kadri muda unavyokwenda ili ipatikane kwa urahisi na ubora wa hali ya juu. Tunafurahi sana kuzungumza na watembeleaji wa tovuti waliohamasika na tunathamini kila maoni tutakayoyapokea.Tovuti hii ya Mkoa wa Mwanza inamilikiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Msanii kutoka Wasafi Classic Baby maarufu kama Harmonize baada ya kuwa na collable kibao kupitia ngoma zake na nyingine alizoshirikishwa na wasanii wenzake, sasa ameachia video Mpya wa waimbo wake wa 'SINA'.
Katika video hii mkongwe wa TAKEU STYLE Mr. Nice ameonekana.
Mlolongo wa Habari zinazomhusu Rais Mstaafu Mwinyi
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, hajui “kinachoendelea” eneo la kambi ya jeshi ya usafirishaji-Kunduchi (KTC), MwanaHALISI limegundua.
KUNA matukio mawili yenye kuashiria jinsi Rais Jakaya Kikwete anavyoishiwa uvumilivu kutokana na malumbano ya kimakundi ndani ya chama chake- Chama Cha Mapinduzi (CCM).
KAMATI iliyoundwa kuchunguza chanzo cha milipuko ya mabomu Mbagala, wilayani Temeke, Dar es Salaam, imekabidhi ripoti yake kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Ali Mwinyi
WAZIRI wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi ameahidi kujiuzulu iwapo itagundulika kuwa milipuko ya mabomu, kwenye ghala la silaha katika kambi ya jeshi, Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam ilitokana na uzembe.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi amekuwa mmoja wa mawaziri wanaosema ukweli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, Ametowa Wito Kwa Wafanyabiashara Zanzibar Watumie Vema Azma ya Serikali ya Kuwapunguzia Ushuru wa Bidhaa. - ZanziNews
Home HABARI MATUKIO Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, Ametowa Wito Kwa Wafanyabiashara Zanzibar Watumie Vema Azma ya Serikali ya Kuwapunguzia Ushuru wa Bidhaa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Alhajj Ali Mohamed Shein, Ametowa Wito Kwa Wafanyabiashara Zanzibar Watumie Vema Azma ya Serikali ya Kuwapunguzia Ushuru wa Bidhaa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa risala ya kuukaribisha Mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi wa zanzibar na tanzania kwa ujumla katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,pia amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi kuwa na mashirikiano ya pamoja na kumcha Mwenyeezi Mungu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wafanyabiashara wa jumla na reja reja waitumie vyema azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwapunguzia ushuru wa bidhaa za chakula katika mwezi wa Ramadhani, ili wananchi wapate bidhaa hizo kwa bei nafuu.
Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo katika risala maalum aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari katika kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1439 Hijria sawa na mwaka 2018 Miladia.
Alieleza kuwa wafanyabiashara wanapaswa kujitahidi kuwa waadilifu, waaminifu na kutenda haki katika kufanya biashara zao pamoja na kuhakikisha kuwa vipimo vyao vya kuuzia bidhaa ni vya halali kwani ni kinyume na sheria watu kudhulumiana katika vipimo.
Kutokana na hali hiyo, Alhaj Dk. Shein aliziagiza Taasisi zinazohusika kulisimamia vyema jambo hilo na wasichelee kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobanika, kufanya biashara kinyume na sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Aidha, Alhaj Dk. Shein aliwahimiza wananchi kujiandaa na Ramadhani kwa kufanya zaidi mambo mema na ibada za Saumu, Sala na utoaji Sadaka katika mwezi huo wote sambamba na kuzidisha kusoma Qur-an na kuielewa pamoja na Hadith za Bwana Mtume Muhammad (S.A.W), ili waweze kuzitekeleza ibada zao vizuri.
Pia, Alhaj Dk. Shein alisisitiza kuwa katika mwezi wa Ramadhani himizo linatolewa katika kuzidi kutendeana wema na ihsani na kusisitiza kuwa utoaji wa sadaka ni jambo la msingi ili wenye kipato kidogo nao wawe wenye furaha katika mwezi huo.
Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa Ramadhani mwaka huu imekuja ikiwa bado msimu wa mvua za Masika unaendelea hivyo, aliwaomba wananchi kwa umoja wao washirikiane katika kuiweka miji yao katika usafi ili wajiepushe na janga la maradhi ya kipindupindu pamoja na maradhi mengine ya miripuko.
Hivyo, Alhaj Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi wanaomiliki mikahawa na nyumba za starehe wajitahidi kuzingatia sheria,taratibu na utamaduni uliopo ili kuzuia kero na maudhi kwa wananchi wenzao wenye kutekeleza ibada ya funga.
Pia Alhaj Dk. Shen, aliwataka madereva na watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani hasa wakati wa jioni ambapo watu wengi huwa wanakimbilia kufutari, huku akiahidi kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuimarisha ulinzi wa watu na mali zao kwa kushirikiana na vijana wa ulinzi shirikishi ili wananchi wapate utulivu na kutekeleza saumu kwa amani.
Kama kawaida yake Alhaj Dk. Shein aliwakumbusha viongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wachukue hatua ya kuwapelekea maji wananchi kwa magari kwenye maeneo yao wanayoishi ambayo huduma hizo zimepungua.
Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza jinsi uchumi wa Zanzibar ulivyoimarika sambamba na utoaji wa huduma na ustawi wa wananchi huku akiwapongeza wakulima wa karafuu kwa mafanikio makubwa yaliopatikana ambapo msimu uliopita jumla ya tani za karafuu 8,539.39 zenye thamani ya TZS bilioni 119.14 zimenunuliwa na Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) hadi Mei 15 mwaka huu.
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUSHUGHULIKIA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA - SUFIANIMAFOTO
Home Siasa WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUSHUGHULIKIA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUSHUGHULIKIA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa. Wajumbe wa Kamati walifanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Omary Seif Abeid na Bw. Mihayo Juma N'hunga Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (aliyesimama) akiongea na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Muungano Bw. Baraka Rajab Baraka.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao pia ni wajumbe wa kamati ya Kusimamia viongozi wakuu wa kitaifa wamekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mh. January Makamba, Jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo la kuzungumzia baadhi ya changamoto za Muungano na kubadilishana mawazo katika maeneo ya Muungano.
Waziri Makamba aliwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo, na kusema kuwa ujio wao unaonyesha dhamira nzuri ya kuwawakilisha wananchi wa Zanzibar na kuimarisha Muungano uliodumu kwa miaka hamsini na saba (53) sasa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Omary Seif Abeid ambaye pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba, alisema kuwa, pande hizi mbili za Muungano hazina Budi kuwakumbuka waasisi wa Muungano huo Hayati Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuunganisha pande mbili hizi na kupatikana kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kuwa anaeubeza Muungano anajibeza mwenyewe.
Mawaziri Wakuu wa zamani Edward Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Taifa na Fredrick Sumaye leo wamemtembelea gerezani Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema kwa lengo la kumsalimia kiongozi huyo.
Lowassa ameongozana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro na Bob Lowassa, hadi Gereza Kuu la Kisongo Mjini Arusha na kumjulia hali Lema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema anao mkakati wa kupita kila nyumba kuwapima wanaume saratani ya......
waziri amtumbua mkurugenzi wa bodi ya korosho
Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha......
MTOTO WA KITAA: MPAMBANO MASUMBWI UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Mei 03 kila mwaka wanahabari na wadau wa habari huungana pamoja kuadhimisha “Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani” ambayo iliasisiwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1993.
Pamoja na mambo mengine, maadhimisho haya hulenga kutambua mchango wa vyombo vya habari pamoja na kuwakumbuka wanahabari waliopata madhara kutokana na kazi zao.
Jijini Mwanza, baadhi ya wanahabari wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na maadhimisho haya ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma yakiambatana na kaulimbiu isemayo “Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari, Haki na Utawala wa Sheria”.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Kassim Suleiman Khamis anatarajiwa kukosa michezo yote iliyosalia katika Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup yanayoendelea nchini Kenya.
Daktari Mkuu wa Zanzibar Heroes, Mohd Said alithibitisha taarifa hizo za kukosa huduma ya mshambuliaji huyo.
“Awali tulitegemea angeweza kuipata nusu fainali na mchezo wa mwisho, lakini mpaka sasa dalili hiyo haipo tena na atalazimika kukosa mashindano yote haya ukiwemo mchezo wa kesho dhidi ya Uganda na ule wa mwisho”.
Kassim ndie kinara wa kufunga mabao kwa upande wa Zanzibar baada ya kufunga mabao mawili yote akitokea benchi katika michezo Heroes iliposhinda 3-1 dhidi ya Rwanda na ule wa 2-1 dhidi ya Tanzania bara na kupelekea vilabu vingi ikiwemo Simba kuhitaji huduma yake.
Kamera ya mtandao huu imelimulika tukio baya la ajari iliyohusisha pikipiki mbili eneo la Club Royal karibu na lango la kuingilia chuo cha Utumishi wa Umma cha Tabora zamani UHAZILI.
Mashuhuda waliuambia mtandao huu kuwa wanalalamikia jeshi la polisi kuto kujitokeza mapema eneo la tukio licha ya kuwa hapana umbali unaozidi mita 100 kutoka eneo la tukio, mfuatiliaji wa tukio aliwahoji kama kuna yeyote aliyetoa taarifa kituoni dhidi ya tukio hilo lakini hakupata majibu.
Abiria na mhanga wa ajali hiyo akiwa anaugulia maumivu baada ya ajali iliyotokea muda mfupi maeneo ya Club Royal karibu na geti kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI
Askari wa Jeshi la usalama barabarani akijongea eneo la tukio. Inakadiriwa ni zaidi ya dakika 15 au zaidi (Kwa mujibu wa mashuhuda) zilipita ndipo askari alijitokeza eneo la tukio licha ya tukio hilo kutokea umbali wa mita za makadirio zisizozidi 100 kutoka kituo kukuu cha Polisi mjini Tabora.
Askari akifuatilia tukio hilo baada ya dakika zinazokadiriwa na mashuhuda wa tukio kuwa ni zaidi ya 15 toka ajari imetokea.
Home HABARI PICHA WANAFUNZI WAKIPATIWA ELIMU KUHUSU BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE MJINI DODOMA
WANAFUNZI WAKIPATIWA ELIMU KUHUSU BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE MJINI DODOMA
Afisa Habari (Itifaki) wa Bunge, Ndg. Patson Sobha (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Miyuji walipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mjini Dodoma.
Afisa Habari (Itifaki) wa Bunge, Ndg. Patson Sobha akizungumza na wageni Mbali mbali waliotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea Mjini Dodoma. PICHA NA OFISI YA BUNGE
Hapa ni mzazi mwenzie Andrew na mtoto wao mpendwa Zoe wakiwa mbele ya mwili wa marehemu.Mwili wa marehemu utawasiri Dar es Salaam siku ya jumanne na jumatano ndugu na jamaa wa Dar_Es_Salaam wata Ibada ya misa na kuaaga mwili ndani ya kanisa la Lutheran nyuma ya Ubungo Plaza siku ya jumatano asubuhi kisha safari ya Dodoma jioni na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis May 05.
Mwakilishi wa ubalozi wa Tanzania hapa Marekani angeongea mbele ya watu waliojitokeza ndani ya kanisa kwa ajili ya Ibada ya misa na kuaga mwili wa Andrew.
Mzazi mwenza wa marehemu Andrew akitoa neno mbele ya watu waliojitokeza kuja kuaga mwili wa marehemu.
Majonzi kwa kila mmoja aliepita mbele ya mwili marehemu.
Ny Ebra kutoka New York nae ni mmoja kati ya watu waliotoka nje ya Houston, Texas kwaajili ya kuaaga mwili wa Andrew, hapa Ebra akipata ukodak na Emmy mzazi mwenza wa marehemu Andrew na mtoto wao Zoe nnje ya kanisa baada ya kuaaga mwili pamoja na Ibada ya misa.
Shirika la msaada, Save the Children, limeonya kuwa ukosefu wa msaada unaathiri jitihada za kimataifa kuwasaidia wakimbizi wa Syria wakati msimu wa baridi unawadia.
Linasema hakuna nguo nzito, blanketi na makaazi ya kutosha. Shirika hilo linasema theluji na baridi kali zitaifanya hali kuwa mbaya zaidi katika wiki zinazokuja.
Hazina maalum iliyoundwa kuwasaidia wakimbizi ina upungufu wa dola milioni mia mbili.